Barua ya Sakina ya kujiuzulu hii hapa

Status
Not open for further replies.
Ukiitazama hiyo barua ya Sakina inaelekea imetoka ofisi ya Ndg Mr.Mshana!ndiye aliye scan na kuitundika humu,ukitazama waliye pelekewa nakala ni watu wa 5 ile sehemu yenye Jina la Mr Mshana ndipo paliopo kuwa ticked kwa hiyo ina maana hiyo barua ilioyo kuwa scan imetoka ofisi ya Mshana!

...si lazima, kwani haiwezekani kuwa mtu aliamua kuiscan, ikiwa na tiki, kabla ya kupelekwa ofsini kwa Mr Mshana?
 
Assuming maelezo ya Sakina ni kweli, i.e. Mengi/Israel, namshauri akaombe kuajiriwa na gazeti la Uhuru, halafu aandike habari za kusifia CUF, CHADEMA etc;)

Swadakta domokrasi,
Na kama kuna mtu anaweza kuthibitisha hapa kwamba kuna chombo cha habari kiko huru kutenda kazi zake bila kutekeleza interest za mmiliki na aje hapa afanye hivyo.Mtu anapoamuakuanzisha biashara hasa hii ya habari anakuwa na malengo mengine fulani fulani tofauti na kufanya biashara na kupata faida. Wote tunajua namna vyombo vya serikali vinavyotoa habari zao, vyombo vya watu binafsi halikadhalika.
Ukitazama kuanzia TBC, IPP, MWANACHI COMMUNICATION, HABARI CORP, BUSINESS TIMES, UHURU PUBLICATION, SAHARA COMMUNICATION, RADIO MARIA, RADIO TUMAINI & GAZETI TUMAINI, WAPO RADIO, RADIO SAUTI YA QURAN, n.k, n.k, kila chombo kinafanya kazi kwa mujibu wa interest za mmiliki.Hakuna mwandishi atakuja hapa leo atudanganye kwamba yeye yuko huru kuandika ama kutangaza kile anachotaka yeye kwa mujibu wa taaluma yake pasipo kujali maslahi ya mmiliki, labda wandishi wa habari ambao wao wenyewe ndio wamiliki ndio hawana mtu wa kuwapangia nini cha kuripoti.
 
Assuming maelezo ya Sakina ni kweli, i.e. Mengi/Israel, namshauri akaombe kuajiriwa na gazeti la Uhuru, halafu aandike habari za kusifia CUF, CHADEMA etc;)
Sakina hili soo kajitakia mwenyewe.Wengi tukijiuliza hivi atakuwepo pale mpaka lini?
Anajaribu kuelezea jinsi alivyoiendeleza IPP na business yake na kuonyesha jinsi Editors wasivyo waaminifu au kuwa ni uozo.
Anachokosea ni kutambua kuwa pale vilevile alikuwa MUAJIRIWA wa Mengi.Sakina hana share na Mengi katika kuanzisha na kuendesha IPP na biashara ile ya habari.
Vilevile Sakina anajaribu kuingilia kujinafasi kwa "mzee wa misifa" Mengi kwa kujaribu naye kuonana na Mabalozi! Hasa Balozi wa Palestina huku akijua wazi msimo wa bosi wake!
Kama alikuwa halijui hilo basi hana nafasi katika kampuni za IPP.Uhusiano wa ushauri kwa Mengi na wale waIsraeli ni wa siku nyingi sana , au pengine akijaribu kujipima ubavu? Either way she was finished.
Kama alivyoandika hapo juu domokrasi, ukiwa Editor wa magazeti ya Serikali au Chama, andika kitu kinachoenda kinyume na msimamo wa mwenye gazeti na aanzaa kuhesabu siku zako za kutafuta kazi nyingine.
 
