Barua ya wazi kwa Rais Samia Suluhu Hassan kuhusu hali ya haki jinai nchini

Tito Magoti, Pole sana kwa yaliyokupata Ila huwezi jua kwanini Mungu akaacha ukapata majanga haha.

Kwa akili yangu, Mungu alitaka uende ukaone jinsi raia wanavyoteseka na mfumo mbovu wa Sheria na haki nchini. Wewe ndiyo sauti yao.

Hata Kama Rais SSH hataliona hili, Mimi ninaliona ni zaidi ya Thesis ya Masters/ PhD.

Nakushauri ulisimamie kwa kutafuta wahisani watakao ku-support uwasemee wasio na sauti kupitia Asasi za Kiraia.

Mungu akubariki sana
Hata sisi tuliolisikia je hatunajambo lolote lakufanya hatakwakiga kelele pia tutashindwa kwani sauti yawengi ipo pamoja na mingu Sasa niwakati wakuamka watanzania unajua kwanini mungu alimchukua mwendazake mungu alisikia sauti zawatanzani bado watanzania hawanapesa lakini wanafura unafikili nikwanini?
 
Kweli tupu, Mwendazake alikuwa nuksi kila mahali. Sala za waliodhulumiwa wakiomba kwa Mungu kwa pamoja, Mungu amesikia na AKAMUONDOSHA, Shetani mbaya sana yule
 
Tito Magoti, Pole sana kwa yaliyokupata Ila huwezi jua kwanini Mungu akaacha ukapata majanga haha.

Kwa akili yangu, Mungu alitaka uende ukaone jinsi raia wanavyoteseka na mfumo mbovu wa Sheria na haki nchini. Wewe ndiyo sauti yao.

Hata Kama Rais SSH hataliona hili, Mimi ninaliona ni zaidi ya Thesis ya Masters/ PhD.

Nakushauri ulisimamie kwa kutafuta wahisani watakao ku-support uwasemee wasio na sauti kupitia Asasi za Kiraia.

Mungu akubariki sana
Stuxnet: Asante kwa maoni na ushauri wako.
 
Hata sisi tuliolisikia je hatunajambo lolote lakufanya hatakwakiga kelele pia tutashindwa kwani sauti yawengi ipo pamoja na mingu Sasa niwakati wakuamka watanzania unajua kwanini mungu alimchukua mwendazake mungu alisikia sauti zawatanzani bado watanzania hawanapesa lakini wanafura unafikili nikwanini?
Nakubaliana na wewe MO. Tujumuishe nguvu zetu kuna kitu tunaweza kufanya kwaajili yetu na Taifa letu.
 
Hili andiko limenitoa machozi. Nimelia kama mtoto mdogo. Ukatili gani huu!, imenikumbusha miaka fulani huko nyuma niliwahi kuwekwa mahabusu. Kilikuwa chumba kidogo chenye joto kali sana. Baada ya saa kadhaa nilihisi kiu ya maji, wale jamaa walikataa kabisa kunipa maji ya kunywa. Hali ilikuwa mbaya sana, nilihisi naweza kuzimia. Niliamua kupiga kelele kwa nguvu. Jamaa mmoja ambaye alikuwa na chembe za ubinadamu akawaambia wenzake " tumpeni maji ya kunywa huyu ni binadamu", basi nikaletewa maji kwenye kopo fulani hivi ,nadhani lilikuwa kopo la chooni. Nilikunywa yale maji bila kujali.

Pole sana ,Tito Magoti , Mungu wetu ni mkuu sana atafanya jambo.
 
Asante, na pole kwetu sote, ndugu yangu! Kuna mambo yakizungumzwa kama yalivyo tutakataana na kutafutana. Lakini itoshe kusema kwamba Taifa hili ni letu sote, tushiriki kulifanya kuwa sehemu salama kwa kila mmoja wetu. Hatuna sababu ya kuacha kuishi kwa furaha wakati tukijua shida iko wapi. Tujisahihishe.
 
Mateso katika vituo vya polisi
Mheshimiwa Rais, watu wa Mungu wameteswa sana. Mateso yasiyomithilika. Sio lazima ikutokee ndio ukubaliane na mimi kwamba watu wanateswa. Mshirika wangu Mdude Nyagali, ambaye sasa analipa gharama ya kuikosoa Serikali yake, aliwahi kutoa ushuhuda wa mateso aliyopata akiwa mateka kizuizini mikononi mwa dola la awamu ya tano. Licha ya kwamba Mdude awalitaja watu na taasisi zilizoshiriki kumtesa, hakuna aliyechukuliwa hatua hadi sasa. Mateso yapo ni wakati mwafaka wa kujisahihisha.
yaani umeandika andiko refu zuri lakini ulipofika hapa umejivua nguo mwenyewe hivi unaweza kuwa na ushirka na mdude nyagali wewe? kijana asiyesikia la mkuu ? huyu alionywatoka kitambo sana akakaidi hivi matusi aliyokuwa anatukana ulikuwa unayasoma?kwahiyo na wewe ulikuwa unaita huo ni ukosoaji? muwe mnatumia akili mdude acheni asote kwanza kidogo hata hivyo hajasota huyo alitakiwa apelekwe stakishari akanyooshwe vizuri ili akitoka amuheshimu mkubwa na mdogo unaooandika mambo mazuri usiingize na ujinga wanaofanya wenzio
 
Ndugu yangu. You don't have to be bitter on this. Mdude ni mshirika wangu. Ni ndugu yangu. Kwa taafifa: hakuna mamlaka yoyote iliyomtamka komredi Mdude kuwa mhalifu hadi nukta hii. Na hata akitamkwa kuwa mhalifu, haimuondolei ubinadamu wake. Na siwezi kumkana kwaajili hiyo. Ukimnyooshea kidole mwenzako, kuwa na hakika kwamba kipo kidole kinakuelekea wewe. Mimi sikutambui pungufu ya matusi na muono wako wa masuala!
 
yaani umeandika andiko refu zuri lakini ulipofika hapa umejivua nguo mwenyewe hivi unaweza kuwa na ushirka na mdude nyagali wewe? kijana asiyesikia la mkuu ? huyu alionywatoka kitambo sana akakaidi hivi matusi aliyokuwa anatukana ulikuwa unayasoma?kwahiyo na wewe ulikuwa unaita huo ni ukosoaji? muwe mnatumia akili mdude acheni asote kwanza kidogo hata hivyo hajasota huyo alitakiwa apelekwe stakishari akanyooshwe vizuri ili akitoka amuheshimu mkubwa na mdogo unaooandika mambo mazuri usiingize na ujinga wanaofanya wenzio
Hata muuaji ana haki ndugu yangu. Inamaana Tanzania mtu kusema ukweli ni matusi?
Ila Mungu hanywi maji, Mdude yuko magereza, yeye yuko kwenye tumbo la ardhi. Kuna la kujifunza hapa.
 
yaani umeandika andiko refu zuri lakini ulipofika hapa umejivua nguo mwenyewe hivi unaweza kuwa na ushirka na mdude nyagali wewe? kijana asiyesikia la mkuu ? huyu alionywatoka kitambo sana akakaidi hivi matusi aliyokuwa anatukana ulikuwa unayasoma?kwahiyo na wewe ulikuwa unaita huo ni ukosoaji? muwe mnatumia akili mdude acheni asote kwanza kidogo hata hivyo hajasota huyo alitakiwa apelekwe stakishari akanyooshwe vizuri ili akitoka amuheshimu mkubwa na mdogo unaooandika mambo mazuri usiingize na ujinga wanaofanya wenzio
Ukisikia kuwa Tanzania Ina wapumbavu wengi ujue tunaponzwa na maboya kama haya akina Iboya2021.

Unasema kabisa kuwa Mdude alikuwa anamtukana Rais Magufuli, sawa tuseme kweli kamtukana.

Sasa nikuulize swali; Kwa nini asikamatwe kwa taratibu za Polisi na kufunguliwa mashtaka ya kutukana kadri ya mwenendo wa makaosa ya jinai?

Pili kwa nini walimteka na kumfungulia mashtaka ya kusafirisha dawa za kulevya?

Hata usiponijibu, nakuhakikishia kuwa Mdude atatoka lakini Magufuli ataendelea kuliwa na minyoo na sisimizi huko alikofukiwa
 
Mengi ya hayo anayoelezea Tito aliyashuhudia chini ya utawala wa shujaa wako!
Hili andiko ni bora sana.

Yanahitajika mageuzi makubwa mno. Ikibidi kiwepo chombo huru cha kufatilia haki za mahabusu.

Bora zitungwe sheria kali kwa wataobainika kuvunja hayo wasiyopenda lakini si kuumiza watu.

