Barua ya Wazi kwa familia ya Ali Hassan Mwinyi

Missile of the Nation

JF-Expert Member
May 24, 2018
13,498
51,092
Kwenu Familia ya Ali Hassan Mwinyi

1. Mzee Ali Hassan Mwinyi
Ulijiuzulu miaka ya 1970 kwa sababu ya mauaji ya watu wasio na hatia wakiwa katika mikono ya dola, leo napenda nikufahamishe mzee wetu kuwa kuna wananchi wa Zanzibar, wasio na hatia wanauawa Zanzibar bila haki, bila sababu za msingi isipokuwa tu ili mwana aliyetoka katika viuno vyako awe mtawala bila ridhaa ya wananchi wa Zanzibar.

Mzee Mwinyi, Ule uungwana ambao Watanzania walikufahamia, leo hii napenda upate taarifa kuwa kuna Wazanzibar leo damu zao zinagusa ardhi pasi na haki ili tu mwanao awe mtawala.

Umefanya nini mzee wetu mzee Mwinyi kuzuia dhulma hii ya watu wasio na hatia?. Utamueleza nini ALLAH wewe mzee wetu kwa kubariki na kushiriki kumuandalia mwanao utawala huko Zanzibar kwa kujitia upofu, kujisogeza karibu na watawala wa sasa, kuimba mapambio ili tu mwanao awe mtawala wa huko?

Mzee wetu mzee Mwinyi utawala uliopatikana kwa damu za watu kumwagika utaisaidiaje familia yako hapa duniani na ahera?

Nimekuandikia haya kwa sababu Hussein ni mwanao, laiti ungemkanya kuwa jambo analoshiriki lina viashiria vyote vya dhulma na hivyo aache angekusikiliza.

Lakini sasa itasaidia nini mnaswali, mnafunga, mnaenda kuhijji Makka lakini mwanao anashiriki dhulma ya waziwazi?

2. Kwako Hussein Mwinyi
Mwenyezi Mungu anasema kwenye Qur'an kuwa "Inna Llaha la yuflihu dhalimuun", Ikimaanisha hakika ya Mwenyezi Mungu hawafanyi madhalimu kuwa ni wenye kufaulu. Hebu tusemezane Hussein, Uko tayari damu kiasi gani ya Wananchi wasio na hatia wa Zanzibar imewagike ilimradi tu uwe raisi?

Uraisi una faida gani kwako kama ili uufikie lazima upande miili ya wananchi wa Zanzibar waliolazwa barabarani kwa risasi?

3. Kwako Abdullah na Abbasi Mwinyi
Mmemshauri nini Mzee wenu na Kaka yenu aachane na Uraisi huu unaoonekana umejaa damu za Wazanzibar zisizo ba hatia?
Je mko tayari familia yenu ikumbukwe na Watanzania na Wazanzibari kama familia ya dhulma?

Je mlimshauri kaka yenu aachane na jambo hili ambalo kimsingi linakwenda kumpa madhambi makubwa kwa kushiriki kwake kwenye dhulma ya kutisha?

Nyinyi kama familia mna shida gani, kama Majumba mnajengewa, kama pensheni ya mzee iko palepale, asilimia 80% ya mshahara wa rais wa sasa anapata. Sasa kutaka madaraka yote hata kutojali uhai wa wananchi wa Zanzibar mnatafuta nini?

4. Kwako mama yetu Sitti Mwinyi
Mama, Wazanzibar wanakufa mama, wanapigwa risasi, watu wanakua wajane, watu wanapoteza mama, baba zao huko Zanzibar, kwa sababu mwanao Hussein anataka madaraka kwa gharama yoyote!

Mama Umechukua hatua gani kumwambia mwanao aachane na jambo lenye dhulma ndani yake?
Ufalme na mamlaka utamsaidia nini kama ili kuufikia shuruti damu za watu zimwagike?

