Barua ya wazi kwa Mheshimiwa Rais.

Chizi Maarifa

JF-Expert Member
Jul 29, 2013
4,037
2,000
BARUA YA WAZI KWA MH. RAIS
Kwako Mh. Rais.Kwanza shikamoo, Natumain X-
MASS ilipita vyema. Najua pia utakuwa una
uchovu wa safari na kaz pia. Mimi hali yangu ni
kama jana tu Mchana Nzi Usiku Mbu. Kipind hiki
ni waz unafikiria namna gani upangue Baraza la
Mawazir, Mkuu kaz ni ngumu,lLakin umewah hata
kumfikiria Kaka yao Mkubwa? Naye ni mzigo tena
wa miba.hilo lipo dhahir,lakin pia nakuomba sana
'USIJAZIE MAPENGO' pata muda tafakari nani
anaweza kukusaidia kma si kutusaidia sisi
wananch. Usiendelee kutubebesha mizigo ya
misumal mabegan mwetu kwa kutupa Mawaziri
mizigo. Mkuu, safari hii usiangalie nani
Ndugu,Rafiki,Shemej na Jamaa. Tuwekee
Mawaziri ambao vijana siku hizi wanawaita
'JEMBE' naamini ktk nchi yenye watu zaidi ya Mil
40 hawakosekan watu wenye mapenz mema kwa
nch hii. Hao wengne walioitwa mzigo ni wakat wa
kuwatua sasa. Nashukuru kwa kuwa Rais wangu
Msikivu, Mwonaji utasikia kilio hiki. Nisisahau pia
kukupa salamu toka huku. Wanakisalimia sana na
wanauliza utakuja lini kututembelea? Huku sisi
Jua tu kali mkuu....sijui nyie huko. Lakini
tunamshukuru Mungu kikubwa Uhai. Nisikuchoshe
nikuache upumzike. Haya kaz njema Mzee.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom