Barua ya wazi kwa Mzee Bakhresa, Gharib wa GSM na Mo Dewji: Wakati mkiwekeza katika michezo, isaidieni jamii pia kwenye mambo mengine ya maana

Missile of the Nation

JF-Expert Member
May 24, 2018
13,498
51,092
Ndugu Gharib, Mzee Bakhresa na Mo Dewji

Amani ya Mwenyezi Mungu iwe nanyi

Nichukue fursa hii kukupongezeni kwa jitihada zenu za kuinua michezo, hakika uwekezaji wenu utasaidia kuinua michezo nchini, kutoa ajira kwa vijana wetu wanaoshiriki ligi n. k

Lakini pamoja na hayo, naomba niongee na nyie mambo yafuatayo:

1. Hebu sasa isaidieni jamii kuwekeza kwenye mambo mengine ya msingi zaidi

Siwapangii namna ya kutumia pesa zenu, lakini je mnalionaje wazo la nyinyi kusaidia mambo ya maana zaidi kuliko hii mipiramipira?, Kwa mfano mnaonaje mkitengeneza makampuni ya uwezeshaji vijana wetu kwa kufinance startups zao?, kutengeneza funds mbalimbali za kusidia wenye uhitaji kama vile Yatima, Vikongwe n. k?

2. Saidieni Waislamu wajinyanyue kielimu

Nyinyi ni matajiri wa kiislamu, na jamii ya waislamu wenzenu iko nyuma sana kielimu, Takwimu zinaonyesha wazi katika madhehebu ya dini yanayoongoza kwa umiliki mdogo wa shule na mifumo ya huduma za jamii ni Waislamu, pia wako wachache vyuoni na katika ajira rasmi za serikali. Sasa nyie kama waislamu mliobarikiwa, Mnawasaidiaje Waislamu wenzenu kujikwamua kielimu?
Maana naona mipesa mingi mnaiingiza katika mpira. Je, vipi Waislamu wenzenu mnawasaidiaje? Na nyie tengenezeni Ahera yenu, pamoja na kuwekeza katika hii "michezomichezo" ya duniani, hebu wekezeni na ahera kwa kuinua waislamu wenzenu!

3. Ongezeni investment katika nyanja zinazoweza kutoa ajira zaidi kwa wananchi wa chini

Sina wasiwasi na uzalendo wenu, lakini naamini mna potential ya kuinvest kwenye sekta zinazoweza kugusa maisha ya wananchi wetu wengi, hii mipesa mnayomwaga kwenye mpira, kwanini msifikirie pia kufanya kilimo, tena kufanya kilimo. kwa kulenga watu wetu masikini? What if msianze kutafutia watu wetu masoko huko nje? What if msiweke dhamira ya kupanua ununuzi wa mazao ya wakulima zaidi? Nafahamu kuwa Mzee Bakhresa na Mo wanafanya kilimo ktk hatua kadha wa kadha, lakini hapa nazungumzia kilimo strategic kwa ajili ya kuwainua wakulima wadogowadogo na kutia ajira kwa vijana wetu.

Mwisho kabisa ningependa kumalizia kwa kusema kuwa, SIWAPANGII namna ya KUTUMIA PESA YENU lakini mimi kama mwanadamu na Mtanzania naona kuwa wakati mkiwekeza kwenye Mpira mbona hamuwekezi na kwenye mambo mengine ya maana zaidi kuliko mpira?

Ziko wapi universities, Au State of art schools, Au hospitali za maana mnazojenga nchini?

Ziko wapi investments za kumuinua mtu wa chini kwa kumjengea capacity?

Na pia mbona hamuinvest vya kutosha kusaidia waislamu wenzenu kielimu na kiuchumi?

Hayo tu!

Assalam aleikum
 
Mo mbona kawekeza sana na katoa ajira nyingi sana maana anatengeneza hadi viberiti au pia bakhresa nae ana viwanda vingi tu na ametoa ajira nyingi sana labda mtoa thread niambie kwani mambo mengine ni yapi apo maana haiwezekn wao waguse nyanja zote maana wale ni wafanyabiashara faida kwanza.
 
Ahera ni muhimu sana kuliko dunia
Mkuu, kama biblia inatambua dini ni yakweli ni ya kusaidia mayatima, kusaidia wajane, kutembelea wafungwa, kutenda matendo mema lakini haijaweka exactly dini ni ipi siwezi bishana na wewe ambaye unaamini kwamba dini yenu ni muhimu kuliko nyingine.

Naomba niseme hivi, jitahidi sana tena sana. Unapokuza vijana wako au tunapokuza vijana wetu ijapokuwa tunahitaji walelewe ndani ya dini ila tujitahidi sana tena sana waipate elimu pia ya Duniani kwa wingi itaondoa tabaka la fikra isiyo angavu.
 
Back
Top Bottom