Barua ya wazi kwa mweshimiwa Dr Slaa na Rev Mtikila | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Barua ya wazi kwa mweshimiwa Dr Slaa na Rev Mtikila

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by rosemarie, Jun 14, 2011.

 1. rosemarie

  rosemarie JF-Expert Member

  #1
  Jun 14, 2011
  Joined: Mar 22, 2011
  Messages: 6,767
  Likes Received: 1,023
  Trophy Points: 280
  Tuna kama mwezi mzima tangu shutuma juu ya ridwan kikwete au mtoto wa rais
  Kuwekwa hadharani na nyie viongozi wakuu kabisa wa upinzani,

  Mnakumbuka mlitutangazia watanzania kuhusu hali halisi ya mtoto wa rais anavyotumia mamlaka au mgongo wa baba yake kwa kujitajirisha na mali za ufisadi.
  Mimi binafsi nilipenda sana kujua nini hatma ya hizi shutuma kwani limekuwa ni jambo la kawaida viongozi kutumia madaraka yao kuwanufaisha ndugu,jamaa,marafiki,na sasa watoto,
  Kwa kweli watanzania tulihuzunishwa mno na hali ile hasa ikizingatia taifa letu lipo katika hali mbaya ya viongozi kutumia ikulu yetu takatifu kujinufaisha,

  Kwa kuwa mtoto wa rais alitoa siku saba kwa nyie waheshimiwa kumwomba radhi au msipofanya hivyo atafungua kesi mahakamani,
  Kwa kuwa siku saba zimeisha na mmekataa kumwomba radhi,
  Kwa kuwa anajua kabisa mmekataa kumwomba radhi na hachukui hatua yoyote,

  Naomba kwa niaba ya watanzania wenzangu tunaoitakia mema nchi yetu mfanye yafuatayo:

  Watanzania tunawaomba mpelekeni mahakamani Yule kijana ili tuweze kujua hali halisi
  • Kwa kufanya vile mahakama itawaeleza watanzania kuhusu ukweli wa jambo hili
  • Kwa kumpeleka mahakamani ni dhairi ameshindwa kuwapeleka ninyi mahakamani na tafsiri yake ni kwamba hajui asemalo,
  • Na inatuonyesha jinsi huyo kijani alivyopoteza fedha zetu kwa kusomeshwa sheria na kutokujua kuitumia sheria
  Waheshiwa kama hamna muda wa kufanya hivyo sisi tupo tayari kumpeleka mahakamani, tunaitaji vithibitisho vyenu ambavyo ni ushaidi,mkiweza kunipa ushaidi mimi binafsi nitampeleka mbele ya vyombo vya sheria,
  Naomba sana msiendelee kukaa kimya, yeye ameshindwa kuchukua hatua labda kwa kuona hizo shutuma zina ukweli ndani yake.

  Imetumwa kwa:Dr Slaa slaa@chadema.or.tz
  Imetumwa kwa Rev Mtikila dp- watanganyika@yahoo.com
  From- rosemarykimaro@gmail.com
   
 2. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #2
  Jun 14, 2011
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Ni vizuri kuwakumbusha maana inawezekana kuwa wamesahau kutokana na kazi nyingi. Naamini kuwa mambo kama haya ni ya kuyshikia bango mpaka mwisho wake ili kupata kile wanachokitarajia. kama wakiwa wanasema tu hivihivi na kuyaacha tu hivihivi, watu wataona kama wanapiga siasa
   
 3. luvcyna

  luvcyna JF-Expert Member

  #3
  Jun 14, 2011
  Joined: Feb 24, 2009
  Messages: 1,441
  Likes Received: 1,034
  Trophy Points: 280
  Dada yangu huo ndio tunaita Uzalendo.. siku nyingi nilikuwa najiuliza ni vipi nikitaka kuchukua hataua kwa ushahidi huu mdogo nilionao. Kuna vitu anavyovifanya huyu bwana mdogo vinatia huzuni mno. Na hapo ndipo nilianza kuamini kauli ya Director wangu, "Umasikini wa Mtanzania hautaisha kirahisi kwa mfumo tulionao kwani ni kitu kichokuwa Planned na viongozi wa nchi." Umasikini umeplaniwa na viongozi? Jibu ninalopata hapa ni ili maslahi yao yazidi kudumu.

  Kuna machache nikijaribu kuyatizama yanayomhusu huyu bwana nadhani ingekuwa kwa nchi inayosimamia sheria na haki nisingesita hata kidogo kuyavalia njuga..niliwahi kwenda Mbozi mwaka jana kikazi, ndipo nikakutana na kampuni moja ya usafirishaji ambapo baada ya kufatilia kwa undani zaidi nikagundua mmiliki ni huyu bwana mdogo..kwa kifupi ubadhirifu wa fedha unaofanywa na hii kampuni unakuja hasa pale ambapo wizara ya kilimo inapoiundia au kuiandalia mazingira ya kupata zabuni (tenda) za usafirishaji pasipo hata kuwepo na ulazima wa kufanya hivyo. Nitatoa case moja, katika uhamishaji wa chakula kinachohifadhiwa katika maghala ya chakula ya Taifa kutoka kanda moja kwenda nyingine. Utaratibu ambao hufanyika inapotokea uzalishaji wa chakula katika kanda kuwa hafifu hivyo kulazimu kuhamishiwa chakula hicho toka kanda yenye uzalishaji mkubwa. Katika msimu wa chakula wa mwaka 2010, uhamishwaji huu ambao ninaamini haukuwa wa lazima kwani wakati huo kwa kanda ya kaskazini kulikuwa na uzalishaji mkubwa lakini kampuni hii ikapewa tender ya kuhamisha chakula kutoka kanda ya kusini na kisha kulipwa ma bilioni ya fedha kwa tani zilizohamishwa. Kwa hali ya kawaida gharama ya kusafirisha kilo moja ingeweza kununua kilo tatu zaidi katika kanda ya juu ambapo wakulima walikuwa wakiiomba serikali inunue mazao yao bila kusikilizwa na kuambulia ahadi za changa la macho kwa kununuliwa kiasi kidogo ili kura zao zisipotee wakati wa uchaguzi huku chakula kikiendela kuhamishwa kwa gharama kubwa ilihali wakulima wakiachwa solemba na mazao yao.

  Sasa swali linakuja katika juhudi hizi za kuzishughulikia tuhuma kama hizi. ni wapi pa kupata sapoti? mfumo wa mahakama hizi elekezi utakunusuru kweli?vp hawa wa usalama wa taifa wanaofata maagizo, tutasalimika kweli wakigundua kuna harakati za namna hiyo?
   
 4. NATA

  NATA JF-Expert Member

  #4
  Jun 14, 2011
  Joined: May 10, 2007
  Messages: 4,516
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  Watanganyika kwa siasa hawajambo kunawengine walitoa masaa 48 kwa mkuu cjui hao pia wameishia wapi.
   
 5. F

  FUSO JF-Expert Member

  #5
  Jun 14, 2011
  Joined: Nov 19, 2010
  Messages: 11,860
  Likes Received: 2,338
  Trophy Points: 280
  Alitoa siku saba, mwambe aende mahakamani. asipoenda sisi wananchi tunajua yote yaliyosemwa juu yake ni ya kweli na ndivyo tunavyoamini as of now.
   
 6. Shark

  Shark JF-Expert Member

  #6
  Jun 14, 2011
  Joined: Jan 25, 2010
  Messages: 20,105
  Likes Received: 7,359
  Trophy Points: 280
  Nyie mtakua mmetumwa tu, tena na nape,
  mnataka kujua nguvu, point, ushahid wa upinzani ukoje ili mjipange jins ya kuchomoka.
  Riz1 ashaitwa fisadi, yeye ndo wa kwenda mahakamani kama anaona amesingiziwa.
  Vingapi vina ushahidi wa wazi kama kagoda, deep green n.k na hakuna lililofanyika?
   
 7. jogi

  jogi JF-Expert Member

  #7
  Jun 14, 2011
  Joined: Sep 25, 2010
  Messages: 19,335
  Likes Received: 12,801
  Trophy Points: 280
  tuliambiwa kikwata asipowataja wauza unga tumdharau. nielewe tumdharau kikwata, KIKWATA=BAISKELI YA MBAO haina nyororo wala pedeli, na hii ndiyo jinsi ya kumdharau, AKITOA AHADI MSIMSADIKI, AKIWAALIKA MSIHUDHURIE, AKIWATUMA ZINGATIENI KATIBA, SHERIA ZA NCHI/SHERIA YA MAUMBILE NA UTAIFA KATIKA KUTEKELEZA WAJIBU WENU, mpotosheni kadri muwezavyo, akisema ovyo msifieni huku mkimng’ong’a, AKIWAOMBEA KURA WAGOMBEA WANYIMENI HATA NAFASI YA KUCHAKACHUA, AKISTAAFU MPANDISHENI KIZIMBANI PAMOJA NA MASHTAKA MENGINE, KULIHUJUMU TAIFA, KUIFILISI TANZANIA, KUPANDA MBEGU ZA UDINI NA KUZIMWAGILIA MAJI ZIKUE, KUTUMIA MADARAKA YAKE VIBAYA, MSISAHAU KUMFILISI YEYE NA FAMILIA YAKE.
   
 8. mgen

  mgen JF-Expert Member

  #8
  Jun 14, 2011
  Joined: Nov 18, 2010
  Messages: 15,162
  Likes Received: 1,893
  Trophy Points: 280
  Uko nchi gani!Mbona kupitia mjengoni ameshataja, mchungaji mwenye jina la kinaijeria, na kanisa lake! mpaka mama cline amempongeza anavyoendesha hiyo vita, laah!
   
 9. saitama_kein

  saitama_kein JF-Expert Member

  #9
  Jun 14, 2011
  Joined: Oct 29, 2009
  Messages: 982
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  Mahakamani zetu za bongo kweli haki inapatika?? Kitendawili...............
   
 10. Mohammed Shossi

  Mohammed Shossi Verified User

  #10
  Jun 14, 2011
  Joined: Jan 17, 2011
  Messages: 3,986
  Likes Received: 123
  Trophy Points: 160
  Hapo kwenye red wao wenyewe wangekuwa navyo wasingebwabwaja kijana ni mhangaikaji haina maana kuwa mtoto wa Rais basi usihangaike kwani huyo Rais ana mtoto mmoja tu? mbona wapo wengine wa kiume lakini hawana huo utajiri? yaani wewe ulitaka Riz1 awe sawa na wewe? kumbuka hata vidole havilingani ndio maana Miraji Kikwete halingani na Riz1 Kikwete.

  Ushauri kwa uliowaandikia hiyo barua ya wazi ni kuwa tumechoka kusikia huyu fisadi na yule msafi! tunataka watangaze sera zao tuzijue ili ambao hatuna vyama tuweze kuambua kuweka turufu zetu kwao. Maana kama mimi binafsi mtu akiniuliza sera za cdm nitamwambia kutaja list ya wanaotuhumiwa ufisadi, kugomea vikao (sometimes) na kuandamana. Sijui wewe mwandishi wa barua ya wazi unazijua sera za chama?
   
 11. kifrogi

  kifrogi Member

  #11
  Jun 14, 2011
  Joined: Jun 8, 2011
  Messages: 42
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wamesahau.
   
 12. Sooth

  Sooth JF-Expert Member

  #12
  Jun 14, 2011
  Joined: Apr 27, 2009
  Messages: 3,773
  Likes Received: 4,494
  Trophy Points: 280
  CDM is presently the leading opposition party. Get over it! Get used to it!
   
 13. X

  XWY BOYZ Member

  #13
  Jun 14, 2011
  Joined: Jun 12, 2011
  Messages: 8
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Sioni sababu ya dr kuwapeleka mahakaman, kwa kuwa anaehukumu kesi ni mteuliwa wa babake (kesi ya mifupa usiipeleke kwa fisi). Dr tutangazie uma tutumie nguvu zetu kuwachomoa hao nya*n, inauma saana kiongoz wa juu kutuhumiwa afu ushindwe kujitetea
   
 14. Echolima

  Echolima JF-Expert Member

  #14
  Jun 14, 2011
  Joined: Oct 28, 2007
  Messages: 3,169
  Likes Received: 531
  Trophy Points: 280
  Hao walioandika hiyo barua ya wazi wametumwa Kama alishindwa kuwapeleka mahakamani yeye huyo aliyeahidi kuwapeleka basi walioandika hiyo barua wampeleke mahakamani kwa ushahidi wao wenyewe na wasiombe kwa DR.
  Kama kweli wana uchungu na Uzalendo kwa nini wasione uchungu kwa mikataba mibovu NK???
   
Loading...