Barua ya wazi kwa Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe: CHADEMA Isikubali kuonewa

Unaweza kuwa sahihi kuhusu Mbowe, lakini sijasikia hao wengine wa vyama ulivyotaja wakikoswakoswa na risasi za polisi wala kupelekwa Segerea.

Hii inaonyesha ufikri wako una kasoro, hata kama unajihisi uko huru kama ulivyoeleza mwanzo.

Naona huna tofauti na hawa wanasiasa unaowalalamikia, kwa sababu mambo yao ni sawa na haya yako, ya kukana kwamba hawapo kama unavyowaelezea wewe.
Kwenye maisha kila mtu ana power ya kurisk anavyoweza.

The more the risks, the more the rewards.

Mnyika wa 2010 siyo Mnyika wa 2020. Sasa hivi ni tajiri, hayuko tayari kufia uwanja wa mapambano wakati ameshapata maisha.

Zitto wa 2005 siyo Zitto wa 2020, sasa hivi ni tajiri na ana familia. Anachukua risks kwa tahadhali siyo kama enzi hizo.

Mbowe anaijua nguvu ya Dola, anajitahidi sana kufanya marishiano ya tahadhali ili aendelee kunufaika.

Mwaka 2010-2015, CDM ilikuwa inapata zaidibya 300M kila mwezi kwa miaka 5.

Mwaka 2015-2020, CDM imechuma 450M kila mwezi kwa miaka 5 ambazo ni kodi za Walalahoi bila JASHO.

Kwanini Mbowe asikipambanie chama chake kwa manufaa yake. Hata Mrema ambaye mara kibao yuko kwenye majukwaa ya CCM hawezi kutekeleza chama chake.

Mboww hawezi kurushiwa risasi eti kwasababu anapambania vijana hawana AJIRA, watu wamedhulumiwa ARDHI, KODI au wanawake hawana MAJI.

Ukioona anapambania kitu katikati ya hatari ya risasi ni lazima itakuwa inahusu MASLAHI yake kama Masuala ya UCHAGUZI kuporwa, kunyimwa fomu za Kugombea au Mikutano yake ya kisiasa KUZUIWA.

Kama wanasiasa wanacyoangalia mambo yao, sioni sababu ya mtu mwingine yoyote na yeye kutoangalia mambo yake.
 
Ndugu Freeman!
Mara nyingi umesikika ukitaka sana siasa za uungwana, siasa za akupigaye shavu la kushoto basi mgeuzie la kulia. Hilo ni jambo zuri lakini hiyo falsafa yako inafanya kazi katika nchi za watawala ambao ni sober minded, siyo katika nchi ambayo watawala wameamua liwalo na liwe kwenye kusimika mifumo ya dhulma, uonevu ukandamizaji na kufanya lolote ilimradi waendelee kubaki madarakani hata kama si kwa ridhaa za wananchi.

Ndugu Mbowe
Tone yako ya kupenda maridhiano watawala wanaitafsiri kama uoga.

Huu uonevu mnaofanyiwa na watawala wa kunyimwa haki zenu za kufanya siasa kinyume cha katiba mtaendelea kufanyiwa mpaka siku mtakapoamua kusema sasa inatosha!

Ndugu Mbowe, Huu ni muda sasa wa kuvunja confidence hii ya watawala ambayo kimsingi wameshajiaminisha kuwa hamna uwezo, wala guts za kufanya chochote. Hii chain mkiifanikiwa kuivunja mtakuwa katika position nzuri za kuadvance haki zenu za kisiasa nchini.

Huu ni muda muafaka wa kuraise stake katika utawala wa nchi hii ili waone kuwa kutawala kinyume cha sheria na katiba ni kitu chenye gharama, kwa hiyo lazima ufanye yafuatayo:

1. Ni muda muafaka sasa wewe kuhimiza Wafuasi wako wasitii maagizo batili
Toa maagizo yako kwenye machinery nzima ya chama chako, Viongozi na wanachama wa chama chako wasitii maagizo haramu ya watawala katika maeneo yao. Kwa mfano kama Wamezuia mikutano, wewe waagize wafanye mikutano. Wewe usijali wala kuhofu maagizo yako yatafanyiwa kazi kwa kiwango gani, lakini wewe toa agizo la kichama, vikao na mikutano ifanyike. Katika hili kuna watakaofanikiwa kufanya hiyo mikutano kuna watakaoshindwa kwa sababu mbalimbali, lakini ni lazima tuvunje hii chain ya utii haramu wa maagizo haramu yaliyo kinyume cha sheria

2. Ni lazima CHADEMA iendelee kuwin huruma ya wananchi
Haya matendo mnayofanyiwa ya uonevu na ukandamizaji, wananchi wanayaona. Sasa ni muda muafaka wa kuyadocument vizuri, kuyaamplify ili wananchi wengi wayaone. Uonevu ambao watawala wanawafanyia kama mtaweza kuwashitakia, uungwaji mkono utakuwa ni mkubwa, na utaendekea kukua siku baada ya siku

3. Ndugu Mbowe ni muda wa Uongozi wa CHADEMA kusacrifice zaidi
Ndugu Mbowe, kama nilivyokueleza huko juu, kuna ulazima wa kuvunja chain hii ya uonevu, hili halitifanyika bila uongozi wa CHADEMA kujitoa mhanga(kusacrifice), Ni lazima uongozi wa CHADEMA uitishe mikutano ya wazi ambayo ni ya haki kisheria, ikizuiwa kinyume cha sheria Viongozi wa CHADEMA wasitii, Kubalini kusacrifice hata Jela lakini haki yenu kama Chama muipate. Na hii mikutano isiwe one day event, itisheni hii mikutano mara kwa mara mpaka watawala waone kuwa gharama za kupambana na CHADEMA ni kubwa kuliko kutenda haki.

Ndugu Mbowe, Hii chain ya nyie kuonewa hamtaivunja mpaka msacrifice, muwe tayari kwenda jela kwa ajili ya course hiyo

4. Ni lazima CHADEMA itumie fursa za serikali ya CCM kuboronga kwenye uchumi ili kuvuna sapoti ya wananchi
Ndugu Mbowe, Kimsingi, CCM wanajua measures zao za kiuchumi ni unpopular kwa wananchi, pia wanajua legitimacy yao ya kisiasa kwa wananchi ni ndogo sana, kwa hiyo wanachokifanya ni kujaribu kwa nguvu zote kuweka ukuta baina yenu na wananchi ili msiwape hao watawala kibano cha kisiasa. Ni lazima message yenu sasa muiegemeze katika ugumu wa maisha ambayo wananchi wanapitia na kwenye fact kuwa tumefika hapa kwa sababu ya utawaka mbovu wa CCM na wananchi hawana wawakilishi waliotokana na ridhaa zao. Tumieni kila opportunity, tengenezeni talking points za matatizo ya kiuchumi muzisambaze hadi huko chini kwa viongozi wenu wa ngazi za chini ili waweze kuwaeleza wananchi kwa ufasaha kabisa madhila ya utawala wa CCM kwenye maisha yao, na namna CCM inavyopekekea wao kuwa na maisha Magumu

5. Ni muda muafaka wa kumuomba kila mwanachadema afanye kazi ya kusambaza ujumbe wa Chama
Ndugu Mbowe, CCM wanadhani wanaweza kudhibiti moto wa CHADEMA kwa kuthibiti uongozi ambao uko structured, kwamba wakidhibiti let say viongozi wa matawi, mashina, kanda na viongozi Taifa basi wataweza kukithibiti Chama. Sasa ni muda muafaka wa Chadema kutoa muongozo kwa kila mwanachama na shabiki na Chadema kufanya kazi za chama za kusambaza jumbe na sera za chama. Agiza kila mtu, afikishe ujumbe na sera za chama kwa marafiki, kwa majirani n. k. Yaani kwenye suala la kusambaza jumbe za CHAMA isiwe muda wote centralized bali nyakati kama hizi ngumu mnazozuiwa kuorganise iwe ni decentralized. Hii itawezesha ujumbe kufika pale ambapo watawala hawataki mfike!

