Barua ya wazi kwa Rais Samia Suluhu Hassan

Hae Mosu

Member
Dec 23, 2019
36
25
Awali ya yote nipende kukusalimu kwa salamu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (yaani 'kazi iendelee')

Nikupe pole kwa kazi nzito ya kuongoza hili taifa letu na pia nakupa hongera ya kufikia nafasi hiyo ya cheo cha juu kabisa kisiasa.

DHUMUNI LA BARUA HII.

Mimi kitaaluma ni mwalimu na ninakuandikia barua hii ya wazi nikiwa na dukuduku moyoni na nikaona ni vema na haki kukuandikia hapa kwani ninaamini una wasaidizi wake wengi ambao wako humu na watakufikishia:

SUALA LA AJIRA ZA UALIMU.

Mh.Rais, Kiukweli suala hili ni pasua kichwa na linaumiza sana. Mnamo Jumapili ya tarehe 9/5/2021, Waziri wa TAMISEMI, Bi. Ummy Mwalimu alitangaza ajira za ualimu na afya. Ajira za ualimu, zilizotangazwa, zipi , 6949 ambazo alisema zinapaswa kuombwa na walimu waliohitimu kati ya 2012 na 2019.

Sasa hapo ndipo ninapata wasiwasi na ninaumia sana kwa sababu SERIKALI IMESHINDWA KUWA NA MPANGILIO KATIKA KUAJIRI yaani leo imefikia hatua kijana anayeachwa shuleni kidato cha kwanza na mtu anayehitimu kidato cha sita anatangulia kupata ajira ya ualimu mapema tena kwa masomo sawasawa.Mfano, mhitimu wa 2019 anapata ajira serikalini mapema zaidi ya mhitimu wa 2012
Binafsi hii si sawa na nakuomba mama uliangalie suala hili kwa kina na serikali izingatie 'seniority' katika kuajiri kwa ni wengi wanazeekea nyumbani bila kazi na wanakuwa mizigo kwa ndugu zao.

SUALA LA KUJITOLEA ILI KUAJIRIWA SERIKALINI

Mh. Rais, Kiukweli, hili suala limepelekea uwepo wa rushwa sana kwani ni vigumu sana kwa mtu kujitolea bure katika taasisi ilihali naye ana mahitaji yake. Mwalimu ana mahitaji ya muhimu kama malazi, makazi na chakula. Je, ni wangapi wanapata mahitaji yao hayo bila kufanya kazi ya kuingiza kipato? Hivyo, hili suala nalo uliangalie kwani, hata bungeni, limezungumziwa na waziri na naibu wake kama kigezo cha kuajiriwa serikalini.

MWISHO
Mh. Rais, Mtaani ni kugumu sana na kulingana na namna sera ya elimu ilivyobadilika, hasa 2018, imepelekea shule nyingi za binafsi kudorora na nyingi zitakuwa hazipo kufikia mwaka 2025.

Mh. Rais, Kwa uzoefu wangu huko vijijini kama Uyui, misungwi, misenyi, karagwe, sengerema, kwimba, rorya na buchosa bado kuna uhitaji mkubwa wa walimu. Hivyo, nakuomba utuajiri walimu wengi ili tuweze kuwapa elimu bora watoto wa wanyonge kwani ajira hizi 6949 hazitoshi kukidhi mahitaji katika shule zetu hasa huko vijijini.

Nikutakie kazi njema na Mola akulinde na azidi kukupa hekima na busara katika kila jambo utendalo. Asante

Wako
Mwalimu
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom