Barua ya wazi kwa JPM- Sheria ya Bodi ya Mikopo ya mwaka 2016

Bila bumu nisingeweza kusoma so naishukuru sana bodi kwa hilo, ila baadaye nilikuja ‘kukengeuka’ na kuona hilo deni ni kubwa mno bora niache kuajiriwa kuliko kukatwa nitumike bure.... hiyo ni pesa pekee ya serikali ambayo kama raia nimeifaidi so kama hakuna namna nyingine ya kuniwajibisha nje ya ajira naomba tu tusisumbuane.
Serikali siwadai ajira ili wanilipe mshahara, nami msinidai bumu tufanye kama nimechukua GAWIO langu kama raia mwema.... win-win situation na kwa kweli sina mpango wa kulipa.
Kaka.. huko mbele hutafanya hata biashara hadi ulipe deni.
 
Nikikuwa ktk wa mwanzo kuanza kulipa deni 1ml plus. Mwajiri wangu akaagizwa kunikata kwa miaka tisa. Ilipokamilika tisa nikaenda HESLB wakaniambia bado nadaiwa kwa mujibu wa sharia hiyo ya 2016. Mi nikasimamisha mikato. Nangoja tukutane mahakamani tukapambane kisheria.
Safi sana.. rudisha mrejesho mkuu maana ni wengi sheria ya 2016 imewabana.
 
kumbe ni hatari sana, langu lilikuwa 26m/- sasa limebaki 9m/- ila napumulia mashine hali ni mbaya kuliko maelezo.

Hiyo 9 Mil ni kwenye salary slip yako au ni statement ya Bodi uliyopewa hivi karibuni?
 
Kama hujui hiyo sheria kasome au weka facts hapa. Usitoke nje yaa mada.

Kama ungekuwa kweli upo bodi na ni competent basi ungekuwa ushaweka maelezo ya kina. Badala yake unadokoa dokoa kama kuku wa kienyeji. Eti usidanganye. Ndilo unaloweza kutamka.

Waajiriwa wote wanapata barua la kuongezeka kwa deni Wewe unasema unadanganya umma, are you mad !

Au icho Kifungu mlikipenyeza wenyewe au mna kiimplement tofauti.

Na tutaanza kukifuatilia uhalisia wake, na kama kweli mnafanyaa umafia kama kawaida yenu tutawafungulia mashtaka.
Sijawahi sikia hiki unachosema wewe.

Hakuna hiyo percent kila mwaka endapo utaanza kukatwa.

Ila kama hujakatwa kabisa ndo kinaongezeka hiko kiasi.
 
Nikikuwa ktk wa mwanzo kuanza kulipa deni 1ml plus. Mwajiri wangu akaagizwa kunikata kwa miaka tisa. Ilipokamilika tisa nikaenda HESLB wakaniambia bado nadaiwa kwa mujibu wa sharia hiyo ya 2016. Mi nikasimamisha mikato. Nangoja tukutane mahakamani tukapambane kisheria.
Hakuna taasisi yyte ya fedha inatoa pesa bila liba, hilo litakuwa ni kweli kbsa.
Huo ni utumwa kbsa bora kujiajili mwenye.
 
Sijawahi sikia hiki unachosema wewe.

Hakuna hiyo percent kila mwaka endapo utaanza kukatwa.

Ila kama hujakatwa kabisa ndo kinaongezeka hiko kiasi.

Mara ya mwisho kufuatilia mambo yako Bodi ya Mikopo ni lini ?

Maana humu ndani wengi sana mnapaswa kuelimishwa. Na nimegundua watu wengi hawajui kwasababu hawalipi umuhimu hili deni mpaka siku aje akabwe kooni.

Hii ni changamoto, mdaiwa hajui mabadiliko na mwenendo wa deni lake.
 