Mama ukweli ni kuwa mwanao hakubaliki Zanzibar, ni nguvu tu ya dhulma inatumika ili kumsimika madarakani.
Mama mwambie Hussein aachane na biashara hii ya uraisi si njema kwake, si njema kwa sababu njia anayopita imejaa mateso, manyanyaso, dhulma ya kutisha kwa watu waz Zanzibar.

Nimalizie kwa kuwakumbusha ndugu zangu wa familia ya Mzee Mwinyi

Allah anasema katika Qur'an tukufu
"Laa Tudhlim walaa tudhlmuun"
Maana yake Msidhulumu na wala msidhulumiwe

Sasa ni jukumu lenu enyi familia ya Mwinyi kujipima na kuona kama ndugu yenu Hussein Mwinyi anashiriki katika dhulma dhidi ya Wazanzibar na mjiangalie dhima yenu mbele ya ALLAH ni ipi, maana mtaulizwa, mlikuwa wapi wakati dhulma ikifanywa na mmoja wa wana familia yenu akishiriki kikamilifu na nyie mlifanya nini kuizuia? !

Nimefikisha kwenu!
 
Ibilisi yuko kazini sasa, japo wao watakudanganya wanamtanguliza Mungu
 
NA KWA MAONO YANGU Alhaji Mzee hamalizi huu mwaka kabla ya kupambana na adhabu ya akhera

Mzee Mwinyi unataka nini tena katika dunia hii ambacho bado hujakipata?

Laiti ungemkanya mwanao aachane na hii dhulma, damu za wananchi wasio na hatia wa Zanzibar zisingemwagwa kama tunavyoshuhudia leo!

Leo kweli Mzee Mwinyi na mwanao mnataka Wazanzibar wawalaani kama walivyomlaani Mkapa kwa mauaji aliyowatendea mwaka 2001?
 
Mzee Mwinyi ni mzee wa miaka 95 lakini bado anaipambania dunia utadhani kijana wa miaka 20

Mzee Mwinyi unataka nini tena katika dunia hii ambacho bado hujakipata?

Laiti ungemkanya mwanao aachane na hii dhulma, damu za wananchi wasio na hatia wa Zanzibar zisingemwagwa kama tunavyoshuhudia leo!

Leo kweli Mzee Mwinyi na mwanao mnataka Wazanzibar wawalaani kama walivyomlaani Mkapa kwa mauaji aliyowatendea mwaka 2001?

Miaka 95 ni umri wa kujiandaa kurudi kwa Muumba na sio kushiriki dhuluma dhidi ya wanadamu wenzako
 
Ole wao, Mungu hadhihakiwi. Eti ni familia mcha Mungu!!! Kwa mtindo huu moto wa ahera utaanza kuwaunguza hapa duniani na hatimaye ahera. Damu inayomwagika Zanzibar ni kuni za kuinguza familia hii na ukoo wote wa Magufuli.
 
NA KWA MAONO YANGU Alhaji Mzee hamalizi huu mwaka kabla ya kupambana na adhabu ya akhera

Wewe unaijua siku yako ya mwisho?

Kumbuka wako wanaoondoka wakiwa tumboni mwa mama zao, wapo wanaoondoka wakiwa watoto wachanga, wapo wanaoondoka wakiwa vijana pia. Mungu hapangiwagi bali anaombwa. Jiombee heri na usiwaombee wengine kifo

Maalim Seif kama mhamasishaji mkuu wa fujo Zanzibar anayewatuma wazanzibar kupiga police huku yeye na familia yake wakiwa salama majumbani mwao ana la kujibu juu ya haya yanayoendelea
 
Wewe unaijua siku yako ya mwisho?

Kumbuka wako wanaoondoka wakiwa tumboni mwa mama zao, wapo wanaoondoka wakiwa watoto wachanga, wapo wanaoondoka wakiwa vijana pia. Mungu hapangiwagi bali anaombwa. Jiombee heri na usiwaombee wengine kifo

Maalim Seif kama mhamasishaji mkuu wa fujo Zanzibar huku yeye na familia yake wakiwa salama majumbani mwao ana la kujibu juu ya haya yanayoendelea
siongei na wapuuzii
 
Back
Top Bottom