Barua ya wazi kwa chama changu: Hatari iliyoletwa na UKAWA

Ilongailunga

JF-Expert Member
Jan 18, 2012
1,388
895
UCHAGUZI wa serikali za mitaa umetoa funzo moja kubwa, kuwa sasa CCM haipaswi kudharau kile kinachoitwa ukawa waswahili husema ukicheka na nyani utavuna mabua.

Ni kweli CCM imeshinda viti vingi vya mitaa, vijiji na vitongoji lakini pia ni dhahiri kuwa pale ambapo CCM walipokumbana na UKAWA mchuano ulikuwa mkali sana na pengine ilibidi Howard Webb aamue matokeo. Watu wa mikakati ndani ya chama ni vema wakatambua ukweli huo na waje na majibu ya changamoto hiyo mpya.

Ni rahisi sana kuona hatari iliyopo kisiasa na kimkakati kwa chama chetu pendwa kuacha hichi kinachoitwa ukawa kiendelee, mosi, chama kitashindwa kutambua shabaha(target) katika uga wa mapambano ya kisiasa, kwa vile kitajikuta kina target nyingi (CUF, CHADEMA, NCCR) tena shabaha hizo zinabadilika kila kata na kila jimbo hapa itakuwa ni vigumu sana kuifanya mikakati ya kitaifa isinyae na ipinde(to shrink and bend) kuikabili kila shabaha.

Hapa ieleweke kuwa hali ni tofauti sana kila chama kikishindana chenyewe kwa vile nguvu ya vyama vinavyounda ukawa itapungua sana kwani itabidi vishindane vyenyewe na pia vishindane na chama tawala.

Pili sasa ni vigumu sana kupenyeza siasa za kipropaganda za kufanya vyama hivi vitengwe na jamii, kwani itakuwa ni vigumu kutafuta hoja moja kwa vyama vyote, hapa nisisitize kuwa hata ile hofu ya baadhi wananchi kuwa vyama hivi vinamuelekeo wa kidini au kikanda taratibu inaanza kutoweka na kufutika kabisa matokeo yake UKAWA imefanikiwa kuwaunganisha zaidi watu wa dini na kanda mbalimbali na kutengeneza political front kubwa zaidi.

Tatu, kuendelea kuacha Ukawa uishi maana yake itawahamasisha zaidi watu kujihusisha na siasa za siku hata siku(Political mobilization) hatari niinayoiona hapo nikuwa CCM haitakuwa active actor katika hiyo political mobilization kama mtaalamu mmoja wa sayansi ya siasa alivyosema “if you cannot mobilize you have neither control nor influence on those people”(kama huwezi kuhamasisha hutakuwa na udhibiti wala ushawishi kwa watu waliohamasika-tafsiri yangu) ni wazi kuwa kundi kubwa la wanasiasa “wapya” litajiunga na siasa za upinzani.

Hii haina maana kuwa chama hakita pata wafuasi au wanachama wapya la hasha kitapata ILA wengi wao watakuwa ni wale wanayoitazama leo yao badala ya kesho ya chama.

Nne ni vema tukajiuliza katika siasa za dunia ya tatu utawezaje kudhibiti nidhamu ndani ya chama huku ukiacha upinzani ukue na hatimaye kuanza kuwa na nguvu kubwa? Jibu ni wazi kuwa huwezi kwakuwa kutakuwa na political altenative kwa wanasiasa, kuwa sasa mtu ataona ni mkubwa kuliko chama kwa kuwa sasa chama chake(CCM) si muhimu kwa yeye kupata nafasi ya kuchaguliwa, ikumbukwe kuwa siasa za dunia ya tatu sio za kiitikadi bali kwa kiwango kikubwa ni siasa za kiuongozi.

