Barua Ya Wazi Kwa Mwana Sultani : Ridhiwani Kikwete, | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Barua Ya Wazi Kwa Mwana Sultani : Ridhiwani Kikwete,

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Muke Ya Muzungu, Sep 11, 2012.

Thread Status:
Not open for further replies.
 1. Muke Ya Muzungu

  Muke Ya Muzungu JF-Expert Member

  #1
  Sep 11, 2012
  Joined: Jun 17, 2009
  Messages: 3,451
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 0
  Bwana Ridhiwani,

  Ni matumaini yangu kwamba umzima wa afya popote pale ulipo. Ninaandika hii barua kwa huzuni kubwa nikitarajia ya kwamba yote yaliyomo utayashughulikia ipasavyo na haraka iwezekanavo.

  Kwanza kabisa, hongera kwa kuwa mwana wa Sultani (mtoto wa Rais). Hii nafasi imekupa jeuri kubwa kiasi kwamba nchi unaiona kama yako. Kwa muda mrefu tumekustahi sana kutokana na tabia yako ya kuingilia vitu vingi visivyokuhusu na hata kutumia jina la baba yako kufanya ufisadi mwingi kama unavyofanya sasa.

  Magari unayomiliki yote tunayafahamu vizuri yakiwa ni ya thamani kubwa huku ukiwadanganya watanzania unamiliki Toyota Camry tu. Ridhiwani, unazo Landcruizer VX V8 mbili. Toyota Camry, Toyota Harrier, Hummer, Mercedes ML, BMW X6, Pamoja na Range Rover Hata na mwenzio January Makamba mwenye ukwasi wa fedha na miradi za kutisha pia tuna data zake. Asidanganye watu anamiliki Pickup double Cabin wakati anayo BMW X5, Landcruiser V8 pamoja na Gari alilomnyang'anya shemeji yake Mr. Gray.

  Ridhiwani, yale malori (Freightliner 100) uliyoficha kwa David Mosha yaliyotoka Marekani tunajua ukweli wake wote. Hii ni mifano tu na wala sio swala la leo. Swala la leo ni kuhusu uchaguzi wa UVCCM hapa Dodoma. Tangu juzi, vijana wengi waliotegemea kuchaguliwa kidemokrasia wameingiwa na wasiwasi kutokana na uroho wako.

  Jinsi unavyozivuruga timu za mipira hasa yanga na Simmba ndivyo jinsi unavokivuruga CCM. Majuzi tu wanasimba wamelia sana baada ya wewe kuingia kati na kuwanyang'anya mchezaji wao kutoka Burudi ambaye umempeleka Yanga. Nchi yote ilinyamaza hakuna aliyekufatilia. Ila, nakuhakikishia kwamba, hatutaweza kunyamaza ukiendelea na hii tabia ya sasa hivi, hapa Dodoma kwenye uchaguzi wa UVCCM. Vijana wengi masikini wasio na mafisadi nyuma yao wanalalamika, kwamba ndoto zao za uongozi zinayeyuka kutokana na shinikizo za Ridhiwani.

  Unalazimisha watu kumpigia kura mamluki wako, na wale wanaogombea nafasi kadhaa unajaribu kuwakatisha tamaa na hata kuwatolea vitisho wasigombee nafasi zao ili tu mtu wako apite. Umetoa hela nyingi na tayari tumesharodhesha majina ya vijana waliopokea hela zako. Ridhiwani, napenda kukukumbusha kwamba wewe siyo Rais. Rais ni baba yako. Hauna nafasi yoyote ya uongozi katika hii nchi. Tabia yako italeta machafuko. Hauwezi kuteua wakuu wa wilaya, wakuu wa mikoa, mawaziri na hata wakurugenzi kana kwamba wewe ndiye rais. Unayemchukia mara moja anaishi maisha magumu na hata kupoteza ajira.

