Barua ya wazi kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania dhidi ya sakata la watumishi hewa

mtendaji wa kijiji

JF-Expert Member
Jul 3, 2012
533
114
Ndugu Mheshimiwa Raisi wa Jamhuri ya Muungano Wa Tanzania,

Kwanza kabisa napenda kukupongeza kwa jitihada zako za dhati unazozionyesha za nia ya dhati ya kuleta ukombozi wa kiuchumi kwa Wa Tazania wa kipata cha chini. Mimi binafsi sina shaka tena na wewe ingawa hapo kabla ya uchaguzi sikuwahi kuwa Muumini wako yaani kiukweli hata kura sikukupigia lakini ilikuwa ni haki yangu kidemokrasia kumchagua mtu ambaye nilidhani atatua mzigo wa umasikini tulio twishwa na Uongozi wa awamu 2 zilizopita kwa sababu ya Kula Bila kufikiria hatima ya kesho.

Madhumuni Ya Barua Hii nikukujulisha kwamba hakika wewe ndiwe ambaye ulikuwa Chaguo La Mungu Japo wengi hatukuamini. Hata hivyo sasa tumeamini kwani imedhihirika kwamba hata wale waliodhani utawabeba Waendelee kufaidi keki ya taifa wenyewe kwa Ufisadi na udhalimu Sasa wanatamani aidha kuhama katika nchi hii au kufanya Juhudi za kuku Kwamisha. Nakuhakikishia kwamba wanaokuombea mabaya ni wa chache na tunao kuombea Heri tupo wengi bila kujali itakadi zetu

Ndugu Mheshimiwa Raisi Nipende kukupongeza kwa dhati kutoka katika chembe ya moyo wangu kwa kutumbua jipu lililokuwa limeiva sana la Wafanyakazi hewa. Hakika hapo uligusa penyewe na kusababisha wale waliokuwa wanatumia Mirija ya Wafanyakazi walio Fariki, Walio stafu, waliosimamishwa na kuachishwa kazi kwa utoro Kuwaletea fedha za bwerere kila Mwezi kuwa katika Hali ya Kizungumkuti.

Mimi Ni mmoja wa Vijana ambaye kwasasa nipo kijijini nalima Vitunguu kisha na viuza kwa wafanya Biashara wana leta huko mjini walipo Mafisadi japo hata bei ninayo uza yaweza kuwa ya kulanguliwa lakini pia kwa Wasifu wangu nilihitimu shahada yangu ya Kwanza tangu mwaka 2011 na Baada ya kukosa ajira nikaamua kurudi shamba kulima vitunguu ili Wa Tanzania wenzangu wanaotumbuliwa majipu sasa wapate kiungo hicho muhimu sana kwa Mboga

Si Hitaji Kukuchosha sana na Baua yangu hii ya Wazi kwako na si kama ninatamani kupata kazi Serikalini Lakini kwani nimesharidhika na kilimo Nina Maombi Matatu Kwako ambayo Ninaamini wewe kama ulivyo Tumwa Na Mungu kuwahurumia wa Tanzania Unaweza kuyatekeleza.

  • Kwanza Ninaomba Kwa Speed uliyo Ingia Nayo Madarakani uitumie kuhakikisha wale wote ambao walikuwa wana kula fedha za Bure kwa kutumia majina ya wafanyakazi walio Fariki, Kustaafu, Kusimamishwa Kazini na Huenda ambayo hayapo katika dunia hii Uwaadhibu wote na kuhakikisha wanaenda Rumande Kutumikia adhabu ya vifungo

  • Kwasababu Halimashauri zilizokutwa na wafanya kazi hawa hewa zinayo Budget ambayo ilisha tengwa kwaajili ya Mishahara . Nakuomba uwaangalie kwa huruma Vijana walio mtaani waliomaliza elimu zao kwa ngazi tofauti wanaotafuta ajira utoe tamko la kujaza nafasi hizo Mara Moja

  • Kupitia Ofisi ya Sekretariet Ya Ajira Naamini wapo Vijana wengi waliopo katika Kanzi Data (Data Base) Ambao wana sifa za kufanya kazi katika nafasi tofauti zilizo Kuwa Hewa. Nakuomba utoe agizo kwa mamlaka husika zipeleke maombi katika tume Hiyo na Tume Hiy0 ipewe amri ya kutumia kumbukumbu zao Kuajiri wale Vijana wenye sifa walio katika kanzi Data
  • Bado Wafanya kazi hewa wapo wengi sio hao tu walioripotiwa na wakuu wa Mikoa. . Watu wa Hazina wanashirikiana sana na watu wa halimashauri kuendelea kulipa wafanya kazi hewa Tunakuomba uunde tume itakayo fanya kazi kimya kimya ili list iliyo wasilishwa kwako na wakuu wa mikoa iwe reviewed na watakao kuwa wame toa ripoti pungufu wasulubiwe barabara kama Ulivyo msulubu mama Anna Kilango
Mwisho nipende Kukushukuru kwa kutumia muda wako kusoma Barua Hii ya Mwananchi asiye kupigia kura lakini anaye kukubali kwamba umetumwa na Mungu uondoe udhalimu, ufisadi na uzandiki ulio kuwa katika serikali iliyopita kwa kutumbua majipu bila kuangalia uso wa Mwenye Jipu. Aidha Kama uliwahi kusshairi la kama mnataka mali mtaipata Shambani nitumie wasaa huu kukusihi uweke nguvu ya kutoshwa kwenye Kilimo na Viwanda Hatimaye ndoto zako za kuifanya Nchi kukua Kiuchumi zitafikia katika kilele.

Wako
Mkulima Wa Vitunguu
Tafadhali wafanyakazi wa Ikulu mpelekkeni Raisi Barua hii
 
Sijui kama Raisi atapata muda wa kuisoma barua yako maana yuko bize kutumbua majipu pengine kesho atatangaza wakuu wapya wa wilaya lakini ni vizuri aipate kwa wakati ili ayafanyie kazi maombi yako.
 
ukimuona anapita hapo mpe link aisome
Sijui kama Raisi atapata muda wa kuisoma barua yako maana yuko bize kutumbua majipu pengine kesho atatangaza wakuu wapya wa wilaya lakini ni vizuri aipate kwa wakati ili ayafanyie kazi maombi yako.
 
Back
Top Bottom