Barua ya Sakina ya kujiuzulu hii hapa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Barua ya Sakina ya kujiuzulu hii hapa

Discussion in 'Jamii Intelligence' started by deepesttthroat, Jul 4, 2009.

Thread Status:
Not open for further replies.
 1. d

  deepesttthroat New Member

  #1
  Jul 4, 2009
  Joined: Jul 3, 2009
  Messages: 2
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mambo ndiyo hayo!
   

  Attached Files:

 2. Mauza uza

  Mauza uza JF-Expert Member

  #2
  Jul 4, 2009
  Joined: Jul 24, 2008
  Messages: 2,068
  Likes Received: 785
  Trophy Points: 280
  very low!and poor Sakina...LOL.A resignation letter not supposed to be that looong.She just need to resign and thats it.No explanations like that.Poor Sakina!!!:confused:
   
 3. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #3
  Jul 4, 2009
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160

  Sasa wewe unaongea vitu gani? Barua ulizozoea wewe zina urefu gani?
   
 4. Dingswayo

  Dingswayo JF-Expert Member

  #4
  Jul 4, 2009
  Joined: May 26, 2009
  Messages: 4,011
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 145
  And who said that the Zionists do not control the world media? Hii kali sana, mpaka Tanzania?
   
 5. Kasheshe

  Kasheshe JF-Expert Member

  #5
  Jul 4, 2009
  Joined: Jun 29, 2007
  Messages: 4,690
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 145
  Yaliyosemwa na Rostam hayoooo, Loud and Clear.

  Du! Mh. Mengi huoni aibu kuwa kuchagulia editors cha kuandika?
   
 6. Mauza uza

  Mauza uza JF-Expert Member

  #6
  Jul 4, 2009
  Joined: Jul 24, 2008
  Messages: 2,068
  Likes Received: 785
  Trophy Points: 280
  resignation letter= no need ya kuweka achievements zako...lol.hio sio CV unaomba kazi.Unajiuzulu basi mchezo umekwisha malalamiko mengi ya kazi gani?????
  job true true!!!lol
   
 7. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #7
  Jul 4, 2009
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  Hayo ni maoni yako...

  Mi naona alichofanya kimetulia maana ameeleza kinaga ubaga nini sababu za yeye kuachia ngazi..hilo ndo la msingi..Hatupo high school kufunzana grammar au letter writing
   
 8. Kasheshe

  Kasheshe JF-Expert Member

  #8
  Jul 4, 2009
  Joined: Jun 29, 2007
  Messages: 4,690
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 145
  Yeap kuonyesha kwa nini unajiuzulu ni professionalism.

  BTW:

  Key things to note:-
  • I embarked into recruit highly skilled personnel, whose presence has given a great boost to the Guardian Newspapers.

  • The word "re-launch" featured very much in her letter!
  • ... the newsroom was in a dilapidated stage, both physically and emotionally
  • ... the management has come up with financial recovery plan for unprofitable The Guardian Ltd....
  • ...trashy newspapers... Sema Usikike and Taifa Letu
   
 9. E

  Epitome Member

  #9
  Jul 4, 2009
  Joined: Apr 27, 2009
  Messages: 10
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wewe kweli ndo maana ukajiita mauza uza. Sasa ndo nimeamini. Unashangaa nini sasa kwenye hiyo barua?
   
 10. Raia Fulani

  Raia Fulani JF-Expert Member

  #10
  Jul 4, 2009
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 10,219
  Likes Received: 84
  Trophy Points: 145
  mwanzo nilimchukulia huyu dada kirahisi tu nikadhani kwa vile Mengi kawalipuwa waajemi wale, basi dada kamaindi. kumbe sio. she is focused, professional, dedicated, loyal, etc. huu ugonjwa umezagaa sana wa kuchanganya kazi na maslahi binafsi. kwa mtu anayependa kujikomba, atafanya kile bosi anataka hata kama sio professional, ila kwa mtu makini kama sakina ni tofauti. namsifu sana huyu dada. kwa mara nyingine inadhihirisha ni jinsi gani ngozi yetu ilivyo na matatizo. nilikuwa nasoma gurdian muda si mrefu nikashangaa naendelea tu kitu ambacho si kawaida kwangu. kumbe kuna kazi imefanyika ndani ya mwaka mmoja tu! ya kuliboresha. once again, the problem with africans is implementation and maintenance
   
 11. Yo Yo

  Yo Yo JF-Expert Member

  #11
  Jul 4, 2009
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 11,247
  Likes Received: 73
  Trophy Points: 0
  bwa ha ha ha ha mwanakijiji msemaji wa mengi yuko wapi?
   
 12. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #12
  Jul 4, 2009
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 11,606
  Likes Received: 3,906
  Trophy Points: 280

  desa hili sina , naomba reference mkuu utausadia wengi
   
 13. M

  MpendaTz JF-Expert Member

  #13
  Jul 4, 2009
  Joined: May 15, 2009
  Messages: 1,579
  Likes Received: 116
  Trophy Points: 160
  Inaonyesha ameshindwa hata kuficha kidogo, kuwa alikuwa anafanya kazi yake siyo ya Boss wake! Waajiriwa wa aina hii ni hatari sana. Kichwa ngumu sana, inaonekana wazi. Nadhani Mengi alikuja kufahamu !a bit late" ndiyo maana akajaribu kumhamisha sumu ikamtoka. Inaonekana angekubali kuhamia alikotakiwa kuhamia asingelikuwa tena na "feedback" nzuri kwa washirika wake. However, Mengi anatakiwa kutafuta " much better replacement" be it loacal or international.
   
 14. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #14
  Jul 4, 2009
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0

  Hii ni stori ya upande mmoja of course – hatujapata bado upande wa pili. Ukweli wa huyu mama utakuja kujulikana tu.

  Lakini habari zinazotoka newsroom ya IPP-Media zinaonyesha kuwa mzee Mengi alimshtukia mama huyu Mdosi kwamba ni “pandikizi” wa wale mapapa aliyowataja – akina RA. Wanavyosema wenyewe kule IPP ni kwamba alivuta mzigo kabambe kutoka kwao ili awe anawatolea siri za IPP Media nk.

  Kwa hivyo Sakina sasa akiajiriwa Habari Corporation haitashangaza – tusubiri tu.

  Kuna uongo wa dhahiri katika barua yake hiyo ya kujiuzuru – na hasa katika suala la kumkumbatia balozi wa Palestina kuwa ndiyo sababu ambayo ilimwondoa pale, kwani Mengi ana mahusiano mazuri na Israel.

  Hii kaiweka kwa sababu eti tu Mengi ana uhusiano na kampuni ya Coca Cola ambayo inamilikiwa na Wayahudi. Sidhani kama sababu hii ni strong – hasa ukiona bidhaa hizo za coca Cola zinavyouzwa katika nchi za Kiarabu, pamoja na sehemu za Wapalestina.

  Lakini kikubwa ni kwamba Sakina katunga uongo, kwa sababu miaka kama miwili au mitatu nyuma, ITV ilitoa coverage ya tukio ambapo balozi wa zamani wa Palestina, akiandama na timu ya maripota wa ITV na Guardian walikwenda Mkuranga ku-cover tukio la kumtuza mtoto mmoja aliyezaliwa na ulemavu pale na ambaye wazazi wake walimpa jina la Arafat.

  Balozi huyo alimvalisha medali yenye picha ya Arafat na pia kutoa misaada mingine ya pesa nk kwa mtoto huyo na wazazi wake. Hii coverage ilisimamiwa na Kyondo Mshana wa Guardian na ripota wengine wa ITV.

  Mimi nadhani ITV itatoa hiyo footage kuonyesha jinsi balozi wa Palestina alivyokarimiwa na ITV ili ku-mprove Sakina wrong. Jee wakati huo Mengi hakuwa na uhusiano na Coca Cola?

  Aidha kuna mwana JF mmoja hapo juu kasema eti Sakina amethibitisha habari kwamba Mengi anaamrisha habari zipi zitoke na zipi zisitoke kwenye magazeti. Pengine sipingi hilo, lakini ukijua jinsi RA anavyoamrisha wahariri wa magazeti yake kutoa habari anazotaka yeye, utaona ya Mengi ni “cha mtoto.”

  Mnakijua kilichonfanya Atilio Tagalile aliyekuwa Mhariri Mkuu wake kujiuzulu? Mnakijua kilichomuondoa Rosemary Mwakitwange kama CEO wa New Habari Corporation? Ni hayo hayo – kulazimisha kuwekwa kwa stori zisizokuwa na maadili kabisa - za kutetea ufisadi na mafisadi – hakuna kingine. Mkiweza muulizeni Mama Mwakitwange.

  RA amejaza ma-yesmen katika newsroom yake. Nani asiyejua u-spin doctor wa Muhimgo Rweyemamu, Manyerere Jackton na wengine?

   
 15. Kwetunikwetu

  Kwetunikwetu JF-Expert Member

  #15
  Jul 4, 2009
  Joined: Dec 23, 2007
  Messages: 1,544
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Sakina kaeleza mazuri yake yote kadri alivyoona yanapaswa, thats great. Lakini bahati mbaya hatufahamu weakness zake....ambazo bila shaka zipo. Pili, hizo success zote alizotaja its okay but watu hufanya kazi kama team work, sio kweli mawazo yake tu ndio yalileta success zote hizo, bali michango ya wenzake pia. Kuhusu hiyo collision ya mwisho sababu ya kuhost balozi wa Palestina ameona ni gia tu ya kutokea kwa vile alishasema tangu mwanzo walipingana kuhusu magazeti ya udaku.... na kwa hali ilivyo sasa Mengi Vs Mafisadi sio rahisi kwa Mengi kumsikiliza Sakina juu ya hilo. So Mengi alipoona Sakina anasumbua kuhusu hizo issues then akaona amweke pembeni, lakini as usual tumezoea kupanda, so mtu akiona anashuka anaona bora ajiachie..

  Mtizamo wangu, naweza kupingwa..
   
 16. LazyDog

  LazyDog JF-Expert Member

  #16
  Jul 4, 2009
  Joined: Apr 10, 2008
  Messages: 2,478
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135
  Deepesttthroat, una maoni yoyote mkuu? ;)
   
 17. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #17
  Jul 4, 2009
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0


  Kuhusu issue ya coverage ya mtoto mlemavu nami nakumbuka kuiona hiyo coverage katika ITV, nadhani ilikuwa mid 2006. Mengi hana uhasama na Wapalestina, Sakina ni muongo sana -- atafute sababu nyingine kwa nini ghafla alionekana hakutakiwa pale.

  Namwomba Mengi aitafute hiyo footage na kumtumia Sakina, na pia airudie katika ITV.
   
 18. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #18
  Jul 4, 2009
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Hata mimi nakumbuka hiyo coverage ya ITV na balozi wa Palestina - nadhani yule aliyeondoka, siyo huyu, kwani muda umepita kidogo.

  Lakini issue ni vipi anaandika barua ya kujiuzulu ndefu hivyo na kutoa malalamiko ya upande mmoja na kuileak (au alitaka iwe leaked) humu JF? Anataka sympathy ya nani? Kama aliyakoroga kule Guardian, basi ni ayanywe tu polepole, kama wanavyofanya wengi, akiwemo huyo mama Mwakitwange aliyetajwa hapo juu -- kimya kimya tu aliondoka New habari, bila kupayuka hovyo!

  Hayo ya kumkandia Mengi bila shaka amefundishwa na hao waliomtuma kwenda huko Guardian -- wale mafisadi mapapa. Nadhani itakuwa ni hivyo tu.
   
 19. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #19
  Jul 4, 2009
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Zak, wewe ni muandishi mzuri na nakuheshimu kwa hoja zako... nakubaliana na wewe hata kwenye hili, ila jaribu ku-play neutral kidogo hatujui kama ni sakina aliyelikisha hiyo letter au la!! pia kuna mengi behind the closed doors.. hatujui sakina atajikisiaje kama barua yake confidential imewekwa humu bila ridhaa yake

  ...fun loving criminal....
   
 20. macho_mdiliko

  macho_mdiliko JF-Expert Member

  #20
  Jul 4, 2009
  Joined: Mar 10, 2008
  Messages: 6,437
  Likes Received: 2,352
  Trophy Points: 280
  Mh....ku-play neutral unakujua wewe? Wacha kunivunja mbavu bwana!!
   
Thread Status:
Not open for further replies.
Loading...