Barua ya wazi kwa Bashiru Ally, Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi: Manung'uniko ya Waislamu lazima yafanyiwe kazi

Tanzania haina dini lakini Wakiristo ni wanufaika zaidi wa ajira na teuzi za serikali.
Kutokana na kunufaika huko wengi miongoni mwao wananufaika na mishahara iliyostable, Bima ya Afya nzuri, Pensheni za uzeeni, mikopo benki n. k
Matokeo yake wanao uwezo wa kusomesha watoto wao shule nzuri, kuwa na makazi stable.
Wakati huo Waislamu kutokana na kutonufaika ipasavyo na keki hiyo ya Taifa ya ajira za serikali , maisha yao yanakuwa siyo bora kama wakiristo, hawanufaiki na bima mzuri ya Afya, pensheni, na faida nyingi zitokanazo na mishahara ya serikali. Sasa katika hali kama hiyo Waislamu wanakuwa kama raia daraja la pili katika nchi yao. Hili halikubaliki, na lazima lifanyiwe kazi ili kuweka usawa na kuondoa manung'uniko ambayo kwa kweli ni madai ya msingi!. Hata mtu ujifanye vipi kuyapuuza, lakini ni madai halali na ya msingi sana!
Tatizo mnaichagua ccm ikataeni ili yafutike haya, mtaendelea kuburuzwa na kulalamika Hadi mwisho
 
Mleta mada huwa anapenda kujitutumua kujitia mjuzi kumbe bwege tu mchochezi siku zote asiye na hoja za maana.

Kila siku anajidai ohh TISS walione hili ,oh Raisi

Huyu Ni Chadema frustrated Sana maisha kapigika
Bwege ni wewe.
 
Yes, ni vicious circle! Tatizo letu kubwa ni 'mfumo kristo' ambao kwa sehemu kubwa unatufanya tusione dhulma mbalimbali. Ni kama mfumo dume tu unavyofanya kazi. ...inahitaji tafakari kubwa kuweza kuziona dhulma mbalimbali. Ndio sababu hata kiongozi akiwa muislamu, mfumo huo unamfanya asione hizo dhulma. Ni kama ilivyo kwa mfumo dume, hata viongozi wanawake wanajikuta wakitenda kulingana na mfumo unavyotaka.

Sasa badala ya kuwafunga midomo watu wanaweza kutuonesha dhulma hizo na udhaifu wa mfumo uliopo, tungewaacha waseme ili kuweza kufanyia marekebisho. Hata kama hatukubaliani na wanayosema au kuyataka, lakini ni muhimu kusikiliza perspectives zao kwa sababu kuna kitu tutajifunza.

Bahati nzuri nchi yetu imechanganyika sana. Mimi ni mkristo, lakini ninao ndugu wa damu waislamu. Ninaamini watu wengi pia tupo hivyo.

Tuwasikilize wanachosema......kati yake zipo hoja zenye mashiko tu kama tukiamua kusikiliza objectively.

Well said!
Thanks
 
  • Thanks
Reactions: SMU
SUALA LA ELIMU WAISLAMU WENGI HAWALIPI KIPAUMBELE TUACHENI KUSINGIZIA WAKRISTO. ELIMU DUNIA SI KIPAUMBELE KWETU. KWA NINI TUNAFUCHA UDHAIFU?
Una uhakika na hili au umekaririshwa?
nini? Ikiwa huna umakini katika mabandiko ya nini kutumia herufi kubwa tuone wajua kuandika?
Oooh nilisahau "hata wa la saba mnatosha!"
 
Hakuna cha inferiority complex hapa. Huwezi kuteua 80% watu wa dini moja halafu ukaona hilo siyo tatizo!

Wote ni Watanzania, walipa kodi nchi hii, lazima keki ya Taifa igawanywe kwa haki.

Angekuwa rais Muislamu akateua 80% Waislamu nchi hii ingetawalika? , si mgechonga sana humu mitandaoni kama mlivyochonga kipindi kile JK alivyokuwa akiwapa vijinafasi waislamu angalauangalau hata kama kiujumla Wakiristo walikuwa bado ni wengi zaidi kwenye hizo nafasi?
Hujajua dini yangu ni ipo hivyo huna moral authority ya kuizungumzia...nadhani kwa haraka haraka tatizo linalokusumbua wewe ni pamoja na kundi kubwa la watu wa aina yako kiupeo, ambao nadhani mlimezeshwa sana elimu ya akhera zaidi na mkasahau kwamba ili kufika huko ni lazima mpitie duniani of whom elimu dunia hamkuandaliwa...pole sana Subiri mambo ya uchaguzi yakiisha basi serikali itakujengea msikiti wa kitaifa ambao utakua imamu na utaruhusiwa kuuongoza na kuingiza kwenye uongozi watu wa aina yako! Ila kwa kuwa wewe umeshachelewa basi usimnyime mwanao elimu isije kuwa tena naye akaja kuwa na mentality kama yako baadaye!
 
Waislamu njia waliyochagua iko sahihi ya biashara Sio Elimu

Wafanyabiashara wengi nchi hii Ni waislamu.Matajiri wakubwa Ni waislamu kuanzia Bakheresa ,mohaned Dewji ,manji nk

Biashara ndogo dar es salaam nzima asilimia 90 zimeshikwa na waislamu aangalia daladala,petrostation malori mengi ya mizigo na mafuta wamiliki waislamu

Aangalia hata Watu wasafi nchi nzima kuanzia nguo,nywele nyumba,chooni,bafuni waislamu ndio wanaongoza kwa usafi

Nenda kula vizuri na mapishi hakuna anayewapita waislamu . Wanawake na wasichana na vijana na wazee wa kiislamu Huwezi mkuta mchafu kuanzia kichwani Hadi nguo Hadi mguuni

Kifupi elimu ya kujitegemea kwa waislamu iko juu Sana .Wengi wasio na kipato wanaolilia ajira Ni wakristo waliosoma !!!

Waislamu wasio Soma wala hawalakamikii ajira na Wala hawaishobokei Kama wakristo

Muislamu ajira aweza fanya ili tu apate mtaji akaanzishe chake wachache wanaokomaa Hadi kustaafu hao wengi huwa wasomi wakiolemazwa na elimu ya mfumo Kristo ambayo haihimizi Sana kujitegemea Bali kuwa tegemezi kusubiri serikali itoe ajira no

Tusilaumu waislamu kutosoma mfumo wao wa maisha unawaelekeza zaidi kwenye kujitegemea zaidi Sio kusoma uajiriwe au upate uteuzi!!!!
True,tatizo sio mfumo elimu Kikristo
Tatizo tuliharibu mifumo ya elimu tukaleta elimu siasa badala ya elimu vitendo elimu ujasilimali ili watu watumie fursa.
Mafundisho ya uislam yamekamilika kila idara hata kwenye nadharia za uongozi huwa awaumizi na kukomoa watu, nadharia zao zimesimama kwenye maendeleo ya watu na sio vitu.
 
Hujajua dini yangu ni ipo hivyo huna moral authority ya kuizungumzia...nadhani kwa haraka haraka tatizo linalokusumbua wewe ni pamoja na kundi kubwa la watu wa aina yako kiupeo, ambao nadhani mlimezeshwa sana elimu ya akhera zaidi na mkasahau kwamba ili kufika huko ni lazima mpitie duniani of whom elimu dunia hamkuandaliwa...pole sana Subiri mambo ya uchaguzi yakiisha basi serikali itakujengea msikiti wa kitaifa ambao utakua imamu na utaruhusiwa kuuongoza na kuingiza kwenye uongozi watu wa aina yako! Ila kwa kuwa wewe umeshachelewa basi usimnyime mwanao elimu isije kuwa tena naye akaja kuwa na mentality kama yako baadaye!

Kejeli na vijembe vya hivi tumeshavizoea.

Lakini Waislamu wataendelea kudai haki yao nchini, haiwezekani teuzi na ajira za 80% kwa watu wa dini moja na wengine only 20%. Hii siyo fair ni ufini huu!

Waislamu hawawezi kukatishwa tamaa kutaka usawa katika nchi kwa kauli za namna hii!
 
Hujajua dini yangu ni ipo hivyo huna moral authority ya kuizungumzia...nadhani kwa haraka haraka tatizo linalokusumbua wewe ni pamoja na kundi kubwa la watu wa aina yako kiupeo, ambao nadhani mlimezeshwa sana elimu ya akhera zaidi na mkasahau kwamba ili kufika huko ni lazima mpitie duniani of whom elimu dunia hamkuandaliwa...pole sana Subiri mambo ya uchaguzi yakiisha basi serikali itakujengea msikiti wa kitaifa ambao utakua imamu na utaruhusiwa kuuongoza na kuingiza kwenye uongozi watu wa aina yako! Ila kwa kuwa wewe umeshachelewa basi usimnyime mwanao elimu isije kuwa tena naye akaja kuwa na mentality kama yako baadaye!
Naona hata nawe kuna kitu umemezeshwa. Na ni kawaida ya mtumwa yeyote wa nafsi kuimba asichokijua. Leo hii ni karne ya 21 bado mmejirudisha miaka ya 60 huku mkisahau wakati bado babu zenu wanasheta maporini Tanga ndiko kulikuwa na shule ya kwanza kwa elimu ya kizungu na kabla ya hapo mnajisahaulisha kwamba hao mnaowaona leo hawana elimu ndio waliojua kusoma na kuandika mikataba na barua... alau nenda makumbusho kisha uje na hizo propaganda zenu humu.
 
Yaani ndugu yangu wewe hata akili yako hupendi kuishughulisha.yaani maneno machache hayo nayo unataka ukariri? Kusoma hujui hata kuangalia picha?

Mficha maradhi mauti humuumbua. Mimi nmekulia kibiti, nenda maneremango ,nenda mchukwi wananifahamu. Ni mkazi wa pwani.nafahamu jinsi ambavyo nime struggle mimi kusoma tena kwa msaada wa kafirs.sisi wasafi tumefungua madrasa nyingi sana huko kwetu siyo shule.misikiti ipo mingi si jambo baya but tuna shule chache sana za kwetu. Hata hiyo hospital ya mchukwi imejengwa kati kati ya waislamu ikiwa ni ya Kanisa.

Tusijazane ujinga. Nmekaa bagamoyo,vikindu n.k nmefanya projects nyingi na mashirika mbalimbali kuhamasisha watu wa pwani ambao asilimia 90 ni waislamu waende shule.nafahamu ninachoongea.mimi elimu imenisaidia kiasi kwamba siangalii mambo kwa jicho la kidini.naangalia kwa uhalisia.

Nmesoma shule ya sekondari kibiti miaka hiyo asilimia kubwa walikuwa ni wageni si wakazi wa pale ndo walikuwa wanasoma.nlianza na wenzangu 8 shulenj tulimaliza wawili.sita waliiishia form 2. Hao wanaume. Wasichana walikuwa 14 ninaowafahamu waliomaliza form 4 walikuwa 3 wengine waliaolewa wakiwa form 2 na form 1. Waliozwa baada ya kuvunja ungo.

So nakwambia ninachokifahamu. Kwa maeneo nliyoishi.kibiti,vikindu,maneromango,samvula chole,bagamoyo,ruvu,kibaha na hata dar. Wenyeji ni wazaramo.angalia wangapi wana elimu ya maana? Wangapi wana maisha mazuri.

Waliojenga wengi Dar ni Wasukuma,Wanyakyusa,Wachaga,Wahaya na Wakinga miaka hii. Ndo ambao utaona wamejitawanya dar. Ukiacha wahindi kule posta na waarabu kiasi flan mitaa ya ilala,magomeni na kinondoni.

Mimi naifahamu dar kijana,nafahamu maeneo mengi na mambo mengi.
Una uhakika na hili au umekaririshwa?
nini? Ikiwa huna umakini katika mabandiko ya nini kutumia herufi kubwa tuone wajua kuandika?
Oooh nilisahau "hata wa la saba mnatosha!"
 
Naona hata nawe kuna kitu umemezeshwa. Na ni kawaida ya mtumwa yeyote wa nafsi kuimba asichokijua. Leo hii ni karne ya 21 bado mmejirudisha miaka ya 60 huku mkisahau wakati bado babu zenu wanasheta maporini Tanga ndiko kulikuwa na shule ya kwanza kwa elimu ya kizungu na kabla ya hapo mnajisahaulisha kwamba hao mnaowaona leo hawana elimu ndio waliojua kusoma na kuandika mikataba na barua... alau nenda makumbusho kisha uje na hizo propaganda zenu humu.
Chief ujue una ghubu? Umeachwa? Maana huambiliki ati! Umeniganda kama luba sijui kama umekumbuka hata swala ya alfajiri..
 
Kejeli na vijembe vya hivi tumeshavizoea.

Lakini Waislamu wataendelea kudai haki yao nchini, haiwezekani teuzi na ajira za 80% kwa watu wa dini moja na wengine only 20%. Hii siyo fair ni ufini huu!

Waislamu hawawezi kukatishwa tamaa kutaka usawa katika nchi kwa kauli za namna hii!
Pingeni dhuluma October kukomesha yote haya yasijirudie, tupinge ukanda, ukabila, udini kwenye teuzi.
 
Yaani ndugu yangu wewe hata akili yako hupendi kuishughulisha.yaani maneno machache hayo nayo unataka ukariri? Kusoma hujui hata kuangalia picha?

Mficha maradhi mauti humuumbua. Mimi nmekulia kibiti, nenda maneremango ,nenda mchukwi wananifahamu. Ni mkazi wa pwani.nafahamu jinsi ambavyo nime struggle mimi kusoma tena kwa msaada wa kafirs.sisi wasafi tumefungua madrasa nyingi sana huko kwetu siyo shule.misikiti ipo mingi si jambo baya but tuna shule chache sana za kwetu. Hata hiyo hospital ya mchukwi imejengwa kati kati ya waislamu ikiwa ni ya Kanisa.

Tusijazane ujinga. Nmekaa bagamoyo,vikindu n.k nmefanya projects nyingi na mashirika mbalimbali kuhamasisha watu wa pwani ambao asilimia 90 ni waislamu waende shule.nafahamu ninachoongea.mimi elimu imenisaidia kiasi kwamba siangalii mambo kwa jicho la kidini.naangalia kwa uhalisia.

Nmesoma shule ya sekondari kibiti miaka hiyo asilimia kubwa walikuwa ni wageni si wakazi wa pale ndo walikuwa wanasoma.nlianza na wenzangu 8 shulenj tulimaliza wawili.sita waliiishia form 2. Hao wanaume. Wasichana walikuwa 14 ninaowafahamu waliomaliza form 4 walikuwa 3 wengine waliaolewa wakiwa form 2 na form 1. Waliozwa baada ya kuvunja ungo.

So nakwambia ninachokifahamu. Kwa maeneo nliyoishi.kibiti,vikindu,maneromango,samvula chole,bagamoyo,ruvu,kibaha na hata dar. Wenyeji ni wazaramo.angalia wangapi wana elimu ya maana? Wangapi wana maisha mazuri.

Waliojenga wengi Dar ni Wasukuma,Wanyakyusa,Wachaga,Wahaya na Wakinga miaka hii. Ndo ambao utaona wamejitawanya dar. Ukiacha wahindi kule posta na waarabu kiasi flan mitaa ya ilala,magomeni na kinondoni.

Mimi naifahamu dar kijana,nafahamu maeneo mengi na mambo mengi.
Umenena vyema...kisha hawa hawa wanataka wapewe hisani ya dini kwenye so called keki ya taifa ha ha haaaa.... Huyu bwana anapaswa kupewa tu futari na si keki ya taifa kama anavyoidai
 
CCM NI WATU WA AJABU SANA. NASIKIA HUKO KILOLO, IRINGA WAMEIKARIBISHA FAMILIA YA MZEE MMOJA ALIWAHI KUWA MTUMISHI ASIYE MWAMINIFU WA KANISA FULANI KUBWA TU LENYE WAUMINI WENGI IRINGA MJINI NA WILAYANI KILOLO ILI WAWAPE UBUNGE. HII FAMILIA NA NDUGU YAO WAMEIBA PALE CHUO KIKUU CHA IRINGA, ZAMANI CHUO KIKUU TUMAINI HADI CHUO KINAFILISIKA. NAWAONEA HURUMA HAO NDUGU ZANGU NA WATANI ZANGU WA KILOLO. NI SAWA NA KUMWACHIA FISI BUCHA. HAWA JAMAA NASIKIA WANA SIFA ZA UZINZI, TABIA MBAYA ZOTE WANAZO. NASIKIA KAMA SI BUSARA TU ZA KANISA HUYO MZEE WA FAMILIA ANGEFUNGWA KWA UBADHIRIFU KANISANI. NASIKIA PIA HADI SASA YUPO CHINI YA UCHUNGUZI WA TAKUKURU KWA WIZI WA MALI NA FEDHA ZA CHUO HICHO KINACHOMILIKIWA NA HILO KANISA LINALOAMINI WOKOVU KWA NJIA YA IMANI KATIKA YESU KRISTO NA KATIKA INJILI YA YESU KRISTO AOKOAYE. NI KANISA LENYE MCHANGO MKUBWA KWA MAENDELEO YA KIMWILI NA KIROHO HASA IRINGA MJINI, IRINGA VIJIJINI NA WILAYA YA KILOLO. NI KANISA LILILOANZISHWA NA WAMISIONARI TOKA UJERUMANI.
 
Ndugu Bashiru Ally,
Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi

Mimi ni mwananchi, raia wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Nimeamua kuchukua wasaa huu kukuandikia haya yafuatayo, kwani kwa haya niyaandikayo naamini ni ya msingi sana katika kukuza umoja na mshikamano wa Taifa letu vitu ambavyo ni muhimu sana katika kuimarisha amani ya Taifa letu. Kwa muktadha huu kuna nukta chache ningependa kukueleza ili chama chako cha Mapinduzi ambacho wewe ni mfuatiliaji mkuu wa utekelezaji wa Ilani yake ni lazima uzielewe na uhakikishe chama chako kinazifanyia kazi.

Ndugu Ponda alisoma waraka mzito sana, waraka wenye mambo mengi yanayohusu Taifa letu kiujumla na mengine exclusively yanayowahusu waislamu. kwa hiyo mimi nitakijikita katika yale yanayowahusu Waislamu.

1. Mosi kuna malalamiko ya muda mrefu ya kuhusu Waislamu kufanywa raia daraja la pili nchini.
Kwa miaka mingi tangu uraisi wa Mwalimu Nyerere, kumekuwepo na malalamiko mengi kutoka kwa waislamu, kuwa kuna ubaguzi wa kimfumo dhidi yao, miaka ya zamani walikuwa wakitolea mifano kwenye nafasi za elimu ya juu, kuwa inakuwaje Wanaoanzishwa shule darasa la kwanza kuna mamilioni ya vijana wa kiislamu, lakini ukiangalia huko kwenye elimu ya juu vyuoni, waislamu ni wachache sana?

Madai haya ya waislamu yamekuwepo, wengi wamekuwa wakimrejea Kighoma Malima kuwa alisaidia kufanya reforms kadha wa kadha alipoteuliwa na Rais wa awamu ya pili kuwa waziri wa Elimu, Mimi sitaki kujadili ukweli au uongo wa haya madai, bali nataka nikueleze kuwa hizi sentiment zipo katika jamii, waislamu wamekuwa wakizizungumza hizi habari kwa muda mrefu kama sehemu ya historia yao katika harakati za kutafuta namna ya kunufaika na matunda ya uhuru. Ubaya wa historia ni kuwa historia haifi.

Ndugu katibu mkuu ipo haja ya Chama cha Mapinduzi kuja mbele, kuweka rekodi sawa kiwaeleze waislamu kuwa chenyewe kama chama ambacho kwa kauli ya muasisi mwenyewe wa chama hiki aliwahi kukiri waislamu kuwa nyuma kielimu wakati wa uhuru, kije kiwaambie Waislamu, sisi kama chama tumefanya kadha wa kadha juu yenu na sasa hivi tumepata mafanikio kadha wa kadha kwenye suala hili la Elimu. Kwanini hii hoja ya elimu ni muhimu sana? Kwa sababu Elimu inaambatana na ajira, na teuzi mbalimbali serikalini na katika utumishi wa umma. Kwa maana mara nyingi waislamu wanapouliza swali kuwa mbona proportion yetu kwenye teuzi na ajira haiakisi wingi wetu wamekuwa wajibiwa kuwa hamjasoma!

2. Chama cha Mapinduzi lazima kiitake serikali yake itende haki kwa makundi yote ya kijamii
Kwa mujibu wa waraka uliosomwa na Sheikh Ponda, unaoonyesha uwiano wa teuzi kati ya Watanzania wenye imani ya Kikiristo na Watanzania wenye Imani ya Kiislamu ni kwa uwiano wa asilimia 80% wakiristo, na 20%Waislamu.
Ndugu Katibu mkuu by all standards hii haijakaa sawa hata kidogo. Haiyumkiniki katika Taifa ambalo populationwise kila kundi kati ya hayo mawili ndani ya jamii lina idadi kubwa ya kutosha tu ya watu katika jamii lakini linapokuja katika utumishi wa umma na teuzi za serikali kundi moja liko overrepsented huku jingine likionekana likiwa na idadi finyu sana, Kwa namna zozote zile hii asilimia ya 80% kwa 20% haiakisi uhalisia wa demography ya wananchi kwa muktadha wa makundi ya imani zao.