Ieleweke kuwa si dhamira yangu kushauri kuwa vyama vya upinzani vifutike lakini ni wazi kuwa kukua kwa vyama vya upinzani ni kudumaa kwa chama tawala, hivyo chama tawala hakipaswi kukaa na kukunja mikono bila kufikiria na kupanga mikakati ya kupigania uwepo wake na nafasi yake katika nchi, CCM inaweza kufanya wait and see strategic kusubiri UKAWA usambaratike, viongozi wa ukawa wakifanya hivyo wanajua watakuwa wamejigeuza kuwa alaughing stock, CCM iamke sasa na itupilie mbali shuka kubwa ililojifunika hadi usoni mpaka haioni mwanga wa kijua cha asubuhi, iamke ibadili mikakati yake ya mapambano dhidi ya adui mpya anayetumia mbinu mpya, kumeshapambazuka!
 
Ushauri mzuri sana huu ila it's too late to hold ..CCM haiponi katu kwani Mungu kashaamua kuwaponya watesi wake
 
Pia mjitaidi kumfundisha NApe nnauye hesabu za kujumlisha na asilimia

kwamba ikiwa mwaka 2009 ulikuwa na viti 153 kwa sifuri za ukawa na sasa 2014 umebakiwa na 78 kati ya 153 unakuwa hujashinda bali umepoteza au umeshindwa kwa asilimia -49%
 
Pia mjitaidi kumfundisha NApe nnauye hesabu za kujumlisha na asilimia

kwamba ikiwa mwaka 2009 ulikuwa na viti 153 kwa sifuri za ukawa na sasa 2014 umebakiwa na 78 kati ya 153 unakuwa hujashinda bali umepoteza au umeshindwa kwa asilimia -49%

Nape hesabu ndogo kama hizi anazijua ila kajifanya El Sahaf!
 
Uwezi kutegemea kuongoza kwa kuweka mapingamizi,nadhani katika katiba mpya kama kuna sehemu ya kuongezea basi ili la mapingamizi ya hila liwekwe,kuwa inapoonekana kuna dosari mgombea apewe siku mbili za kurekebisha dosari hizo na sio kusubiri eleventh hour unaleta mapingamizi.Ushindi wa mapingamizi sio ushindi bali ni ushindi wa hila
 
Ni uchambuzi mzuri, umejikita kwenye uhalisia. Tatizo lilipo ni wakati tu.

CCM haijatamani kukubali hilo na imeendelea kung'ang'ania mbinu na mikakati ileile ya wakati wa nyuma ilhali wakati hautamani tena uhai wa mikakati husika.

Mabadiliko ya kizazi yanahitaji mifumo ya kisiasa iendane na uhalisia wake la sivyo utawaongoza watu wanaoweza kugeuka na kukupigia kura ya chuki na kumpa uongozi hata asiye na mwelekeo. Mazoea yanaigharimu CCM.

Wanaoaminika ni kizazi kipya, akina Nape na wengine wa aina yake wamekosa innovation (ubunifu) wa kuendesha siasa mpya ndani ya chama kikongwe! Itawagharimu
 
Good analysis. Lakini lazima tujue kwamba dunia inabadilika. I personally kwa sasa naona kama raia wa Tanzania wajibu wangu ni kujiandikisha na kupiga kura. And I did that last weekend. And I saw the impact of a single vote. Tatizo la CCM nadhani haioni haja ya kuwatumikia wale walioichagua. Ila kuwaneemesha wachache wenye connection. CCM should faithfully heed maneno ya Bob Marley (you cant fool ALL the people ALL the time). Its human nature.

From my point..change will certainly come in Tanzania (in the next decade majority ya CCM bungeni itakuwa historia-mark my words!). Swala is how are we prepared (vyama, viongozi na wananchi) kupokea na kumanage hayo mabadiliko? Tukiweza hili, tutakuwa tumeuvuka na kushinda mtihani mkubwa katika taifa letu pendwa.

Kitu ambacho Mbowe na wenzake wamefanikiwa (na naamini wataongeza nguvu) ni kuwafanya watanzania wajiamini kwamba they are incharge of their own destiny! And I must salute them for this vision!

That change is coming? Sidhani kama kuna binadamu au mwananchi yeyote bado ana wasi wasi na hili. Labda wale waliousingizini tuu.

Masanja
 
Uwezi kutegemea kuongoza kwa kuweka mapingamizi,nadhani katika katiba mpya kama kuna sehemu ya kuongezea basi ili la mapingamizi ya hila liwekwe,kuwa inapoonekana kuna dosari mgombea apewe siku mbili za kurekebisha dosari hizo na sio kusubiri eleventh hour unaleta mapingamizi.Ushindi wa mapingamizi sio ushindi bali ni ushindi wa hila

Acha niongeze kama kunatokea pingamizi bax uchaguzi eneo hilo uahilishe hadi mgombea na chama husika walekebishe au walete mgombea mwingne
 
Uwezi kutegemea kuongoza kwa kuweka mapingamizi,nadhani katika katiba mpya kama kuna sehemu ya kuongezea basi ili la mapingamizi ya hila liwekwe,kuwa inapoonekana kuna dosari mgombea apewe siku mbili za kurekebisha dosari hizo na sio kusubiri eleventh hour unaleta mapingamizi.Ushindi wa mapingamizi sio ushindi bali ni ushindi wa hila

Na kuunga mkono.Na inatakiwa iwekwe kuwa hakuna kiongozi atakaye chukuliwa kama alikosa ushindani.Ni lazima pawepo ushindani.Viongozi wa kuchaguliwalazima wachaguliwe na Raia wote wa eneo husika.

Vinginevyo tutafika mahali tutaambiwa RAIS kapita bila kupingwa.Hata wakati wa nyerere hakuna Mbunge aliyepita bila kupingwa iweje leo tunasikia ati kuna wabunge wamepita bila kupingwa.

Hivi huyu mpunge akipigiwakura na asilimia 90 ya wapiga kura wake wamevote HAPANA,inamaana hatakiwi.

Na kama NEC italiweka vyema basi kama imeshindikana basi huyu tunayesemaamepita bila kupingwa apigiwe kura na wote tuone hayo ni kweli?Na kama hajapata 60% ya kura zote basi ina maana hata wananchi wake hawamtaki.

Serikali inatakiwa ijue kwa lazima kuwa unapokuwa na vyama vingi basi wajue na HAKI lazimaiwe wazi kwa kila raia bila kujali itikadi zetu
 
Ni uchambuzi mzuri, umejikita kwenye uhalisia. Tatizo lilipo ni wakati tu. CCM haijatamani kukubali hilo na imeendelea kung'ang'ania mbinu na mikakati ileile ya wakati wa nyuma ilhali wakati hautamani tena uhai wa mikakati husika. Mabadiliko ya kizazi yanahitaji mifumo ya kisiasa iendane na uhalisia wake la sivyo utawaongoza watu wanaoweza kugeuka na kukupigia kura ya chuki na kumpa uongozi hata asiye na mwelekeo. Mazoea yanaigharimu CCM. Wanaoaminika ni kizazi kipya, akina Nape na wengine wa aina yake wamekosa innovation (ubunifu) wa kuendesha siasa mpya ndani ya chama kikongwe! Itawagharimu

Yes. CCM imekosa innovation. Na kama unaona hata hawa the so called kizazi kipya wamekuwa watu wa kulinda status quo. Maana nao wamefika pale kwa sababu wazee wao walikuwa watu wa system (I personally nilijua akina January, Nape nk..) wangekuwa watu wenye vision tofauti. Juzi nilivyoangalia majibu ya akina Saada Mkuya, Angela Kairuki nk bungeni), you could clearly see the emptiness in their heads. Ukiangalia majibu ya kina Nape you see the boy is still in the 19th century politics za kipropaganda.

Sasa compare the likes of Nape/Angela Kairuki/Saada Mkuya na mnyika/Halima Mdee/Lissu et al! (perhaps you can say ni kwa sababu wako upinzani but for sure you can see hata ujengaji wa hoja ni miles apart! and the answer is simple! Katika kundi la kina Mnyika na Mdee ni wapinzani lakini hakuna aliyebebwa! They earned their right to be there.