My view: what was the intention here? was this an appraisal or letter of resignation? A poweful resignation letter is short, and to the point, she already has mentioned "as per the contract", so why a litany? The rest of the details she should have discussed face-to-face with her employer. Perhaps she knew this was bound to leak and that's why she put it in writing. That's calculating to me. And who says media follows ethics? Cheap pretext. Ask for balanced news from Western media on Africa.
 
"Kwa heri Sakina, tulikupenda lakini mafisadi walikupenda zaidi..."
_________________________
Sauti Ya Simba:
Umenikuna hapo Mzee wangu. Na hii ndiyo iwe eptaph ya mama huyu wa Kidosi -- ajenti wa mafisadi, aliyedhani wanaJF ni wpumbavu kama anavyofikiri. (ingawa wako baadhi ni wapumbavu).
 
It is indeed very sad to see sakina leae IPP Media.
It seems Mr MENGI is already in the claws of Zionists and this is dangerous for Tanzania!
We wait and see............but Mr Mengi is also very frienddly to Muslims..Will he agree if the Zionists tell him not to?
 
Afadhali ameondoka kwa MNAFIKI,MBAGUZI na FISADI nyangumi,(mengi) how can a trusted lady like her work with such a human being?? she deserve more than working with mengi LoL
 
It is indeed very sad to see sakina leae IPP Media.
It seems Mr MENGI is already in the claws of Zionists and this is dangerous for Tanzania!
We wait and see............but Mr Mengi is also very frienddly to Muslims..Will he agree if the Zionists tell him not to?

Mengi could be a friend of ''muslims'' but I highly doubt he is a friend of Muslims!
 
nadhani wote tuliosoma barua hii tumeona jinsi mengi alivyo mpuuzi na mbaguzi.

nenda dada, kama vp hata huo mwezi mmoja achana nao. huyu mzee mpuuzi sana, kumbe hata front page yeye ndo huwa anasema ikae vip!!!!?
 
Wna Jamii nimesoma barua ya resignation ya Sakina Datoo kwend kwa boss wake amabayo ina mambo mengi sana, jamabo ambalo naomba kuuliza je alichokifanya Sakina kwa kuandika ile barua ambayo inamhusu yeye na mwajiri wake na kuipost Huku Jamii ni sawa!! Na je IPP hawana zile document za confidentiality, kwa sababu naona mengi aliyo yaandika mle ni internal information amabazo zilipaswa kuwa siri kai yake na mwajiri wake,

Does it add value sie tukiresign tupost zile barua humu

Naomba msaada
 
Wna Jamii nimesoma barua ya resignation ya Sakina Datoo kwend kwa boss wake amabayo ina mambo mengi sana, jamabo ambalo naomba kuuliza je alichokifanya Sakina kwa kuandika ile barua ambayo inamhusu yeye na mwajiri wake na kuipost Huku Jamii ni sawa!! Na je IPP hawana zile document za confidentiality, kwa sababu naona mengi aliyo yaandika mle ni internal information amabazo zilipaswa kuwa siri kai yake na mwajiri wake,

Does it add value sie tukiresign tupost zile barua humu

Naomba msaada

Privacy and confidentiality has an Act/ in other countries is being adopted to private agreement. Mwajiri na mwajiriwa lazima waingie mkataba wa kufichiana siri. Labda bongo sijui na kama ipo basi Datoo anaweza chukuliwa hatua za kinidhamu za kufujisha siri za mikataba.

Pili resignation ina kopi kweli? Mimi huku ughaibuni nilistaafu kazi nikasaini fomu pia nikaziacha sikuondoka na kopi yoyote. Labda huyo Datoo kaitunga yake.

Wakuu nawasilisha tu! haka kahoja.
 
watu wengine kwani ile thread imefutwa?si uweke hukohuko.Halafu nakureport sasa hivi nani kakwambia aliyepost ile barua ni Sakina, naona unaanza ku speculate ID za watu.
 
Tuache mambo ya assumptions hapa....hatujui hii barua imeingiaje hapa katka JF....hii mjadala imeendelea sana sasa....hakuna haja kuanzisha thread nyingine...kama kupost views ile thread ya zamani ipo bado...
 
