Barua ya wazi kwa Dada Halima Mdee

Kwako Dada Halima Mdee.

Sikupi pole kwa misukosuko iliyokukuta kwa sababu naamini unaistahili kutokana na kitendo ulichokifanya.

Nitakuwa mnafiki kujifanya nakuonea huruma, wakati kiukweli kabisa sikuonei huruma hata kidogo, maana naamini kuwa tamaa ya fedha kuliko Kuheshimu imani ya wananchi uliyopewa ni ubinafsi wa hali ya juu kupitiliza na lolote lililokukuta baada ya usaliti huo hupaswi kufutwa machozi, maana umeshiriki dhambi kubwa mno ya kutaka kufifisha ndoto za mamilioni ya wananchi walioweka imani katika upinzani na kwako binafsi wakiamini tuko pamoja bega kwa bega katika jitihada za kujenga Taifa la demokrasia zaidi, utawala bora zaidi, haki zaidi n. k

IIa nataka niongee na wewe mambo yafuatayo kukusaidia tu kiroho safi.

1. Tunaheshimu mchango wako kwa upinzani, tunakuomba usiendelee kushiriki kumnyonga mtoto uliyesaidia kumlea

Uongo mbaya, Halima unaomchango mkubwa, tena mkubwa kabisa kwenye kukua kwa upinzani nchini, Hiyo credit kamwe hatutokuondolea kwa sababu ni sehemu ya jasho lako. Kwa muktadha huo nakuomba sana, usikubali CCM wakugeuza kombora la kuibomoa kazi yako uliyoifanya kwa zaidi ya miaka 15, Usichana wako, the best years ya maisha yako uliitumia kwenye kujenga upinzani, japo umenikera kishenzi na naamini adhabu uliyopata ni haki yako, lakini nakuomba usikubali njama za CCM kukugeuza askari wa kuibomoa kazi yako mwenyewe.

CCM wanataka uvunje nyumba uliyoijenga, Usikubali, wewe waambie kuwa siyo kazi yangu kupambana na CHADEMA, hiyo ni kazi yenu. Wakatalie katakata, hao wanataka kukuchoresha na kuplay divide and rule.

2. Kula huo mpunga wa bure wa Ndugai, kisha tulia, lakini usikubali wakugeuze snitch

Halima kuna maisha baada ya migogoro, huko mbeleni utakuja kukaa na wapinzani kwenye kujadili issues, ni kama tu juzi aina Ndugai wamekutesa Bungeni, kukudhalilisha, kukuweka mahabusu, na kukufanyia kila aina ya ghilba lakini leo eti wanajifanya ni wema kwako. Halima hii ngoma usiichukulie personal, wewe kuwa low profile, usiwe kama yule mvulana Lijualikali, anapayuka na kuongea ujinga baada ya kufukuzwa, hiyo haikunsaisia yeye wala kutikisa CHADEMA.

Sasa wewe una akili kuliko Lijualikali, usifuate nyayo zake. Wewe kula huo mpunga wa Ndugai, buy time kisha uone siasa zitakunjuka vipi huko mbeleni, Lakini achana na kuiattack CHADEMA.

CHADEMA ya sasa hivi ni wananchi na siyo Mbowe, ni kupoteza muda kumshambulia Mbowe. Sisi wananchi tumesimama na maamuzi ya kamati kuu, kwa hiyo wewe kausha tu, kula hizo hela, tukutane huko mbele ya safari tuyajenge maana siasa haina rafiki wa kudumu au adui wa kudumu bali maslahi, Tatizo wewe uliweka mbele maslahi yako zaidi kuliko sisi wananchi ndo maana tunakuona fala

3. Kama Ndugai atakulindia ubunge wako achana na ishu za mahakama

Kwa sasa huaminiki ndani ya chama, hata ukipewa huo uanachama wa mahakama haikusaidii chochote kisiasa, Itakuwa ni mbinu tu ya hao handlers wako kuleta mgogoro tu ndani ya chama chako cha zamani ulichokipenda sana.

Wanaweza kukupa masharti kuwa ili wakulibdie ubunge wako sharti uende mahakamani kupigania uanschama wako, Sasa ngoja nikuibie siri, yaani jinsi wewe unavyoutaka huo Ubunge ili uoige hela, ndivyo jinsi na wao wanavyotamani wewe na wazinguaji wenzako wengine 18 muendelee kubaki Bungeni, maana kamwe hawatoweza kuwatoa Bungeni kwa hoja eti nyie siyo wanachama tena wa CHADEMA, wakifanya hivyo nao watajivua nguo mbele ya umma kuwa walibariki mchakato haramu wa kuwaapisheni kuwa Wabunge.

Kwa hiyo msiwe na wasiwasi, Ndugai atake asitake lazima atawalinda tu ili kulinda heshima ya Taasisi yake. Kwa hiyo msikubali kwenda mahakamani maana mtazidi kuwakasirisha wananchi zaidi, mtadharaulia zaidi, mtachukiwa zaidi.

Sasa akili ni hivi, wewe nyuti, kula huo mpunga wa CCM, achana na mahakama, huna haja ya kwenda mahakamani maana nina uhakika mpunga wako huko bungeni uko palepale. Usishiriki kuwasaidia hao waliokuibia kura na kukudhalisha kwa kukupa Viti Maalum

4. Wewe ni mpinzani wa asili, endelea kupiga kazi huenda tukakufikiriafikiria

Sasa kwa kuwa wewe siyo mwanachama tena wa CHADEMA, lakini tunatambua mchango wako kwenye upinzani, unayo nafasi ya kumend ties na wananchi. Lazima uwe na subira sana kwenye hili, lazima uombe msamaha kwa wananchi kwa vitendo. Japo umekula haramu, umejirahisisha mbele ya madhalimu kwa sababu ya njaa yako ambayo kwa namna moja imekuwa engineered makusudi na watesi wenu ambao leo hii wanajidanya kuwapendeni kumbe ni unafiki mtupu.

