Barua ya wazi kwa Tundu Antipass Lissu

Maramla

JF-Expert Member
Jan 8, 2014
581
642
Kwako Mhe. Tundu Antipass Lissu
S.L.P wodini, Ubelgiji

Kwanza nianze kwa kukuombea uendelee kupata afya njema huko wodini unapoendelea na matibabu na nikupongeze kwa kutumia muda wako kuandika neno kwa kiongozi wako wa nchi. Naamini yeye kwa utashi wake, kama umemfikishia andiko lako (au ulituma mitandaoni tu?), anaweza kuamua apatapo wasaa kusoma na kukujibu.

Nikiwa raia kama wewe ambavyo umetumia haki yako kwa mujibu wa ibara ya 18 ya Katiba kutoa maoni yako, nami nimeona nichangie mawili matatu katika andiko lako kwa sababu mbili:

Mosi, pamoja na kudai kumwandikia Rais andiko lako, ama wewe mwenyewe au mawakala wako wamelisambaza hadharani na limechapishwa.

Pili, nimeona umejadili masuala zaidi ya wewe na Rais, mambo ya kitaifa. Basi nami nitayasemea yale ya kitaifa.

*Sakata la Makonda na Utawala wa Sheria*

Umeanza kwa kumpongeza Mhe. Rais alivyosimamia utawala wa sheria katika sakata la Makontena ya Makonda lakini ukabeza kuwa Rais amelizungumza hili kwa upole lakini pia ukajaribu kujenga hoja kuwa huu uwe mwanzo wa Rais kuheshimu utawala wa sheria.

Nami nianze hapo hapo. Nikupongeze kwa mara ya kwanza katika maisha yako naona nawe umeandika kwa upole sana, ukiachana na ile tabia yako ya kijinga ya kukurupuka na kuropoka ropoka kama wale jamaa wabeba zege. Hongera. Bila shaka yapo uliyoyatafakari ukiwa wodini.

*Rais aanze kufuata utawala wa sheria*

Katika andiko lako umejaribu kujenga hoja kuwa amri ya Rais kumtaka Makonda afuate sheria kwa kulipa kodi iwe mwanzo wa Rais kufuata sheria. Nimekuelewa, tofauti na uropokaji wako wa mwanzo, hapa umetumia tafsida kuwa Rais au nchi haifuati sheria au Makonda kabebwa. Najua uko wodini yako ambayo hukumbuki.

Juzi tu lilitokea sakata la kodi ya mafuta, Rais pia alisisitiza sheria ifuatwe na kodi zilipwe. Kwa wale wafanyabiashara hukuandika andiko kushinikiza hatua zaidi!

Nataka kukubaliana nawe kuhusu umuhimu wa kufuata sheria kama ulivyosema lakini pia nikukosoe zaidi kuwa usipotoshe umma kama vile nchini hii sheria hazifuatwi au anapokuja Makonda zinakuwa tofauti.

Wewe umekuwa mbunge kwa mujibu wa taratibu za kisheria, sheria zisingefuatwa usingekuwa mbunge. Tena nakumbuka ubunge wako umepata kupingwa Mahakamani, kama sheria zisingekuruhusu wewe kupigania ubunge wako na kama sheria zisingeiruhusu Mahakama kutafsiri sheria bila shaka usingekuwa mbunge.

Kwa hiyo pamoja na kukupongeza hapo awali kuwa umepona kidogo kuropokaropoka, bado kuna vidalili kuwa unavimaradhi vya kuzungumza mambo kijumla jumla. Naamini hili utalifanyikazi huko wodini.

Nikukumbushe tu Tanzania ni nchi inayofuata na kuheshimu sheria ndio maana hata wewe umeshinda kesi kadhaa Mahakamani, ukiwa mwanasiasa umeruhusiwa kuwa Rais wa Mawakili nchini na kuivuruga kabisa TLS ukaitumia kisiasa na leo iko hoi haina uhalali tena wa kuiongoza tasnia ya sheria.

Serikali ni watu inawezekana wakawepo watu wachache wanaokiuka sheria lakini ndio maana siku zote Rais Magufuli amehakikisha sheria zinachukua mkondo wake ndio maana wapo viongozi wameonywa kwa kukiuka sheria, wapo ambao wamechukuliwa hatua, wapo ambao wapo Mahakamani lakini wako ambao kwa kufuatwa sheria wamepata haki zao kama Mwenyekiti wako Freeman Mbowe ambaye pamoja na kumpiga msimamizi wa kituo kule Hai hatimaye aliachiwa huru na Mahakama.

Lakini nikukumbushe, kama wewe ni mpiganaji wa haki wa utawala wa sheria, ungekuwa wa busara na wa maana sana kwa Taifa kama ungemkumbusha pia Rais katika barua yako juu ya uvunjaji wa sheria unaofanywa na watu mbalimbali kikiwemo Chama chako kuitisha maandamano bila kibali, Mwenyekiti wako wa Chadema Taifa kuchochea mauaji kwa kauli zake chafu.

