Shark
JF-Expert Member
- Jan 25, 2010
- 29,455
- 29,134
Ndugu Waziri
Mimi ni mmojawapo ya wamiliki wa viwanja vilivyopimwa na kugawiwa na Serikali, kilichopo kitalu (block) namba 10. Mradi huu wa viwanja vya serikali, kama ilivyo miradi mingine ya aina hii inatakiwa ipatiwe miundombinu yote kama Umeme, maji na barabara na Serikali yako, ambayo gharama zake hufidiwa katika gharama za maombi ambayo mmiliki wa kiwanja analipa wakati wa kuomba hapo mwanzo.
Hali iliyopo kibada kwa sasa inasikitisha kwa kweli ambapo Miundombinu ya Barabara na Umeme imewekwa kwa upendeleo/ubaguzi ikiishia kitalu (block) namba sita tu, tena upande mmoja tu wa kulia mwa barabara na kuicha sehemu zingine zikibaki bila miundombinu hii muhimu, hapo maji pia ndio hakuna kabisa. Hatuelewi kwanini mkandarasi wa Wizara/manispaa ameamua kuishia katikati ya kazi wakati viwanja hivi vilipimwa na kuuzwa kwa pamoja.
Kwa upande wa barabara, Hali hii inasababisha watu kuendelea kutumia njia za zamani ambazo zinapita kwenye viwanja vya watu ambao hawajaanza kujenga wakisubiri miundombinu iletwe. Njia hizi ambazo zinapita viwanjani mwa watu nyingi zina michanga hivyo hazipitiki kwa urahisi, huku wengine tukiingia kwnye matatizo na majirani zetu pale unapoamua kuziba njia ili uanze ujenzi. Hii inasababisha eneo lionekane kama "skwata", wakati kiukweli kama miundombinu yote ikipelekwa na pakajengwa pale, itakua ni mojawapo ya maeneo ambayo yanavutia kwa jiji la dar es salaam.
Kwa upande wa Umeme, inatupasa tufunge solar au jenereta hata kwa kwa eneo ambalo umeme haupo mbali sana na barabara, tuseme nusu kilometa kwani nguzo za umeme pamoja na usambazaji wake ambao ulitakiwa ufanywe na serikali haujafanyika. Ujenzi unaoendelea kibada ni wa nyumba za kisasa ambazo mchana zinavutia sana pamoja na uchache wake, lakini usiku ni hatari kwani nyumba ziko mbalimbali sana kwa kua wamiliki wengi wa viwanja wamegoma kuendelea na ujenzi kusubiri huo umeme na barabara ziwekwe ambao hatujui ni lini.
Hii inarudisha nyuma maendeleo ya eneo hili, ambapo eneo la pori ambalo halijajengwa ni kubwa kuliko eneo lililojenwa/endelezwa. Watu watabaki kuuziana tu viwanja kutoka umiliki wa mmoja kwenda kwa mwingine bila mtu kufikiria kujenga sababu ya eneo hilo kutelekezwa na serikali.
Naandika barua hii kukuomba uliangalie hili suala, ikiwezekana basi magari makubwa ya kuchonga barabara yapelekwe eneo hilo baada ya block 6 ili kutengeneza barabara za mitaani wakati unafanya juhudi kuwasiliana na Waziri muhusika wa mambo ya umeme Prof. Sospeter Muhongo ili aweke miundombinu ya umeme watu tuanze Ujenzi.
Natumai barua yangu hii utaipata na kuifanyia kazi ipasavyo na kwa muda muafaka.
Nakala kwa: Halima Mdee (Waziri Kivuli - Nyumba na Maendeleo ya Makazi)
Wako, Shark
YAH: UCHONGAJI WA BARABARA ZA MITAA - KIBADA
Husika na kichwa cha habari hapo juu, Natumai u-mzima wa afya, na unaendelea vizuri na shughuli zako za kila siku za ujenzi wa taifa katika madaraka na majukumu yako kama Waziri wa Nyumba na Maendeleo ya Makazi.

Last edited by a moderator: