Barua ya wazi kwa Askofu Emmaus Bandekile Mwamakula

CalvinKimaro

JF-Expert Member
Sep 11, 2017
244
312
Amani iwe kwako!

Mimi nikiwa kama muumini wa Kanisa lako la Moravian la Uamsho Tanzania & Afrika Mashariki nimeshangazwa na ujumbe ulioutuma katika barua ya wazi kwa Mhe. Rais Dkt. John Pombe Magufuli kwani umeacha jukumu la msingi uliloitiwa na Mungu la kutuhubiria wananchi ili tuokoke na kumrudia Mungu.

Inafikirisha kukuona Askofu wangu ukiacha majukumu yako na kuanza kufanya siasa, najiuliza huo wito aliopewa na Mungu ni kwa ajili ya kuhubiri neno au kufanya siasa?

Nawaomba Mhe.Rais Magufuli pamoja na washauri wake na Watanzania kwa ujumla wenu muupuuze ujumbe huo alioutoa kwani hauna nia njema ya kutujenga Wananchi zaidi ya kutugawa.

Askofu wangu Mwamakula umesema kuwa unataka kufanya "Matembezi ya Hiyari" nchi nzima yenye lengo la kuuhamasisha Umma wa Tanzania kuhusu Kuunda Tume Huru ya Uchaguzi na Kuandika Katiba Mpya. Najiuliza tu hivi nilishawahi kukusikia au kukuona ukifanya matembezi ya hiyari kuhamasisha watu kumjua Mungu na kuokoka? Jibu ni hapana!.

Kwanini ufanye matembezi hayo wakati matembezi ya kiimani hujawahi kufanya!? Hapo ndipo napata jibu kuwa matembezi hayo hayajaandaliwa na wewe bali wanasiasa ambao wanakutumia kutuvuruga wananchi baada ya kushindwa kutimiza azma yao ya kuvuruga uchaguzi Mkuu na kuiingiza nchi katika machafuko kipindi cha uchaguzi Mkuu Mwezi Oktoba 2020.

Matembezi hayo unayoyaita "Matembezi ya Hiyari" yanalenga kuhamasisha Wananchi kuandamana katika mikoa yote ya Tanzania na wilaya zake zote katika kipindi chote cha mwaka 2021 kufanya fujo kinyume na sheria za nchi.

Ikumbukwe kuwa mara baada ya Uchaguzi Mkuu wa 28 Oktoba 2020, vyama vya upinzani pamoja na wewe Askofu mlitoa tamko kupitia Vyombo vya Habari kuwa Uchaguzi haukuwa huru na haki, mlihamasisha Wananchi kufanya maandamano kupinga matokeo ya uchaguzi, kudai kuundwa kwa Tume Huru ya Uchaguzi na kutaka Uchaguzi urudiwe.

Ni dhahiri Wananchi walishangazwa na madai hayo na wakayapuuza kwa kutojitokeza kufanya maandamano hayo ambayo ndani yake mliandaa vikundi vya wahuni kuchoma matairi ya magari barabarani, kuvunja maduka ya watu, kuchoma moto vituo vya mafuta na kufanya vurungu kwa Wananchi wengine ambao wasingekuwa tayari kuwaunga mkono.

Pia nasikia kuwa katika Matembezi hayo vikundi hivyo vya kufanya fujo mmeviandaa ili kutimiza yale mliyokusudia kuyafanya baada ya matokeo ya uchaguzi. Mmeandaa vijana wa kufanya fujo ili kuwalazimisha Polisi kutumia nguvu kuwadhibiti.

Ninapenda Askofu wangu Mwamakula utambue kuwa kwa mtazamo wangu, tangu matokeo ya Uchaguzi yalivyotangazwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) pamekuwa na juhudi kubwa ya vyama vya upinzani nchini kuwatumia viongozi wa dini ukiwemo wewe kujenga chuki na uhasama miongoni mwa Watanzania! kwa lengo la kulinda maslahi ya watu binafsi ambao ni Tundu Lissu na Freeman Mbowe.

Hali hii ya uhasama, chuki na kuwagawa Watanzania kwa ajili ya maslahi ya watu binafsi katika nchi haiwezi kuachwa kuendelea. Ni lazima sote kwa pamoja tukemee tabia hii mpya ambayo imeanza kujitokeza nchini, yakuwatumia viongozi wa dini kufanya siasa.

Ni kwa sababu hiyo, naamini kuwa "Matembezi ya Hiyari" yatatoa fursa kwa wafuasi wa upinzani kuanzisha mijadala ya kulilaumu Jeshi la Polisi kwani mtakapokatazwa kufanya matembezi mtaanza kulalamika kuwa mnaonewa na kunyimwa Uhuru jambo ambao si kweli. Kwa ujumla matembezi hayo yatahatarisha amani, suala la Kuundwa kwa Tume Huru ya Uchaguzi na Kuandikwa kwa Katiba Mpya unalitumia tu kama kisingizio cha kuhalalisha vurugu mlizopanga kuzifanya.

"Matembezi ya Hiyari" yatasimamisha shughuli za uzalishaji katika nchi, kwani mmepanga kufunga barabara na shughuli za kijamii kwa wakati huo.

Matembezi hayo yatavilazimu Vyombo vya Dola kutumia nguvu kuzuia au kuvuruga vikundi vya wahuni mliowaandaa kufanya vurugu wakati wa matembezi hayo.
Hivyo kuvifanya vyombo vya usalama kuonekana kuwa havitendi haki.

Mwisho ninapenda nikusihi Askofu wangu Mwamakula kutumia njia sahihi za kudai haki yako ambayo kwa namna moja au nyingine unahisi inaporwa badala ya kufanya matembezi ambayo yatazalisha vurugu na kutugawa Wananchi.

Ni imani yangu kuwa Mungu atasema na nafsi yako kuitii mamlaka kwani hata neno la Mungu katika biblia limetuagiza kutii mamlaka iliyo Kuu (Warumi 13:1) "Kila mtu na aitii mamlaka iliyo kuu, kwa maana hakuna mamlaka isiyotoka kwa Mungu na ile iliyopo imeamriwa na Mungu".

Pia nawasihii Watanzania wenzangu kupuuza matembezi hayo na kujikita katika shughuli za ujenzi wa Taifa letu.

Mungu atusaidie kutambua mema na mabaya na atufanye kuwa nguzo za kudumisha amani na umoja. Waovu wasipate nafasi ya kuharibu nchi yetu iliyojaa amani na utulivu!.

Mungu Ibariki Tanzania.

Lusajo Mwakanyamale.
 
Huyo si Askofu hata kidogo Yesu aliwatuma wahubiri kuwa tubuni na kuiamini Injili lakini Mwamakula anahubiria watu waiamini katiba mpya sijui tume hutlru ya uchaguzi nk hayo mahubiri Yesu hakumtuma.
 
Huyo si Askofu hata kidogo Yesu aliwatuma wahubiri kuwa TUbuni na kuiamini Injili lakini Mwamakula anahubiria watu waiamini katiba mpya sijui tume hutlru ya uchaguzi nk hayo mahubiri Yesu hakumtuma
Mjinga ni yule mtu anaedhani kuwa kazi ya viongozi wa dini ni kutoa mahubiri ya watu kwenda Mbinguni tu!

Tunajua vibaraka mpo kazini ili kutekeleza majukumu yenu mliyopewa na walio watuma.
 
Mjinga ni yule mtu anaedhani kuwa kazi ya viongozi wa dini ni kutoa mahubiri ya watu kwenda Mbinguni tu!

Tunajua vibaraka mpo kazini ili kutekeleza majukumu yenu mliyopewa na walio watuma.
ielewe dini ya kikristo faza.

Yesu Kristo aliuwawa kwa hira za kupakwa na watawala tokea akiwa mdogo, hakuna siku alijinasibisha na siasa za watawala,sicho kilichomleta,na ndio sababu hata wakati anakamatwa alikemea mapambano.

Hizi dini za kuamini askofu anajua zaidi kuliko watu wengine, ndio zitaangamiza waumini. Askofu nayeye kama binaadam ana ujinga mwingi tu.
 
Mjinga ni yule mtu anaedhani kuwa kazi ya viongozi wa dini ni kutoa mahubiri ya watu kwenda Mbinguni tu!

Tunajua vibaraka mpo kazini ili kutekeleza majukumu yenu mliyopewa na walio watuma.
sasa kazi ya mchungaji ni nini mkuu? hahaha kuna watu mnajifanya mnaelewa kila kitu hadi siri za Mungu yaani.
 
sasa kazi ya mchungaji ni nini mkuu? hahaha kuna watu mnajifanya mnaelewa kila kitu hadi siri za Mungu yaani.
Yaelekea wewe huna utamaduni wa kusoma vitabu vya dini.

Katika Biblia na Quran, kuna visa vingi sana vinavyo onyesha jinsi Mungu alivyo shughulika na wanadamu kwa namna mbalimbali.

Biblia: Utawala wa mabavu, ukosefu wa haki, ni moja tu ya sababu zilifanya Mungu akamtuma Musa Misri kwenda kuliokoa taifa la Israeli.

Quran: Mtu Mohammed pia amepigana vita vingi sana vya kudai haki, hasa hasa wakati akitoka Madna kwenda Maka.

Hiyo ni mifano tu na ipo mingi sana.

Jibidiishe kusoma vitabu vya dini akili yako itapevuka.
 
Huyo si Askofu hata kidogo Yesu aliwatuma wahubiri kuwa TUbuni na kuiamini Injili lakini Mwamakula anahubiria watu waiamini katiba mpya sijui tume hutlru ya uchaguzi nk hayo mahubiri Yesu hakumtuma
Utaendajr huko mbinguni bila kukemea huo uovu wa shetani?
 
Utaendajr huko mbinguni bila kukemea huo uovu wa shetani ?
Kazi ya askofu sio kukemea binadamu ni kuhubiri injili watu watubu na kuiamini injili sio kitu kingine kama anataka kukemea Mapepo ndiyo ayakemee sio binadamu. Hakuna mahali panasema kemea binadamu mwenzio kwa jina laYesu ni mapepo tu ndiyo yanayotakiwa kukemewa na askofu.
 
Huyo si Askofu hata kidogo Yesu aliwatuma wahubiri kuwa TUbuni na kuiamini Injili lakini Mwamakula anahubiria watu waiamini katiba mpya sijui tume hutlru ya uchaguzi nk hayo mahubiri Yesu hakumtuma

Askofu yupo sahihi kabisa, kama kiongozi wa dini anaona kabisa wananchi hawatendewi haki na hakuna anaewatetea ni haki yake askofu kujitokeza na kupaaza sauti.

Tena atakua ni mnafki kama atakaa kimya huku akihubiri kumrudia tu mungu na wakati waumini wake wanateseka kwa kukosa uhuru na amani na furaha ya nafsi.
 
ASKOFU YUPO SAHIHI KABISA, KAMA KIONGOZI WA DINI ANAONA KABISA WANANCHI HAWATENDEWI HAKI
Askofu ni mwakilishi wa Mungu duniani sio mwakilishi wa watu! Wawakilishi wa watu ni wanasiasa kama wabunge, na viongozi wa siasa

Kazi yake kutamka sauti ya Mungu sio ya watu!
 
Yaelekea wewe huna utamaduni wa kusoma vitabu vya dini.
Katika Biblia na Quran, kuna visa vingi sana vinavyo onyesha jinsi Mungu alivyo shughulika na wanadamu kwa namna mbalimbali.
Biblia: Utawala wa mabavu, ukosefu wa haki, ni moja tu ya sababu zilifanya Mungu akamtuma Musa Misri kwenda kuliokoa taifa la Israeli.

Quran: Mtu Mohammed pia amepigana vita vingi sana vya kudai haki, hasa hasa wakati akitoka Madna kwenda Maka.

Hiyo ni mifano tu na ipo mingi sana.
Jibidiishe kusoma vitabu vya dini akili yako itapevuka.
acha kutudanganya bhana, huyo mchungaji Mungu hawezi kumtuma kudai katiba Mungu anakutuma kuokoa kondoo waliopotea kama wewe kwa kuhubiri habari njema ile iletayo wokovu. Injili yenye uwezo wa kuwabadiri hata watawala na sio kutumia mineno ya kisiasa. Alafu wachungaji wengine
 
Vipi KWAJIMA(Kwa sautibya jiwe) yeye ni askofu?
Huyo si Askofu hata kidogo Yesu aliwatuma wahubiri kuwa TUbuni na kuiamini Injili lakini Mwamakula anahubiria watu waiamini katiba mpya sijui tume hutlru ya uchaguzi nk hayo mahubiri Yesu hakumtuma
 
Back
Top Bottom