Barua ya Wazi kwa Rais Kikwete Kuhusu Zimbabwe

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,474
39,987
Na. M. M. Mwanakijiji

Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

YAH: Iongoze Afrika kupinga utawala wa kidhalimu wa Robert Mugabe

Naomba husika na kichwa hicho cha habari;

Hivi hadi nini kitokee ndipo viongozi wetu wataona kuwa kinachoendelea Zimbabwe ni aibu ya bara letu, na udhalilishaji wa utu, hadhi, na tunu ya mwafrika? Ni mpaka nini kifanyike ndipo tutaweza kuchukua msimamo wa kupinga uvunjaji mkubwa wa haki za binadamu, na kuchukua msimamo ulio dhahiri dhidi ya Robert Mugabe? Kwanini Tanzania nchi ambayo inadai katika Katiba yake kuwa "kila mtu anastahili haki ya kutambuliwa na kuthaminiwa utu wake" ifumbie macho utu wa wana wa Zimbabwe ambao wanateswa katika mikono ya utawala wa kidhalimu wa Robert Mugabe?

Inakuwaje wanasiasa wetu na wabunge wetu wanashindwa kutoa msimamo wa kulaani kauli za kidikteta ambazo zimekuwa zikitolewa na utawala wa Robert Mugabe? Hivi kweli tunahitaji wazungu kutuonesha kuwa kinachotokea Zimbabwe hakina mfano wa haki za binadamu? HIvi kweli tunataka hadi Amnesty International na Human Rights Watch waje na kutuambia kuwa ya Mugabe ni uovu uliokithiri?

Je tumekuwa watii na wenye kuheshimu sura za watu kiasi hiki hadi tunaogopa kumwambia kuwa "tunashukuru kwa mchango wako lakini kwa hili tunakukana"? Je hakuna watu waliofanya mambo mazuri huko nyuma na katika maisha yao ya baadaye wakaharibu na historia zao zikatajwa na nyota pembeni?

Wale wanaolalamikia ukiukwaji wa haki za binadamu kule Palestine, Iraq na Afghanistani, walioandamana ujio wa Bush na ambao wakitetea haki za watu wa huko wako wapi leo hii wakati ndugu zetu wanaishi maisha ya wasiwasi na hofu kubwa chini ya mkono wenye kucha ndefu zichomazo wa Robert Mugabe?

Wakati umefika kwa viongozi wetu kuacha mazingaombwe ya diplomasia ya ukimya ambayo kimsingi ni ukimya wa kidiplomasia. Ni ukimya ambao unaendelea kutoa kibali kwa Utawala haramu wa Robert Mugabe kuendelea kutesa wananchi wa nchi hiyo. Je sisi Tanzania ambao tuliwahi kukiri katika imani zetu kuwa "binadamu wote ni sawa, na Afrika ni moja" leo hii tuko wapi?

Mch. Martin Luther King alipoandika barua yake kutoka Jela ya Alabama alisema wazi kuwa "udhalimu mahali fulani, ni udhalimu mahali pote" Je tunaweza vipi kukaa katika "kisiwa cha amani" wakati ndugu zetu wanateseka na kufanywa wakimbizi katika nchi yao wenyewe. Kwanini kina Morgan na wenzao waonekane si wananchi wa Zimbabwe kweli kwa sababu tu wanataka kuiokoa nchi yao?

Nini ambacho utawala wako unaogopa kusema na kufanya mbele ya Robert Mugabe? Hivi tukimtolea uvivu na kumuita kwa jina lake kuwa ni dikteta na kusema kuwa yanayofanyika Zimbabwe hayana nafasi katika bara la Afrika Mugabe atasema nini? Atatufanya nini? Hii heshima ya wazee ni heshima kweli wakati mzee anasimamia ubakaji na utesaji wa watu wake?

Naomba kutoa wito wa wazi, wa moja kwa moja na usio na utata kwako uwa Mhe. Kikwete kama Rais wa Tanzania, nchi ambayo imetoa na kulipa kwa damu ili nchi hizi za kusini mwa Afrika ziwe huru, asimame sasa na kusema "kama kutosha inatosha". Rais Kikwete ukiwakilisha mawazo ya kizazi kipya uungane na Botswana kwa kumwita Balozi wa Zimbabwe nchini na kuonesha kutokufurahishwa na yanayoendelea Zimbabwe.

Zaidi ya yote, Rais Kikwete akiwa ni Mwenyekiti wa AU aitishe mkutano wa haraka kati ya Morgan na Mugabe Jijini Dar (na si mtu mwingine nje yao) ili kujadiliana na kukubaliana jinsi uchaguzi wa marudio utakavyokuwa na kupata uhakika kuwa kila mmoja wao ataheshimu matokeo ya uchaguzi huo. Kikwete anaweza kufanya hivyo kwa kutumia kivuli cha NEPAD ambamo ndani yake kuna "African Peer Review Mechanism". Huu ni wakati wa kuonesha uongozi.

Na endapo Mugabe hatokuwa tayari kusikiliza ushauri wa rafiki, basi wakati umefika wa kuvunja uhusiano wetu wa kidiplomasia na Zimbabwe. Itauma, lakini inabidi.

Nikukumbushe maneno ya Rais Nyerere kwenye mkutano wa Jumuiya ya Madola mwanzoni mwa miaka ya sitini ambapo hoja ya kukubali kuiingiza Afrika ya Kusini katika jumuiya hiyo. Nyerere alisema wazi kuwa kwa kadiri ya kwamba siasa za kibaguzi zilikuwepo Afrika ya Kusini basi Afrika ya Kusini haiwezi kuwa mwanachama. Na akatamka yale maneno mashuhuri ya msimamo wa kiongozi mbele ya Malkia "Mkiwapigia kura kuwaingiza Afrika ya Kusini, mtakuwa mmepika kura kututoa sisi". Na hoja ya Mwalimu ikashinda.

Na ni Mwalimu huyo huyo ambaye alizungumzia suala la "uraia" baada ya Idi Amin kuanza kuhoji uraia wa waasia wa Uganda na kuanza sera zake za kibaguzi kule. Mwalimu alizungumza siku ile August 21, 1972 pale Chuo cha Ualimu Chang'ombe, Mwalimu alisema hivi "Afrika lazima ikatae kudhalilishwa, kunyonywa, na kusukumwa sukumwa. Na kwa moyo huo huo ni lazima tukatae kuwadhalilisha, kuwanyonya, na kuwasukuma sukuma wengine. Ni lazima tutende siyo maneno tu".

Mhe. Rais, Afrika inadhalilishwa na vitendo vya Mugabe na mashabiki wake. Afrika inafanywa duni kwa viongozi kama yeye. Ni kweli tuna matatizo yetu Tanzania, nafahamu tuna kashfa zetu za mambo ya fedha nchini na uongozi wa kishkaji; nafahamu wazi kabisa ndani ya CCM na serikali kuna kubebana na kulindana. Lakini ukweli ni wazi kuwa hatujafikia walipofikia Zimbabwe, hatujafikia mahali pa kufanyana vibaya kiasi cha Zimbabwe. Ni kweli tuna matatizo yetu lakini tukiyaweka ya Zimbabwe upande wa pili, ya kwetu yanaonekana ni kheri tupu!

Sisemi upuuzie matatizo yetu, sitoi ushauri kuwa ya kwetu kwa vile ni madogo basi usiyafuatilie. La hasha, ninachosema ni kuwa chukua msimamo kama kiongozi na kwa niaba ya wale waliotangulia mbele ya haki, kwa niaba ya wale waliomwaga damu yao kukomboa bara letu, usimame na kumwambia Mugabe inatosha na saa na wakati wake umepita aamue kujiuzulu na kustaafu kwani yeye kama wanadamu wengine, atakufa tu, na Zimbabwe itatawaliwa na mwingine. Mugabe hana ubavu wa kuzuia hatima ya nchi hiyo, na siku moja wengine watasimama mahali pake.

