Barua ya CHADEMA kama Bunge lilipokea kwanini Naibu Spika anakataa?

Lord OSAGYEFO

JF-Expert Member
Feb 19, 2021
3,086
4,881
Nimekuwa najiuliza hawa Viongozi walioapa kuilinda na kufanya kazi zao kwa kuheshimu Katba kwanini wanasema uongo? Juzi ktk kikao cha Bunge Mmoja wa Wanachama waliofukuzwa na Chadema aliliambia Bunge kuwa alifukuzwa uanachama lakini kwa Nguvu na Sauti kali Naibu Spika akamwamuru eti Afute hiyo kauli na Naibu Spika akadai Bunge halijapokea Barua toka Chadema ya kuwafukuzwa Wakati Ofisi ya Bunge na Tume zote zilikwishapokea. Kutokana na Bunge kupokea hiyo Barua basi ni wazi Naibu Spika Kalidanganya Bunge na Wabunge wako kimya.

Je, kwanini Naibu Spika aseme Uongo?

Je, Mtu anapolidanganya Bunge Sheria inasemaje?

Kwanini Spika yupo Kimya licha ya kupokea hiyo Barua?

Kwanini Serikali inawalipa Mishahara Wabunge ambao hawana Sifa baada ya kufukuzwa na Chama chao? Mh. Rais huwa ni wizi wa Fedha za Serikali unaofanywa kwa Makusudi na Bunge.
 
Ili kukata mzizi wa fitna ni wakati sasa Chadema waandike barua nyingine (itakuwa ya tatu) kulitaarifu Bunge kuhusu kufukuzwa uanachama wa wahusika waweke rekodi sawa maana ndimi za uongo ni nyingi sana; yaani uongo umekuwa mojawapo ya sifa za viongozi wa kiserikali.
 
Yeye J J Mnyika hiyo barua aliipeleka kwa Spika au kwa Katibu wa bunge?
Barua ya kiofisi sio sawa na ya kutongoza kwamba inaweza tumwa hata kupitia mtoto, unapohoji barua ilipelekwa kwa spika au katibu wa bunge maana yako ni ipi?

Kwamba CHADEMA hawajui utaratibu wa kuwasiliana na ofisi ya bunge na wapo bungeni tangu 1995? Hicho kipindi chote hawakuwahi kuwasiliana na bunge?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Barua ya kiofisi sio sawa na ya kutongoza kwamba inaweza tumwa hata kupitia mtoto, unapohoji barua ilipelekwa kwa spika au katibu wa bunge maana yako ni ipi?
Sasa kama wanajua mbona barua yao haionekani kwenye kumbukumbu za bunge?
 
Tulia na Ndugai wanadhani hizi ni enzi za Pombe aliewatuma kuvuruga bunge.

1619591109211.png
 
Samahani Comrade, how old are you?
Mambo ya kienyeji hayo ndio madhara yake.

Tatizo la covid 19 lilishakuwa la kisheria ilimpasa J J Mnyika kuwa makini badala ya kurudia kosa lile lile alilolifanya Tume ya uchaguzi.

Jiulize kwanini barua za Mnyika tu ndio zinazua sintofahamu?
 
Sasa kama wanajua mbona barua yao haionekani kwenye kumbukumbu za bunge?
Kuona ni kuamua bwashee, mfano ungesema hujaona post yangu naanzaje kukulazimisha?

Hii inadhihirisha tulivyo na mifumo mibovu inayoweza kuingiliwa na hisia za wajinga kwa manufaa yao binafsi na hakuna check and balance, ndio sabab unaona Meko aliweza kuagiza bunge na mahakama tena hadharani watende kwa kadri ya utashi wake yeye.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huwa ni kawaida ya nyumbu kuona yuko salama mbele ya mdomo wa Simba.

Rais Samia wanyooshe tena.
 
Back
Top Bottom