Barua ya wazi kwa Rais JK na Waziri Mkuu MP

bwegebwege

JF-Expert Member
Jul 30, 2010
1,071
185
Kwenu waheshimiwa!

Salaam!!

Hii ni barua yangu kwenu; najua itawafikia! Kama hamtaisoma wenyewe kupitia JF basi najua wale tunaowaita "wapambe" watakudokezeni nini kimeandikwa, haijalishi mtaupataje ujumbe, nitafurahi kuikia mmeipata!! Niwape angalizo tu; msinune mnapoisoma, eleweni kwamba na mimi nakerwa na mambo ambayo kwa miaka zaidi ya arobaini sasa, si serikali wala mbunge wangu amekuwa akiyasimiamia kwa nguvu zote! Kama mtanzania (mtanganyika to be precise, maana si kuna "wanzanzibari'??) nimeona niwashirikishe nyie kwenye haya muhimu ( ni mtazamo wangu tu)
Kwanza nichukue fursha hii kuwapongezeni kurudi tena kuongoza serikali. Nitofautiane na Mheshimiwa Kikwete kwenye ile hotuba yako mara baada ya kuapishwa kwamba "ulipata ushindi wa kishindo"! Ukitazama takwimu za waliopiga kura, na wale waliopigia kura wagombea wengine; kasha ukifuatilia malalamiko dhidi ya chama chako katika "kuchakachua matokeo",, jinsi tume ya uchaguzi ilivyoonyesha udahifu wa wazi uliopelekea baadhi ya wagiombea wenu, na wewe mwenyewe (kupitia nguvu ya viongozi wa serikali wasio waaminifu na waliokosa uadilifu) utagundua hukupita "kwa kishindo" ila kwa "mbinde"!! Ukiacha hilo, rejea ushindi wako uliokuweka madarakani 2005, wastani wa kura za mwaka ule na hizi sa sasa inaonyesha wazi kwamba watanzania ama hawakiungi tena mkono chama chako au wamekuchoka; au wanahitaji chama mbadala kuongoza nchi!! Kwa jibu lolote lile ni wazi WATANZANIA WENGI HAWAJARIDHIKA NA UTENDAJI WA SERIKALI YAKO!! Uchaguzi uliopita ni ujumbe tosha kwako kamanda, sasa ni wakati wa kurekebisha kasoro ili uondoke na sifa nzuri!!
Kwa mtoto wa mkulima, Pinda, nakupongeza sana. Niliona kipindi chote cha uchaguzi umekuwa na pilika za safari na kumuwakilisha kiongozi wetu sehemu mbalimbali, kule NY, India etc! Hukufanya kampeni, ulipita bila kupingwa jimboni kwako, lakini hata wapinzani hawakuona umuhimu wa kuweka mtu kushindana nawe…ni dalili njema, lakini hazimaanishi kwamba wewe ni msafi kihivyo!! Wahenga walisema samaki mmoja akioza wote wameoza!! Wewe ulikuwa ni kiranja mkuu katika serikali ya JK, amekupa tena TANO nyingine, hebu basi hizi tano uzifanyie kweli, watanzania wengi wamekuwa wanakuona wewe MPOLE SANA, haukemei upuuzi unaofanywa na baadhi ya viongozi wa serikali; hausimamii ipasavyo na hauwawajibishi watendaji wakuu wanaoboronga…zaidi ya watumishi wachache wa halmashauri kama yule jamaa wa Bagamoyo…hivi ulimfunga yule? Au baada ya magazeti kuandika ikawa ndiyo mwisho?? Haya mjomba, wewe kama mimi ni watoto wa wakulima, tunatarajia mengi kutoka kwako miaka hii mitano ijayo, hebu changamkia tenda mjomba, WAPELEKE MCHAKAMCHAKA kama enzi zile za Bulombora au Mafinga JKT, we si ulipitia kule??
Sasa wakuu mimi naomba nitumie fuursa ya JF kuwafikishia yangu ya moyoni, najua mna sera na kila kitu ila watanzania tumechoshwa na sera, kanuni, ilani za uchaguzi (mwaka 2010 sijui ilikuwa ilani ya uchakachuzi?)…Sisi tunataka kuona watu wanawajibika si kwa faida yao bali kwa faida ya wananchi!! Yafuatayo ni maoni yangu

