Barua ya wazi kwa Rais: Mhesimiwa, Mungu ametusikia sasa na wewe tusikie

Hata kumuomba Mungu pia ni njia sahihi sana ya kujikinga na maradhi mbalimbali ikiwemo korona.

lkn pia Serikali haijapuuzia au kudharau ugonjwa wa Korona kama mtoa mada anavyo taka tuamini.

serikali kupitia wizara ya Afya mara kadhaa imetoa elimu ya kujikinga kama ifuatavyo;

Wizara imehimiza;

1. matumizi ya dawa zetu za asili, amabazo zimethibitishwa na TBS na kwa sasa zimesambazwa ktk maduka ya madawa nchi zima, dawa hizo mahsusi kwa matatizo ya upumuaji.
lkn pia kuna kupiga nyungu, kunawa mikono, kuto kushikana mikono au kukariana, kutumia vitakasa mikono n.k

2. hakuna mahali serikali imepiga marufuku uvaaji wa barakoa.
Nakumbuka ktk awamu ya kwanza ya korona Rais alihimiza kuwa ni bora kila mtu akajitengenezea barakoa yake mwenyewe kuliko kununua zile zinazotengenezwa nje ya nchi.

3. sio kwamba serikali inashindwa kuagiza/kuingiza chanjo kutoka nchi zingine lkn Rais wetu kwa nia njema ya kuwalinda watanzania alisema hapana....ni bora wataaalamu wetu wachakarike wakishirikiana na wabobezi tutengeneze chanjo yetu hapahapa, haswa kwa kuzingatia kuwa inaonyesha korona sio ugonjwa kama yalivyo magonjwa ya mlipuko.....korona ni ugonjwa amabao inaonekana tunaweza kusogea nao muda mrefu kama ilivyo malaria, ukimwi n.k

dhamira ya Rais mara zote amelenga kutulinda na aina yoyote ile ya kupata madhara either yawe ya direct or indirect, yawe tumeyaona kwa macho na akili zetu au ambayo sisi hatujayabaini, Mara zote Rais ametulinda sana tena sana. naaamini watanzania wote tuko salama sana chini ya Rais wetu Magufuli.

kwa mtizamo wangu hata ktk awamu ya kwanza ya korona naweza kusema tuliharakisha kuchukua hatua ya lockdown, maaana haikuwa njia sahihi na hilo lilithibitishwa pia na baadhi ya nchi ambazo zilifanya lokcdown ya muda mrefu, badae waliona wamekosea sana.
namuunga mkono Rais Magufuli kwa msimamo wa kuto kutoa amri ya lokcdown.
pia namuunga Rais kwa msimamo wa kutokubali kuletewa chanjo za nje.
tuendelee kujikinga na kutumia dawa zetu za asili lkn bila kusahau kumuomba Mungu kwani bila Mungu hakuna kitakacho wezekana.
Tufunge na tumuombe Mungu hakika sisi kama watanzania tutaushinda ugonjwa huu wa korona.
 
Rais Wa Jamhuri Ya Muungano Wa Tanzania
Ameshausoma Huu Ujumbe, Sasa Hivi
Chukua Tahadhali
 
Walioweka lokidowni wote wamezifungua na bado tatizo lipo,mnapomsikiliza Raisi mengine naona yanawapita na mnachagua yale mliyotulia nayo,

Mnataka Raisi afanye au aseme kitu gani ? Akili zenu zipo wapi ? afunge mashule ? Afunge safari za kuingia na kutoka mkoa kwa mkoa,wilaya kwa wilaya kijiji kwa kijiji mtaa kwa mtaa ??

Kuna shemu mmekosea mliambiwa habari ya nyungu mmeachana nayo,mbona wimbi la mwanzo wanancho nyote mlikuwa mnapiga nyungu,mlipozoea na kuona mafanikio mkawacha,sasa Rais akisema yeye kila siku anapiga nyungu mtasemaje ? Na tunamuona anachanganyika na watu kila aina.
Nyungu ni zoezi endelevu.

Wewe unawaza lockdown tu! Soma umuelewe jamaa. Anachotqka serikali ikubali kabisa kuwa ugonjwa huu upo na unaua watu ili watu wachukue tahadhari, siyo kutuambia eti changamoto ya upumuaji mara phneumonia, watu wanaona kawaida tu na ndipo maambukizi yanapozidi.
 
Mtoa mada kaeleza vizuri tu na objectively siju kwanini wengine wanampinga.
Uongozi ni kwa mfano na kutumia busara. Hekima pia ni muhimu.
Hapa kuna tatizo lakini watetezi hawakubali na tatizo lizidi.
Mtu unakuja na jibu rahisi la NYUNGU
Dunia inajitahidi. Tafiti zinafanywa hatua zimechukuliwa lakini katika vita hii ya pamoja tunabeza tunatuhumu hizo jitihada. Hata chanjo tunabeza bila hata ya facts za kisayansi.
Ni ajabu sana.
Vita dhidi ya korona ni kati ya Dunia na virusi vya covid. Iweje tunanyosheana vidole?
Mbona hata India wametengeneza chanjo? Sisi jukimu letu lipi pamoja na kusali na kupiga nyungu?
 
Back
Top Bottom