Barua ya wazi kwa Chancellor ST Augustine University Mwanza

kimbweto

Member
Oct 6, 2012
53
189
Ndugu,mimi ni mwanafunzi niliyemaliza chuo st Augustine mwanza campass 2017 baada ya kumaliza chuo nilibaini kwamba cheti changu cha chuo kimekosewa majina.

Nikafanya taratibu zote kufaikisha zoezi la marekebisho ya cheti. Hadi hivi sasa kwa takribani miezi nane nimekuwa nikifatilia cheti kwenye ofisi zako haswaa ofisi ya Corporate. Lakini nimekuwa nikipigwa dana dana,njoo leo,njoo kesho lakini hakuna cha kueleweka.

Ndugu Chancellor katika ofisi zako kumekuwa na ugumu kwa watia saini kusaini cheti changu,sijajua tatizo ni nini, saini ya chancellor, saini ya deputy na vice zimekuwa kama dhahabu, licha ya kuwa kusaini na kunipa cheti changu ni wajibu wenu.

Nimepoteza muda mwingi na nimekuwa nashindwa hata kuomba kibarua kwa kuwa cheti changu mmezuia watumishi wa Mungu nyinyi.

Nawakumbusheni nilipokuwa nachelewesha malipo kwenye chuo chenu mlikuwa mkinipiga penati sasa kwa nini hamuwajibiki?

Kibaya zaidi elimu ya chuo kikuu nimeipata pasina mkopo kwa kujishughulisha na shughuli za ujenzi wa kusaidia iweje kusaini cheti mtumie miezi zaidi ya nane?

Chuo kina jina kubwa la mwanafalsafa ST Augustine wa Hippo lakini mnashindwa kufikiria adha tunayoipata masikini kama mimi ambaye umeninyima nafasi kwa sekunde zako mbili za kusaini cheti wewe na wafuasi wako.

Ndugu Chancellor kinachosumbua chuoni mwako ni kutokuwa na uwajibikaji na usimamizi kutokuwa makini. Wakuu wa maofisi wanafanya safari binafsi pasi na tazama maslahi ya chuo. Watumishi hawawajibiki wanatumia muda mwingi kuchat na simu zao huku wakishindwa kutambua majukumu yao.

Mwisho ofisi ya Corporate chuoni mwako iwekwe watu wenye kufanya kazi kwa weledi na kutambua majukumu yao. Pia naomba hayo niliyoyaeleza uyafanyie kazi kwelikweli.

ACCEPT CONSTRUCTIVE CRITICISM.
 
Chancelor ulishamuandikia barua hakurespond? (Maana unapotoa malalamiko kama haya publicly kuna kuharibu image za taasisi za watu).
 
Kusoma tanzania kunakufanya uolewe (kuajiriwa) kwa kweli. Samahanini kuajiriwa ni kuolewa mlioajiriwa mapovu ruksa.
.
Ushapata elimu jiajiri (owa) masuala ya kupata saini za V.C na Chancellor fuatilia taratiiiiiibu.
 
Pole lakini nasikitika vyuo vyetu sijui vimekuwaje. Yaani graduates mnavyoandika... Hata Kiswahili kimewashinda! Hivi vyeti mnavyozungumzia sijui mmevipaje? Ama ndivyo vile anavyoongea Dr Shule? Mathalani hii "Cooperate" ndio nini? Hata punctuation inayofundishwa primary na secondary inawashinda! Naamini watu wa corporate wamekusikia. Wasije tu wakaweka jina "Kimbweto" kwenye cheti chako wakati jina ni la JF tu.
 
Hujui tofauti ya utengenezaji na utiaji saini wa transcript na certificate! Hizi ni
Documents 2 tofauti zenye utaratibu tofauti wa production and signing. The latter involves external supplier and its production/reproduction to rectify changes/correction of names may take even a year. Kuna usiri mkubwa kwenye utengenezaji wake ili kuminimize fake certificates!! Vinaweza kutengenezwa hata nje ya nchi. Dogo, umeenda shule ila hujaelimika.
 
dogo kesho ripoti kwa paroko aliyekaribu na wewe kwa ajiri ya kukuhoji nidhamu yako yenye ukakasi.
 
Msomi anakuaje hivi nikipewa cheti ntakuwa msomi,we utakuwa mwalim mwenzangu,maana walim tupo critical utafikiri hamna mikopo
 
dogo kesho ripoti kwa paroko aliyekaribu na wewe kwa ajiri ya kukuhoji nidhamu yako yenye ukakasi.
Yaani mtu anadai haki yake ambayo alii inunua na kuutumia muda wake wa miaka kibao kuweza kuipata ", then mnamuambia kwamba Hana nidhamu"... Acheni kumtisha dogo Aisee"... hatujui hela aliyokuwa anaitumia kusoma aliipata kwenye mazingira yapi
 
Hujui tofauti ya utengenezaji na utiaji saini wa transcript na certificate! Hizi ni
Documents 2 tofauti zenye utaratibu tofauti wa production and signing. The latter involves external supplier and its production/reproduction to rectify changes/correction of names may take even a year. Kuna usiri mkubwa kwenye utengenezaji wake ili kuminimize fake certificates!! Vinaweza kutengenezwa hata nje ya nchi. Dogo, umeenda shule ila hujaelimika.
we nawe hujaelimika pia, maana kama ungekuwa umeelimika ungempa mwongozo wa nini afanye na sio kumtusi
 
Kusoma tanzania kunakufanya uolewe (kuajiriwa) kwa kweli. Samahanini kuajiriwa ni kuolewa mlioajiriwa mapovu ruksa.
.
Ushapata elimu jiajiri (owa) masuala ya kupata saini za V.C na Chancellor fuatilia taratiiiiiibu.
mkuu niambie venture yako ilipo ...nije kukutembelea najua ntapata ushauri wa jinsi ya kuwekeza (kujiajiri)..maana inaonekana una mafanikio sana kwa kujiajiri
 
Pole lakini nasikitika vyuo vyetu sijui vimekuwaje. Yaani graduates mnavyoandika... Hata Kiswahili kimewashinda! Hivi vyeti mnavyozungumzia sijui mmevipaje? Ama ndivyo vile anavyoongea Dr Shule? Mathalani hii "Cooperate" ndio nini? Hata punctuation inayofundishwa primary na secondary inawashinda! Naamini watu wa corporate wamekusikia. Wasije tu wakaweka jina "Kimbweto" kwenye cheti chako wakati jina ni la JF tu.
Mkuu katika hili anahitaji kusaidiwa kwanza baadae utaleta hayo.
 
Back
Top Bottom