Akiamua kuachia ngazi sasa na kufanya mapatano ya kisiasa na wale walioumia chini yake, labda historia itamuonea huruma. Lakini Zimbabwe haiwezi kuendelea jinsi ilivyo, huku sisi rafiki zao na ndugu zao tukikaa nje kuangalia. Mhe. Rais, onesha msimamo sasa, na uliongoze Taifa letu kuchukua msimamo dhidi ya Mugabe ili tuwape nafasi ya ndugu zetu wa Zimbabwe ya kuishi katika nchi ya amani, utulivu, na mshikamano.

Sijaomba vingi, lakini hilo nakuomba kwa machozi.

Nimalizie kwa kukumbusha maneno haya ya baba wa Taifa tena alipozungumza mwaka 1959 kwenye mkutano ule uliofanyika Uingereza Juni 26 (karibu miaka 50 kamili iliyopita). Katika mkutano huo uliokuwa unazungumzia Afrika ya Kusini na utawala wa Makaburu Mwalimu alisema maneno haya "Serikali ya Afrika ya Kusini inapigana na historia, ni wao watakaoshindwa. Tunafahamu harakati za ukombozi zitafanikiwa katika Afrika ya Kusini. Kama tunajiamini tutashinda".

Mheshimiwa, Mugabe anashindana na historia na kwa hakika atashindwa; harakati za mabadiliko ya kisiasa yanayoendelea yatafanikiwa, na kama sisi sote tunajiamini kwamba tuko sahihi basi tutashinda. Tuongoze katika hili kwani bwana mdogo kutoka Botswana ameshaonesha njia.

Wasalaam katika Kuliinua Bara letu

M. M. M.
 
Mkuu ni kweli mambo yanayotokea Zimbabwe yanatia ganzi masikio, halafu Mugabe na kijana Bright Matonga anasema hakuna vurugu jamani aibu aibu kwetu Waafrika. Naunga mkono barua yako Mkuu, Kwanini AU inamwogopa Mugabe?
 
Matatizo ya ZIMBABWE NI GEAR YAKE ILI AKUMBATIWE NA WAFADHILI ESP MAREKANI NA UK ILI ASIBANWE KWENYE UMAFIOSO WAKE!
HASTAHILI HATA KUWA MWENYEKITI WA AU TENA!
SCRAP THIS CRAP...PLS!!
 
MWKJJ
ni wajibu wetu kumweleza huyu MR President
Lakini kama ya Tanzania yamemshinda, je unadhani atayaweza ya Zimbabwe??
Huyu matatizo matupu kwa nchi yetu jamani

Huyu Jokeri hamwezi Mugabe hata kidogo....wameshindwa akina Blair sembuse yeye? Akijifanya kimbelembele atatukanwa kama alivotukanwa Jendayi Fraser....ahahahahahahaaa.....Mugabe kiboko!!!
 
Huyu hafai tena kuwa KIONGOZI WA AFRIKA!
Huyu arudishwe nyumbani na BUNGE tuwashighulike hawa wasituletee uhuni kabisa!
Mi nakwambia tutapambana nao EVERYWHERE!
Hakuna pa kupumulia kwasababu nimeshagundua wanafikiri UCHAWI UNAVUKA BAHARI...Kama wana MISUKULE NI HAO HAO!
Anatafuta UMAARUFU MBELE YA MATAIFA HAYA YA MAGHARIBI ILI KUNEGOTIATE NA KUWEZA KULINDWA HATA KAMA WAKIENDELEZA UMAFIOSO WAO AMBAO UKO LIVE KABISA!
Marekani walishataka UWAJIBIKAJI...Halafu wakalegeza masharti...Mara wakampigia kifua huko AU ili awe Mwenye Kiti...Msishangae akiamuru jeshi la AU kwa kushirikiana na US na UK ama NATO kumuondoa Mugabe huku wakimpachika Tsvangirai NA KURUDISHA MASHAMBA YOTE MIKONONI MWA MABEPARI UPYA!
 
Wazimbabwe wana matatizo yao na sisi tuna yetu...Tena makubwa sana...Wasituletee uhuni hawa!
Hivi inawezekana kweli TAIFA LIMEROGWA?
HIVI KWELI BADO KUNA MAMBO YA VYAMA NA KUTETEANA HUMU BADO YANAENDELEA?
KAMA KUNA WANAOJUA YALE TUSIYOYAJUA HALAFU WANANYAMAZA KIMYA...THEN KUTAKUWA NA MUSHKELI WALAHI VILE!
 
Kudos Mzee Mwanakijiji

Mugabe hawezi kutotii amri inayotoka kwa rais wa Tanzania, katu kwa sababu anafahamu aliingia kwa mgongo mkubwa sana wa Tanzania na kama akileta longolongo tuwe wa kwanza kuvunja uhusiano wetu wa kibalozi. The time is now or never.

JK ni lazima aonyeshe uongozi katika hili hatuwezi tena kamwe kuzungukwa na hizi taka taka kwenye karne ya 21.
 
Mafanikio ya Zimbabwe leo ama kesho JF tutakuwa tumechangia .Tuendelee kufungua macho tusilale mapema wao hawalali ama wakilala wanaamka mapema kuwanga si mmeona wenyewe Dodoma ?
 
Mafanikio ya ZIMBABWE HAYAWEZI KUPATIKANA BILA MWENYEKITI SAFI WA AU!
ARUDISHWE NYUMBANI HUYU TUANZE UPYA!
ZE COMEDY ZE END!
 
Kudos Mzee Mwanakijiji

Mugabe hawezi kutotii amri inayotoka kwa rais wa Tanzania, katu kwa sababu anafahamu aliingia kwa mgongo mkubwa sana wa Tanzania na kama akileta longolongo tuwe wa kwanza kuvunja uhusiano wetu wa kibalozi. The time is now or never.

JK ni lazima aonyeshe uongozi katika hili hatuwezi tena kamwe kuzungukwa na hizi taka taka kwenye karne ya 21.

Aliingia kwa mgongo wa WATANZANIA lakini si WATANZANIA HAWA MAFIOSO!
Sasa huyu MTU akipewa nafasi ya kuwasaidia hawa watu wa magharibi si watamlinda na hapo ndio kifo cha haki kwa mtanzania?
Kwani MUGABE AKITAKA KUISHI KWA RAHA MADARAKANI LEO SI ATAWAKUBALIA TU HAO WATU KILA KITU?
Arudi nyumbani huyu!
BUNGE LIFANYE KAZI WALIYOAPA MBELE ZA MUNGU KUWAFANYIA WATANZANIA LA SIVYO UCHAWI WAO NI KWELI UTAWAUA!
 
Jmushi 1

Kama kiswahili kimekushinda andika kimombo tu tutakuelewa na kukujibu vizuri.

What are you talking about? Do you really know what you wrote?
 
Acha hizo wewe Dua...Endelea kuomba dua tu Mungu aliponye Taifa letu!
Afadhali hata yule Dua Said alikuwa akijua kandanda...Talking about sieleweki kwasababu ya kiswahili....

Kikwete akipewa nafasi ya kujichotea sifa toka kwa mataifa ya magharibi...Then hiyo ndiyo njia yake ya kuendelea kulindwa ili abaki madarakani!
Hizo ni negotiations za ***************Arudi nyumbani huyu....Hawezi kuwa upande mmoja!
Wazimbabwe wana matatizo yao lakini yetu ni makubwa sana tu!

NB:Nilivyoelewa kuingia kwa mgongo wetu...Najua ulimaanisha harakati zao za kumng'oa mkoloni!
Si kina Kikwete waliofanya hivyo NI KAZI YA KINA MWALIMU NA WAZALENDO WENGINE!

Mwalimu mwenyewe hakumtaka KIKWETE WALA LOWASSA HADI ANAENDA KABURINI!

Leo hii kafa...Na sasa ni mitambiko KABURINI KWA MWALIMU NA UCHAWI BUNGENI....Huku akijinusuru kwa kutafuta sifa kwenye mataifa ya magharibi kwa mgongo wa Zimbabwe huku Tanzania yenyeyewe ikikabiliwa na ***** unaoongozwa na YEYE!

