Barua ya wazi kwa Mbunge Nape Nnauye

Joel Kisoka

Member
Dec 21, 2018
23
31
Ndugu Nape salaam,

Kati ya jambo lililonishangaza na kunifikirisha Sana ni kile ulichochapisha Ndugu Nape Nnauye ambaye ulipuuzia kuwa wewe ni mbunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na muwakilishi wa wananchi wa Jimbo lako la Mtama.

Katika kumjibu Ndugu Humphrey Polepole ambaye alitangaza kufanya "Press" yaani mahojiano na wanahabari Ndugu Nape uliandika;

"Aaaah kirobotoulishindwa akiwepo godfather utaweza leo?!!? Kina wenyewe shekh! Lakini ni kawaida punda roho ikiwa inaacha mwili hutupa mateke NONSENSE!!"

Najiuliza kwamba unaposema Chama kina wenyewe unamaanisha kipi hasa, au kisa Polepole ametoka katika familia isiyo na jina kwnye historia ya chama cha mapinduzi na wewe umetoka kwenye familia yenye jina kwenye chama .

Kauli Ile Nape imeonyesha waziwazi kwamba familia zenu nyie mnaojiona kama ndio wanachama wa CCM kwelikweli kama familia yako mlichukizwa na kitendo cha Hayati Rais John Pombe Magufuli kuteua watendaji wa chama wapya bila kujali kujuana na maswala ya kulipana fadhila Bali alizingatia uchapaji kazi na maslahi mapana ya Taifa na katika Hilo baadhi yenu mkawa kafara ili kupisha kazi zilizoleta baraka na Neema Kwa Watanzania maskini tena hao mnatudharau na kutuona kama wapambe wenu.

Nape unaonyesha waziwazi kwamba wewe ni mnafiki tena mtaka madaraka Tu na wala Huna Nia njema wala malengo ya kimaendeleo kwenye taifa hili Kwa sababu unajionyesha waziwazi sasa kwamba hata kule kuomba msamaha Ikulu ilikua ni ili usipate vikwazo kwenye chama wakati wa uchaguzi wa 2020 upitishwe uendelee kuila nchi kama ulivyozoea ingawa Kwa kiwango cha chini wakati huo Kwa sababu ulizoea kupiga vikubwa zamani, ukaona isiwe tabu usikose kabisa.

Nimekaa nikakuwazia Sana mwenye CCM yako, nikahisi labda una ahadi umepewa na Mungu kuhusu kesho yako maana si Kwa kauli shombo unazotoa Ila nikakumbuka kauli za namna hii hujaanza Leo na zilikuponza wakati huo ukawa mdogo kama punje ya mchicha na sio kuwa mpole Tu ukawa mwenye adabu Kwa watu wote hata uliowazidi umri na vyeo Ila sasa umejishau naomba nikuambie Ndugu Nape bado Una safari ndefu kwenye hili unalotaka kulitengeneza na nikushauri uwe umeshajipanga na namna ya kulimaliza.

Ulitoa kauli kama hizi kwenye serikali ya awamu ya tano kabla ya kutumbuliwa bila kujua unamkera bosi wako na matokeo yake ukadhalilika na mwishoni kabisa ukawa repented hili naliona Hadi sasa na waziwazi nakuona unafikia mwisho mbaya kwenye hili Kwa sababu ya kidomodomo.

Mwenzako aliyekuwa kama wewe kaonyesha ukomavu na sasa karudia heshima yake ya awali kapewa uwaziri wewe bado mamlaka zinakuona hujakomaa na Kwa hilo huwashauri hata kidogo wakupe nafasi Yani Kwa kifupi pilikapilika zako zote unajitekenya na kucheka mwenyewe, Unaowalenga wala hata hawana mda na mbilinge zako mitandaoni, wanatazama unayofanya wanainama wanatikisa vichwa wanaendelea kuperuzi yenye mantiki na yale ya msingi.

Kwa kutambua kuwa mwakani utafanyika uchaguzi ndani ya chama cha mapinduzi Ndugu Nape Nnauye naona umeanza sasa kujikombakomba kujifanya unaendana na maono ya mama Ila ni unafiki kwani nafahamu unabembeleza madaraka Tu ili uyapate iwe fimbo ya kunyooshea usiowapenda, endelea Baba kujaribu bahati yako Ila kuwa makini na hapa nikukumbushe Tu ndugu;

"We don't have permanent friends neither do we have permanent enemies in politics but rather we have a permanent interest"

CHEZA SALAMA!!
View attachment 2041509View attachment 2041511
 
Huyu Nape aliyewaita wenzake magamba kaanza tena kutapika?
Aliyedai Lowassa ni Kama dodoki?
Kumbe ndo mwenye hati miliki CCM?
Bakiza maneno Nape,teuzi tu inakufanya uwaite wengine kiroboto?,umeshika kesho ya wanadamu wewe?
 
Polepole pole kwa yanayokukuta. Iwe funzo kwako kutegemea mtu. Jitahidi kuwa wewe mwenyewe. Maendeleo hayana chama.
 
Back
Top Bottom