Barua ya wazi kwa Rais wa dola ya Zanzibar dr. Ali Muhammed Shein | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Barua ya wazi kwa Rais wa dola ya Zanzibar dr. Ali Muhammed Shein

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Kakke, Aug 24, 2012.

 1. Kakke

  Kakke JF-Expert Member

  #1
  Aug 24, 2012
  Joined: Dec 4, 2010
  Messages: 1,797
  Likes Received: 389
  Trophy Points: 180
  [h=1][/h]Written by Stonetown (Kiongozi) // 24/08/2012 // Habari // 3 Comments

  [​IMG]
  BARUA YA WAZI KWA RAIS WA DOLA YA ZANZIBAR DR. ALI MUHAMMED SHEIN
  BISMILLAHI ‘RRAHMANI ‘RRAHIM
  Kila sifa njema zinamstahikia Allah, Subhanah wa Taala, isofichika kwake dhulma wala harudishi dua ya mwenye kudhulumiwa. Rehma na amani zimshukie Mtume Muhmmad (s.a.w) kipenzi chake na cha umma, mtetezi wa waliodhulimiwa hata kabla ya kupewa Utume.
  Mhishimiwa Rais,
  Kwa mapenzi makubwa, baada ya kuisoma kwa utulivu khutuba yako ya siku tukufu ya Iddil Alfitri, nimelazimika kuandika barua hii kufuatana na kauli mbiu ya Mtume Muhammad (s.a.w) inayosema:
  “…Dini ni nasaha…nasaha kwa Allah (S.w.T) na ni nasaha kwa Mtume (s.a.w.) na kwa viongozi wa Waislamu na kwa watu wote…”
  Mh. Rais;
  Ni kweli nchi yeti ya Zanzibar imechafuliwa jina lake kuwa ni nchi ya amani kama ilivyogeuzwa nchi yetu na ndugu zetu na kufanywa kuwa ni koloni lao baada ya mkoloni Mwingereza kutupa uhuru mwaka 1963 na kuwa na kiti chetu Umoja wa Mataifa huku walimwengu wote wakishuhudia; kiti ambacho kwa uwezo wake Allah atakirejesha karibuni na wewe ukiwa rais wa Zanzibar au uliyemwakilisha kuweza kuketi juu yake Insha’allah na sisi wananchi wako wa Zanzibar tukifurahikia jambo hilo adhimu.
  Mh.Rais;
  Ni kweli nchi yetu inatiwa dosari lakini si kweli kuwa wananchi wa Zanzibar ndio wanaosababisha dosari hiyo na doa hilo la uvunjifu wa amani; ushahidi wa maneno haya tutaupata tukirejea na kutizama kwa jicho la uadilifu na insafu katika matukio tafauti. Kwa hakika tukifanya hivyo tutagundua bila ya taabu kuwa Jeshi la Polisi la Tanzania ndio wahusika wakuu na waanzilishi wa vurugu na uvunjifu wa amani ya nchi yetu ya Zanzibar kwa mara zote tatu, nikimaanisha machafuko yaliyotokea tarehe 25-26/5/2012 mjini Zanzibar na yale ya kuhujumu waumini na kunajisi misiskiti tarehe 17/6/2012, Donge, Mahonda na Mkokotoni pamoja na hujuma ya tarehe 20/7/2012 msikitini pia dhidi ya Waislamu walokusanyika msikiti wa Mbuyuni kuwasalia ndugu zao waliofariki kwa ajali ya meli ya Mv. Skaget. Waislamu tulihujumiwa ndani ya msikiti. Jeshi la polisi halikusita hapo bali liliwaingilia wananchi wanyonge mpaka ndani ya nyumba zao na kuwatendea matendo haramiya ya chuki na uhuni na katika waliotendewa matendo hayo maovu walikuwa wanawake na watoto wachanga. Polisi hao wakhalifu wa sharia waharibifu wa amani walifika hadi ya kutupa mabomu ya madawa makali ndani ya majumba ya raia bila ya kujali athari zitakazowasibu watoto wachanga na wanawake wenye kunyonyesha. Iwapo jeshi la polisi lililopewa jukumu la kulinda sharia, kuweka amani na kuwahami wananchi na mali zao ndio wenye kuvunja shariakwa kuwahujumu watu bila ya sababu, wananchi na haki zao zitalindwa na nani?
  Mh.Rais;
  Matokeo ya ukiukwaji wa sharia na haki za binadamu yaliyopelekea kuiharibia nchi yetu ya Zanzibar sifa yake ya amani na utulivu yamesababishwa na jeshi la polisi la Tanzania lililoacha kutekeleza wajibu wake wa kutunza amani ya nchi yetu Zanzibar . La kusikitisha zaidi ni kuwepo baadhi ya watendaji wako wa karibu wanaopotosha ukweli na kuifanyia khiyana nchi yetu ya Zanzibar kwa kufikisha kwako taarifa za uongo zilizopelekea kuitia doa na kuiharibu khutuba yako ilojaa maneno matukufu ya Allah Subhanah wa Taala pamoja na mafunzo kutoka Sunna za Mtume (s.a.w), khutuba ambayo ilitarajiwa kukemea dhulma za jeshi la polisi dhidi ya Waiislam na nyumba tukufu za Allah (S.w.T) iliyohujumiwa pamoja na wanawake na watoto wachanga ndani ya majumba kama ulivotetea makanisa na kubainisha hatari na ubaya wa walioyachoma makanisa hayo kwa lengo la kutaka kuanzisha fitna baina ya Waislam na jirani zao Wakristo waliokaribishwa nchini Zanzibar na kuishi pamoja nao miaka mingi kwa amani kiasi ambacho haijawahi kutokea Muislamu kulitusi kanisa licha kulichoma moto, kwani hayo ni kinyume na mafunzo ya dini yetu tukufu ya Kiislamu.
  Mh.Rais;
  Watu wanaokuwa karibu na Rais ni watu muhimu sana katika kufanikisha dhana ya uadilifu na utawala bora na wa haki usioogopa kukemea maovu hata kama walotenda au kuteleza ni Jeshi la Polisi kwani pia wao ni binaadamu siajabu kutenda makosa kwa maksudi seuze kuteleza, Allah Sbhanah wa Taala anatwambia: “…Enyi mloamini kuweni wasimamizi wa Allah wenye kushuhudia ukweli hata kama ni dhidi ya nafsi zenu…” Kwa hivyo, kosa kubwa zaidi ni kuuficha ukweli au kumpotosha kiongozi wa nchi hadi kufikia kuwashushia sifa wasiostahiki, wahuni ambao waliwatendea ya uhuni na dhulma kubwa hata wanawake na watoto. Ni khatari wadhulumiwa wanapofikishwa kumshtakia Mfalme wa Mbingu na Ardhi juu ya dhulma wanazotendewa. Isitoshe, khiyana ya watu kamaa hao wa karibu na viongozi kila inapojikariri khiyana hiyo inajenga hisiya kwa wenyeji wa nchi hii ambao wengi wao ni Waislamu kuwa wanabaguliwa, na sio wao tu bali hata kudharauliwa nyumba zao tukufu za ibada na kuthaminiwa makanisa peke yake. Sisi Waislamu hatutaki nyumba zozote za ibada zidharauliwe. Nyumba zote za ibada lazima ziwekewe hishima zinazostahiki.
  Mh.Rais;
  Kwa heshma zote naomba zichunguzwe sana sifa mbili kwa watu wote wa karibu na viongozi, sifa mbazo ni hatari kuzikosa tena zinaweza kuiangamiza nchi yetu tukufu ya Zanzibar . Sifa hizo si nyengine illa ni ukweli na uaminifu ambazo ni kinyume na uwongo na khiyana.
  Yarabbi Muumba Mbingu na Ardhi, usieshindwa na jambo, tunakuomba muhifadhi Rais wetu, turejeshee nchi yetu kwa salama na amani, DOLA HURU YA ZANZIBAR, wastiri wanawake na watoto wachanga majumbani na Wazanzibari wote tunaodhulumiwa kwa kudai uhuru wa nchi yetu ya Zanzibar uloporwa na jirani zetu, ndugu zetu baada ya kutoka kwa wakoloni.
  Amir Mkuu, Jumuiya ya Maimamu Zanzibar
  Farid Hadi Ahmed
   
 2. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #2
  Aug 24, 2012
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 303
  Trophy Points: 160
  hongera kwa kiswahili kizuri.
   
 3. bibikuku

  bibikuku JF-Expert Member

  #3
  Aug 24, 2012
  Joined: Feb 16, 2011
  Messages: 828
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  naona mauzauza tu hapa, sijui macho yangu au la
   
 4. TITAN

  TITAN JF-Expert Member

  #4
  Aug 24, 2012
  Joined: Dec 13, 2010
  Messages: 309
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Bado mmegoma kuhesabiwa?
   
 5. Nguruvi3

  Nguruvi3 Platinum Member

  #5
  Aug 24, 2012
  Joined: Jun 21, 2010
  Messages: 12,223
  Likes Received: 7,344
  Trophy Points: 280
  Ningeshauri Kakke uiondoe barua hii ili kumtendea haki Sheikh Farid.
  Binafsi nachelea kuichambua kumsitiri mzee.
  Please!
   
 6. t

  tusichoke JF-Expert Member

  #6
  Aug 24, 2012
  Joined: Apr 2, 2011
  Messages: 1,286
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  kila mtu ana uhuru wa kutoa maoni ,yaheshimiwe
   
 7. Globu

  Globu JF-Expert Member

  #7
  Aug 24, 2012
  Joined: Jan 12, 2011
  Messages: 7,975
  Likes Received: 175
  Trophy Points: 160
  Ulojo= Urojo.
   
 8. J

  JokaKuu Platinum Member

  #8
  Aug 24, 2012
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,781
  Likes Received: 5,021
  Trophy Points: 280
  Kakke,

  ..hii peleka mzalendo.net.

  ..hivi kwanini mnatubagua wa-Tanganyika ktk mitandao yenu?
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 9. m

  mkigoma JF-Expert Member

  #9
  Aug 24, 2012
  Joined: Jul 26, 2011
  Messages: 1,182
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  msikate tamaa si mbali mtapata taifa lenu la zanzibar. nasi tutaendelea kupambana na makafiri huku bara japo mavichwa yao ni magumu kama mawe lakini inshaallah wataelewa tu.
   
 10. F

  Funge JF-Expert Member

  #10
  Aug 24, 2012
  Joined: Jun 10, 2011
  Messages: 585
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  Makafiri nao wanafahamu kwamba kupambana na Umma wa Jini Kiongozi si kazi ndogo. Bila shaka watatumia elimu dunia zaidi. Maana kwa wengi wa nduguze kibwengo na jini maimuna elimu dunia ni haba
   
 11. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #11
  Aug 24, 2012
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  kwanini usimwandikie awaongoze mtoke kwenye Muungano ili pate 'dola" yenu iliyoporwa na ndugu zenu? Andamaneni kwenda Ikulu ya Zanzibar kumtaka Shein ajiondoe CCM na kuwaongoza kwenye uhuru ili muwe nyuma yake. Mbona ni rahisi hivyo!
   
 12. Bishop Hiluka

  Bishop Hiluka Verified User

  #12
  Aug 24, 2012
  Joined: Aug 12, 2011
  Messages: 4,101
  Likes Received: 1,425
  Trophy Points: 280
  Duh, kweli debe tupu haliachi kupiga kelele...
   
 13. idawa

  idawa JF-Expert Member

  #13
  Aug 24, 2012
  Joined: Jan 20, 2012
  Messages: 18,539
  Likes Received: 10,460
  Trophy Points: 280
  mkuu kongosho masihara hayo.!
   
 14. idawa

  idawa JF-Expert Member

  #14
  Aug 24, 2012
  Joined: Jan 20, 2012
  Messages: 18,539
  Likes Received: 10,460
  Trophy Points: 280
  Mfti kasema kama hutashiriki sensa basi wewe kafiri. Je wewe upo tayari kuitwa kafiri.?
   
 15. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #15
  Aug 24, 2012
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,874
  Likes Received: 6,227
  Trophy Points: 280
  mna mambo nyie.....
   
 16. b

  bagamoyo JF-Expert Member

  #16
  Aug 25, 2012
  Joined: Jan 14, 2010
  Messages: 4,530
  Likes Received: 2,113
  Trophy Points: 280
  MOD au hata wewe mdau 'Kakke' wa Stone Town fanya uhariri kwa kutuwekea japo paragraphs na 'spaces' tuweze kusoma hoja zako bila taaaabu!
   
 17. Mkimbizi

  Mkimbizi JF-Expert Member

  #17
  Aug 25, 2012
  Joined: Aug 23, 2008
  Messages: 222
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Sisi mnaotuita makafiri tuende wapi sasa? Mkishapambana na kututoa makafiri mtaanza kuangaliana Sunni au Shia, then pua ndefu au pana, nywele fupi au za kusokota, mchagga au msukuma.

  Nashindwa kuelewa kwanini Zanzibar isikubaliwe ijitenge maana wananikera sana na maneno ya kibaguzi.

  Tokeni
   
Loading...