Barua ya wazi kwa Tundu Lissu kumuonya dhidi ya kutetea masikini na wapumbavu

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Mar 24, 2018
21,730
52,633
BARUA YA WAZI KWA TUNDU LISU

Na, Robert Heriel
Taikon wa Fasihi,
S.L.P 9977, JIBI,
Kutoka Nyota ya Tibeli.
30, 07. 2020.

YAH: KUKUONYA DHIDI YA KUTETEA MASIKINI NA WAPUMBAVU.

Ndugu Mhe Lisu, Kichwa cha habari hapo juu cha husika.

Ninafuraha kubwa kukuandikia barua hii ya wazi ambapo najua watu wengi wataisoma nawe itakufikia. Utanisamehe ikiwa njia hii niliyoitumia pengine isikufurahishe lakini ni katika hali ya kukupa ujumbe wenye manufaa wewe na wale wote wenye tabia kama zako, mimi nikiwa mmoja wao.

Mhe. Lisu, nimekufuatilia kwa miaka saba sasa, sisemi nakufahamu lakini angalau ninachakusema kidogo kukuhusu. Umejipambanua kama mtu apendaye haki, mtu apendaye utawala wa sheria, mtu apendaye demokrasia. Lisu umekuwa mstari wa mbele kukemea maonevu uyaonayo ndani ya nchi yako, umejigeuza kama msemaji wa wanaoonewa, kutetea wanyonge wanaonyimwa haki zao. Upo sawa, lakini umekosea jambo moja; nalo ni kushindwa kujua unatetea watu wa aina gani. Hilo ndilo kosa lako kuu.

Huwezi tetea haki za masikini ukabaki salama, huwezi tetea haki za wapumbavu ukabaki salama. Huwezi tetea watu wasiojielewa, huwezi tetea watu wasiojua unapigania nini kwao, huko ni kujitafutia matatizo makubwa ambayo hao unaowatetea hawatakusaidia kitu kwa sababu wao ni wapumbavu na masikini.

Kikawaida masikini ni watu wasiojithamini, watu wasio na shukrani, watu wasiojitambua, wengi wao ni wachawi, wanga, watu wasio na fadhila, masikini ukimsaidia huyo huyo ndio atakuja kukusema unajidai, ukimtetea masikini au mpumbavu huyo huyo ndio atakuambia unakihere here. Kamwe nakusihi acha mara moja kuhangaika na masikini.

Masikini unachoweza kuwasaidia ni kuwadhulumu hata kile kidogo walichonacho, kuwabagua, kuwatenga, kuwadharau, hicho ndicho wakipendacho masikini. Lakini ukijifanya unawapenda, unawajali nakuhakikishia unajiingiza mkenge, utaumia, utasagika na hakika utamalizika.

Nikukumbushe Ndugu Mhe. Lisu, hakuna aliyewahi kuwatetea masikini, na kuwapigania masikini akabaki salama. Wote waliojiingiza katika harakati hizo walikufa vifo vibaya, wengine walipewa adhabu kali za kuliwa na mamba, kuliwa na simba, kuchomwa moto, wakapotea na kuangamia.

Katika Dini, wapo Manabii walikuja kutetea haki za wanyonge, haki za masikini lakini wote waliuawa, tena wakazomewa na hao hao masikini. Nakupa mifano ya watu katika dini waliokuwa wanaharakati kama wewe, Musa, ndiye yule Mlawi aliyewatoa waisrael Misri, naye aliwapigania watumwa wale na kutaka kuwa uhuru wao. walichomlipa wote tunajua, walianza kulalamika kuwa bora warudishwe utumwani Misri kuliko kuwa huru Kanaani katika nchi yao. Mungu alitaka kuwaua lakini Kihere here cha Musa akawatetea, siku zilizofuata wakataka kumuua Musa wasijue huyo ndiye aliwatetea wasiuawe na Mungu. Musa alipowashtaki kwa Mungu, Mungu akamuambia, wewe si uliwatetea hao masikini, watumwa, wapumbavu wasiojielewa. Acha wakuue ili uwe na akili. Musa akabaki katumbua macho. Biblia inasema, Mungu aliwafyeka wote njiani, akambakiza Joshua na Kalebu. Huwezi kukomboa masikini, huwezi komboa watumwa, huwezi komboa wapumbavu ukabaki salama. Kuwatetea wapumbavu ni kutaka kutofika kanaani, usishangae kwa nini Musa hakufika Kanaani, aliwaendekeza wapumbavu wale.

