Barua ya wazi kwa Mhe. Rais

mpandambegu

New Member
Dec 29, 2018
4
2
Kwanza nianze kwa kukupongeza Mhe. Rais kwa kutatua suala la " formula" ya mafao ya uzeeni, iliyoleta mkanganyiko mkubwa. Umeweza kufumbua sintofaham iliyokuwa ikiwakabili Watumishi katika sekta ya UMMA wanaochangia PSSSF na wale wa sekta BINAFSI wanaochangia NSSF.

Pamoja na hili zuri ulilolifanya Mhe. Rais, kuna suala la malimbikizo ya malipo "arrears" ambalo uliwahi kulitolea maelekezo, LAKINI mpaka sasa kundi kubwa la watumishi kuanzia wa TAMISEMI hata wa Serikali Kuu bado wanadai kutolipwa malimbikizo yao., jambo ambalo kimsingi ni kinyume na maagizo yako.

Kwakuwa bado Serikali yako inaendelea kutafakari suala la mishahara ya watumishi pamoja na stahiki zao mbalimbali ikiwemo kuwapandisha vyeo; pengine ungelipa ufumbuzi hili la arrears ambalo liko wazi kwa utekelezaji.

Mwisho, nikutakie heri ya mwaka mpya 2019 tukiwa tunaelekea mwaka wa nne wa Serikali yako ya awamu ya tano.
 
Kuna hamisho zimedoda Mkuu
Madeni ya watumishi wa Umma ni mengi sana yatatakiwa kulipwa tu one day
Subiri tuone.
 
Back
Top Bottom