6. Ni lazima kuionyesha sura halisu ya Rais Samia, ajulikane kabisa kuwa naye anaenjoy "urahisi wa Udikteta" na anachukia "ugumu wa demokrasia"
Demokrasia siyo kazi nyepesi, inahitaji kutumia akili zaidi, kujizuia zaidi, kuwa na subira zaidi, maridhiano zaidi. Sasa hayo ni mambo magumu kuliko udikteta ambao madikteta hawataki kuumiza kichwa sana kwenye utawala, wao wanataka kutumia miguvuguvu tu
Sasa Samia inaonekana kabisa anataka kufuata njia za Mtangulizi wake, hataki tabu, anataka kutawala kwa mteremko. Lakini wakati huohuo anataka kuudanganya ulimwengu kuwa yeye ni mwanademokrasia, Hataki kuitwa "DICTATOR". Sasa CHADEMA isikubali kumpa hii blank cheque, kama anafanya Udikteta aitwe dikteta, asakamwe kwa udikteta wake.
Na hapa naungana na John Heche, Acheni kumuita Samia MAMA. hii inampa soft power, na moral authority ambayo connotation ya mama inabeba. Kiufupi kama anavunja katiba ya nchi basi haistahili kuendelea kutumia hilo jina mama, muiteni kwa jina lake halisi, kama ni dikteta basi aitwe Dikteta.

7. Madai ya Katiba mpya ni turufu inayopaswa kutumika kwa nguvu zote
Ndugu Freeman, katika vitu ambavyo wananchi wengi wanakubali, bila kujali mirengo yao ya kisiasa ni katiba mpya. Hii ni turufu kubwa ambayo hata CCM wanashindwa waihandle vipi. Sasa ni muhimu sana nyie kuiframe agenda hii kuwa ni kwa ajili ya masilahi ya wananchi zaidi, katika kufanya hivyo nashauri nyie kama chama mkae muandae points za namna gani Katiba mpya inagusa maisha ya watu moja kwa moja. Hizi talk points zisambazwe kwa makada wenu wote nchi nzima. Lengo hapa ni kuondoa ile spin kuwa nyie mnapigania katiba mpya kwa ajili ya madaraka tu.

Elezeni faida za bunge na mahakama huru, elezeni katiba mpya inapambanaje na ufisadi, elezeni katiba mpya ina uhusiano gani na maji yao, elimu ya, afya yao. Namna hii mtaweza kuwashawishi wananchi wawe active zaidi na zaidi katika kuidai na kuilszimisha serikali ya CCM ilete hiyo katiba mpya. Msiishie tu kuzungumzia ishu ya tume huru ya uchaguzi na madaraka ya rais jinsi yasivyo fair bali onyesheni jinsi vitu hivyo vinavyopelekea maisha ya watu kuwa magumu zaidi.

Mwisho kabisa ndugu Mbowe napenda kukwambia kuwa sasa ni muda muafaka wa kuraise joto la kisiasa nchini, lipandisheni kwa kugomea amri haramu. Fanyeni mikutano hata kama imezuiwa kinyume cha sheria. Hawa hawana mabomu, wala askari wa kutosha wa kuweza kupambana na HAKI

Chairman, mmeonewa kiasi cha kutosha, mmenyanyaswa kiasi cha kutoshao sasa fanya jambo, tumechoka!
Duh! The voice of the oppressed - the lumpen proletarian. We have nothing to lose but our chains. Excellent advise.
 
Kwenye maisha kila mtu ana power ya kurisk anavyoweza.

The more the risks, the more the rewards.

Mnyika wa 2010 siyo Mnyika wa 2020. Sasa hivi ni tajiri, hayuko tayari kufia uwanja wa mapambano wakati ameshapata maisha.

Zitto wa 2005 siyo Zitto wa 2020, sasa hivi ni tajiri na ana familia. Anachukua risks kwa tahadhali siyo kama enzi hizo.

Mbowe anaijua nguvu ya Dola, anajitahidi sana kufanya marishiano ya tahadhali ili aendelee kunufaika.

Mwaka 2010-2015, CDM ilikuwa inapata zaidibya 300M kila mwezi kwa miaka 5.

Mwaka 2015-2020, CDM imechuma 450M kila mwezi kwa miaka 5 ambazo ni kodi za Walalahoi bila JASHO.

Kwanini Mbowe asikipambanie chama chake kwa manufaa yake. Hata Mrema ambaye mara kibao yuko kwenye majukwaa ya CCM hawezi kutekeleza chama chake.

Mboww hawezi kurushiwa risasi eti kwasababu anapambania vijana hawana AJIRA, watu wamedhulumiwa ARDHI, KODI au wanawake hawana MAJI.

Ukioona anapambania kitu katikati ya hatari ya risasi ni lazima itakuwa inahusu MASLAHI yake kama Masuala ya UCHAGUZI kuporwa, kunyimwa fomu za Kugombea au Mikutano yake ya kisiasa KUZUIWA.

Kama wanasiasa wanacyoangalia mambo yao, sioni sababu ya mtu mwingine yoyote na yeye kutoangalia mambo yake.
Itabidi nikujibu, lakini siyo sasa.
Ulichoelezea hapa ndio makosa makubwa yanayofanyika na sasa ndio imekubalika kwamba ndiyo siasa.Pamoja na kukubaliana na wewe kwamba watu wanaojitambulisha kuwa wanasiasa Tanzania kwamba msukumo wao ni hayo manufaa unayoyaelezea, lakini sikubali kwamba kila anayeingia kwenye siasa msukumo ni kunufaika binafsi.

Akina Nyerer hawakusukumwa na hayo unayoyaeleza hapa. Ninakushangaa sana kwamba haya ndiyo mategemeo yako kwa wanasiasa.

Ngoja nikuache kwanza.
 
Kwenye maisha kila mtu ana power ya kurisk anavyoweza.

The more the risks, the more the rewards.

Mnyika wa 2010 siyo Mnyika wa 2020. Sasa hivi ni tajiri, hayuko tayari kufia uwanja wa mapambano wakati ameshapata maisha.

Zitto wa 2005 siyo Zitto wa 2020, sasa hivi ni tajiri na ana familia. Anachukua risks kwa tahadhali siyo kama enzi hizo.

Mbowe anaijua nguvu ya Dola, anajitahidi sana kufanya marishiano ya tahadhali ili aendelee kunufaika.

Mwaka 2010-2015, CDM ilikuwa inapata zaidibya 300M kila mwezi kwa miaka 5.

Mwaka 2015-2020, CDM imechuma 450M kila mwezi kwa miaka 5 ambazo ni kodi za Walalahoi bila JASHO.

Kwanini Mbowe asikipambanie chama chake kwa manufaa yake. Hata Mrema ambaye mara kibao yuko kwenye majukwaa ya CCM hawezi kutekeleza chama chake.

Mboww hawezi kurushiwa risasi eti kwasababu anapambania vijana hawana AJIRA, watu wamedhulumiwa ARDHI, KODI au wanawake hawana MAJI.

Ukioona anapambania kitu katikati ya hatari ya risasi ni lazima itakuwa inahusu MASLAHI yake kama Masuala ya UCHAGUZI kuporwa, kunyimwa fomu za Kugombea au Mikutano yake ya kisiasa KUZUIWA.

Kama wanasiasa wanacyoangalia mambo yao, sioni sababu ya mtu mwingine yoyote na yeye kutoangalia mambo yake.
Nina jibu fupi litakaloridhisha dhana yako hii potofu uliyoelezea hapa juu.

Watu kama wewe ndio mliojazana huko CCM wakati huu, na hawa ndio unaowaelezea hapa vizuri sana.

Hatuna wana siasa huko ndani ya CCM, tuna walaji tu ndiyo sababu hawataki pawepo na usawa katika kushawishi wananchi wapewe ridhaa ya kuongoza.

Hapa unapomsemea Mbowe, sijui kama uliwahi kukaa na Mbowe na hao akina Mnyika wakakueleza hayo uliyoeleza hapa, au unayazungumzia kwa uzoefu wako ndani ya chama cha CCM?

Basi na hata ikiwa hawa wanapigania maslahi yao, ni bora tuwaunge mkono ili na wao wakaonje utamu mliouzoea huko CCM, kwa sabau hamna hati ya kumiliki utamu huo peke yenu.

Inatosha. Ukitaka kuelewa uelewe, usipotaka basi hiyo ni juu yako. In fact umeni'disappoint' sana wewe mzee na mawazo ya aina hiyo.
 
Naona Samia anaingia katika mtego wa CHADEMA

CHADEMA washikilie hapohapo, waendelee kuitisha makongamano na mikutano, wakikamatwa na kuonewa na polisi bado ni news na inawapa wananchi sababu ya kujua kwa nini wanakamatwa na kuonewa.

Chadema isipoe iendelee kuandaa haya makongamano
 
Back
Top Bottom