Kilimo
Zaidi ya silimia 80% ya watanzania wanaishi vijijini (Rura areas) na wanategeme kilimo CHA JEMBE LA MKONO!! Serikali ya CCM haina mikakati ya dhati ya kufufua kilimo, kila siku ni siasa, sasa tunataka kuona VITENDO!! Hili wazo la kilimo kwanza ni zuri lakini HAKUNA COMMITMENT KWA UPANDE WA SERIKALI KUENDELEZA KILIMO. Ni wazi kwamba baadhi ya viongozi (wengi wenu), Mheshimiwa Rais na PM mkiwemo, mnajihusisha na kilimo! Kwenu nyie mnaweza kwa sababu kwanza fedha ipo, pili mnatumia nafasi zenu kupata wataalamu waliobobea, mnajua ni wapi pa kupata fedha (si nyie ndiyo mnaelewa mambo ya EPZ, EPA sijui na nini huko?)!! Sasa mwananchi wa kawaida hawezi kupata msaada huo!! Kwanza hana mtaji, na hata akiutaka akifika benki anapewa masharti magumu (Awe na nyumba yenye hati etc…) sasa kwa mshahara wa 150,000/= tutajenga lini? Kwa mtindo huu wa serikali kutokuwa na mpango wenye urahisi, usiokuwa wa mikwara na rushwa, wa kuwapimia watu viwanja vyao na kutoa hati miliki haraka ni lini mtanzania wa kawaida mwenye kibanda chake ataweza kukiweka kama bond?? Hebu tumieni nafasi zenu, waiteni hao wenye mabenki, Muitenii Benno? (Ndullu) wa BoT, HEBU KAENI NAO HAO MUANGALIE NAMNA GANI MTAWAWEZESHA WATANZANIA WA KAWAIDA KUPATA MIKOPO ILI KUENDELEZA KILIMO!! SI NDIYO UTI WA MGONGO WA UCHUMI WETU?? Hizi benki zinachochea ongezeko la magari/msongamano katika barabara za Dar kwa kutoa mikopo ya magari kwa wananchi; sasa kila mtu analo gari, maana unakatwa moja kwa moja kwenye mshahara!! Kwa mantiki hiyo fedha ipo, hebu sasa waangalie namna gani watasaidia wakulima, mmoja mmoja au vikundi, na serikali iweke utaratibu wa kuwawekea dhamana wananchi wake kupitia serikali za mitaa, vijiji, Kata na kadhalika!! TUWEZESHENI TUINUE KILIMO!!
Sambamba na hilo hebu angalieni uwezekano wa kupunguza wawekezaji kwenye sekta zisizokuwa muhimu sana badala yake ITANGAZENI TANZANIA KWA WAWEKEZAJI WA SEKTA YA KILIMO!! Kuna ranchi za Taifa karibu kila mkoa, tunayo ardhi kubwa na ambayo bado haijatumika vema, hebu waiteni watu watakaoweza kuwekeza huko, kule kilombero, Mang'ula, Chalinze, Rufiji, Njombe, Songea, Kilindi, Mtindiro,Kicheba, Kibaranga, Mjesani, Kyela na kwingeneko….kuna maeneo ambayo kama tunawekeza vema miaka hii mitano mtaona Tanzania inavyopiga hatua!! Hivi wakuu, HAMUONI AIBU KUKUTA NYANYA YA SOUTH AFRICA PALE SHOPRITE? Kweli Tanzania hatuwezi kufuga kuku na kusupply hata kwa domestic market?? Ni kweli?? Hebu fanyeni mambo katika hili jamani….
WAKULIMA WANAKOSA ZANA: Mkitaka kweli kunyanyua kilimo basi hebu wasaidieni watanzania kuwaletea zana za kilimo!! Serikali inaweza hata kufanya biashara kwa kuingiza matrekta kwa wingi na kutuuzia wakulima kwa bei nafuu!! Mbona nchi nzima imejaa PIKIPIKI TU TOKA CHINA? Hao wawekezaji (Wanaoutuletea hadi pikipiki za majina ya ajabu kama « SENGE ») waambiwe sasa bodaboda na vibajaji hatutaki !! Serikali iweke « Public Transport » kwa kuipa uwezo UDA, na kukaribisha wawekezaji wenye uwezo wa kuweka MABASI YA ABIRIA (town buses) yale makubwa, na kuondokana na hizi daladala, HIACE , Bajaj « Chenge » na Bodaboda….WAAMBENI WANAOWEKEZA HAPA HATUHITAJI BAJAJ NA BODABODA, TUNAHITAJI MATREKTA NA MABASI MAKUBWA KWA USAFIRI WA MJINI !!! HATUTAKI WAWEKEZAJI WA PIKIPIKI TU….
Mkiamua nyie inawezekana…hebu tupeni raha watanzania !!

