Rajabu Visenti
Member
- Jun 11, 2019
- 34
- 16
Ndugu Mheshimiwa Rais wetu mpendwa wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. John Pombe Joseph Magufuli,
Kabla ya yote, ninapenda kuchukua nafasi hii kukupa pole na majukumu yako ya kila siku na kukupongeza kwa utendaji wako wa kizalendo unao uonyesha katika taifa letu. Mungu azidi kukupa nguvu zaidi na moyo zaidi wa kizalendo katika kuliongoza taifa hili ili tufikie lengo letu la uchumi wa viwanda. MUNGU wetu mwenye nguvu na uweza wote azidi kukupa nguvu na maono zaidi katika kuongoza na kuliokoa taifa hili.
Ndugu Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, pia nachukua fursa hii kukuomba radhi, sikupenda, niposti hii barua ndani jukwaa hili. Nimejaribu kutumia uwezo wangu wote kutafuta mawasiliano yako lakini sikufanikiwa. Nikaona bora nitume kwa njia hii nikiwa na imani kuwa, unaweza pitia kwenye jukwa hili ukaiona barua yangu.
Ndugu mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, mimi ni kijana wako nina shahada katika fani ya mafuta na gesi. Nilihitimu mwaka 2016. Naandika barua hii ili kuomba msaada wako utusaidie ajira na mafunzo ya vitendo (internship) katika fani ya mafuta na gesi sisi vijana tulio hitimu shahada za mafuta na gesi Tanzania.
Ndugu Mheshimiwa Rais vijana tulio somea fani za mafuta na gesi tunayo hamu kubwa ya kufanya kazi kwa bidii kwenye serikali yetu ya awamu ya tano kwaajili ya maendeleo ya taifa letu kupitia sekta hii mpya ya mafuta na gesi. Tulijitahidi kusoma kwa bidii na kwa moyo ili kuhakikisha tunapata maarifa na ujuzi wa kutosha katika fani hizi ili tuweze kufanya kazi kwa ufanisi katika sekta hii. Walimu wetu nao pia walitufundisha kwa moyo sana na kwa nguvu zao zote ili kuhakikisha wanatoa vijana ambao watakua na maarifa na ujuzi kwaajili ya kusaidia taifa letu katika sekta hii mpya.
Sisi vijana tulio somea fani za mafuta na gesi tupo tayari kufanya kazi yoyote katika fani hizi tulizo somea ili tu na sisi tushiriki kusaidia serikali yetu ya awamu ya tano, katika kujenga uchumi wa viwanda kupitia sekta ya mafuta na gesi na kupitia maarifa na ujuzi tulio upata.
Ndugu Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, nakushukuru sana kwa kusoma ombi langu, nitafurahi sana kama ombi langu litakubaliwa, MUNGU akubariki sana lakini zaidi azidi kukupa uwezo, nguvu na maono mengi zaidi katika kuliongoza taifa hili.