Nyie kama mnataka kuendelea KUMPA KIKWETE ENDELEENI TU!
Mimi si POPOBAWA WALA SIJACHUKULIWA MSUKULE!
WE VIPI?
 
Last edited by a moderator:
Mugabe anajidai kwasababu anaona kwamba amejiimarisha kijeshi kutokana na msaada wa kijeshi wa China.

Pia anaona kwamba kwa kuwa anaopingana nao ni wale waliokuwa wakoloni, basi anafikri wataona haya kumshughulikia.

Pia ana nguvu ya ki-comred kutoka kwa war veterans na kadhalika.

Lakini Tanzania na nchi zingine kwa kushirikisha AU wana wajibu wa kupitisha any resolutions zitakazoikoa Zimbabwe isiangamizwe na Mugabe.

Na moja ya resolutions hizo ni kumtoa Mugabe kinguvu baada ya uchaguzi wa marudio, maana atakuwa ameshinda isivo halali.
 
Guys...This time around i am here to stay...Trust me...
Wakati mustakabali wa Taifa haujulikani kutokana na kugubikwa na wingu zito la kashfa za ufisadi..Pamoja na dilema kwenye muafaka na wenzetu wa visiwani...Nyie mumeamua kumpa moyo Kikwete wa kumshughulikia Mugabe wakati MAFIOSO WANAWANYONYA WANANCHI DAMU LIVE kwa kushirikiana na DON KIKWETE MWENYEWE!

Sasa kuna hiki kituko kinachoitwa BARUA KWA KIKWETE!
Barua ambayo malengo yake ni kuonyesha ni jinsi gani rais wetu mpendwa anavyoyajali majukumu ya uenyekiti wa AU na kupata nafasi ya kushughulikia migogoro na matatizo ya mataifa mengine na kuyapa kipaumbele zaidi ya yale ya Taifa lake!

Na ni jinsi gani alivyo busy and dedicated kulitumikia baraza hilo badala ya Taifa!

Hilo siyo baya!

Baya ni kwamba kuna mustakabali muhimu wa taifa anaokabiliana nao at this moment!

NB:Kuna waliokuwa wakitaka apewe muda...Muda umekwisha na sasa wanashindwa kumtetea na naona wanaleta..."THE MUGABE FACTOR"...Mimi naandika tu ili kizazi kijacho kipate HISTORIA YA KWELI HATA KAMA TUTAKUFA KWENYE MPAMBANO!

Je ni wakati wa watanzania kuliangalia hili?
 
Mugabe anajidai kwasababu anaona kwamba amejiimarisha kijeshi kutokana na msaada wa kijeshi wa China.

Pia anaona kwamba kwa kuwa anaopingana nao ni wale waliokuwa wakoloni, basi anafikri wataona haya kumshughulikia.

Pia ana nguvu ya ki-comred kutoka kwa war veterans na kadhalika.

Lakini Tanzania na nchi zingine kwa kushirikisha AU wana wajibu wa kupitisha any resolutions zitakazoikoa Zimbabwe isiangamizwe na Mugabe.

Na moja ya resolutions hizo ni kumtoa Mugabe kinguvu baada ya uchaguzi wa marudio, maana atakuwa ameshinda isivo halali.

Richie tutawasaidia Wazimbabwe lakini si chini ya KIKWETE...Huyu *****!
Alimweka vipi MWANYIKA KWENYE KAMATI YA UCHUNGUZI YA EPA WAKATI NI MAFIA WA RICHMOND?
ALIMWEKA VIPI ZITTO KWENYE KAPU LA MAFISADI ILI KUMCHAFUA NA KUIVURUGA NCHI?
WE UNAFIKIRI KWANINI WATU WANATAKA MGOMBEA BINAFSI NA WAMECHOSHWA NA VYAMA?
VIRUSI VIRUSI VIRUSI...EVERYWHERE!
 
