Barua ya wazi kwa Dada Halima Mdee

Missile of the Nation

JF-Expert Member
May 24, 2018
13,495
51,089
Kwako Dada Halima Mdee.

Sikupi pole kwa misukosuko iliyokukuta kwa sababu naamini unaistahili kutokana na kitendo ulichokifanya.

Nitakuwa mnafiki kujifanya nakuonea huruma, wakati kiukweli kabisa sikuonei huruma hata kidogo, maana naamini kuwa tamaa ya fedha kuliko Kuheshimu imani ya wananchi uliyopewa ni ubinafsi wa hali ya juu kupitiliza na lolote lililokukuta baada ya usaliti huo hupaswi kufutwa machozi, maana umeshiriki dhambi kubwa mno ya kutaka kufifisha ndoto za mamilioni ya wananchi walioweka imani katika upinzani na kwako binafsi wakiamini tuko pamoja bega kwa bega katika jitihada za kujenga Taifa la demokrasia zaidi, utawala bora zaidi, haki zaidi n. k

IIa nataka niongee na wewe mambo yafuatayo kukusaidia tu kiroho safi.

1. Tunaheshimu mchango wako kwa upinzani, tunakuomba usiendelee kushiriki kumnyonga mtoto uliyesaidia kumlea

Uongo mbaya, Halima unaomchango mkubwa, tena mkubwa kabisa kwenye kukua kwa upinzani nchini, Hiyo credit kamwe hatutokuondolea kwa sababu ni sehemu ya jasho lako. Kwa muktadha huo nakuomba sana, usikubali CCM wakugeuza kombora la kuibomoa kazi yako uliyoifanya kwa zaidi ya miaka 15, Usichana wako, the best years ya maisha yako uliitumia kwenye kujenga upinzani, japo umenikera kishenzi na naamini adhabu uliyopata ni haki yako, lakini nakuomba usikubali njama za CCM kukugeuza askari wa kuibomoa kazi yako mwenyewe.

CCM wanataka uvunje nyumba uliyoijenga, Usikubali, wewe waambie kuwa siyo kazi yangu kupambana na CHADEMA, hiyo ni kazi yenu. Wakatalie katakata, hao wanataka kukuchoresha na kuplay divide and rule.

2. Kula huo mpunga wa bure wa Ndugai, kisha tulia, lakini usikubali wakugeuze snitch

Halima kuna maisha baada ya migogoro, huko mbeleni utakuja kukaa na wapinzani kwenye kujadili issues, ni kama tu juzi akina Ndugai wamekutesa Bungeni, kukudhalilisha, kukuweka mahabusu, na kukufanyia kila aina ya ghilba lakini leo eti wanajifanya ni wema kwako. Halima hii ngoma usiichukulie personal, wewe kuwa low profile, usiwe kama yule mvulana Lijualikali, anapayuka na kuongea ujinga baada ya kufukuzwa, hiyo haikumsaidia yeye wala kutikisa CHADEMA.

Sasa wewe una akili kuliko Lijualikali, usifuate nyayo zake. Wewe kula huo mpunga wa Ndugai, buy time kisha uone siasa zitakunjuka vipi huko mbeleni, Lakini achana na kuiattack CHADEMA.

CHADEMA ya sasa hivi ni wananchi na siyo Mbowe, ni kupoteza muda kumshambulia Mbowe. Sisi wananchi tumesimama na maamuzi ya kamati kuu, kwa hiyo wewe kausha tu, kula hizo hela, tukutane huko mbele ya safari tuyajenge maana siasa haina rafiki wa kudumu au adui wa kudumu bali maslahi, Tatizo wewe uliweka mbele maslahi yako binafsi zaidi kuliko sisi wananchi ndo maana tunakuona fala

3. Kama Ndugai atakulindia ubunge wako achana na ishu za mahakama

Kwa sasa huaminiki ndani ya chama, hata ukipewa huo uanachama wa mahakama haikusaidii chochote kisiasa, Itakuwa ni mbinu tu ya hao handlers wako kuleta mgogoro tu ndani ya chama chako cha zamani ulichokipenda sana.

Wanaweza kukupa masharti kuwa ili wakulindie ubunge wako sharti uende mahakamani kupigania uanachama wako, Sasa ngoja nikuibie siri, yaani jinsi wewe unavyoutaka huo Ubunge ili upige hela, ndivyo jinsi na wao wanavyotamani wewe na wazinguaji wenzako wengine 18 muendelee kubaki Bungeni, maana kamwe hawatoweza kuwatoa Bungeni kwa hoja eti nyie siyo wanachama tena wa CHADEMA, wakifanya hivyo nao watajivua nguo mbele ya umma kuwa walibariki mchakato haramu wa kuwaapisheni kuwa Wabunge.