Katiba
Katiba ndiyo kila kitu!! Kwa katiba hii iliyopo ambayo kila siku inawekewa viraka bado Tanzania itaendelea kuwa nyuma katika demokrasia na katika dhana nzima ya kuwawajibisha viongozi wazembe!! Nimecheka sana Waziri wa Sheria na Katiba aliposema eti wanaodai katiba mpya ni "watu wa mtaani"…na serikali haiwezi kufanya kitu hadi ipokee maombi kimaandishi!!" Hii kwa lugha rahisi ni DHARAU KUBWA iliyoonyeshwa na waziri, ambaye hana hata wiki tangu aingie ofisini kwake!! Watanzania tutarajie nini kwake huyu? Hebu nawaombeni nyie mkemeeni huyu, aelewe cheo ni dhamana aliyopewa na wananchi, lazima kuwatumikia!! Huwezi kuwadharau watanzania waliokuweka madarakani, yeye sasa anatumikia watu wote bila kujali dini na itikadi za kichama, asikurupuke na kutupa majibu yake ya "mipasho"!! Hivi wale "wanazuoni" waliobobea pale UDSM kama Dr Kitila na Professor Lwaitama, ; au wanazuoni wastaafu kama Professor Shivji na Professor Mwesiga Baregu na wengineo amabo wamekuwa wakishauri Katiba ibadilishwe anawaona ni "laymen"??
Kaka na Mjomba, hebu lipeni hili suala kipaumbele. Watanzania wanataka KATIBA IBADILISHWE!! Tunaogopa nini kuitisha kura ya maoni? Mbona Nyerere hakuogopa kuitisha kura ya maoni kuingiza demokrasia ya vyama vingi?

