Barua ya wazi kwa Rais Kikwete na wana-CCM wote

Membensamba

Senior Member
Nov 4, 2010
157
10
Yapo mambo ambayo mtu kufaulu kuyafanya kunahitaji sana kusoma hali ya hewa. Mifano ni kama kilimo, kuruka kwa ndege, na kuabiri baharini kwa boat. Haya na mengine mengi mtu ukiyaendea bila kwanza kusoma hali ya hewa unaweza hata kupoteza maisha. Hali kadhalika kutokusoma hali ya hewa kisiasa kunaweza kumuua mtu kisiasa, au kuleta madhara na machafuko makubwa. Umefika wakati kwako kiongozi wa nchi, na wanaccm wenzako kusoma hali ya hewa ya kisiasa Tanzania ili kufanya maamuzi mazito muhimu kwa faida ya mustakabali wa nchii hii.

Nchi yetu kisiasa naweza kusema iko njia panda sasa. Ni lazima kifanyike kitu la sivyo madhara yanaweza kuwa mabaya sana baadaye. Huko nyuma kuliweza kufanyika mizengwe mingi kisiasa na wananchi wasielewe wala wasijali. Mwamko ulikuwa mdogo sana wa watu kisiasa. Walio wengi walikuwa hawafikiri mambo critically. Sasa ni tofauti, hasa mijini ambako watu wengi wanapata information mbalimbali. Sasa, tofauti na jana, watu wameanza kuelewa kuwa nchi ni yao, siyo ya viongozi, wameelewa kuwa viongozi ni watumishi wao na siyo mabwana wao, wameelewa na wanazidi kuelewa kwa kasi sana kuwa rasilimali za nchi hii wamepewa wao na Mwenyezi Mungu na sio wageni. Wako tayari sasa kuliko wakati mwingine wowote kupigania haki zao, na wanazidi kujifunza hili kwa kasi kubwa.

Hii ndiyo sababu ccm mmepoteza majimbo mengi mijini kuliko vijijini. Ndiyo sababu vijana wamekuja juu wakiwa na sura mpya kabisa kisiasa utadhani sio wale watz tuliowazoea. Message hapa ni kwamba nchi inabadilika kwa haraka. Tz ya leo siyo ile ya "zidumu fikra za mwenyekiti." Mabadiliko haya hawezi kuzuiwa, ni mkondo wa kiulimwengu, ni byproduct ya globalisation. Kuyazuia utaumia tu mwenyewe.

Ushauri wangu kwako mheshimiwa rais na ccm wenzako ni huu: Kubalini kufanya marekebisho ya katiba, yatakayoruhusu mfumo wa vyama vingi kufanya kazi kweli kweli. Najua hata wewe na wenzako mnajua fika kuwa katiba inapokataza kuhoji au kuchunguza matokeo ya uchaguzi kwa raisi inatoa mwanya mkubwa sana wa tume kuwa na kura turufu kwa upande wa raisi, na huu ni udikteta usiovumilika katika dunia ya leo. Kitendo cha ccm kukubali katiba mpya kitakijengea heshima miongoni mwa watanzania na dunia. Lakini mking'ang'ania kubaki na katiba hii mnaionesha dunia kuwa wenyewe ni madikteta na mna uhafidhina usiokubalika katika kizazi kipya. Nini matokeo yake, bila shaka ni fujo, machafuko ya kisiasa siku za usoni. Ni muhimu kufahamu kuwa mwanadamu akinyimwa haki yake kwa kitambo cha kuzidi uvumilivu wa kibinadamu hatimaye hugeuka mnyama. Sisi sio bora kuliko wale waliouana huko Kenya.

Naomba mhe, na ccm kwa ujumla, msipuuze dalili hizi mnazoziona leo. Hata wabunge wa chadema kutoka bungeni mbele yako siyo neno dogo. Usione ni uadui kwako binafsi, ona ni changamoto ya kufanyia kazi. Nenda mbele zaidi ya hapo. Kumbuka watz waliopiga kura ni wachache sana. Yawezekana kabisa wengine wamekata tamaa kupiga kura kwa kule tu kujua kuwa kura yao katika mfumo uliopo sasa haiheshimiwi. Ujue kuwa watu wakifika hapo watataka haki kwa namna nyingine. Nawaombea tafakari ya hekima. Acheni malumbano na chadema, kaeni pamoja mtatue matatizo yetu. Wapinzani na ccm, wote sisi ni watz. na hakuna aliye na haki za uraia kuliko mwenzake.

Mungu ibariki Tz.
 
safi sana kaka mie naomba umtumie kupitia barua pepe ya ikulu, maelezo yamesimama sana. kama anaskia na askie
 
I salute you Sir. Hii imekaa vizuri sana. Sasa naomba umwekee kwenye FACEBOOK yake aipate laiv, ila ana kichwa ngumu huyo.
 
Tatizo CCM hawasomi, labda kwa demonstrations!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom