Barua ya wazi kwa profesa tibaijuka - arusha | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Barua ya wazi kwa profesa tibaijuka - arusha

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by lodi, Jan 27, 2011.

 1. l

  lodi New Member

  #1
  Jan 27, 2011
  Joined: Oct 23, 2010
  Messages: 2
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi ,Profesa Anna Tibaijuka, sisi ni wakulima na wafugaji wa vijiji vya Kiserian, Olkerian na Nduruma, katika Kata ya Moshono na Mlangarini jijini Arusha.

  Tunakuandikia barua hii kwa masikitiko kukujulisha manyanyaso na mahangaiko tunayopata baada ya ardhi yetu tuliyorithi kutoka kwa mababu zetu zaidi ya karne moja iliyopita kunyanganywa na Jeshi la Wananchi (JWTZ),kambi ya Tanganyika packers.

  Historia ya eneo
  hili na umaarufu wake ulianza kabla ya mwaka 1942 ambapo mfugaji raia wa kigeni alipewa eneo hilo na serikali ya kikoloni wakati huo ajenge machinjio na kiwanda cha nyama tayari kusafirishwa nje ya nchi.

  Miongoni mwetu tulishiriki kazi mbalimbali katika kiwanda hicho ikiwa ni pamoja na kulisha mifugo kabla ya kuchinjwa hivyo tunafahamu fika historia ya eneo hilo na mipaka yake dhidi ya mipaka ya vijiji na makazi yetu.

  Eneo la Tanganyika Packers lina ukubwa wa ekari 113,waliposhindwa kuendesha machinjio na usafirishaji nyama ,taasisi nyingine ya HYPERLINK htt:t.a.m.tu.na/t_blank T.A.M.TU.na baadae ya udhibiti wa ndege waharibifu (bird control)iliyochukua majengo hayo kabla ya serikali kuhamishia taasisi zake hizo eneo la Tengeru na kuyaacha majengo hayo.

  Wakati wa vita vya Kagera 1978,hadi mwanzoni mwa mwaka 1981 baada ya vita,JWTZ lilipewa eneo hilo kwa ajili ya matumizi yake wakati wa vita,hii ni kwa sababu mmiliki wa majengo hayo pamoja na eneo hilo vilichukuliwa na Serikali.

  Wakati vifaa na zana za kivita za Jeshi zikiwa zimehifadhiwa hapo, sisi tulishapeleka maombi yetu Serikalini juu ya azma yetu ya kutaka kuyageuza majengo hayo kuwa madarasa na mabweni ya shule ya Sekondari au Chuo ili watoto wetu na Watanzania wengine wapate fursa ya kupata elimu hapo na eneo liliko nje lirudishwe chini ya miliki ya Serikali ya Kijiji.

  kwa bahati mbaya jeshi limetumia njia isiyo mwafaka walipong'ang'ania kubaki na kupora ardhi hiyo licha ya Raisi wa wakati huo,Mwalimu julius Nyerere,kuwataka kuhama katika eneo hilo ambalo ni makazi ya wanavijiji na kurudi kambini kwao au watafutiwe sehemu nyingine ya kuhifadhi vifaa vyao.

  Baada ya kuchukua eneo hilo lenye ukubwa wa ekari 113, Jeshi halikuridhika , sasa limeweka alama zake hadi katikati ya makazi yetu,na kuna taarifa za sisi na watoto wetu kuhamishwa hadi kusikojulikana.

  Mwishoni mwa mwaka jana,Idara ya Ardhi Halmashauri ya Arusha,ilipima na kutathmini ardhi na mali zetu zikiwamo nyumba na wengine kukatazwa kufanya shughuli yoyote inayotupatia kipato kama kilimo kwa madai kuwa serikali inahitaji eneo hilo.

  Profesa Tibaijuka ,sisi wananchi wa maeneo yetu,kwa kusogeza huduma za maji,shule za msingi na sekondarori,zahanati,makanisa na msikiti,je nani atafaidi juhudi zetu hizi ?

  Sasa hivi tunahangaika,hatuna chakula,hatujui hatma yetu,tumelalamika kwa muda mrefu hakuna anayesikiliza kilio chetu,malalamiko yetu yamepitia ngazi zote tangu kijiji hadi ofisi ya Mkuu wa mkoa wa Arusha,lakini hakuna hatua yoyote iliyochukuliwa.

  Mbunge wetu wa wakati huo Elisa Mollel,alishawasilisha tatizo hili bungeni ambapo Waziri wa Ulinzi,Hussein Mwinyi,alitangaza kuwa wananchi wakae katika maeneo yao na jeshi libaki katika majengo ya Tanganyika Packers,lakini hali haijawa hivyo.

  Ndio maana tumekuandikia barua hii kwa kuwa dhamira na jitihada zako ni kushughulikia matatizo ya ardhi katika maeneo mbalimbali nchini.

  Ndio maana tumekuandikia barua hii kwa kuwa dhamira na jitihada zako ni kushughulikia matatizo ya ardhi katika maeneo mblimbali nchini.

  hatutaki kuamini kuwa serikali yetu sio sikivu hata isiwasikilize wananchi wake katika matatizo kama haya yanayoathiri maisha kutokana na kukosa mahali pa kujitafutia kipato halali baada ya ardhi ambayo ndio rasilimali yenye thamani kubwa kunyanganywa.

  Kwa kuwa kuna utawala wa haki wa sheria, tunaomba wewe mwenyewe uje katika vijiji hivi,utusikilize tukueleze bayana kuhusu mgogoro huu kati yetu na JWTZ ili mwenye haki ya kubaki katika eneo hili aptiwe haki hiyo, hatutaki kuwa Wakimbizi katika nchi ya babu na bibi zetu.

  Mwisho tunakuomba utumie busara zako katika kushughulikia mgogoro hu ili tuendelee kuishi kwa amani katika nchi yetu.

  MUNGU IBARIKI TANZANIA.

  Ni sisi wananchi wa Olkerian,Kiserian na Nduruma Mkoa wa Arusha.
   
Loading...