Elimu
Jamani; tangu nikiwa mdogo nimesikia elimu ni msingi wa maendeleo ya Taifa hili!! Mojawapo ya sababu zilizowafanya nyie kupewa dhamana ya kuongoza nchi ni elimu yenu! (japo si saaana)!! Hakuna nchi duniani inaweza kuendelea kama HATUWEKEZI KWENYE ELIMU!! Niwaombe basi msimamie hili vizuri! Ni wazi shule za kata bila walimu hazisaidii; kuongeza idadi ya shule bila kuboresha maisha ya walimu (kimaslahi, mafunzo nk) ni bure kabisa!! Kuongeza shule zenye kufuata mitaala ya nje (British Curriculum na mingineyo) bila kuwepo bodi madhubuti ye elimu hiyo au Wizara madhubuti itakayofanya ukaguzi na kusimamia kwa karibu kuona kwamba elimu inayotolewa ina KIWANGO KINACHOSTAHILI pia ni kazi bure kabisa….matokeo yake tunaishia kuwa na watoto wanaoongea kiinglishi lakini "kiwango/ubora cha elimu yao" ni duni!! Kama tutakubali kuwa na shule za namna hii ambazo zinaingiza katika mitaala yake TAMADUNI ZA NJE ZAIDI ZINAZOKINGANA NA UTAMADUNI WETU nayo ni kazi bure kabisa, ndiyo hapo tunaishia kuwa na vijana wengi wa sasa waliopo mashuleni wanakuwa wanaiga utamaduni usiofaa (Ambao wanajifunza kwenye hizi shule…St. sijui Anne, St. Prisca, St. Salma, St. Winnie au zile zinajitambulisha kwa …International School etc); kama wizara husika haisimamii ipasavyo kwa ujumla HATUWAJENGI VIJANA, TUNAWABOMOA!! Ndiyo maana ukifika chuo kikuu sasa hivi unakutana na mchanganyiko maalumu ambao unaifanya elimu iwe paralyzed…VIWANGO DUNI NI WENGI JAPO WANAWEZA KUONGEA KIMOMBO!! WANAFUNZI HAWANA MAADILI MEMA KWA KUWA WAMEKUWA NA MSINGI MBAYA KWENYE SHULE WALIZOTOKA!! Hebu mwambieni waziri muhusika alitazame hili!!
Ukiacha hayo SERA YA SERIKALI YA CCM KATIKA ELIMU INAJIKANGANYA ZAIDI!! Kwa mfano, manasema KISWAHILI NI LUGHA YA TAIFA, lakini mitaala kweny evyuo haijabadilika….wekeni kwanza mfumo bora utakaowezesha KISWAHILI KUPATA NGUVU….Otherwise ni kazi bure kabisa!! Hivi mnajua hadi leo, pamoja na kwamba serikali ilidai kwamba usaili kila ofisi na taasisi za serikali ufanywe kwa KISWAHILI…bado kuna watu wanakoseshwa kazi kwa kuwa "eti hawafahamu kiinglishi"? Kama tunataka ku-promote Kiswahili basi isiwe suala la ndani tu, anzieni nje! PAMBANENI KULE UN ili kiswahili kiwe mojawapo ya lugha zinazotambulika kimataifa !! Ikiwa ni lugh mojawapo ya UN, watanzania wengi wataajiriwa na UN, Wawekezaji wanaokuja watalazimika kutumia kiswahili kama lugha ya kazi…itakuwa ni boost kubwa !! Kwa sasa hivi kumwambia mtanzania akazanie kiswahili maana ni lugha ya taifa, then hakitambuliwi kimataifa, halafu waajari wote (Hasa wawekezaji) wanapotaka uwe unajua kimombo zaidi…) hii ni kumuumiza msomi wa kitanzania !! Hebu tuliangalie hili…..WATANZANIA TUNAHITAJI MAPINDUZI KATIKA ELIMU NA USIMAMIAJI WA MAKINI KWENYE VIWANGO VYA ELIMU/MITAALA !!

Naomba nikanywe maji ; Itaendelea……
 
kwa kua milango ya ikulu iko wazi hata kwa waendesha baiskeli watokao geita,nakushauri u print uipeleke mweyewe pale ikulu kwa mkuu,am sure utapokelewa tu kwa mikono miwili kam ayule jamaa mana ww una ushauri mzuri.......
 
kwa kua milango ya ikulu iko wazi hata kwa waendesha baiskeli watokao geita,nakushauri u print uipeleke mweyewe pale ikulu kwa mkuu,am sure utapokelewa tu kwa mikono miwili kam ayule jamaa mana ww una ushauri mzuri.......


Usifanye hivyo anakudanganya watakuua kwa kisingizio kwamba ulikuwa unarushiana risasi na walinzi, unafikiri hili chapisho ni zuri
 
ushauri uliowapa hawa viongozi wakuu wa nchi ni bomba sana.nina uhakika PINDA atakuwa amekuelewa vizuri sana ila shida ni kuwa hana maamuzi ya moja kwa moja bila kukubaliwa na boss wake. tatizo ni kwa huyo baba ridhiwan, kwanza uwezo wake wa kuelewa ni mdogo,anaweza kuwa hajapata chochote katika iyo barua, pili hata kama amekuelewa hawezi kuamua kitu mpaka kikubaliwe na rostam na lowassa.
 
kwa kua milango ya ikulu iko wazi hata kwa waendesha baiskeli watokao geita,nakushauri u print uipeleke mweyewe pale ikulu kwa mkuu,am sure utapokelewa tu kwa mikono miwili kam ayule jamaa mana ww una ushauri mzuri.......

wale jamaa wanapiga bwana, Atakuwa ameipata mkuu!
 
Back
Top Bottom