Last edited by a moderator:
Guys...This time around i am here to stay...Trust me...
Wakati mustakabali wa Taifa haujulikani kutokana na kugubikwa na wingu zito la kashfa za ufisadi..Pamoja na dilema kwenye muafaka na wenzetu wa visiwani...Nyie mumeamua kumpa moyo Kikwete wa kumshghlikia Mugabe wakati MAFIOSO WANAWANYONYA WANANCHI DAMU LIVE!
[SIZE=3[B]]Sasa kuna hiki kituko kinachoitwa BARUA KWA KIKWETE![/B][/SIZE]
Barua ambayo malengo yake ni kuonyesha ni jinsi gani rais wetu mpendwa anavyoyajali majukumu ya uenyekiti wa AU na kupata nafasi ya kushughulikia migogoro na matatizo ya mataifa mengine na kuyapa kipaumbele zaidi ya yale ya Taifa lake!

Na ni jinsi gani alivyo busy and dedicated kulitumikia baraza hilo badala ya Taifa!

Hilo siyo baya!

Baya ni kwamba kuna mustakabali muhimu wa taifa anaokabiliana nao at this moment!

Je ni wakati wa watanzania kuliangalia hili?

kwa vile hiki ni kituko ni bora uachane nacho ili kituko hiki kiendelee. Una mambo mengi ya kuzungumzia na kuuliza hivyo itakuwa vizuri ukiendelea kwenye mada hizo na uachane na "kituko" hiki. Barua hii imesemwa ni ya wazi kwenda kwa Kikwete, na kwa vile wewe dunia yako inazunguka Tanzania, na binadamu wanaostahili kutetewa ni Watanzania tu, na ya kwamba uovu sehemu nyingine haukuhusu isipokuwa unaowagusa Watanzania, na kwa vile mada hii wewe kwako ni kituko, nakushauri uendelee kuzungumzia mambo ya Watanzania pekee haya ya kimataifa hayuko katika upeo wako. Endelea kuishi na kufikiri katika box la "Tanzania tu"...
 
Wakuu
Matatizo yanayoikumba Zimba si kosa la Mugabe.

Mutakumbuka matatizo yameanza baada ya wazungu kufukuzwa,hivyo basi inaodhihirisha ni jinsi gani wazungu walivyo wanoko na washenzi hadi wakacreate dudu la uhakika lililozaa matatizo yooote haya muyaonayo zimbabwe.

Neno moja nalolitaka kwenu watanzania ni kutafutia njia ya kumsadia mugabe na watu wake waondokane na hali mbaya ya kiuchumi then maissue ya siasa yafute.
Hata huyo Tsava akichukua nchi bado ni kibaraka tuu wa wazungu,hakuna jipya,zaidi ya ukoloni mpya.
 
Richie tutawasaidia Wazimbabwe lakini si chini ya KIKWETE...Huyu mafia!
Alimweka vipi MWANYIKA KWENYE KAMATI YA UCHUNGUZI YA EPA WAKATI NI MAFIA WA RICHMOND?
ALIMWEKA VIPI ZITTO KWENYE KAPU LA MAFISADI ILI KUMCHAFUA NA KUIVURUGA NCHI?
WE UNAFIKIRI KWANINI WATU WANATAKA MGOMBEA BINAFSI NA WAMECHOSHWA NA VYAMA?
VIRUSI VIRUSI VIRUSI...EVERYWHERE!

Nakuomba mara moja tu acha kumuita Rais Kikwete "Mafia". Hoja zako haziwi na nguvu kwa kubatiza watu majina ya namna hiyo au haioneshi kuwa unachukuzwa zaidi na yanayoendelea nchini. Kumuita Rais wa Jamhuri yetu kuwa ni "mafia" siyo tu kutudhihakisha lakini ni madai ambayo ukiambiwa uyatetee kwa jina hilo hutoweza. Tofauti za kisiasa hazina maana kuanza kuita watu majina ya namna hiyo.

Binafsi siamini kama JF ni mahali pake.
 
Mwanakijiji,

Inaonekana huyu kijana ana kiburi na ujeuri wa makusudi, kuwalinda wahalifu na marafiki zake, kama anashindwa kukemea chochote bongo basi Zimbabwe itakuwa ni sikio la kufa kwake.

Gm
 
Back
Top Bottom