Na changamoto kubwa kwa CCM ni kwamba kizazi cha leo kina taka maisha mazuri (kizazi cha instagram, facebook, twiter nk)..na wakijua kwamba wanayakosa au yanakwamishwa na CCM..my friend huna chako. nA HAWA NDO WATAIONDOA ccm Madarakani. Lakini vile vile..sasa hivi kuna mwamko wa hali ya juu sana wa siasa vijijini! na wengi wanaamini na wanazidi kuamini kwamba adui ni CCM! Na hilo ni tatizo.

Kwangu mimi honestly sioni ni namna gani tena CCM inaweza kutoa promises za maisha bora zaidi ya kuleta hayo maisha/kujenga misingi hayo maisha yapatikane.....people are tired! That should be the message to the party politiburo in Lumumba and Dodoma. And I see the dark future especially hii katiba pendekezwa ikipita! I tell you guys..people will pay the price! Not very far from today.


Indeed, This is an interesting time to be a Tanzanian! After all kukata tamaa ni vibaya aise!
 
Masanja

Ninaamni CCM bado ina hazina ya watu wa kimkakati kubadili hali hii, chama hakipaswi tena kuwaweka front line wasemaji wenye kutumia mantiki bila hoja kwa sasa watanzania wanaweza kufikiri haraka na kugundua fallacies, kinahitaji watu watulivu wenye kufikiri vizuri kimkakati
 
Last edited by a moderator:
Nafikiri suala la ulipaji fadhila linawagharimu sana ccm,,,, anyway ila ktk bunge lililopita tumeshuhudia kwa kiasi kikubwa kuwa wengi wa wabunge ccm ni vilaza tena wa kutupwa maana mjadala ulipoanza walianza kuchangia kwa kuropoka na sehemu kubwa ni kwenye mapendekezo tu ya pac bila kudadavua juu ya ukokotoaji wa hesabu uliofanywa na cag then pccb wao walifanya uchunguzi wa kina,,,, ilipowadia wkt wa kujenga hoja nadhani kila mtu alijionea waliokuwa wanazungumza mjengoni ni lissu,,mdee,,mnyika,,,kafulila acha tu
 
Inaongeza majina kwa sasa inaitwa CHAMA CHA MAPINGAMIZI.Maana bila mapingamizi CCM hakuna
Uchaguzi wa Serikali za mitaa hautupi taswira halisi ya kutuwezesha kubashiri matokeo ya chaguzi zijazo kwa sababu uliathiriwa na mapingamizi mengi na kasoro nyingi sana. Uchaguzi wa Katiba pendekezwa ndio unaweza kutupatia taswira halisi kama watu watajiandikisha kwa wingi na kupiga kura ya uchaguzi wa Katiba, kama hakutakuwa na mizengwe mingine. Kwa matokeo ya huo twaweza kubashiri matokeo ya 2015 lakini huu wa sasa ni danganya toto ingawa haina ubishi kuwa Upinzani ni tishio kwa CCM!
 
Uchaguzi wa Serikali za mitaa hautupi taswira halisi ya kutuwezesha kubashiri matokeo ya chaguzi zijazo kwa sababu uliathiriwa na mapingamizi mengi na kasoro nyingi sana. Uchaguzi wa Katiba pendekezwa ndio unaweza kutupatia taswira halisi kama watu watajiandikisha kwa wingi na kupiga kura ya uchaguzi wa Katiba, kama hakutakuwa na mizengwe mingine. Kwa matokeo ya huo twaweza kubashiri matokeo ya 2015 lakini huu wa sasa ni danganya toto ingawa haina ubishi kuwa Upinzani ni tishio kwa CCM!

Ukiangalia na TREND ya ugandamizaji wa demokrasia,haki za watanzania kumpigia kura kiongozi wamtakaye,polisi kutumika vibaya ni changamoto ambazo tumesiona.Sasa jiulize kungekuwa na HAKI kidogo tu kama uchaguzi mkuu unavyokuwaunadhanileo tungekuwatunasemaje?

Upinzani wamejitahidi sana.Hebu jiulize kiongozi unayetaka kumchagua kawekewa PINGAMIZI na CCM unaenda kumchagua nani?
 
Back
Top Bottom