Mtesi wenu aligundua kuwa kuwachapa risasi ni counterproductive na inabackfire, sasa njia nzuri ni kuwachapa kiuchumi na kimahakama na hiyo ndo modus operandi yake, na kweli amefanikiwa ndiyo maana wengi katika kambi yenu wameunga mkono juhudi, na bahati mbaya na wewe Dada Halima hii teknic ya "njaa" imekusomba na wewe.

Sasa iko hivi pambana sana kurudisha credibility kwetu, humohumo bungeni endelea kuzungumzia issues za wananchi. Kama ukitukosha huenda tukakufikiria kidogokidogo, lakini ukigeuka na kuwa mwanasiasa "malayamalaya", hakuna atakayekuwa na time wewe tena!

5. Jifunze wewe Dada, mafanikio ni zaidi ya pesa

Usaliti ni kansa, ondoa hii kansa once and for all. Hata ukienda CCM, kama una mentality hizi za kusalitisaliti sababu ya vijipesa na fursa, kamwe huwezi kuwa msaada kwa Taifa. Sellouts hawana nafasi kwenye mabaraza ya watu wa heshima. Jirekebishe!
acha kumpotosha mtu mwenye Elimu yake bro. wewe ndo ulimsomesha Mdee kwani, huo sio muda wa Mdee kutumia Elimu yake kwenye siasa za uanaharakati na ubishi.
 
Nilichokielewa ni kuwa watu wengi wana wivu na halima kwa sababu ubunge una hela

Ingekuwa ubunge hauna ishu yoyote ya yy kupata pesa sidhan kama kelele zote zingekuwepo

Barua yako ni mzuri Sana but umeongea kutokana na kusikiliza na kuamini upande mmoja

Let's wait kwa press ya Mdee then tusikie upande wa pili

Coz maybe ni kweli myika alipeleka majina 30 but kosa la Mdee ni kuedit hayo majina bila ruhusa ya kamati kuu
Sure! Na ni Mnyika alienda gerezani akamtoa nusrat usiku kabla ya case yake mahakamani!
 
Hapokei tena hizo barua maana amepokea nyingi sana ndani ya wiki hii nyingi hazina maana!
Hahahah amekuwa amekuwa shujaa leo siyo tena mpinga maendeleo. Yule uliyeshangilia alipotaka kuwapa na policcm/ magereza ? Yule ambaye ukiimba aozzee gerezani cc tukachanga kumtoa? Yule aliyefungiwa mwaka mzima na speaker ndugai??? Kwakweli mtu mweusi kama wewe unas Shida kubwa sana kichwani. Namlaani aliyeanzisha chuo cha mwalimu nyerere.kule mnakofundishana kuiba kura
 
Ndiyo maana waiocheza mchezo huu wameanza kuondoewa chamani kina PoaPoa. Ngoma imedunda waitaka kudanganya Jumuiya za kimataifa kuwa kuna upinzani Tanzania wamejikuta wameshidwa, hakukuwa na namna nyingine zaidi ya kuanza kuwaondoa chamani, waweze kuja na mbinu mpya. CCM wakae meza moja na CHADEMA basi. Watu kama Msekwa watunga katiba ya nchi wamesema hao si wabunge unadhani Jumuiya za Kimataifa zitawaeewa hata kama Ndungai ataendeea kuwainda Covid 19. Mabeberu hawatatoa pesa zao maana wataona hiozo kamati CCM wanazongangania ziundwe na wapinzania ni feck, magumashi tuu. Mabeberu wana akiii huwezi kuwadanganya kwa njia za kitoto hivyo wakupe pesa za waipa kodi wao.
 
Sure! Na ni Mnyika alienda gerezani akamtoa nusrat usiku kabla ya case yake mahakamani!
Mbona cheq alikuwa anapelekewa gerezani wakati bavicha wanataka kutoa ela? Yote yanawezekana as long as mwenyewe ameridhika

Kama jela alikaa yy na familia yake ndio ilikuwa inaumia, na yy amekubali kuwa mbunge Sasa shida ni nn
 
Mbona cheq alikuwa anapelekewa gerezani wakati bavicha wanataka kutoa ela? Yote yanawezekana as long as mwenyewe ameridhika

Kama jela alikaa yy na familia yake ndio ilikuwa inaumia, na yy amekubali kuwa mbunge Sasa shida ni nn
Kuna utaratibu was kutolewa gerezani usiku!? Ebu fafanua kidogo
 
Njaa mbaya sana kaka,,,

Heshima ni bora kuliko fedha, na utu ni bora kuliko dhahabu!"

Halima Mdee alipaswa kujifunza kwa wabunge wenzake waliohama chadema na kujiunga na ccm kwamadai ya kuunga mkono juhudi jinsi walivyopigwa chini na wajumbe!

Mwana kulitafuta mwana kulipata!

Mwana kilanga hakaliwi matanga!
 
Mbunge unakaa bungeni miaka kumi na mitano , kumi , mitano mshahara mnono , opportunity kibao , pension ya mamilioni halafu huna hata mradi wowote ule wa kukuingizia kipato ? Ni akili matope ? . Matokeo yake ndio haya kununuliws kwa vijisenti .
 
Back
Top Bottom