Barua ya TFF kwa Bodi ya Ligi ni ya kutuandaa Kisaikolojia Wadau wa Soka nchini kwa Taarifa yao inayokuja siku si nyingi

MINOCYCLINE

JF-Expert Member
Apr 2, 2015
8,011
16,748
Baada ya TFF kuona Mechi za Nusu Fainali ya ASFC zinahusisha Timu Kubwa na zenye Ushawishi nchini Simba, Yanga, Azam na hata Biashara United FC tayari Krav Maga nimeshtukia Jambo.

Barua kutoka TFF kwenda kwa Bodi ya Ligi ( TPLB ) jana kuwa ihakiki Viwanja vya Ali Hassan Mwinyi ( Tabora ), Majimaji ( Ruvuma ) na Lake Tanganyika ( Kigoma ) kama vipo tayari Kuchezewa Mechi hizo ni kutaka tu Kutuzuga na Kutuandaa Kisaikolojia Wadau wa Soka nchini Tanzania.

Kinachoenda Kufanyika hapa ni kwamba Majibu ya TPLB yatasema Viwanja Tajwa hapo juu haviko tayari hivyo TFF ipange Viwanja vingine vizuri vya Kuchezea Mechi hizo Mbili kama si Tatu zenye Mvuto wa Kipekee nchini.

Kwakuwa tayari TFF wameshajua kuwa wana uwezo wa Kutengeneza Pesa Kubwa sana kuanzia ngazi hii ya Nusu Fainali na ile ya Fainali kama Simba na Yanga zitashinda Mechi zao Krav Maga nimehisi yafuatayo kutangazwa Siku si nyingi.

Kwakuwa inajulikana kuwa Ngome ya Simba SC ni Mkoa wa Arusha hivyo Mechi ya Azam na Simba ( Nusu Fainali ya ASFC ) itaamriwa icheze huko Sheikh Amri Abeid Kaluta ( Arusha ) ambako najua Nyomi litakuwa Kubwa na TFF kupata Mapato makubwa.

Kwakuwa inajulikana kuwa Ngome ya Yanga SC ni Mkoa wa Mwanza hivyo Mechi ya Biashara United na Yanga ( Nusu Fainali ya ASFC ) itaamriwa ikachezwe CCM Kirumba ( Mwanza ) ambako najua Nyomi lake litakuwa si la Kitoto na TFF kupata Mapato mengi tu.

Baada ya Mechi hizo za Nusu Fainali ya ASFC Kuchezwa na TFF najua tu watalazimisha Simba na Yanga zitinge Fainali tegemeni Fainali yake Kuamriwa ichezwe Uwanja mkubwa wa Benjamin Mkapa ambako hapo TFF ndiyo wanaenda Kupata Mapato ya Kufuru kwakuwa Mechi hiyo itakuwa na Mvuto baada ya Kuhairishwa Kwake Kipuuzi ( Kipumbavu ) tarehe 8 May, 2021.

Hivyo basi kwakuwa Uchaguzi Mkuu wa TFF unaenda Kufanyika tarehe 7 August, 2021 huenda Mkakati huu wa Siri ambao Krav Maga ( Mzee wa Nongwa na Fukua Fukua ) nimeuhisi ni kwamba Bajeti za Mkutano huo mkubwa wa TFF na Pesa za Kuhongea Wajumbe wa Mkutano Mkuu huo zitategemea Mapato ya kuanzia Mechi za Nusu Fainali ya ASFC, Fainali ya ASFC na ile Mechi ya Watani wa Jadi ( Simba na Yanga ) inayojulikana katika Ratiba ya tarehe 3 July, 2021.

Ukibarikiwa Akili nyingi ni raha sana tu.
 
Tafadhali Moderator na JamiiForums ( Moderators wa JamiiForums ) nisaidieni kuniwekea Kichwa cha Habari kisomeke ....Barua ya TFF kwa Bodi ya Ligi jana ni ya kutuandaa Kisaikolojia Wadau wa Soka nchini kwa Taarifa yao inayokuja siku si nyingi....

Nitawashukuruni na Akhsanteni nyote.
 
Hapo hakuna shida kama kweli tff wanamkakati huo wa kupata mapato kumbuka hata hizo timu watavuna mapato kwenye hizo mechi.
Fun base ya Simba na Yanga ipo mikoa yote Tanzania sio Mwanza na Arusha tu.

Kikubwa mechi zichezeshwe kwa haki kusiwe na upendeleo kwa timu yoyote.
 
Bila shaka wewe utakua utopolo lia lia maana fainal ni Simba na yangu kwa vyovyote vile lazma game itapigwa Kwamkapa, uwanja Wa kigoma unauwezo wakubeba watu 500 tu, wasi wasi wako ni upi mkuu.
 
Itakuwa bora sana kama hizi game zikahamishwa kuletwa ktk viwanja vikubwa kama CCM KIRUMBA au MKAPA STADIUM

Maana ni aibu Simba vs Yanga kucheza uwanja mbovu wa Lake Tanganyika
 
Mpira ni pesa sio huduma kila mtu apate. Unapeleka mpira Sumbawanga au kigoma ili iweje pumbafu sana. Peleka kwenye hela ushaona FIFA au hata CAF wanaleta Tanzania.
 
Bila shaka wewe utakua utopolo lia lia maana fainal ni Simba na yangu kwa vyovyote vile lazma game itapigwa Kwamkapa, uwanja Wa kigoma unauwezo wakubeba watu 500 tu, wasi wasi wako ni upi mkuu.
Uwanja wa Lake Tanganyika Kigoma, kama ungekuwa majukwaa yake yamejengwa vizuri au ukifanyiwa ukarabati wote. Ndio Uwanja mkubwa kuliko Vyote Tanzania.
Lake Tanganyika ni Uwanja mkubwa sana,wa Taifa unasubiri pale!
 
Angalau tumebakiwa na ma GT kama wewe lakini isije ikawa umekopy!
Acha Kunitukana Kirejareja tafadhali Ndugu sawa? Signature yangu tu katika ID yangu inabeba 100% ya Uhalisia wangu kama Binadamu.

" Gifted Intellectually, Knowledgeable, Challenger and Well Informed "
 
Hiyo
Baada ya TFF kuona Mechi za Nusu Fainali ya ASFC zinahusisha Timu Kubwa na zenye Ushawishi nchini Simba, Yanga, Azam na hata Biashara United FC tayari Krav Maga nimeshtukia Jambo.

Barua kutoka TFF kwenda kwa Bodi ya Ligi ( TPLB ) jana kuwa ihakiki Viwanja vya Ali Hassan Mwinyi ( Tabora ), Majimaji ( Ruvuma ) na Lake Tanganyika ( Kigoma ) kama vipo tayari Kuchezewa Mechi hizo ni kutaka tu Kutuzuga na Kutuandaa Kisaikolojia Wadau wa Soka nchini Tanzania.

Kinachoenda Kufanyika hapa ni kwamba Majibu ya TPLB yatasema Viwanja Tajwa hapo juu haviko tayari hivyo TFF ipange Viwanja vingine vizuri vya Kuchezea Mechi hizo Mbili kama si Tatu zenye Mvuto wa Kipekee nchini.

Kwakuwa tayari TFF wameshajua kuwa wana uwezo wa Kutengeneza Pesa Kubwa sana kuanzia ngazi hii ya Nusu Fainali na ile ya Fainali kama Simba na Yanga zitashinda Mechi zao Krav Maga nimehisi yafuatayo kutangazwa Siku si nyingi.

Kwakuwa inajulikana kuwa Ngome ya Simba SC ni Mkoa wa Arusha hivyo Mechi ya Azam na Simba ( Nusu Fainali ya ASFC ) itaamriwa icheze huko Sheikh Amri Abeid Kaluta ( Arusha ) ambako najua Nyomi litakuwa Kubwa na TFF kupata Mapato makubwa.

Kwakuwa inajulikana kuwa Ngome ya Yanga SC ni Mkoa wa Mwanza hivyo Mechi ya Biashara United na Yanga ( Nusu Fainali ya ASFC ) itaamriwa ikachezwe CCM Kirumba ( Mwanza ) ambako najua Nyomi lake litakuwa si la Kitoto na TFF kupata Mapato mengi tu.

Baada ya Mechi hizo za Nusu Fainali ya ASFC Kuchezwa na TFF najua tu watalazimisha Simba na Yanga zitinge Fainali tegemeni Fainali yake Kuamriwa ichezwe Uwanja mkubwa wa Benjamin Mkapa ambako hapo TFF ndiyo wanaenda Kupata Mapato ya Kufuru kwakuwa Mechi hiyo itakuwa na Mvuto baada ya Kuhairishwa Kwake Kipuuzi ( Kipumbavu ) tarehe 8 May, 2021.

Hivyo basi kwakuwa Uchaguzi Mkuu wa TFF unaenda Kufanyika tarehe 7 August, 2021 huenda Mkakati huu wa Siri ambao Krav Maga ( Mzee wa Nongwa na Fukua Fukua ) nimeuhisi ni kwamba Bajeti za Mkutano huo mkubwa wa TFF na Pesa za Kuhongea Wajumbe wa Mkutano Mkuu huo zitategemea Mapato ya kuanzia Mechi za Nusu Fainali ya ASFC, Fainali ya ASFC na ile Mechi ya Watani wa Jadi ( Simba na Yanga ) inayojulikana katika Ratiba ya tarehe 3 July, 2021.

Ukibarikiwa Akili nyingi ni raha sana tu.
Hiyo takataka utopolo ndio umeipeleka fainal kizembe namna hiyo? Unawajua Azam au unaongea. Recently ushawaona uto wakicheza?
Fatilia mpira dogo Acha ramli ramli.
 
Kwanza kupeleka fainali na nusu fainali huko yalikuwa ni maamuzi ya kipumbavu sana.

Huwezi kuona fainali ya FA cup inachezwa uwanja wa Blackpool au Oldham Athletics.
 
Back
Top Bottom