  Usijisahau kwamba madaraka mliyo nayo ni ya milele. Hata wakina Seif-Al Islam walikuwa kama wewe na mwisho wao umeuona. Huku ndiko mnakotupeleka wana wa Sultani. Usidhanie na wala usijidanganye kwamba watanzania wanakuogopa. Tunakuomba ubadilike. Asante sana Kunisikiliza

  Honorable MP (CCM): Dodoma
   
 2. M

  MIGNON JF-Expert Member

  #2
  Sep 11, 2012
  Joined: Nov 23, 2009
  Messages: 2,587
  Likes Received: 1,563
  Trophy Points: 280
  Ungetuwekea ushahidi zaidi lakini hata hivyo kuna dalili za ukweli.
  Mosha anayetajwa hapa amaemekana amenunua Lamboghini kutoka kwa mtoto SSB na thamani kwa TShs ni ka bilioni na ushee.
  Juzi nikiwa mtwara kuna kiwanja cha wazi baada ya Ofisi za Magereza za mkoa na nimekuta kimezungushiwa ukuta katika kuuliza nikaambiwa na Ritz.
  Kuna mwekezaji alinunua shamba la mkonge Mikindani nikaelezwa jamaa nae ananyanganywa lakini Ritz yuko nyuma ya hilo.
  Kama ni kweli ndugu yangu Ritz nawe ukiwa Muislamu nakukumbusha jambo moja muhimu," DUNIA SI LOLOTE ILA STAREHE ZENYE KUPITA NA KUDANGANYA" Quran tukufu.
   
 3. masopakyindi

  masopakyindi JF-Expert Member

  #3
  Sep 11, 2012
  Joined: Jul 5, 2011
  Messages: 13,918
  Likes Received: 2,347
  Trophy Points: 280
  Du, mkuu Mheshimiwa MP,umejiunga JF kumpa vipande vyake Riz?
  Nenda mbali kidogo, nenda pale Maelezo,kuwa mjasiri bana!
   
 4. Azipa

  Azipa JF-Expert Member

  #4
  Sep 11, 2012
  Joined: Mar 19, 2012
  Messages: 1,072
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 145
  Vita vya panzi furaha kwa kunguru.....nadhani nimeipatia hiyo methali
   
 5. Muke Ya Muzungu

  Muke Ya Muzungu JF-Expert Member

  #5
  Sep 11, 2012
  Joined: Jun 17, 2009
  Messages: 3,451
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 0
  Hii kali, kumbe Riz1 aliingilia yule jamaa kuletwa yanga? mimi nilikuwa nadhani ni mambo tu ya mtaani.
  Duh Ri1 kiboko. Riz kula baba haya maisha mafupi
   
 6. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #6
  Sep 11, 2012
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Na mwenye masikio asikie.
   
 7. Shark

  Shark JF-Expert Member

  #7
  Sep 11, 2012
  Joined: Jan 25, 2010
  Messages: 20,105
  Likes Received: 7,363
  Trophy Points: 280
  I will be back!!
   
 8. Dumelambegu

  Dumelambegu JF-Expert Member

  #8
  Sep 11, 2012
  Joined: Jan 28, 2011
  Messages: 1,052
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Duuu, huyu kijana ni kiboko siyo mchezo. Nasikia hata kiwanda cha nyama kinachokarabatiwa Shinyanga Mjini ambacho viongozi wa mkoa kwa kushinikizwa na ccm wamempatia mwarabu mmoja ambaye ana uhusiano mkubwa na Riz1. Inasemekana hicho kiwanda ilikuwa apewe mwekezaji serious kutoka Kenya au Australia. Ndiyo mambo ya bongo hayo!
   
 9. Wingu

  Wingu JF-Expert Member

  #9
  Sep 11, 2012
  Joined: Jan 14, 2011
  Messages: 4,326
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Njaa mbaya sana.Usikate tamaa baba pambana utatoka tu acha majungu.Pole kwa kupigwa chini UVCCM siku nyingine usiendekeze njaa huna pesa kaa pembeni wanaume wafanye kazi.Hujasikiaga mwenye nguvu mpishe wewe unaleta ubishi.Na ukileta maneno mneno yako hata mke utapokonywa wewe.Wanaume hawalii hivyo
   
 10. mtotowamjini

  mtotowamjini JF-Expert Member

  #10
  Sep 11, 2012
  Joined: Apr 23, 2012
  Messages: 4,540
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Juzi nimeona lambo la moshi lina private number delinaceo dah nikasema si mchezo vijana washaanza kutesa mjini hapa
   
 11. aye

  aye JF-Expert Member

  #11
  Sep 11, 2012
  Joined: Oct 6, 2010
  Messages: 1,987
  Likes Received: 249
  Trophy Points: 160
  du kazi kwelikweli kijana anatisha balaa
   
 12. m

  majebere JF-Expert Member

  #12
  Sep 11, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 4,520
  Likes Received: 568
  Trophy Points: 280
  Hii ulipost wakati uko kitchen party?maana naona maneno yote yakimbea mbea.
   
 13. F

  Fitinamwiko JF-Expert Member

  #13
  Sep 11, 2012
  Joined: Aug 13, 2012
  Messages: 4,810
  Likes Received: 255
  Trophy Points: 180
  3 more years, then puuuuu chali = segerea
   
 14. M

  MALAGASHIMBA Member

  #14
  Sep 11, 2012
  Joined: Dec 7, 2011
  Messages: 71
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 13
  Ndugu,CCM ina wenyewe na wenyewe ndiyo hao, kilichokurudisha ccm ni nini?baada ya ccj kubuma ungeendelea mbele sio kurudi ccm,utalalamika mpaka basi,wenzio hawaangalii.
   
 15. Ncha

  Ncha JF-Expert Member

  #15
  Sep 11, 2012
  Joined: Jul 8, 2008
  Messages: 254
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Hivi hii ni mada ya kuletwa na GT!!!??? hapa si pa udaku, huna data kaa kimya
   
 16. King'asti

  King'asti JF-Expert Member

  #16
  Sep 11, 2012
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 27,508
  Likes Received: 2,249
  Trophy Points: 280
  jeuri ya kifisadi. Ati huna pesa kaa pembeni! Ni kwa zamu lakini
   
 17. M

  Mbozib JF-Expert Member

  #17
  Sep 11, 2012
  Joined: Apr 9, 2012
  Messages: 409
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Miaka iliyobaki ni miwili na ushehe .mwache kijana atese kabla hayaja mfika ya seif al islam gadafi.
   
 18. Questt

  Questt JF-Expert Member

  #18
  Sep 11, 2012
  Joined: Oct 8, 2009
  Messages: 3,013
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Ndugu yangu usiseme humuogopi Riz 1 wewe!! UNAMUOGOPA... tena unamuogopa sana tu..... Kwa sababu ungekuwa humuogopi ungeenda pale Habari malelezo ukamchana kama ulivyomchana hapa!! Si unaona mtu kama Mtikila na Dr. Slaa walivyofanya??? Wale hawamuogopi Riz1! walimwambia live na mpk sasa tunasubiri awafikishe mahakani koz ndiyo ahadi aliyoitoa!!!!
   
 19. Questt

  Questt JF-Expert Member

  #19
  Sep 11, 2012
  Joined: Oct 8, 2009
  Messages: 3,013
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135

  Kama anapanga safu ya uongozi unategemea hayo yatamfika??? Hao anaowaweka hawatamlinda????
   
 20. King Kong III

  King Kong III JF-Expert Member

  #20
  Sep 11, 2012
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 25,153
  Likes Received: 2,402
  Trophy Points: 280
  Ehee riz1 ohoo riz1 ongea na mshua!!!
  1.Wazee wanalalamika hawajalipwa mafao yao
  2.Nssf/ppf vp mbona kimya? Au mnakusanya mafungu?
  3.Bandarini mbona wizi unaongezeka?
  4.Ajira mil1 mshatimiza na zipi au hadi na hizi za kuokota makopo?
  5.David Mosha hela kapata wapi,delina ichunguzeni wapi Dr Hosea?
  6.Policcm sasa ndio majambazi na wezi mnawachukulia hatua gani?

  Eheee riz1 ongea na mshua ohoo riz1
   
Thread Status:
Not open for further replies.
Loading...