Barua ya wazi kwa malkia wa Uingereza, lolote na liwe | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Barua ya wazi kwa malkia wa Uingereza, lolote na liwe

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by mansakankanmusa, Jun 13, 2012.

 1. mansakankanmusa

  mansakankanmusa JF-Expert Member

  #1
  Jun 13, 2012
  Joined: Sep 30, 2010
  Messages: 4,090
  Likes Received: 602
  Trophy Points: 280
  Barua ya wazi kwa Malkia wa uingereza, MNIRUHUSU niongee nae japo kwa maandishi na najua wale wenzetu kule westminister mtafikisha ujumbe wangu.

  Wale wenzetu wanaokimbilia umoja wa mataifa kupeleka matatizo yao nadhani kwetu sio mahala pema ni kwa huyu kiongozi wa dola ya England,

  wakati mmoja niliwahi kuwaza sana, kwamba kwa nini tumepata nafasi na hatuitumii? Na kwa nini tuliwaambia wale watu watuachie tuwe huru wakatuachia/ na kwanini tuliwaambia mnatunyanyasa na bado tunanyanyasika/ na vipi tulishangilia uhuru na hatuuoni uhuru wenyewe?

  Kwa kifupi sana nielezee kwa nini nataka turejeshwe kwa dola ya malkia wa uingereza kama walivyokuwa wametushilia ili tujue moja kwamba tuko chini yake kuliko kuwa chini ya walaghai waliowalaghai wazungu watuachie kumbe tunaangukia mikononi mwao?

  Kabla sijaenda mbali nitoe nafasi kwa wana JF mnipe mwongozo, mawazo yenu, au niache kwa nini tusirudi kwenye ukoloni tuliozoea?

  kama mtakumbuka kisiwa cha mayote kilishawahi omba kirudishwe mikononi mwa wafaransa, sitaki kujua kama wamerudi au laa, mimi niko Tanzania na nadhani nitetee nchi na watu wetu..karibuni wana JF
   
 2. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #2
  Jun 13, 2012
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,332
  Likes Received: 19,497
  Trophy Points: 280
  KAMA KWELI MAWAZO YENU YAMEFIKA MWISHO MMEJISHINDWA HADI MNATAMANI KURUDI KWENYE UKOLONI ILI MUTAWALIWE NA WAZUNGU BASI MIMI Sina la kuchangia nimeona nikusaidie ku edit tu ndio mchango wangu
   
 3. k

  kitenuly JF-Expert Member

  #3
  Jun 13, 2012
  Joined: Apr 1, 2012
  Messages: 336
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Linaweza kuwa jambo bora ila waje watushape maana tumepoteza dira, utamaduni endelevu kwa taifa, akili, maadili, uwajibikaji na uzalendo nk, hata ktk pitapita zangu vijijini nilikuta wazee wakiongea kwanini wakoloni wasirudi tena? maana haya maisha ya uhuru ni magumu kuliko ya ukoloni,
   
 4. Globu

  Globu JF-Expert Member

  #4
  Jun 13, 2012
  Joined: Jan 12, 2011
  Messages: 7,975
  Likes Received: 175
  Trophy Points: 160
  Duh!! Hii kali. MiAfrika ndivyo tulivyo.
   
 5. Kiranja Mkuu

  Kiranja Mkuu JF-Expert Member

  #5
  Jun 13, 2012
  Joined: Feb 18, 2010
  Messages: 2,100
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  mbombo ngafu, watu wana hamu ya kucharazwa bakora mbele ya wake zao
   
 6. Nyetk

  Nyetk JF-Expert Member

  #6
  Jun 13, 2012
  Joined: Feb 28, 2012
  Messages: 1,624
  Likes Received: 819
  Trophy Points: 280
  Asante mkuu Saint Ivunga. Ile ya kwake nilishinwa kabisa kuisoma.
   
 7. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #7
  Jun 13, 2012
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  Unahitaji upevuke kifikra. Kama hujitambui kuwa uko katika nchi huru, ni dhahiri u-mtumwa wa fikira na anayekutawala ni huyo anayekulisha sumu ya maneno kwamba unaishi utumwani. Hebu jiulize, kama huyo anayekulisha sumu hiyo kama naye ana mawazo kama ya kwako ya kuendelea kutawaliwa na wakoloni. Akili za kuambiwa changanya na za kwako.
   
 8. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #8
  Jun 13, 2012
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  Huyo anayetamani ukoloni si amwambie baba yake amcharaze fimbo?
   
 9. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #9
  Jun 13, 2012
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  Mkuu tatizo siyo huyo anayetamani kutawaliwa na wakoloni, tatizo ni wale walikosa uzalendo na kuwalisha sumu ya maneno watanzania wasiojua kupembua pumba na mchele. Hawa wanahitaji kuelimishwa kuwa hao wanaowalisha hizo sumu hawana nia njema na nchi yetu.
   
 10. Henge

  Henge JF-Expert Member

  #10
  Jun 13, 2012
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 6,765
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  Ndo maana zanzibar wanataka nchi yao, unaweza ona anayetaka haya ni mtu mzima tu!
   
 11. R

  RMA JF-Expert Member

  #11
  Jun 13, 2012
  Joined: Oct 10, 2010
  Messages: 409
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hebu tunaomba ui-draft hiyo barua kwa kiingereza tuone!!!

   
 12. JingalaFalsafa

  JingalaFalsafa JF-Expert Member

  #12
  Jun 13, 2012
  Joined: Apr 13, 2012
  Messages: 759
  Likes Received: 98
  Trophy Points: 45
  Kosa lako ni kutoona nafasi yako na kuicheza inavyostahili. Unavyodhani wewd ukoloni huu tulionao kuna watu maalumu wa kuuondoa, ni KOSA KUBWA. Je, bado unathamin uhai wako na kupuuza wa watoto wako? Tulishazikwa hai, tusiache watoto wetu wakutwe na haya. Hakuna tofauti kubwa ya malkia kuwepo ama laa, kote ni unyonge mkubwa kila kona. UMEFANYA NINI KAMA RAIA MWEMA KATIKA KUONDOA UNYONGE HUU? Mimi na wewe tunaweza. Nguvu yetu ni UMOJA na KUTHUBUTU.
  (inferiority complex ni mbaya sana)
  Mungu wetu anaita.
   
 13. M

  Mwanaweja JF-Expert Member

  #13
  Jun 13, 2012
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 3,576
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  ongopa sana kuwa mtumwa kwa kutokujua nchi nyingi za kiafrika ukatae, ukubali zimo ndani ya utumwa ikiwemo Tanzania kutokana na viongozi wetu kuwa watumwa wa kutumikishwa kimawazo, kifikra hata kiraslimali ni aibu sana. hata kama utasema hutaki wazungu waje kututawala viongozi wetu walisharuhusu utumwa. mafano mdogo tu kwa nini wazawa hawapewi kipaumbele kumiliki ardhi lakini wageni wanapewa maeneo ya makubwa ya kutisha kwa mfano lile la mpanda 300,000ha amepewa mwekezaji kwa miaka 200 je, hapo utasema hatujatawaliwa? wanyama wetu waliotoka kupitia KIA je, kweli walitoka bila serikali kujua? leo hii tunaamua kununua au kubadilishana faru kutoka ungereza kweli????? nchi iliyo na raslimali za kila aina inakuwa maskini wa kutupya. tufikirieni kwa undani haswa kupitia viongozi tulio wapa dhamana ya kutututmikia wanafanya nini na kwa faida ya nani?
   
 14. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #14
  Jun 13, 2012
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,297
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Haya tunayoyapitia ukitrace historia ata Ulaya waliyapitia!
  So with time tutaondokana nayo kijana usijari!
  Come 2015 kila kitu kitakuwa okey but if and only if chama cha upinzani kikichukua nchi ili CCM wakae benchi for a while waonje joto ya jiwe ili wajipange upya!Maana wamejisahau as if wana hati miliki na Tz
   
 15. Fredrick Sanga

  Fredrick Sanga JF-Expert Member

  #15
  Jun 13, 2012
  Joined: Jan 27, 2011
  Messages: 3,148
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Ndio Tanganyika Huru.
   
 16. J

  John W. Mlacha Verified User

  #16
  Jun 13, 2012
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 3,515
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280
  ili malkia aweze kuisoma au sio? ngoja arudi hapa
   
 17. Sangarara

  Sangarara JF-Expert Member

  #17
  Jun 13, 2012
  Joined: Sep 29, 2011
  Messages: 13,048
  Likes Received: 549
  Trophy Points: 280
  Hii ni hoja ya msingi pia, naunga mkono hoja, turudi kwenye Milki ya Uingereza.
   
 18. Andrew Nyerere

  Andrew Nyerere Verified User

  #18
  Jun 13, 2012
  Joined: Nov 10, 2008
  Messages: 3,025
  Likes Received: 1,203
  Trophy Points: 280
  Hakuna sababu ya kuitafsiri. Kule wapo wakalimani. Aliyetoa hii hoja afahamu kwamba hii imekwishafika Clarence House. Nimeicopy ,I am going to post it right now to Prince Charles.
   
 19. simplemind

  simplemind JF-Expert Member

  #19
  Jun 13, 2012
  Joined: Apr 10, 2009
  Messages: 11,806
  Likes Received: 2,579
  Trophy Points: 280
  Mswahili hawezi kujitawala.

  Mswahili hawezi kusimamia uchumi.

  Naunga mkono hoja mia kwa mia.

  Yes for re-colonization of Tanzania. Karibu Malkia Elizabeti.
   
 20. Asnam

  Asnam JF-Expert Member

  #20
  Jun 13, 2012
  Joined: Jan 18, 2012
  Messages: 4,268
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 135
  mmmh yaani mtu unatamani ukoloni katika karne hii yale maisha ya kikoloni utayaweza kweli wewe mtoto wa ugali wa sembe au unaongea kufurahisha ulimi wako,hata wanao wakiiona hii post watakudharau na kukushushia heshima kabisa,bora uwaze ni jinsi gani ya kutatua matatizo ya nchi yako kuliko unavyoviwaza ubongoni mwako naamini hujui uliwazalo lina madhara yapi waulize babu zako watakupa majibu mazuri ya mawazo yako..
   
Loading...