Barua ya pili kwa Rais Dkt. Magufuli baada ya barua ya awali kutotoa matunda, vyombo husika naomba mfikishe

FrankLutazamba

JF-Expert Member
Aug 9, 2018
449
408
Rais kama ni ushindi wa kishindo umepata, tunayajua haya kwa kuwa tuna bwana anayetupa majibu. Rais kilio changu ni kufukuzwa kazi bila kufuatwa kwa utaratibu wala kuhojiwa achilia mbali nilikuwa naumwa na taarifa nilitoa, sikukaa kimya niliandika barua Tamisemi kwa George Mkuchika wakati huo akiwa waziri wa Tamisemi

Walikaa miezi miwili wakanijibu niende ajira vijana na wenye ulemavu,sikwenda nikaomba ushauri kwa kada wa Chama chetu Humfrey Polepole, yeye akanishauri niwaone na kufungua shauri CMA, namshukuru sana kwani sikuwa najua, kumpigia mtu wa CMA wa Mwanza akasema mda umepita miaka name sasa

Lakini Rais mwaka 2018 niliwahi kukuandikia barua ukiwa ikulu Magogoni watumishi wako wakadai barua yangu imekufikia hivyo naomba unitendee haki.

Sasa hivi na Mimi nimenunua beberu, navizia ukitembelea huku nilipo nikupe kama zawadi nilie na shida yangu labda utanisaidia na Mimi ni mwanachama hai wa CCM na huwa nakipa kura kwa hili siwezi badilika.

Nina imani barua hii itakufikia kwa wakati kwani najua intelijensia yetu hailali na IPO macho sawa na Jua, linapenya mwanga kila mahali na kwa msaada wa Mungu wanaweza, basi utoe maamuzi ili ndugu na jamaa waridhike, mbona umetatua mengi na wengine ni wagombea sasa.

Asante.
 
Labda uwaroge ndio wakuajiri tena .
Kaimbe ule wimbo wa mbere kwa mbere.
Mwenzako juzi alikuwa anaomba ushauri baada ya mama yake mzazi aliyemtegemea huenda angeachana na baba yake mzazi kurudiana na mume wake. Alimshawishi mama waachane na baba yeye apate chochote kitu kutoka kwa mama.
 
Nilifikiri kweli unashida nikusaidie lakini baada ya kusoma paragraph ya tatu na kuendelea nikagundua kumbe na soma ujumbe wa "Utopolo". Basi Wasalimie huko ulipo!
Nisaidie kama unaweza,huo ni uandishi hujui uandike kipi kitakuwa bora
 
Unaongea ishu serious af unachanganya dhihaka ndani yake? Kijana unajua Rais ni taasisi?
 
Unasikitisha sana, unaomba msaada kwenye issue serous kiasi hicho halafu unamwambia rais umpe beberu ? Hapo tu umeshapoteza legitimacy ya hiyo barua
Hata mimi binafsi nimeshangazwa sana na huyu mleta lalamiko, nadhani hata wale wenye nia na uwezo wa kumsaidia watampuuza baada ya kuandika utoto kwenye lalamiko lake.
 
Rais kama ni ushindi wa kishindo umepata, tunayajua haya kwa kuwa tuna bwana anayetupa majibu. Rais kilio changu ni kufukuzwa kazi bila kufuatwa kwa utaratibu wala kuhojiwa achilia mbali nilikuwa naumwa na taarifa nilitoa, sikukaa kimya niliandika barua Tamisemi kwa George Mkuchika wakati huo akiwa waziri wa Tamisemi

Walikaa miezi miwili wakanijibu niende ajira vijana na wenye ulemavu,sikwenda nikaomba ushauri kwa kada wa Chama chetu Humfrey Polepole, yeye akanishauri niwaone na kufungua shauri CMA, namshukuru sana kwani sikuwa najua, kumpigia mtu wa CMA wa Mwanza akasema mda umepita miaka name sasa

Lakini Rais mwaka 2018 niliwahi kukuandikia barua ukiwa ikulu Magogoni watumishi wako wakadai barua yangu imekufikia hivyo naomba unitendee haki.

Sasa hivi na Mimi nimenunua beberu, navizia ukitembelea huku nilipo nikupe kama zawadi nilie na shida yangu labda utanisaidia na Mimi ni mwanachama hai wa CCM na huwa nakipa kura kwa hili siwezi badilika.

Nina imani barua hii itakufikia kwa wakati kwani najua intelijensia yetu hailali na IPO macho sawa na Jua, linapenya mwanga kila mahali na kwa msaada wa Mungu wanaweza, basi utoe maamuzi ili ndugu na jamaa waridhike, mbona umetatua mengi na wengine ni wagombea sasa.

Asante.
Weka picha yako umevaa tshirt ya fisiem,huku unakata uno lazima utasikilizwa
 
Back
Top Bottom