Chama cha Mapinduzi kinapaswa kuja na kuwaangalia waislamu machoni kiwaambie, wao wana shida gani kwa nini ni wachache katika teuzi hizi za serikali, wao hawana nini ambacho wenzao wanacho kiasi kwamba kundi jingine likiwa jingi katika nafasi hizo za teuzi kuliko wao? Zimekuwepo hoja kuwa hateuliwi mtu kwa sababu ya dini yake bali vigezo vingine, Tunataka chama cha mapinduzi kiwaambie waislamu kuwa labda hawana elimu, siyo wazalendo, ni mafisadi, ni wavivu sana, Au kiwaeleze sababu zozote zenye mashiko kwa nini wingi wao katika jamii hauakisi uwepo wao katika utumishi wa serikali?

Ndugu katibu mkuu, Chama cha mapinduzi kinaweza kuamua kukaa kimya utadhani hili tatizo halipo, lakini mimi ningependa kukiambia kuwa, uwepo au kutokuwepo kwa tatizo hilo siyo hoja, hoja ni kuwa waislamu wamekuwa wakilalamika kwa muda mrefu na sisi tunaoitakia amani nchi hii, tunaona kuwa hili ni bomu linalosubiri kupasuka kama ama rekodi zisipowekwa sawa au kufanyiwa kazi na serikali.

Ndugu katibu mkuu, Chama chako cha mapinduzi au serikali zake kamwe zisidhani kuwa madai haya ya waislamu yataisha iwapo kila siku wanakaa wanaona teuzi za serikali moja baada ya nyingine anateuliwa mtu wa imani nyingine huku wao wakiambiwa eti watu hawateuliwi kwa dini zao bali vigezo vingine, kwa nini hivyo vigezo viwe kwa wingi kwa watu wa imani moja tu?

3. Udini ni ufa mkubwa sana wa jamii yetu na ni lazima wote tuungane kuupiga vita
Ndugu katibu mkuu, kama kuna ufa mkubwa zaidi katika nchi yetu basi ni suala la udini, hili ni tatizo ambalo hatupaswi kulipiga vita kwa maneno bali kwa vitendo, na katika kulipiga vita tatizo hilo lazima tulipige vita huku kila mtu akiona kabisa kuwa tuna dhati ya kufanya hivyo, vipo viashiria nchini kuwa watu wa imani moja wanawekwa kwenye mizania tofauti pindi wanapofanya mambo fulani yenye kuashiria udini, na mambo haya yanawafanya watu wa dini nyingine wajihisi kuwa ni kutokana na mfumo kuinua kundi fulani ndiyo maana kundi hilo linajihisi kufanya mambo with impunity.

Katibu mkuu nitakupa mfano, Mkuu wa mkoa wa mmoja nchini anatoa kauli kuwa Nchi hii iko chini ya kanisa, hasemi iko chini ya Mungu, anasema iko chini ya kanisa na wala hashughulikiwi na serikali ya chana chsko kwa uchochezi. Waziri mmoja mwandamizi anafanya kampeni katika kanisa kwa kutandika bendera ya chama ndani ya madhabahu, Viongozi wa imani moja wakikemea serikali kwa kauli na maandishi (Japo ni haki yao) hawakamatwi lakini kiongozi wa dini ya Kiislamu anaposimama na kutumia haki yake ya kutoa mapendekezo na maoni yake anakamatwa na kuswekwa ndani bila kufikishwa mahakamani ndani ya muda maalumu kinyume cha sheria.

Ndugu katibu mkuu, katika muktadha huu kwa nini Waislamu wasikiwekee chama chako na serikali yake alama ya kuuliza kuwa huenda vinalea na kuendekeza udini wa imani mmoja nchini?

4. Suala la kuhamisha wahadhiri na watumishi 11 wa Imani moja Chuo cha UDOM na kuleta wengine 11 wa imani nyingine linahitaji uchunguzi
Ndugu katibu mkuu, nilistushwa sana na hili suala kama ambavyo lilielezwa kwa kina kwenye waraka wa Sheikh Ponda.
Nimejiuliza kuwa iweje katika utumishi uhamishe watu kwa mkupuo halafu ionekane wote ni wa imani moja halafu waletwe wengine 11 na wote wawe wa imani moja, hili linatoa picha gani, limebeba ajenda gani, hao waliofanya uhamisho huo walitaka kuachieve kitu gani?

Wazungu wana msemo kuwa, ukiona inatweta kama bata, inatembea kama bata na inalia kama bata basi hiyo ni bata. Inawezekana vipi kwa kanuni zozote zile za nasibu uondoe watu 11 wenye kufuata mrengo wa dini moja sehemu halafu wakati huohuo ulete wengine 11 wa dini nyingine kama maamuzi ya kufanya hivyo hayakusukumwa na udini uliokubuhu katika kufanya maamuzi hayo basi ni kitu gani?. Cha kusikitisha zaidi waraka ukaenda mbele na kusema wazi kuwa wengine katika wale waliohamishwa walienda kupewa nafasi za chini kuliko hadhi yao.

Ndugu katibu mkuu, tunakitaka chama chako kifanye uchunguzi au kiilazimishe serikali yake ichunguze na iwaeleze Watanzania ni sababu gani za msingi hatua hiyo ilifikiwa na kwa nini ionekane watu wa dini moja ndiyo wanakumbwa na zoezi la kuondolewa mahali na wakaletwa wengine wote wa imani ya dini nyingine.

Hoja kuwa serikali inaweza kumhamisha yeyote na kumleta yeyote katika utumishi wa umma ni kweli lakini kwa muktadha huu haina mashiko maana inaonyesha kuwa kuna msukumo fulani wa maamuzi ambayo yameacha question marks na kwa kuwa kuna umma hususan wa kiislamu unadhani kuwa kuna nia isiyo njema imesukuma maamuzi hayo, tunakitaka chama cha Mapinduzi kitoe maelezo kwa nini uamuzi tata huo ulifikiwa ili kusafisha hali hii inayoweza kupelekea hisia hasi zinazoweza kupelekea kuvunjika kwa amani.

5. Chama cha mapinduzi na serikali yake kijifunze kwa maandamano yanayotokea marekani kupinga ubaguzi
Huko Marekani kulikuwepo na manung'uniko ya muda mrefu, watu weusi wakilslamika hadharani na sirini kuhusu ubaguzi wa kimfumo dhidi yao, walilamika kuhusu ubaguzi katika uchumi, katika mifumo ya utoaji haki nchini humo, walilamika hadi upataji wa ajira katika serikali ya Shirikisho na hata za majimbo.

Manung'uniko yao yalikuwa yakipuuzwa kwa madai kuwa marekani hakuna ubaguguzi wowote bali ni inferiority complex yao tu na uvivu wao wa kutofanya kazi. Ikawa inatolewa mifano michache kuwa mbona fulani na fulani ni weusi na matajiri, ni wacheza kikapu maarufu, ni wacheza sinema maarufu n. k. Hata hivyo pamoja na kauli hizi donge lilikuwa bado limo katika mioyo ya wamarekani weusi maana wanasema yule avaaye kiatu, yeye ndiye anayeona wapi kinambana. Leo Marekani hali imekuwa tete baada ya wamarekani weusi na wale wapenda haki kuingia mitaani kuonyesha ghadhabu yao juu ya matendo hayo baada ya kifo cha kikatili cha George Floyd kilichosababishwa na ukatili wenye dalili zote za ubaguzi wa rangi.

Ndugu Katibu Mkuu, madai haya ya Waislamu hapa nchini haijalishi ni ya kweli au siyo kweli lakini yapo, madai haya yanahitaji majibu au hatua ya kuyarekebisha ili yasije kuendelea kujenga ghadhabu ya kimya kimya ambayo siku moja ikitoka nje, sisi kama taifa tutakuja kuwa na wakati mgumu sana. Kamwe tusijenge Kiburi kuwa vyombo vya usalama vitawashughulikia wote hao wenye kuleta madai haya. Ndugu katibu mkuu hata katika hivyo vyombo vya usalama kunaweza kukawemo watu walioaminishwa dhana hizo iwapo zitaachwa bila kushughulikiwa na ikitokea hali hiyo Taifa liktakuwa katika sintofahamu kubwa. Wahenga walisema Kinga ni bora kuliko tiba, yatupasa kama Taifa kulitafutia ufumbuzi suala hili badala ya kujidai kuwa halipo.

6. Ni muda muafaka sasa Masheikh walioko jela waachiwe huru bila masharti yoyote
Ndugu katibu mkuu, ni mwaka takriban wa 8 sasa Masheikh wapo jela bila kuhukumiwa na mahakama yoyote, Makosa yao hayajathibitishwa mahakamani, kwa hiyo madai na hoja zilizosomwa na Sheikh Ponda zina. mashiko
Tunakitaka chama cha mapinduzi kiisimamie serikali yake izingatie utawala wa sheria.

Chama kiulize serikali yake, inaendelea kuwashikilia Masheikh hao kwa uhalali upi wa kisheria?. Kama uchunguzi haujakamilika, kama huo uchunguzi haujakamilika miaka 8 utakamilika lini? Je, haki inatendeka kwa hawa masheikh au kuna namna yoyote ya kuamua kuwakomoa?

Ndugu katibu mkuu hawa Masheikh walikamatwa Zanzibar, kama lengo ni Justice au haki kwa nini ilazimishwe washitakiwe Tanzania bara na si hukohuko Zanzibar walipotenda kosa lolote inalodaiwa walitenda?

Hitimisho:
Ndugu katibu mkuu, yapo madai ambayo waislamu wamekuwa wakidai miaka nenda rudi, na kuna mambo wamekuwa wakiyawekea question mark kama vile teuzi katika awamu hii.

Sasa sisi kama raia wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania tunaona kuwa haya madai yasipojibiwa huenda yakaitia nchi katika uwezekano wa kuvunja mshikamano wa kitaifa na kuvunja amani huko mbele.

Sasa kwa kuwa watu wa aina yangu tunaipenda nchi yetu, si busara kuacha kutoa mchango wa mawazo katika mambo kama haya hata kama ni tata kiasi gani(controversial). Ndiyo maana kwa muktadha huu tunakitaka chsma cha Mapinduzi kijibu hoja za waislamu ili kutunza huo mshikamano!

Ndugu Katibu mkuu wa Chama cha Mapinduzi waislamu wana hoja zijibuni

Wako katika ujenzi wa Taifa.

Missile of the Nation (Kombora hatari kabisa la ulinzi wa Taifa)

Nakala kwa:
1. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
2. Waziri Mkuu
3. Mkurugenzi Usalama wa Taifa
SIJUI KAMA NI KWELI ILA NASIKIA HUYU KATIBU MKUU AMETAMKA WAZI KWAMBA WANATUMIA DOLA KUTAWALA NCHI NA KWAMBA WAMEJIFUNZA KWA NCHI ZILIZOSHINDWA KUTUMIA DOLA KUTAWALA WALIONDOLEWA MADARAKANI NA HAJAWAHI KURUDI TENA KURUDI MADARAKA. AMESEMA WAO HAWATAFANYA KOSA HILO BALI WATATUMIA DOLA KISAWASAWA KUTAWALA. HII NI KAULI NZITO TOKA KWA MTU MZITO. NASHANGAA KAMA NI KWELI KWA NINI HAJACHUKULIWA HATUA STAHIKI
 
Tayari ushapagawa jikite kwenye hoja Mkuundugu yangu
Nafikiri unanishawishi nikupandishe mori ili ukajilipue mkuu na mimi siko tayari kumpoteza mpiga kura hivyo basi suala la keki ya taifa achana nalo hadi siku ya Idi tutakumegea kidogo muhimu sasa hakikisha umechagua mgombea nayefaa ...sawa sawa?
 
Nafikiri unanishawishi kiupandishe mori ili ukajilipue mkuu na mimi siko tayari kumpoteza mpiga kura hivyo basi suala la keki ya taifa achana nalo hadi siku ya Idi tutakumegea kidogo muhimu sasa hakikisha umechagua mgombea nayefaa ...sawa sawa?

Akijilipua mbele yako hautobaki salama, na wanaomzunguuka hawatobaki salama, cha msingi tetea haki ya wote ili watu wa kujilipua wasiwepo
 
Back
Top Bottom