Mambo ya HESLB yaache tu. Mkopo wangu ulikuwa around 9M, nimejikuta nalipa karibu 16M, items kwenye kuongezeka deni hazieleweki. Na hamna mjadala
 
Unapotosha sana we jamaa, kama hujaanza kulipa na bodi ya mikopo hawana taarifa zako kweli kunakua na penalty na retention fee. Mi niliomba statement ya balance tena kwa email tuu wakanitumia kila kitu kipo kama nilivyokua napiga hesabu. Hakuna ongezeko la deni wala cost zozote tangu nilipoanza kulipa. Kusoma sheria ni tofauti na kuielewa hiyo sheria. We cha kufanya omba statement ya deni lililobaki kama ulishaanza kulipa utaona. Ingekua hivyo kwamba kila mwaka linaongezeka kwa 6% unafikiri watu wangesubiri uwaongelee au wangeshaongea siku nyingi.?
 
Mara ya mwisho wewe kwenda bodi lin ? Tuanzie hapo? Kwanini unaandika kitu bila kufanya research kwanza?
 
Mwezi wa tano, na hii nilifanya kwa sababu deni limekaribia kuisha kwa mujibu wa salary slip yangu kwa hiyo nikaomba kujua balance kutoka bodi ya mikopo pia. Hakuna extra charges nilizoona mkuu. Ingawa kabla sijaanza kulipa kweli kuna penalty na cost nyingine ziliongezwa ila ni sahihi kabisa.

Je Hii Mada umeielewa vyema?
 
Amin
Mkuu hawa watu wakiwa mbele za watu huwa wanajifanya ni watu wema sana but kiuhalisia si watu wema....ebu mkuu tuwe wakweli katika awamu zote tangu tupate uhuru ni utawala upi ambao umekuwa kinara wa kutunga sheria kandamizi dhidi ya watanzania but haohao watungaji sheria kandamizi ndo kila siku wapo live kwenye ma tv wakijifanya ni watu wema sana....cha msingi ni kumwachia tu mungu atende haki sababu sisi tunaokandamizwa hatuna cha kuwafanya
 
Je Hii Mada umeielewa vyema?
nimekluelewa unapodai kua kuna asilimia 6% za kuongezeka kwa deni kila mwaka kitu amacho sio sahihi hata kidogo, na hata mdau mwingine amekuelewesha kua baada ya kuanza kulipa hakuna extra costs nyingine kama umeshaambiwa deni lako ni milion 16 ndio hizo utakazolipa kwa kipindi hicho. sasa hoja yako sijui ni ipi hapo. mana unajaribu kuaminisha watu kua deni litaongezeka kila mwaka kiasi kwamba litakua deni la maisha. wacha kupotosha watu, deni linatakiwa kulipwa ili wengine nao wanufaike pia. Pia uelewe kwamba kwa kupitia uchambuzi wako huo unaweza ukafanya mtu akaacha kuomba mkopo ilihali sio kweli kabisa na ungemsaidia na angelipa na vizuri tuu na maisha yangeendelea. tatizo tulitaka tusilipe kabisa ndio shida inapokuja. kama sheria umeona ina shida leta hapa hicho kifungu tukijadili ili kisije kikaanza kutumika vibaya ila usidanganye na mfano ulioutoa ni wa uongo kabisa.
 
Bila bumu nisingeweza kusoma so naishukuru sana bodi kwa hilo, ila baadaye nilikuja ‘kukengeuka’ na kuona hilo deni ni kubwa mno bora niache kuajiriwa kuliko kukatwa nitumike bure.... hiyo ni pesa pekee ya serikali ambayo kama raia nimeifaidi so kama hakuna namna nyingine ya kuniwajibisha nje ya ajira naomba tu tusisumbuane.
Serikali siwadai ajira ili wanilipe mshahara, nami msinidai bumu tufanye kama nimechukua GAWIO langu kama raia mwema.... win-win situation na kwa kweli sina mpango wa kulipa.
Hahaha jamaa umenifurahisha
 
Back
Top Bottom