Barua ya wazi kwa mheshimiwa jk | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Barua ya wazi kwa mheshimiwa jk

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by popo, Nov 25, 2008.

 1. p

  popo Member

  #1
  Nov 25, 2008
  Joined: Aug 30, 2008
  Messages: 59
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Naamini wananchi wa Tanzania walipokuchagua kwa wingi walikuwa na Imani Kubwa kwako kwamba Kiongozi ambaye wanayemtaka kuja kutatua matatizo yao ndio wewe JK japo nafahamu wengi walikuwa wanafahamu kwamba ahadi yako ya “Tanzaniz bila umaskini inawezekana” ni vigumu kutekelezeka lakini walikuwa na imani Kubwa kwamba kero za Ubadhirifu wa mali za Umma, ufisadi, rushwa na Upendeleo katika ajira utatokomeza kwa kiasi kikubwa.

  Mwamko wa watu na matumaini yalikuwa makubwa sana kwako na ndio maana watu wengi walijitokeza kukupigia kura huku wengi wakifahamu kwamba CCM walikubania Mwaka 1995. Kwa imani ya wananchi wengi wa Tanzania walijua wewe ndio utakua mbele kuwalinda na uonevu, dhuluma na kutokomeza hali ya ubabaisha ya viongozi wengine ambayo imeendelea kwa kipindi kirefu na wananchi kukata tamaa ya kuishi kwenye nchi yao waipendayo.

  Wananchi wa Tanzania walishachoka na kero za rushwa kwenye idara mbalimbali hasa ajira, rushwa mahospitalini na sehemu nyingine nyingi ambazo ni muhimu kwa maisha ya mwanadamu ya kila siku. Kero za rushwa nadhani ni bughudha ambayo iliwachosha sana watanzania kwani ilifikia hata mgonjwa yupo mahututi bado baadhi ya madaktari au manurse wanadai kidogodogo ili apate matibabu na mpaka ikafikia bunge Kupitisha kitu kinachoitwa Takrima,lakini hapo sitaki kuongelea sana,naachia hapo.

  Leo hii Rais kipenzi cha watanzania amefanya kitendo au tuite maamuzi ambayo anaweza akajutia maishani mwake na watanzania hawatamsamehe kwa hilo, kwanini nasema hivyo

  1. Ameweka maisha ya watu wengine kwenye hatari kuwasamehe mafisadi wa EPA hasa watu ambao walifanya kazi nzuri ya Kutafuta ushaidi na kuwafichua hao madhalimu wa nchi.Ameshindwa hata kuwaomba msamaha walipa kodi kwa maamuzi yake ambayo ni yeye na Mungu wake ndio anajua nini anafikiria.

  Ameunda tume kuchunguza swala hilo,tume imetumia pesa nyingi kulipa posho za wanatume hao na leo hii anakuja kutuambia kwamba amewasamehe ni kichekesho cha aina yake.(Au ndio uwajibikaji wa pamoja),inaonekana ulishaamua kuwasamehe ndio maana zile pesa ambazo walirudisha ulizigawa wakati hule ndio ushaidi ambao ungetumika mahakamani.

  2. Ameshindwa kuwaambia watanzania ni nani uliowasamehe ili wananchi wafahamu kwamba hao watu ni hatari na hawafai kuwa viongozi au kuchaguliwa kuwa viongozi siku za usoni.

  3. Umeficha maelezo ambayo ni muhimu sana kwa wananchi wa Tanzania kwa kutoweka bayana orodha ya majina ya waliukwiba mapesa ya EPA.Kuficha majina hayo ni sawa na kuwaachia watanzania waendelee kula matapishi yao, kwani wananchi wa Tanzania hawatajua kwamba viongozi wanaowachagua kwenye Ubunge au ngazi yoyote ile ni wale mafisadi wa EPA

  4. Kuna watu wengi ambao wamefungwa kwa makosa ya kijinga sana ambao wanaitaji msamaha wa rais kuliko watu wengine wowote na sio hao ambao wameiba pesa nyingi na kustarehe nazo kipindi chote hicho na kujilimbikizia faida Kubwa kutokana na riba au hata kuzifanyia biashara.

  5. Je unataka wananchi wakuamini tena kwa makosa ambayo umewafanyia ya kuwalinda wezi na kusahau kulinda katiba ya nchi ambayo ulikula kiapo kuhakikisha kwamba Sheria za nchi zitafuatwa bila kukiukwa.

  6. Je huoni kwamba wewe mwenyewe umekiuka sheria kwa kusamehe watu ambao pengine hawana makosa yoyote ila wewe umechukua sheria mikononi mwako. ” Someone is not guilty until proven otherwise” Labda hapa utuambie ni kifungu gani cha sheria ulichotumia kuhakikisha hawa jamaa ni wakosaji? Je ulisoma wapi sheria na je unamahakama kichwani mwako? Kwani hata hakimu hufanya maamuzi na baraza lake, Je ndugu Rais wewe ulifanya maamuzi haya na nani?
  mwenyezi Mungu hata kusamehe kwa hilo

  7. Umeanzisha vita wewe mwenyewe na sasa leo hii umegeuka na unakuwa adui wa wananchi na unaanza kupigana na wananchi wako.Wewe ni kiongozi wa aina gani? Kiongozi wa nchi anatakiwa kuwa muwazi kitu ambacho wewe umekishindwa kukitekeleza

  8. Ni nini unawafundisha vijana ambao siku za usoni ndio watakuwa viongozi wetu kwa kitendawili chako hiki cha msamaha kwa watu ambao bado mahakama haijawatia hatiani na wewe kuwasamehe.Je wewe ni mahakama?

  9. Ni nini unawafundisha Watanzania kuhusu sheria za nchi yao,Kwamba ukiiba Fedha au chochote kila na ukijulikana umeiba na ukakubali Kurudisha basi wewe ni mtu safi tu kama watanzania wengine. Tena wewe mwenyewe unamwambia DPP (Director of public prosecution) awafungulie mashitaka wala wote ambao hawajarudisha pesa na sio wezi wa EPA, kwani ambao wamerudisha sio wezi?

  10. Ipo wapi haki kwa watu ambao wanaozea jela kwa makosa ambayo ni yakipuuzi ambayo hukumu yake labda ingekuwa kufagia barabara na kusafisha vyoo vya Hospitali.Je watu kama hawa hawaitaji msamaha kwa sababu tu ni walalahoi na hawana mchango wowote kwako na kwa Taifa?

  11. Je unafahamu kuna wazazi walipigwa viboko kwa kosa la kutolipa Tshs 5,000 tu za mchango wa madawati? Je walistahili adhabu hiyo japo hawakumuibia mtu yoyote?

  12. Je unafahamu unachochea vurugu kwa walimu na wazee wa afrika mashariki kudai haki zao kwa kutofuata sheria kwa kufahamu fika kwamba bila mabavu hawawezi kupata haki zao?

  13. Umeifundisha nini jamii kwa kuwapotezea muda wao mwingi kwa swala ambalo ulikuwa unafahamu fika kwamba utawasamehe wahusika wote waliorudisha pesa.

  14. Je unafikiria kwa maamuzi yako hayo wale wasioweza Kurudisha pesa ukiwafungulia kesi watahukumiwa na kufungwa? Nadhani hapa inakubidi urudi darasani ukasome tena, kwa uelewaji wangu hawataweza kufungwa kwani itakuwa sio kesi kamili bila kuwepo uliowasamehe labda na huyo hakimu awe mbumbumbu.Hapo ni sawa umewasamehe wote na unataka kuwaongopea watanzania tena badala ya kumaliza mjadwala mzima.

  15. Mazingira halisi ya msamaha wa Mafisadi wa EPA ni kwamba wewe pia ni mpokea rushwa na mazingira yanaonyesha wazi kwamba kuna harufu ya rushwa kwenye swala zima la Epa kuanzia mwanzo ulipoamua wezi wa EPA warudishe pesa, ni wazi ukishaamua warudishe pesa hakuna hukumu yoyote itafanyika kwa sababu na wao hawatakuwa wajinga wakubali Kurudisha pesa halafu wapelekwe mahakamani.Kulikuwa na makubaliano tangu hawali na wewe ulikuwa unafahamu lakini ukazidi kulipiga danadana swala zima hilo.

  Kwahiyo tunaloshindwa kuelewa mpaka sasa ni je hawa jamaa unawasamehe kwa kosa gani walilofanya? Kugushi nyaraka/kuibia Serikali/au ni nini? Hapa nadhani watanzania wanaitaji ufafanuzi zaidi.

  16. Kwa kumalizia,Maishani mwako utakumbukwa kwa sababu moja kubwa nayo ni kulinda mafisadi na hata ukifanya mazuri gani hilo litakufuata popote huendapo na itakuwa vigumu kwako kuchukua hatua kwa wengine ambao wanaiba fedha za serikali kwani kuwapeleka mahakamani itakuwa ni uonevu wa hali ya juu na hata Mungu hatokusamehe kwa hilo.

  Ingekuwa vizuri ungeanza upya na kuwasamehe wote waliofungwa hata waziri mkuu Edward lowassa na Karamagi waliyejiuzuru na hapa hafadhali kidogo watanzania labda wanaweza kukuelewa japo bado Mimi itakuwa ni vigumu kukuelewa maishani mwangu.

  Kwa Watanzania
  Ni lini viongozi wetu wataacha upuuzi wao wa kulindana hata kwenye maswala nyeti ya Taifa? Nadhani imefika wakati wananchi wa kusema basi tumechoka na hatutaki tena kufanywa wapuuzi (We need change we can trust but not CCM) hawa jamaa wa CCM watalipeleka Taifa letu kwenye Janga Kubwa la umasikini kama hatutakuwa makini kuhakikisha mabadiliko yanafanyika haraka iwezekanavyo. Bado wanafikiri sisi ni wale wale wakuwapigia kura kwa lolote lile na hatuna njia nyingine.

  Wakati umefika wa kuleta mabadiliko hakuna jinsi nyingine vinginevyo vizazi vyetu vitaishia kwenye Nchi yenye viongozi wezi,wala rushwa.madhalimu na mafisadi.

  Iweje leo hii nchi ambazo zilikuwa na matatizo ya vita kwa kipindi kirefu wameweza kuendelea mpaka kutukuta sisi bado tunanin’ginia kwenye stage hiyo hiyo.

  Jakaya kikwete umejizalilisha na watanzania wote wanakuweka kwenye kundi moja na Mafisadi na wazulmati kwa kudhulumu haki yao ya kisheria.

  Sijui uje na kauli gani kuwaeleza wananchi wako ili waweze kukuelewa lakini kwa upeo wangu wa haraka haraka ni kwamba na wale wote ambao hawaitakii mema Tanzania watakusupoti kwa nguvu zote lakini hata mwenye upeo mdogo katika jamii hawatakusamehe kwa hili.

  Kitu kikubwa ambacho kimekushinda ni kunga’gania madaraka yote na kushindwa kugawa madaraka kwa waziri mkuu wako (Delegation of Authority), matokeo yake waziri mkuu yupo pale kama boya tu na sio mtendaji mkuu wa serikali. Mimi sioni anachokifanya zaidi ya kukuwakilisha Bungeni ambako kimsingi wewe uhitajiki kuwepo pale.

  Mungu Ibariki Tanzania, Mungu Ibariki Afrika, Mungu tubariki tupate Viongozi bora ambao wanajua haki na sheria ni nini kwa maslai ya Taifa na watakaoweza kuondoa dhuluma,kero na kuweza kuwafunga Mafisadi wote.

  My Opinion

  You are hero but now your Zero. Shame on you JK and your real disgusting me.

  Mr JK you are not fit to be president at all. It is serious you need to go and find another career. I know people will see this as a bit weird but for sure he is not fit to be a President.

  I used to hear from Mwalimu Nyerere said to other leaders that they are not ready yet to be President and…………. I thought may be Mwalimu he is selfish and a little bit weird but he is blood right. . May God bless his soul in Peace. Amen

  There is big different between a leader and a manager, May be JK is a manager not a leader

   
 2. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #2
  Nov 26, 2008
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 11,588
  Likes Received: 3,887
  Trophy Points: 280
  labda amesoma hapa maana wengine wengi wanaongezeka kisutu!!!
   
 3. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #3
  Nov 26, 2008
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,574
  Likes Received: 18,509
  Trophy Points: 280
  Naona uliandika siku nyingi ila ukasave naleo ndio umekata na ku paste. Any way kwa vile hii ni barua ya wazi kwa- Mhe. JK atakuwa ameikuta asubuhi mezani kwake maana ninauhakika wa 100 kwa mia jamaa wa UT hapa jf ni sebuleni kwao.

  Jamaa inaonyesha ni jinsi gani alivyo na hasira na usongo na JK. Namshauri pamoja na asira zote, azihifadhi mpaka 2010 aje kuzimalizia kwanye ballot box.
   
Loading...