Pole sana Tito
 
Hizo blah blah za watu wasomi na sijui wacha Mungu zinachosha. Kinachotakiwa sasa ni wananchi wajipatie wenyewe katiba mpya bila hisani au huruma za mtu.
Kwa bahati nzuri Mr. Tito nchi yetu tuna bahati kwamba Waziri wa Sheria, Jaji Mkuu, Katibu Mkuu wizara ya sheria na Mwanasheria Mkuu wa serikali wote ni wasomi wa kiwango cha Professor wa chuo kikuu! Wote pia ni wacha mungu na wazalendo.

Ni matumaini yetu kwamba kwa kushirikiana na bunge waheshimiwa hawa wanalo jukumu na uwezo wa ku reform our nation's justice system na hivyo kumsaidia Rais Samia.

Hata hivyo ni vigumu kuamini tukizingatia mwaka jana nchi yetu ilijitoa ktk mahakama ya afrika ya haki za binadamu! Makao makuu yake Ausha. Can you imagine?
 
Twitter ina audience kubwa zaidi kuliko JF
Nje ya mada, Tito umejiunga hapa JF mwaka 2014 lakini una post chini ya 10! Naona umeona wapi unaweza weka gazeti lako ukaona ni hapa JF, kisha unaenda kushinda Twitter.

Huu mchezo anao Zitto, naye huleta post zake ndefu kisha anakuwa kama karushia mbwa, halafu anaenda zake kushinda Twitter bila kujibu lolote kwenye bandiko lake.

Tito jirekebishe kwa hilo.
 
Tito umepitia madhira ya kesi isiyo na dhamana ili kama mwanasheria uone mapungufu ya sheria na uyaainishe na kusaidia umma na watawala wanaotamani haki.

Vv
 
Hivi ni nini kinazuia kufanaya reforms kwenye sheria kandamizi hasa zinazohusu makosa ya jinai? Jaji Mkuu analalamika, Serikali inalalamika na hata wabunge ambao ndio watungaji wa hizo sheria nao pia wanalalamika, kwamba mrundikano wa mahabusu umesababishwa kwa kiasi kikubwa na uwepo wa sheria za kuzuia dhamana kwenye kesi nyingi. Kwanini hatua hazichukuliwi? Kwanini DPP anapewa mamlaka makubwa kushinda ya mahakama wakati yeye ni upande katika kesi? Au kwa nchi yetu msimamo wa sheria zetu ni kwamba mshitakiwa anakua na hatia mpaka pale mahakama itakapoamua vinginevyo?

Enzi za Mwalimu Nyerere(ukiondoa kipindi kile cha uonevu wa Sokoine na kesi zake za uhujumu uchumi) watuhumiwa waliokua wanakaa mahabusu hadi miaka miwili ni wale wa kesi za mauaji ya kukusudia na wale waliowekwa kizuizini(detention).

Pia kulikua hakuna utaratibu wa vifungo virefu kupitiliza. Kifungo cha maisha na kile cha juu cha miaka saba ilikua ni kwa makosa makubwa na hatari kama ujamabazi wa kutumia silaha au uhaini. Hii ililenga kuwawezesha waliokua wakitumikia adhabu baada ya kutiwa hatiani kwa baadhi ya makosa kujutia na hatimaye kujirekebisha na kuja kua raia wema

Siku hizi kwa mfano mirungi nayo amabyo hadi miaka ya 2005 ilikua ni halali kwa matumizi hapa nchini eti imewekwa kwenye kundi la dawa za kulevya na kibaya na cha ajabu zaidi ukikutwa unasafirisha kilo hamsini na ukashtakiwa nakupatikana na hatia hiyo adhabu yake ni kifungo cha maisha jela!!! Seriously! Ukimfunga jela maisha msafirisha kiroba kimoja cha mirungi umesaidia nini katika taifa na huyo "mhalifu"? Huo ni ukichaa kabisa

Kesi zote zikiwa na dhamana waendesha mashtaka wataacha kupeleka kesi ambazo wanajua hazina kichwa wala miguu na hivyo watu wengi watatoka magerezani na kuendelea na ujenzi wa Taifa huku wakiendelea kufuatilia kesi zao wakiwa nje
 
Mheshimiwa Rais, tunaweza kuboresha; zoezi lifanyike kwa uwazi na bila shuruti – angalau chini ya usimamizi wa taasisi huru kama Mahakama. Makubaliano yanayofanyika nje ya Mahakama na kusajiliwa Mahakamani upo uwezekano kuwa hayamaanishi kauli moja! Tujikosoe!
Well said.
 
Back
Top Bottom