Barua ya mama kwenda kwa mwanaye - siku tatu baada ya mazishi

Mpendwa mwanangu,

Nataka ujue kwa nini nilikufa nikiwa masikini wakati nina mtoto kama wewe.

Mwanangu, nilitaka kukupa baraka zangu kabla sijafa, lakini sasa nimeondoka na baraka zangu.

Chakula changu cha asubuhi, cha mchana na cha usiku kilikuwa miongoni mwa changamoto zangu nilipokuwa hai, lakini wewe umetumia pesa kupika kila aina ya vyakula, nyama na kununua aina mbalimbali za vinywaji siku ya mazishi yangu.

Mwanangu, ulichagua kuupaka mwili wangu uliokufa kwa kutumia mafuta mazuri na manukato yenye kunukia wakati nilipokuwa hai nilitumia mawese kujipaka kwa kukosa mafuta.

Umeivika maiti yangu kwa nguo ghali wakati ulishindwa kuninunulia hata khanga.

Maiti yangu ilipokuwa mochwari ulikuja kunitazama mara kwa mara, kwa nini umeijali maiti yangu wakati ulishindwa kunijali nilipokuwa hai?

Kitu kinachoniuma zaidi ni jeneza la bei kubwa ambalo umeuweka mwili wangu ilhali nilipokuwa hai The most painful niliishi katika nyumba mbovu ambayo haikumaliziwa kujengwa.

Ulipokuwa mdogo nilikaa na njaa ili wewe ule na kushiba, nilivaa nguo kuukuu ili upate nguo za kutosha. Nilidhani utanitunza nikizeeka.

Wakati wa mazishi yangu ulimalizia nyumba, ukaipaka rangi na kuusafisha uwanja ndani ya wiki moja ili tu upate kuadhimisha mauti yangu.

Sasa umeniandikia tanzia ukisema "Mama, nakupenda sana, pumzika kwa amani" - ilhali nimekufa nikiwa na maumivu moyoni.

Mwisho kabisa, mwanangu, nimekuandikia kukukumbusha kuwa hakuna mtu anayempenda mtoto kama mama yake.

MUNGU AKUSAMEHE MWANANGU!
Toa hilo neno la kingereza kwenye hiyo barua.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom