Barua ya TANESCO hii Hapa kwenda EWURA na Wizara ya Muhongo; Muhongo na Bosi Wako Muogopeni Mungu!

Labda niitafsiri then unieleweshe. Barua Inaanza kwa kuzungumzia tariff adjustment ya kipindi kilichopita na kueleza kwamba waliambiwa wapeleke adjustment nyingine mwezi August kwa ajili ya 2017. Kwa hiyo barua hiyo inawasilisha mapendekezo hayo. Ni barua kwenda EWURA na wamemkopi Katibu mkuu. Ni barua kabla ya consultations. Haya wapi sikuelewa? Ieleweke wazi barua hii haina approved price adjustment alizozungumzia Waziri. Kwahiyo haina jipya.

Kwanza umesema barua haiusiani na jambo lilotokea,wakati barua imeelezea walivyopunguza bei ya umeme na sasa wanatuma mapendekezo mapya kwa ajili ya mwaka 2017 kama sheria inavyosema.
Pili wamemkopi Katibu wa wizara ambae anaripoti kwa waziri husika,hapo waziri alipata habari lakini amedanganya umma kuwa hakutaarifiwa.
Tatu,wamesema wameambatanisha mapendekezo yao ya upandishaji kama ambavyo Ewura walisema Tanesco wanaomba kupandisha kwa 18.5%.
 
Ukishajua maana ya CC uje tena kumtetea Mramba.

Au kwa kukusaidia tu ni hivi hiyo Barua uliyoipost iko addressed kwa EWURA na sio KWA WIZARA. Kajifunze uandishi wa barua pia na maana halisi ya Carbon Copy (CC)

Kikubwa zaidi hiyo attached letter inazungumzia decrease ya tarrif na sio kuongezeka. Aliyekutuma hajafanya fair. Mwambie akupe barua ambayo inahusiana na tukio la sasahivi na sio hilo lililopita
Kama lugha imekusumbua uwe muwazi sio kukurupuka na kukomenti vitu usivyovijua soma vizuri hiyo barua ndo utaelewa inazungumzia nini?
 
Nampenda sana Eng. Mramba kwani ni machapa kazi. Ila nakuomba nikuulize maswali mawili:
1. Barua ya majibu iko wapi? tubandikie hapa.
2. kama Ni kweli walilipana hayo mabonus? Wakati wana madeni makubwa huko sijuiIPTL je wewe unaona ni sawa?
Mramba nina hakika hayo mabobnus ni mashiknikizo tu ya viongozi walio chini yako.

Kuna mambo sensitive kama umeme ni vema kuomba ushauri. Mtu unaomba Kupanda kwa bei kisha unatangaza je ilikwishakubaklika?!?!?!


Umemaliza, thanks!
 
Ni kweli mkuu, ni kwa sababu kwa mujibu wa sheria wizara inatakiwa kupewa taarifa tu ila wenye mamlaka ya kupandisha ni hao EWURA. Wizara inapewa taarifa tu na kama ina reservations basi inatakiwa izitoe ukikaa kimya maana yake na wewe umeridhia.
Nahisi issue hapa ni kwamba TANESCO walitakiwa waishirikishe wizara kwanza. Makubaliano ambayo wangekuwa wamefikia ndio TANESCO sasa walitakiwa kuandika hiyo barua kwenda kwa EWURA.

Hapa issue ni kwamba TANESCO imefanya maamuzi bila kumshirikisha bosi wake ambaye ni Wizara. Na kwakuwa MRAMBA inasemekana kuwa alikuwa anatafutwa long tym atumbuliwe watu wakaacha issue mpaka itolewe uamuzi na EWURA ndio wakaja na gia kuwa amekosea. Ila kiukweli alitakiwa ashauriane kwanza na Wizara na hapo ndipo alipokosea
 
Hio barua inazungumzia kushuka kwa umeme na ku submit application mpya ya 2017 lakini haijasema application ya kuongeza tariffs kiingereza cha kawaida sana hicho lakini mtu anashindwa kuelewa...

"New tariff adjustment" mkuu uliishia darasa la 7 au na wewe una PhD lakini lugha inakupiga chenga?
 
Ukishajua maana ya CC uje tena kumtetea Mramba.

Au kwa kukusaidia tu ni hivi hiyo Barua uliyoipost iko addressed kwa EWURA na sio KWA WIZARA. Kajifunze uandishi wa barua pia na maana halisi ya Carbon Copy (CC)

Kikubwa zaidi hiyo attached letter inazungumzia decrease ya tarrif na sio kuongezeka. Aliyekutuma hajafanya fair. Mwambie akupe barua ambayo inahusiana na tukio la sasahivi na sio hilo lililopita
Mkuu soma YAHUSU ya barua yaani RE: SUBMISSION OF YEAR 2017 TARIFF ADJUSTIMENT APPLICATION.

Alafu huwezi kujiuliza swali dogo tu? Punguzo la umeme litoke zamani huko alafu Barua ya Punguzo ije itoke September? Aaagh Mkuu
 
Back
Top Bottom