Yesu naye walimuua, wakamsulubisha, na kumtemea mate. Na wale aliokuwa anawatetea ndio hao hao waliomtukana, walioimba asulubiwe. Huwezi Mkomboa masikini hata siku moja. Huwezi komboa mtu mpumbavu ukasalimika.

Hata kwenye maisha ya kawaida, wale unaowasaidia ndio hao hao watakaogeuka maadui zako. Hao hao ndio watakao kuteta.

Mhe Lisu, naomba nikuonye, na ikikupendeza fuata ushauri wangu. Acha kutetea haki za wapumbavu, haki za masikini, haki za wanyonge sijui upuuzi gani. Mungu mwenyewe atahangaika na watu wake. Ikiwa yeye kaacha watu waonewe wewe unakuja kuwatetea huoni unatafuta maneno.

Masikini ni kama swala au digidigi mbugani, huwezi mgeuza digidigi akawa simba alafu ukabaki salama. Ili mbuga iwe na amani ni lazima swala aliwe, kumtetea swala ni kuchafua amani ya mbugani.

Nature inataka dunia iende hivyo, wote waliojifanya kutetea tabaka la chini walipotezwa, na uhakika ni kuwa watazidi kupotezwa.

Nakushauri; tetea watu wenye akili, watu matajiri, watu wenye nguvu, hao utapata ulinzi, hao hawana unafiki, hao utapata cheo, na utaishi kwa amani.

Matajiri ukiwatetea wanajua thamani ya kile unachokifanya, hivyo nawe watakutetea siku yakikukuta yako. Lakini masikini ukiwatetea kwanza wao wenyewe hawajui thamani yao iweje wajue thamani ya kile ukifanyacho, zaidi sana watakutelekeza siku yakikupata kisha watakuambia ulikuwa unakihere here.

Watu wenye akili ukiwatetea watakulinda, kwa maana wanajali kile ukifanyacho, watakulipa hisani na fadhila. Lakini wapumbavu ukiwatetea hao hao watakuwa wakwanza kukusnitch na kukuuza kwa bei ya kutupwa, mwisho utauawa na kuangamizwa.

Wenye nguvu ukipendekeza kwao, watakulinda. Wao wanajua na kuthamini mchango wako kwao. Lakini sio kwa watu wanyonge na fukara. Wanyonge wataishia kukusengenya na kukuloga, ukiwa mbele yao wanakushangilia ukitoka wanakusema. Wataachaje kukusema ikiwa hawana kazi, kazi yao ni kusengenya watu vijiweni.

Mhe. Lisu, acha kupoteza muda wako. Hutapata zawadi popote pale iwe huku duniani au kwa yule aliyeiumba hii dunia.

Aliyeumba hii dunia ndiye anataka dunia iwe hivi ilivyo, wapumbavu wahenyeke, wenye hekima wale bata. Masikini wachapike, matajiri wale upepo mwanana.

Namna bora ya kumsaidia masikini ni kumdhulumu na kumuonea. Namna bora ya kumsaidia mpumbavu ni kumfundisha upumbavu,.

Kufikia hapa Mhe, Lisu niseme ni matumaini yangu barua hii utakuwa umeielewa. Na utaifanyia kazi.

Wako katika majukumu

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
0693322300
robertheriel99@gmail.com

Nakala moja kwa

1. Tundu Anthipas Lisu
2. Wanaharakati wote
3. Wanamageuzi

Nakala nyingine nitabaki nayo.
 
Niliyemwandikia kaelewa, na wale wenye tabia kama zake pia wataelewa. Wewe kama haikuhusu sio lazima uelewe
Nmesoma nmegundua tunahitaji ukomboz wa kifikra sio hela wala Uhuru Bali Amani...


Hongera kwa mtazamo wako uko sahihi pia,ila naona vyema zaid kama utaongezea kusema MASKINI ANAHITAJI KUKOMBOLEWA KIFIKRA (KUJITAMBUA NA KUWATAMBUA NAFASI YA KILA MTU KTK JAMII) ,Baada ya kujitambua ndio APATIWE amani ili AZIONE FURSA ZA KIUCHUMI kujiendeleza...-ELIMU ELIMU ELIMU-
 
Back
Top Bottom