Uchaguzi 2020 Barua ya Wazi kwa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kuhusu Mwenendo wa Kampeni za Uchaguzi Mkuu (2020) za Mheshimiwa Tundu Lissu

Amani Msumari

JF-Expert Member
Aug 21, 2016
1,830
976
Ndugu mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC),

Ninachukua fursa hii kukupongeza wewe na timu yako kwa kazi ngumu mnayoifanya. Mnafanya kazi zenu kwa weledi na kwa mujibu wa sheria. Hongereni sana.

Kama inavyofahamika, nchi yetu hufanya uchaguzi mkuu wa Rais, wabunge na madiwani kila baada ya Miaka mitano. Hii ni kwa mujibu wa sheria za nchi yetu ambayo ni nchi inayofuata demokrasia ya vyama vingi.

Ndugu mwenyekiti, mwaka huu, 2020 Tanzania itafanya Uchaguzi mkuu wa Rais, wabunge na madiwani. Tayari kampeni za uchaguzi zimeanza kote nchini huku vyama mbalimbali vikizunguka kunadi ilani zao za uchaguzi.

Itakumbukwa kuwa lengo la kampeni hizo Ni kunadi sera za chama husika ili wananchi waweze kufanya maamuzi sahihi siku ya kupiga kura. Kampeni hizi zinatawaliwa na kanuni, sheria na taratibu pamoja na utamaduni wetu Kama watanzania. Hivyo, haitarajiwi kampeni hizi kutumika Kama sehemu ya kuwagawa Watanzania.

Hivi karibuni tumeshuhudia vitendo kadhaa vya uvunjifu wa amani ambavyo mara zote hufanywa na chama kimoja tuu, CHADEMA. Kabla ya kuanza kampeni, tulimsikia Tundu Lissu, mgombea urais wa Tanzania kupitia tiketi ya CHADEMA akiweka wazi kuwa atawaingiza watanzania barabarani Kama hatatangazwa mshindi. Tulishuhudia waandishi wa TBC wakifukuzwa kwenye uzinduzi wa kampeni za CHADEMA pale mbagala kwenye viwanja vya zakhiem.

Tundu Lissu akiwa jijini Mbeya aliendeleza mashambulizi kwa viongozi wa nchi kuwa nchi itawaka Moto usiozimika. Huku akijua kabisa analengo gani, anajenga hoja za kijanja kuwa atadhuriwa na kuwatumbukiza viongozi wa nchi ili wananchi wakose imani na viongozi hao.

Kubwa kuliko ni kauli yake aliyoitoa akiwa Zanzibar akisema Hayati mzee Karume alilazimishwa kusaini makubaliano ya Muungano kinyume na mapenzi yake. Aliunda mbali zaidi kuwaambia ndugu zetu wazanzibar wanachaguliwa viongozi wao na Tanganyika huku akijua fika kuwa vikao hufanyika Dodoma kwasababu ndio makao makuu ya chama cha Mapinduzi.

Kauli hizi anazitoa sio kwa bahati mbaya kwani Mheshimiwa Lissu ni wakili msomi mwenye weledi mkubwa wa masuala ya kisheria. Anafanya hivi kwa makusudi akitumia utaalamu wake wa kisheria kuwashawishi watanzania kuamini uongo ambao unaweza kupelekea uvunjifu wa amani.

Ninaomba nikiwa Kama mtanzania mzalendo ninayeipenda nchi yangu kuwa Mheshimiwa Lissu aonywe na aelekezwe kujikita kwenye kueneza sera za chama chake. Ni muhimu Mheshimiwa Lissu akumbushwe kuwa Kuna maisha baada ya Uchaguzi. Mimi na yeye tunaweza tusiwepo, Ila watanzania ambao ni ndugu, rafiki na watoto wetu wataendelea kuwepo. Hawa wanastahili kesho bora zaidi.

Ni vema Mheshimiwa Lissu akakumbushwa kuwa viongozi wa kisiasa Kama yeye ni watu wenye ushawishi kwa wafuasi wao na kuwa maneno yao yanaweza kuleta Faraja au huzuni, kilio au furaha, upendo au chuki, umoja au utengano zaidi sana kifo au maisha.

UPDATES

Naipongeza tume ya maadili ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi ambayo inaundwa na wajumbe kutoka vyama vinavyoshiriki uchaguzi ikiwemo wajumbe kutoka katika Chama cha Demokrasia na Maendeleo kwa hatua stahiki ilizochukua za kumfungia Mheshimiwa Lissu asifanye kampeni kwa siku Saba.

Ni imani yangu kuwa Mheshimiwa Lissu atajifunza na kuendesha kampeni za kistaarabu.

Nakala:
Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania
Msajili wa Vyama vya Siasa Tanzania
Katibu Mkuu - CHADEMA
Katibu Mkuu - CCM
 
Mgombea wa CCM anapotishia kuwanyima wananchi maendeleo warakapochagua wapinzani unaona ni siasa safi!!

Mgombea wa CCM anapokatisha masomo wanafunzi ili wakasikilize wasichoweza kujibia mitihani unaona sahihi na hukisemi!

Mgombea wa CCM anapohutubia Kisukuma Mwanza, Shinyanga, Simiyu na Geita unaona sawa na husemi!

Wewe ni mwanaCCM unatakiwa kuwaeleza wanaCCM wenzio kwenye platform yenu.
 
Hivi ikitokea Magufuli akapokwa ushindi wake halali, atacheka na Tume?

La msingi Tume ihakikishe kuna uchaguzi huru na wa haki, na mshindi wa kweli na wa haki atangazwe. Yote uliyoandika hapa ni blaa blaa tu.
 
Mgombea wa CCM anapotishia kuwanyima wananchi maendeleo warakapochagua wapinzani unaona ni siasa safi!!
Mgombea wa CCM anapokatisha masomo wanafunzi ili wakasikilize wasichoweza kujibia mitihani unaona sahihi na hukisemi!
Mgombea wa CCM anapohutubia Kisukuma Mwanza, Shinyanga, Simiyu na Geita unaona sawa na husemi!
Wewe ni mwanaCCM unatakiwa kuwaeleza wanaCCM wenzio kwenye platform yenu.
Hajatishia usalama wa taifa letu hata mara moja
 
Kauli hizi anazitoa sio kwa bahati mbaya kwani Mheshimiwa Lissu ni wakili msomi mwenye weledi mkubwa wa masuala ya kisheria. Anafanya hivi kwa makusudi akitumia utaalamu wake wa kisheria kuwashawishi watanzania kuamini uongo ambao unaweza kupelekea uvunjifu wa amani`] Ndugu yangu na wewe unatumia nini kusawishi tume au wasomaji wamuone Lisu anakosea? Kinyume na sifa ulizosema za mkosaji wako!!
 
Hivi ikitokea Magufuli akapokwa ushindi wake halali, atacheka na Tume?

La msingi Tume ihakikishe kuna uchaguzi huru na wa haki, na mshindi wa kweli na wa haki atangazwe. Yote uliyoandika hapa ni blaa blaa tu.
Point hapo ni " Uchaguzi wa huru a haki". Ikitokea umeona hujatendewa haki basi Kuna njia za kisheria za kufuata na sio kumwaga damu ya wananchi
 
[`Kauli hizi anazitoa sio kwa bahati mbaya kwani Mheshimiwa Lissu ni wakili msomi mwenye weledi mkubwa wa masuala ya kisheria. Anafanya hivi kwa makusudi akitumia utaalamu wake wa kisheria kuwashawishi watanzania kuamini uongo ambao unaweza kupelekea uvunjifu wa amani`] Ndugu yangu na wewe unatumia nini kusawishi tume au wasomaji wamuone Lisu anakosea? Kinyume na sifa ulizosema za mkosaji wako!!
Maneno anayotamka yako wazi. Huyu jamaa amejipanga kumwaga damu
 
Lissu anaeleweka kwa wapuuzi tu vibaka waliokosa cha kufanya wanahitaji pesa ya kuja ghafla mfukoni....kama unapiga kazi halali huna neno juu ya magufuri..



Ukweli ni kuwa magufuri anashinda kwa kishindo kikubwa mno ijapokuwa sinaga mambo ya uvyama ila kila maeneo unayopita ushindi uko wazi.alichokosea lissu ni kuwa na siasa za kulalamika kupigwa na hajui nani kampiga.....watanzia wapo wengi wenye matatizo yao awe na siasa za ushawishi siyo za kupaniki ili tuone ana uchungu kumbe ana ajenda yake ya kufinywa kinyeo na wazungu.
 
Back
Top Bottom