Wna Jamii nimesoma barua ya resignation ya Sakina Datoo kwend kwa boss wake amabayo ina mambo mengi sana, jamabo ambalo naomba kuuliza je alichokifanya Sakina kwa kuandika ile barua ambayo inamhusu yeye na mwajiri wake na kuipost Huku Jamii ni sawa!! Na je IPP hawana zile document za confidentiality, kwa sababu naona mengi aliyo yaandika mle ni internal information amabazo zilipaswa kuwa siri kai yake na mwajiri wake,

Does it add value sie tukiresign tupost zile barua humu

Naomba msaada

Kimambo

Nina mashaka kwamba wewe ni Mtanzania kweli, na kama ni Mtanzania, sijui unaweka kipaumbele wapi.... maslahi binafsi au utaifa?

Kama ningekuwa mimi Sakina ningetoa nakala ya hiyo barua ya kudurufu na kuiscan, kisha kuipost humu ndani, lakini bahati nzuri, mzalendo mwenzetu mwenye uchungu na nchi yake ndiye ametusaidia kuweka wazi ukweli wa jinsi Mengi anavyowaburuza watendaji wake, kila siku anasimama jukwaani na kudai kwamba yeye haingilii utendaji wa kazi wa viongozi wa magazeti (sasa yanakosa maana halisi...) ya IPP Media.

Ukisoma kwa undani, kilichompelekea Sakina kujiuzulu, na kukiri wazi wazi sababu zake za kufanya hivyo, ni ukosefu wa maadili, au upotoshwaji wa makusudi wa maadili, unaosimamiwa na Mengi, akidiriki kuwashambulia waziwazi watu anaokinzana nao, ama kwenye maslahi binafsi ya kibiashara, kisiasa au kijamii, kwa sababu anazozijua yeye mwenyewe.

Sakina ameandika waziwazi kwamba yeye hawezi kuwa chombo cha kuendeleza mapambano ya kuwashambulia watu wasio na hatia, wasiostahili kufanyiwa hivyo, kwa kuwa tu, mtu unamiliki chombo kama hicho cha habari, kisha unaamua kufanya utakavyo...

Kimambo, unahoji kama alichokifanya Sakina kiko nje au ndani ya maadili? Kwa nini usiangalie maadili yenyewe yanavyokiukwa, kabla ya kuhoji uhalali au kinyume cha uhalali, wa ku-post hiyo barua hapa? Na, kwa kweli, si kawaida kwa barua kama ile kukutwa humu, ni LULU ya JF, na sisi tumeisoma, tumeshukuru. Wewe unaleta za wapi hapa?

Kimambo, unanikumbusha kauli aliyoitoa Waziri wa Nchi, Hawa Ghasia, kuhusu nyaraka za siri za Serikali. Unataka kuhalalisha watu kuendelea "kukaa kimya" huku wakiwa mashuhuda wa ufisadi? Ufisadi upo kwenye ngazi zote za jamii, na kama mimi ningekuwa mtendaji wa umma (civil servant) ambaye angeona nyaraka za Serikali, ambazo zimepigwa chapa ya SIRI kwa maandishi mekundu, lakini nyaraka ambazo zinastahili kusomwa na UMMA, ningekuwa wa kwanza - kwa usiri mkubwa sana - kuzidurufu, ili UMMA wa WATANZANIA uweze kujua habari zake.

Kuna usemi unaosema: Uovu unastawi kwenye jamii kwa kuwa watu wema wanakaa kimya bila kuupinga.

Uko upande upi, ndugu Kimambo... utawatetea waovu au watu wema?

Kazi kwako!

./Mwana wa Haki

P.S. Kama nimekukera, samahani, lakini.... Utalijua Jiji! Tumechoka kuburuzwa kama ng'ombe! Daima nitasema ukweli!
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom