Barua ya wazi kwa mheshimiwa g.lema.wa arusha mjini. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Barua ya wazi kwa mheshimiwa g.lema.wa arusha mjini.

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by politiki, Feb 13, 2011.

 1. p

  politiki JF-Expert Member

  #1
  Feb 13, 2011
  Joined: Sep 2, 2010
  Messages: 2,356
  Likes Received: 154
  Trophy Points: 160
  CCM na serikali yake mpakaleo hii viko kimya kuhusiana na tukio la kishujaa la wananchi wa misri kwani somehow linawahusu kwani madai ya wananchi wa misri yanafanana na madai ya wananchi wengi wa Tanzania kwa hivi sasa kama vile ukosefu wa ajira kwa vijana, uwizi wa mali za umma, ufisadi uliokithiri na kutowajibika. ni vyema chadema mkaanza kwa kulipongeza na kulitambua tukio lile
  kwani linashabiina na kile kilichotokea Arusha kwa maana ya maandamano ya amani ya wananchi kudai haki zao wakizodhulumiwa na serikali yao.

  Ningependa kupendekeza utangulizi ufuatao ktk hoja yako ya jumatatu kwa kuanza kuungana na Rais Barack Obama wa marekani na wapenda haki wote duniani kwa kuwapongeza waandamanaji wa misri kwa moyo wao wa ushujaa kwa kujitoa mhanga kutetea haki zao kwani mabomu machozi na maji ya kuwasha hayakuweza kufua dafu mbele ya people's power. wananchi wa Arusha wakiwa kama walivyowenzao wa misri walitumia njia inayofanana siku ya 1/5/2011 ya maandamano kupinga dhuluma waliyofanyiwa na serikali kupitia watumishi wake na hasa mkurugezi wa mji wa Arusha kwa kuitisha na kusimamia uchaguzi kinyume cha sheria huku akijua kwa kufanya hivyo anawadhurumu haki yao ya msingi wananchi wa Arusha ya kuchagua meya wanayemtaka kupitia kwa madiwani wao.

  kama tulivyojionea wenyewe huko misri kuwa Haki huwa haiporwi ucheleweshwa tu
  wananchi wa misri waliweza kupata haki pamoja na watawala kuwacheleweshea. kwahiyo ningependa kuchukua fursa hii kuwatia moyo wananchi wenzangu wa Arusha kuwa wasikate tamaa kutafuta haki yao kwani siku itafika wataungana kama wananchi wenzao wa misri kufurahia ushindi kwani Mungu siku zote huwa upande wa wapenda haki. halafu ukitoka hapo anza kumwaga ushahidi wote kuhusiana na nini kilichojiri huko Arusha nakutakia ulinzi wa mwenyezi Mungu awe pamoja nawe.
   
 2. Quinty

  Quinty JF-Expert Member

  #2
  Feb 13, 2011
  Joined: Mar 25, 2010
  Messages: 463
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Hii ni sahihi kabisa tuko pamoja mpaka haki ipatikane...!
   
 3. Architect E.M

  Architect E.M JF-Expert Member

  #3
  Feb 13, 2011
  Joined: Nov 15, 2010
  Messages: 815
  Likes Received: 117
  Trophy Points: 60
  namuaminia sana mbunge wangu lema, japokua serikali will do all it takes kuonekana kwamba ipo sahihi, hata kama proof zinaonesha yenyewe ndo una makosa, but the fact will always remain there, that LEMA is a HERO.... Weather he succeedz or failz in the case ya kesho..wananchi wa jimbo lake bado tunamuona kama shujaa na mkombozi wetu wa ukweli
   
 4. lm317

  lm317 JF-Expert Member

  #4
  Feb 13, 2011
  Joined: Nov 2, 2009
  Messages: 452
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Huo ushauri MURUA
  asante
   
 5. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #5
  Feb 13, 2011
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Thank you politiki

  Nimesoma michango mingi ya kumsaidia bwana Lema na huu nao ni platinum release

  NI mategemeo yangu kwamba wapiganaji wanakusanya maoni, wanajumlisha na ya kwao na siku ya ushahidi itakua surprise kwa watu wanodhani tunaishi kama wanaCCM... wasiosoma wala kuchambua bali kuongozwa na hisia kali na mawazo mgando
   
 6. Mallaba

  Mallaba JF-Expert Member

  #6
  Feb 13, 2011
  Joined: Jan 30, 2008
  Messages: 2,560
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 133
  kweli kabisa, nakubaliana na hoja.
  Ni lazima aanze kwa kuwapongeza waote walioonyesha ujasiri huko Misri na Tunisia.
  Pia awape pole wote waliokufa na kujeruhiwa kwani adha walioipata ndio faida ya mamilioni waliobaki.
   
 7. Nyakageni

  Nyakageni JF-Expert Member

  #7
  Feb 13, 2011
  Joined: Feb 1, 2011
  Messages: 13,948
  Likes Received: 1,274
  Trophy Points: 280
  Lema be strong! People are strongly supporting you. Dont give up even if it will be through the hard way. God blessed you already thats why you are Godbless
   
 8. B

  Byendangwero JF-Expert Member

  #8
  Feb 13, 2011
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 872
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Nashauri kesho wabunge wa CDM wakati wa kuanza bunge waombe muongozo wa Spika kuhusu ni kwanini bunge lisisimame kwa dakika moja kwaajili ya kuwaombea mamia ya mashujaa wa Misri waliopoteza uhai wao uiliopelekea katika kutokomeza ubabe wa Mubarak. Aidha kwa kila mbunge wa CDM atakayechangia aanze kwa kupongeza ujasiri wa wananchi wa Misri waliojitoa muhanga kukomboa nchi yao kutoka kwenye makucha ya mafisadi.
   
 9. T

  Thadeus JF-Expert Member

  #9
  Feb 13, 2011
  Joined: Nov 24, 2007
  Messages: 267
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 35
  Kwa hiyo Mheshimiwa Lema awakusanye wananchi wa Arusha pale Mnara wa Azimio au viwanja vya Unga Limited hadi haki ipatikane???
   
Loading...