Kwa hiyo msiwe na wasiwasi, Ndugai atake asitake lazima atawalinda tu ili kulinda heshima ya taasisi yake. Kwa hiyo msikubali kwenda mahakamani maana mtazidi kuwakasirisha wananchi zaidi, mtadharaulika zaidi, mtachukiwa zaidi.

Sasa akili ni hivi, wewe nyuti, kula huo mpunga wa CCM, achana na mahakama, huna haja ya kwenda mahakamani maana nina uhakika mpunga wako huko bungeni uko palepale. Usishiriki kuwasaidia hao waliokuibia kura na kukudhalisha kwa kukupa pipi ya Viti Maalum, yale ni matusi!

4. Wewe ni mpinzani wa asili, endelea kupiga kazi huenda tukakufikiriafikiria

Sasa kwa kuwa wewe siyo mwanachama tena wa CHADEMA, lakini tunatambua mchango wako kwenye upinzani, unayo nafasi ya kumend ties na wananchi. Lazima uwe na subira sana kwenye hili, lazima uombe msamaha kwa wananchi kwa vitendo. Japo umekula haramu, umejirahisisha mbele ya madhalimu kwa sababu ya njaa yako ambayo kwa namna moja au nyingine imekuwa engineered makusudi na watesi wenu ambao leo hii wanajidanya kuwapendeni kumbe ni unafiki mtupu.

Mtesi wenu aligundua kuwa kuwachapa risasi ni counterproductive na inabackfire, sasa njia nzuri ni kuwachapa kiuchumi na kimahakama na hiyo ndo modus operandi yake, na kweli amefanikiwa ndiyo maana wengi katika kambi yenu wameunga mkono juhudi kutokana na njaa, na bahati mbaya na wewe Dada Halima hii teknic ya "njaa" imekusomba hata wewe.

Sasa iko hivi pambana sana kurudisha credibility kwetu, humohumo bungeni endelea kuzungumzia issues za wananchi. Kama ukitukosha huenda tukakufikiria kidogokidogo, lakini ukigeuka na kuwa mwanasiasa "malayamalaya", hakuna atakayekuwa na time wewe tena!

5. Jifunze wewe Dada, mafanikio ni zaidi ya pesa

Usaliti ni kansa, ondoa hii kansa once and for all. Hata ukienda CCM, kama una mentality hizi za kusalitisaliti sababu ya vijipesa na fursa, kamwe huwezi kuwa msaada kwa Taifa. Sellouts hawana nafasi kwenye mabaraza ya watu wa heshima. Jirekebishe!
 
Hapokei tena hizo barua maana amepokea nyingi sana ndani ya wiki hii nyingi hazina maana!
 
Watu wanashidwa kuelewa na kujifundisha kwamba, mpango wowote wa kufanya uasi, ukishirikiana na "MTANZANIA" tu, jiandae kwamba "MISSION FAILED".

CCM wali miscalculate huu "UPUUZI KWA KIWANGO CHA SGR" wa kuwanunua hao Covid-19. Walijua mission itakuwa success kama walivyokuwa wakinunua "MADIWANI na WABUNGE", ila hawakujua uzito wa hili jambo la kulazimisha na kufoji list ya wabunge wa viti maalum.

Tokea Covid-19 walivyojipeleka kuapishwa bungeni, sisi wengine tulijua its just a matter of time aibu itawafika "NEC, A.G, SPEAKER na CCM". Na ndio dunia itazidi kuidharau na kuigharimu "SERIKALI YA MAGUFULI".

Halima Mdee ajiandae, hakujifunza kwa aliekua mbunge wa Kinondoni (Alifanya uasi baada ya kununuliwa, akapewa ahadi atapata nafasi ya kugombea tena - Mwisho wa siku akasimamishwa kugombea ABBAS TARIMBA) na wengine waliokubali kuuza UTU wao kwa vitisho/rushwa/ahadi za uongo.

Team Covid-19 mpaka sasa hivi wamepatwa na "MSHTUKO KISAIKOLOJIA".

Hawakutegemea watanzania wange react kama walivyo react, na CHADEMA wangefanya maamuzi waliofanya. Walijua wataungwa mkono.

Hawakutegemea process za kisheria za kuwaapisha zinge gubikwa na kasoro. Hawakutegemea kiapo chao kingekua batili. Wameshakuwa na uoga kuanzia uraiani mpaka huko walipo.

Mpaka sasa hivi 16 wapo tayari kumuasi Halima Mdee na kurudi kuomba msamaha, sambamba na kusema ukweli juu ya mpango wote ulivyofanyika A-Z. Ni uoga tu ndio utawacheleweshwa.

Covid-19 watajikuta wamebakia Halima na Ester tu. Na ndio utakuwa mwisho wao "KISIASA" hata wakihamia CCM na kuchaguliwa kuwa wabunge-wateule wa Rais (Ndio kete iliobakia kwao).

WASICHOTAMBUA.

Wabunge wa CCM wote waliopo bungeni hawawakubali, wanawaona nuksi kwenda kwao upande wa CCM, wengi wao wanaona wanakwenda kugombea nafasi za wana CCM kwenye uteuzi. Na wanajiandaa kuanza kuwafanyia fitna na vitimbi.
 
Nilichokielewa ni kuwa watu wengi wana wivu na halima kwa sababu ubunge una hela

Ingekuwa ubunge hauna ishu yoyote ya yy kupata pesa sidhan kama kelele zote zingekuwepo

Barua yako ni mzuri Sana but umeongea kutokana na kusikiliza na kuamini upande mmoja

Let's wait kwa press ya Mdee then tusikie upande wa pili

Coz maybe ni kweli myika alipeleka majina 30 but kosa la Mdee ni kuedit hayo majina bila ruhusa ya kamati kuu
 
Ikiwa spika mstaafu kasema wale hawana sifa za kua wabunge nasubiri kuona janja ya ndugai atawakingia kifua vipi.

Ila mwisho wa siku ata wao ccm wamekuja shituka kuna vitu hawakukamilisha kuweka ili jambo sawa, mfano mahera kaishapishanisha kauli “tarehe 20 alisema hajapokea barua ofisi kwake,ila juzi kajisemea tarehe 19 alikua kapokea maombi.
 
Kwani mwambe si alivuliwa uanachama mbona amekaa bungeni muda wote?
 
Ikiwa spika mstaafu kasema wale hawana sifa za kua wabunge nasubiri kuona janja ya ndugai atawakingia kifua vipi.

Ila mwisho wa siku ata wao ccm wamekuja shituka kuna vitu hawakukamilisha kuweka ili jambo sawa, mfano mahera kaishapishanisha kauli “tarehe 20 alisema hajapokea barua ofisi kwake,ila juzi kajisemea tarehe 19 alikua kapokea maombi.

Dili limebuma location akuendeki
 
Watu wanashidwa kuelewa na kujifundisha kwamba, mpango wowote wa kufanya uasi, ukishirikiana na "MTANZANIA" tu, jiandae kwamba "MISSION FAILED".

CCM wali miscalculate huu "UPUUZI KWA KIWANGO CHA SGR" wa kuwanunua hao Covid-19. Walijua mission itakuwa success kama walivyokuwa wakinunua "MADIWANI na WABUNGE", ila hawakujua uzito wa hili jambo la kulazimisha na kufoji list ya wabunge wa viti maalum.

Tokea Covid-19 walivyojipeleka kuapishwa bungeni, sisi wengine tulijua its just a matter of time aibu itawafika "NEC, A.G, SPEAKER na CCM". Na ndio dunia itazidi kuidharau na kuigharimu "SERIKALI YA MAGUFULI".

Halima Mdee ajiandae, hakujifunza kwa aliekua mbunge wa Kinondoni (Alifanya uasi baada ya kununuliwa, akapewa ahadi atapata nafasi ya kugombea tena - Mwisho wa siku akasimamishwa kugombea ABBAS TARIMBA) na wengine waliokubali kuuza UTU wao kwa vitisho/rushwa/ahadi za uongo.

Team Covid-19 mpaka sasa hivi wamepatwa na "MSHTUKO KISAIKOLOJIA".

Hawakutegemea watanzania wange react kama walivyo react, na CHADEMA wangefanya maamuzi waliofanya. Walijua wataungwa mkono.

Hawakutegemea process za kisheria za kuwaapisha zinge gubikwa na kasoro. Hawakutegemea kiapo chao kingekua batili. Wameshakuwa na uoga kuanzia uraiani mpaka huko walipo.

Mpaka sasa hivi 16 wapo tayari kumuasi Halima Mdee na kurudi kuomba msamaha, sambamba na kusema ukweli juu ya mpango wote ulivyofanyika A-Z. Ni uoga tu ndio utawacheleweshwa.

Covid-19 watajikuta wamebakia Halima na Ester tu. Na ndio utakuwa mwisho wao "KISIASA" hata wakihamia CCM na kuchaguliwa kuwa wabunge-wateule wa Rais (Ndio kete iliobakia kwao).

WASICHOTAMBUA.

Wabunge wa CCM wote waliopo bungeni hawawakubali, wanawaona nuksi kwenda kwao upande wa CCM, wengi wao wanaona wanakwenda kugombea nafasi za wana CCM kwenye ueuzi. Na wanajiandaa kuanza kuwafanyia fitna na vitimbi.
Vipi kama wameenda huko kwa nguvu (si kwa ushawishi)? Nasema "kama..."
 
Back
Top Bottom