*Ndugu Tundu Lissu, Wodini Ubelgiji,*

Najua uko kitandani lakini nikukumbushe pia kwa kupigania kwako utawala wa sheria pia ungemkumbusha Rais kukibana chama chako ambacho kimekiuka sheria za ukaguzi kwa kushindwa kutoa nyaraka kuthibitisha matumizi mbalimbali ya mamilioni ya fedha za ruzuku ambazo ni fedha za umma. Huu ni uvunjifu mkubwa wa sheria ndani ya chama chako.

Lakini juzi tu najua umesikia kule Buyungu katika uchaguzi mdogo kuwa Chama chako kiliungana na ACT ya Zitto Kabwe.

Nimeshangaa, katika kumkumbusha Rais kutekeleza utawala wa sheria, hukumwambia achukue hatua kali kwa mbia wenu ACT ambaye naye amekiuka sheria za ukaguzi kwa kufanya kituko cha mwaka cha kushindwa kabisa kabisa kuwasilisha hesabu zao ili zikaguliwe. Mamilioni yaliyokwenda katika chama hicho hayajulikani yametumikaje hadi sasa.

*Haki za Kisiasa na Haki za Binadamu,*

Katika siasa umegusia haki ya kufanya mikutano ya siasa kuwa Rais ameibana na ukataja kuwa haki hiyo imebainishwa kwa mujibu wa Katiba. Wewe ni mwanasheria nashangaa umempa Rais ushauri mbovu kabisa katika hili.

Nikukumbushe ambacho hukumwambia Rais au umetaka kumwingiza mkenge; haki za kisiasa au haki nyingine zozote zinaendana na wajibu.
Tofauti na ibara uliyoitaja inayotoa haki ya kushiriki siasa nakadhalika, hukumsaidia Rais kuwa akiwa mtetezi mkuu wa Katiba ibara ya 30 ya Katiba inaanisha wajibu wa haki nyingine zote zilizotajwa kuanzia ibara za 12 hadi 29 ikiwemo kulinda amani ya nchi, ustawi wa umma na haki za wengine ambazo yeye anapaswa kuzilinda.

Unaposema Rais kazuia kimakosa mikutano holela ya siasa lazima uzingatie mamlaka yake haya mapana ya kikatiba.

Mikutano yenu mingi ya siasa imesababisha madhara ikiwemo vifo kadhaa ambapo mmeishia kuuhadaa umma. Mabomu yale ya Arusha mlidai mnaoushahidi. Hadi leo hamjapata kuutoa. Watu wamekufa wasio na hatia na kwa mikakati yenu ya kisiasa (na nimeshangaa wala hukuwakumbuka katika barua yako).

Lakini nikukumbushe pia mikutano haijazuiwa, tofauti na ulivyomdanganya Rais bali imewekewa taratibu kulinda haki za wengine kwa mujibu wa ibara ya 30 na wenzako, kwa kuwa wewe uko wodini, wameendelea sana na mikutano yao katika majimbo yao na sasa katika chaguzi ndogo mikutano ya siasa inaendelea kote nchini.

Kumdanganya Rais kuwa hana mamlaka kulinda amani na utulivu ni kosa kubwa sana katika andiko lako. Naamini wote watakusamehe kwa uongo huu wa hadharani.

Lakini umejadili haki za binadamu na kutaja matukio mengi. Bahati mbaya hapa umemchosha tu Rais. Umepiga siasa.

Umeorodhesha mambo ambayo unaamini kabisa ama baadhi yako mahakamani au yanachunguzwa lakini ukakwepa kutaja uhalisia wa baadhi ya mambo hayo.

Nimeshangazwa sana na kudai kwako unapigania haki za binadamu na kukwepa kabisa kutaja jinsi viongozi wa Serikali na polisi walivyouawa kinyama kule Kibiti lakini unaonekana kuwatetea unaodai “wananchi” waliochukuliwa hatua na Polisi kule kule Kibiti. Hapa umemchosha tu Rais.

Nimeshangazwa na wewe mpigania haki za binadamu umetajataja matukio unayosema ya watu kutekwa ukasahahu jinsi wafuasi wa chama chako walivyomteka aliyekuwa mlinzi wa chama chako na bosi wako wa zamani Dkt. Slaa, Bw. Khalid Kagenzi na kumsulubu ipasavyo (majina ya wahusika wa Red Brigade ya chama chake unayo), yupo aliyekuwa Mwenyekiti wenu Temeke Joseph Yona hadi leo anaulemavu kwa kazi za utekaji na utesaji wa vijana maalum wa Chama chenu. Haya yote haujamkumbusha Rais.
Umemtaja Ben Saanan kuwa kapotea, huyu unamuuliza Rais badala ya kumwandikia barua mjumbe wa chama chako na Mbunge wenu Saed Kubenea ambaye alipata kuandika gazetini kuwa Ben Saanane yupo huku pia ukishindwa kumhoji bosi wako Mbowe kwa nini mpaka sasa hataji kabisa suala la “kupotea” Saanane wakati alikuwa msaidizi wake muhimu. Naamini katika barua ya pili hautasahau haya.

Katika eneo hili umezungumzia mambo ya watu kuuawa nilidhani ungemkumbushia pia Mhe. Rais kilio cha mpaka leo cha utata wa mazingira ya kifo cha Makamu Mwenyekiti wa Chama chako, Chacha Wangwe ambaye mpaka sasa bosi wako Mbowe hajapata kukanusha kuhusika nacho.

Nilidhani ungemkumbushia Rais kuhusu kumbana Mbowe katika hili. Zitto Kabwe pia amepata kulalamika kunusurika kuuawa kwa njama za Mbowe enzi zile. Haya ungeyakumbushia pia.

Nimeona pia umekumbushia tukio la wewe kupigwa risasi. Pole sana tena. Hata hivyo sasa unatuambia ulipigwa risasi 16 tu, nilidhani ungemwambia Rais amkemee Mwenyekiti wako anayetangaza kila siku kuwa ulipigwa risasi zaidi ya 30.

Lakini naamini katika barua ijayo utamkumbusha Mhe. Rais kwa nini mpaka leo bado umemzuia dereva wako na umemficha, shahidi muhimu katika kesi hii asihojiwe na chombo chochote cha ndani au nje ya nchi.

Nakutakia mapumziko mema huko Ubelgiji lakini nikaona tu nikuache na hili: fanya haraka basi urudi nyumbani kumenoga. Niko London lakini naona kule nyambani hatupotezi muda tena kujadili ya akina Saanane sijui kila siku hoja za kina Mawazo, kwa sasa ni macho mbele kutazama asali ya anga Dreamliner, Standard Gauge, Stiglers, watu washaiona flyover ya kwanza Tanzania, wanaona huduma za afya zilivyoimarishwa n.k.

Pia nikikukumbusha kuwa nyumbani kumenoga na wenzako (akiwemo Mwenyekiti wako juzi tu hapa), mawaziri, viongozi wakuu na wastaafu wameachana sasa na habari za kuwaza vitanda na wodi za ughaibuni, bali wanatibiwa na kupata tiba hapa hapa nchini.
Watu wanaona maendeleo na si malalamiko. Naamini katika barua yako ijayo, kama wewe kweli ni mpigania haki za binadamu zinazojumuisha haki ya maendeleo na haki ya ustawi wa jamii, hautasita kuyatambua maendeleo haya na kumshukuru Rais kutimiza sheria na haki za binadamu zinazohusu ustawi wa jamii na maendeleo kwa kutekeleza miradi yote hii mikubwa.

Wassalaam, wikiendi ijayo nikipata nafasi nitachomoka kuja kukujulia hali wodini.

Nduguyo katika harakati za siasa na haki za binadamu,

*Political Jurist, zamani UDOM sasa London UK.*
 
Kwako Mhe. Tundu Antipass Lissu_
_S.L.P wodini, Ubelgiji_

Zamani nilivyokuwa nasoma nilijua ukiandika sana kwenye masomo ya arts Unapata marks nyingi kumbe nilikuwa najidanganya?

Kwahvyo na wewe unaona Tundu Lissu akiandika barua yake itakuwa ndefu umeamua kuiga.

Sasa umeandika upuuzi wote. Yani nyinyi keyboard warriors mna shika Sana.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hongera kwa kuwa wa kwanza kumjibu Lissu japo wewe sio mlengwa! Hope umechungulia kuna pahala panahitaji uteuzi..... Utakumbukwa kupitia hili kwa kweli....,Nyumbani kumenoga nafikiri yule boss wa mhimili mmoja kati ya tatu atapunguza safari za India sasa matibabu hapa hapa.
 
Umesahau kumkumbusha pia kuwa nae ajifunze kufuata sheria na taratibu ikitokea kaumia tena..maana kuna haki anazidai kutoka bungeni kama vile alifuata sheria na taratibu..
 
Hivi tu kwa Akiri ya kawaida kabisa we ni saizi ya kumjibu Kamanda Lissu.

Hata Mh Raisi Jiwe atashangaa kuona unajitia kumjibia tena kwa Mtazamo wa kipuuzi kama huu.

Ni dhahiri sasa Raisi wetu anahitaji kushauriwa na watu kama kina Lissu na Wengine wenye Uzalendo wa kweli.
Hapa hakuna cha ushabiki wa Chama wala nini Lissu katoa Taswila Halisi ya Utawala wa sasa na kaonyesha mambo gani yarekebishwe kwa muustakabari mwema wa Nchi.

Nasisitiza tena sio lazima Wote Tupost wengine tubaki Wasomaji kuficha Upumbavu Wetu.
 
Hatuwezi kuvumilia upuuzi wako huu, hovyo sana ww bila shaka umetumwa tu. Ile barua ya mh: Lissu kwenda kwa Mtukufu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, imebeba ujumbe wa maana na Muhim sana kwa kutuwakilisha sisi Watanzania tuliowengi vifuani mwetu, na amegusia mengi tu ambayo kwayo tunaona ni kikwazo na kizingiti kikuu, leo hii wewe unakuja na pumba zako!
 
Back
Top Bottom