Barua ya wazi kwa Rais Magufuli tupe akina "DAU" wengi

AbasMzeEgyptian

JF-Expert Member
Jul 20, 2011
407
312


Mheshimiwa Rais, kwanza nakuamkia shikamoo na hongera sana kwa kuliongoza na kulisimamia ipasavyo taifa letu hili pendwa la Tanzania, sisi wananchi wako wa huku Liwale hasa kata hii ya Mpiga miti tunafarijika sana na mwenendo mzuri wa serikali hii ya awamu ya tano unayoisimamia.


Mheshimiwa Rais, kwa kuwa upo serikalini muda mrefu utakuwa unafahamu vema kuhusu tukio la mwaka jana hapa wilayani kwetu LIWALE, la vurugu kuhusu STAKABADHI GHALANI, kwa kweli huu mfumo ni JIPU na linahitaji kutumbuliwa iwapo kweli unahitaji kuiendeleza nchi hii ambapo sisi wakulima ndio wengi kuliko sekta ingine hapa Tanzania. Sitaki kwenda ndani zaidi kuhusu jipu hili kwani nahofia unaweza ukalitumbua kwa haraka kisha jipu hili likaota tena.


Mheshimiwa Rais; Sisi wakulima ndio watu ambao ni masikini wa kutupwa, japo kuwa ndio sekta yenye wataalamu wengi kuliko sekta yeyote, lipo tatizo ambalo wengi wa viongozi wetu hawalioni, na ndio maana badala ya kutuletea mbegu bora wanatuletea mbolea, balada ya masoko yatakayo nufaisha mkulima mmoja mmoja wanatuletea Stakabadhi ghalani, Tatizo hilo ni kwamba hatuna Viongozi bora, Viongozi wenye kuthubuti, wenye kujituma na wenye mapenzi thabiti ya kuendeleza taifa letu pendwa, viongozi kama Dokta Ramadhani Dau.


Mheshimiwa Rais; Wiki ya jana ulifungua Daraja la kigamoni nimefarijika sana japo nimelioma kwenye video na picha tu, Daraja ambalo ulitueleza kuwa wazo lilianza toka enzi ya mkoloni lakini wazo lilishindikana, ikafika mahali ukapongeza na kusifia jitihada za shirika la NSSF, Bodi yake na hasa ukampongeza Dokta Dau,kwa juhudi zake za kiuongozi katika kufanikisha kwa ujenzi wa daraja hilo.


Mheshimiwa Rais; Daraja limewashinda watu wengi, lakini kuja kwa aliyekuwa mkurugenzi wa NSSF kwako, Daraja liliwezekana, wewe mwenyewe kwa kushirikiana na Dokta Dau, mmejaribu, mkajenga na mmeweza, kwa nini usitutafutie viongozi kama Dau katika sekta yetu hii ya Kilimo? Akina Dau hao walete mapinduzi ya pili ya kijani, watuunganishe na Masoko, Akina Dau watakao simamia vema rasilimali za Taifa hili.


Mheshimiwa Rais; ntakwambia tatizo kubwa linaloikumba nchi yetu, ni kutokuwa na aina ya viongozi kama yako, viongozi kama Dokta Ramadhani Dau, viongozi wenye uwezo wa kusimamia majambo na yakatekelezeka, ni viongozi wawili tu ambao mnastahili pongezi kubwa, wa kwanza ni wewe mwenyewe ulisimamia barabara na zikajengwa na wa pili ni Dau kasimamia Daraja lililomshinda mkoloni na likajengwa, tena kwa pesa zetu za ndani, Hakika watu kama Dau wanastahili kupongezwa, na tunahitaji akina Dau katika sekta ya Kilimo.


Mheshimiwa Rais; Tunakuomba tuletee Dau huku kwenye Korosho, tuletee Dau kwenye Katani, Tuletee viongozi kama Dau kwenye Ufuta na Pamba, tuletee Dau alete mapinduzi ya Kilimo Tanzania.

Mwisho nasema hayo ni mawazo yangu tu yananisumbua kwa muda mrefu sana nimeona kwa kuwa wewe umekuja kwa kauli mbiu ya hapa kazi tu pengine unaweza ukafanyia kazi kwa kutuletea viongozi kama Dau tukasonga mbele.

Nakuombea kwa Mungu akupe hekima na busara katika kutekeleza majukumu Mazito ya kuingoza Tanzania.

Wako katika ujenzi wa Taifa.

Hassan Mchunga
S.L.P 40
Mpiga Miti
Liwale-Lindi
 
Naona hamchoki kumpamba na kumsafisha!! Badilisheni nyimbo jamani hii ishachuja.
 
Naona hamchoki kumpamba na kumsafisha!! Badilisheni nyimbo jamani hii ishachuja.

Imechuja lakini kila kukicha huchoki kuisikiliza, ukiona thread inayomhusu Dau lazima ulete kipwiyo chako, si usome thread zisizo chuja hii waachie waliotayari kusoma vilivyochuja!
 
Imechuja lakini kila kukicha huchoki kuisikiliza, ukiona thread inayomhusu Dau lazima ulete kipwiyo chako, si usome thread zisizo chuja hii waachie waliotayari kusoma vilivyochuja!
Asante ndugu, lakini ni vema ingetumika busara kumwacha Dr. Dau apumzike maana kumuanzishia thread na mijadala kila uchao si vizuri kwa mtu wa caliber yake unless awe anawatuma.
 
Mtoa mada usiwalaghai watanzania! Daraja la Kigamboni ndio la kujigamba hivi eti Dau ndio kiongozi wa kuigwa. You must be joking
 
Dau, Dau, Dau!
JPM ameweka wazi kuwa wazo la kujenga daraja lilikuwepo tangu zamani na kuna majaribio kadhaa ya utekelezaji yalifanyika lakini yakashindikana kwa sababu ya ukosefu wa hela. Safari hii NSSF (sio Dau) wakaingia kwenye biashara hiyo ya kutoa fedha za ujenzi huku wakitazamia kuzirudisha kwa makusanyo ya toll road. Sasa sijui kama chanzo kingekuwa ni mkopo benki ya dunia sijui kama tungemshukuru Mkurugenzi mkuu wa WB kwa staili hii ya Dau. Ngoja PCCB wamalize uchunguzi
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom