Barua ya Albert Einstein kumhusu Mungu yauzwa kwenye mnada kwa bei ya $2.9m(£2.3m).

S V Surovikin

JF-Expert Member
Aug 8, 2015
13,583
32,643
Barua iliyoandikwa kwa hati ya mkono na Albert Einstein, ambapo anajadili suala la dini na imani, imeuzwa kwenye mnada kwa bei ya karibu $2.9m (£2.3m).

Bei hiyo imepita makadirio.

Barua hiyo ambayo kwa utani imekuwa ikiitwa "Barua ya Mungu" aliiandika Einstein mwaka 1954 na ilitarajiwa kuuzwa $1.5m (£1.2m) mnadani New York.

Mwanasayansi huyo aliyeshinda tuzo ya Nobel,aliandika barua hiyo ya ukurasa mmoja unusu akiwa na umri wa miaka 74. Lilikuwa ni kama jibu kwa mwanafalsafa Mjerumani Eric Gutkind kuhusu baadhi ya kazi zake. Gutkind alikuwa pia Myahudi.
Huwa inatazamwa na wengi kama tangazo la msimamo wa Einstein katika mjadala kuhusu sayansi na dini.

"Barua hii yenye uwazi sana, ya kibinafsi iliyoandikwa mwaka mmoja kabla ya kifo cha Einstein inasalia kuwa nyaraka pekee yenye kudhihirisha wazi msimamo wake wa kidini na kifalsafa," taarifa kutoka kwa waendesha mnada wa Christie inasema.

Barua hiyo iliuzwa karibu mara dufu ya bei iliyokadiriwa ambayo ilikuwa kati ya $1m-1.5m. Katika barua hiyo, aliyoiandika kwa Kijerumani ambayo ilikuwa lugha yake asilia, Einstein amekosoa imani ya sasa kumhusu Mungu.

"Neno la Mungu kwangu tu ni jambo la kuelezea udhaifu wa binadamu na ni matokeo ya udhaifu huu wa binadamu," naandika. "Biblia ni mkusanyiko wa hadithi za kale lakini za kuheshimiwa na kutukuzwa, ingawa kwangu zinaonekana zaidi kuwa za kitoto."

Anaendelea: "Hakuna fasiri yoyote, hata iwe ya kina na ya kupambanua zaidi kiasi gani, ambayo kwangu inaweza kubadilisha mtazamo huu wangu."

Mwanafizikia huyo pia anajadili asili na utambulisho wake, Uyahudi.

Anaandika kwamba dini hiyo "ni kama dini nyingine zote , ni mtazamo mpya wa hadithi za kale". "Wayahudi, ambao najivunia kuwa mmoja wao, na ambao nimejikita kwenye mtazamo wao wa maisha, bado kwangu hawana kitu chochote tofauti na wengine," ameandika.

"Kwa yale niliyoyaona, si bora kulikobinadamu wengine, ingawa wamelindwa dhidi ya saratani mbaya zaidi kutokana na kukosa mamlaka. Kando na hayo, sioni kitu chochote "kiteule" kuwahusu." (Aliandika hayo miaka michache tu baada ya Vita Vikuu vya Pili vya Dunia kumalizika, ambapo Wayahudi wengi waliuawa na utawala wa Nazi, na pia taifa la Israel lilikuwa bado halijapata nguvu).

Hii si mara ya kwanza kwa barua ya Enstein kuuzwa mnadani. Mwaka jana, barua aliyomwandikia mwanafunzi wakemia kutoka Italia ambaye alizuiwa kukutana naye iliuzwa $6,100.

Iliuzwa pamoja na barua nyingine za Einstein, ikiwemo barua moja ya mwaka 1928 iliyouzwa $103,000.

Kwenye barua hiyo alikuwa ameeleza mawazo yake kuhusu awamu ya tatu ya kile ambacho baadaye kiligeuka kuwa nadharia kuhusu uhusiano wa vitu kwenye maumbile, kwa Kiingereza Theory of Relativity.

Mwaka 2017, barua yake ambapo alikuwa anatoa ushauri kuhusu maisha yenye furaha iliuzwa $1.56m mjini Jerusalem.
Barua hiyo yenye aya moja tu, inasema: "Maisha ya utulivu na ya kunyenyekea yatakuletea furaha zaidi kuliko juhudi za kutafuta ufanisi na misukosuko inayoambatana na harakati na ufanisi huo."

Einstein aliamini kwamba Mungu yupo?
Einstein alikuwa kwenye kundi la watu ambao imani yao huitwa Pantheism kwa Kiingereza. Ni watu wanaoamini kwamba "Mungu ni kila kitu". Mara kadha, alionyesha mtazamo huu kwenye mawasiliano yake na Rabbi Herbert S. Goldstein, "Ninaamini katika Mungu wa Spinoza, ambaye anajidhihirisha kupitia upatanifu wa vitu vyote vilivyomo, si katika Mungu anayejishughulisha katika hatima na matendo ya binadamu."

Pantheism kwa njia rahisi zaidi ni imani kwamba kila kitu humwakilisha Mungu. Wenye kufuata imani hii mara nyingi hueleza kwamba Mungu ni vitu vyote vilivyopo, au kwamba mambo na vitu vyote ni Mungu.

Kwamba kila ukionacho ni sehemu ya Mungu.Aina ya Pantheism ya Spinoza aliyoiamini Einstein huamini kwamba kila kitu kinafanana na Mungu.

Kwamba Mungu hana ubinafsi na hayajali mambo ya binadamu. Kwa kila kitu kimeundwa na vitu vilevile vya msingi, ambavyo anatoka Mungu.

Kwamba Sheria za Fizikia hazina la kuzipinga, na kwamba kila jambo lina matokeo yake. Kila jambo linalotokea au kuwepo
lilitokana na hitaji lake kuwepo na lilikuwa nia ya Mungu.

Kwamba kwa binadamu, furaha na kuridhika maishani hutokana na kuifahamu dunia na vitu vinavyoizingira badala ya kuomba Mungu aingilie kati.

Benedict de Spinoza alikuwa mwanafalsafa Myahudi aliyezaliwa Uholanzi na wazazi Wayahudi kutoka Ureno Novemba 24, 1632, Amsterdam na akafariki Februari 21, 1677 mjini The Hague, Uholanzi.

Licha ya haya yote Einstein bado alidumisha baadhi ya tamaduni na mila za Wayahudi.

Hali kwamba alikuwa Mwanasayansi na kwamba aliongozwa na fikira katika kuufahamu ulimwengu ilimzuia kuwa na imani ambayo inaweza kuwafanya watu waseme alikuwa wa dini fulani.

Alikataa kupewa mazishi ya kitamaduni ya Wayahudi.

Ingawa bado alikuwa anazungumzia kuhusu kuamini kuhusu Mungu, alikuwa si Mungu wa dini za Kiabrahamu (Kikristo, Kiislamu na Kiyahudi ) na pia hakuwa Mungu anayerejelewa na watu walioamini kwamba Mungu yupo.

Alikuwa mara nyingi anajizuia kujiingiza kwenye mjadala kuhusu nani msema kweli, dini au sayansi.

Aidha, hakutaka kuamini kutumiwa kwa sayansi kama kielelezo katika kuamua maadili.

Wakati wa Vita Vikuu vya Pili vya Dunia, alinukuliwa akisema: "Bado wapo watu, wanaosema Mungu hayupo. Lakini kinachonighadhabisha zaidi ni kwamba huwa wananikuu wanapoeleza msimamo wao huo.

Bwana Kiranga natamani kusikia mtazamo wako kumhusu huyu mtu.
 
Einstein ni moja ya watu walioni inspire ...

Mpaka leo hii nmekua scientist
hio ndio kazi pekee aliyoekewa enstain ni ku-inspre watu tu, ili watu wapate kioo cha kujitazamia na tuamini kuwa elimu imenza na hawa watu ,lakini sio ukweli kuwa alivumbua na kua muanzilishi wa sheria za physics,kila elimu ipo kwa maelfu ya miaka, saivi kila kinachovumbuliwa anapewa mtu jina ili awe yeye ndio alovumbua,kama walovumbua simu,computer umeme,elimu ya kila kitu ilikuwepo kwa maelfu ya miaka,physics yote inajulikana kwa maelfu ya miaka.hii dunia ilikua na civilizations nyingi with technological advancement,ambazo historia zao zimepotwezwa,,,,,sisi tuendelee kuamini tu kila tuanchoambiwa
 
Barua iliyoandikwa kwa hati ya mkono na Albert
Einstein, ambapo anajadili suala la dini na imani,
imeuzwa kwenye mnada kwa bei ya karibu $2.9m
(£2.3m).
Bei hiyo imepita makadirio.
Barua hiyo ambayo kwa utani imekuwa ikiitwa "Barua
ya Mungu" aliiandika Einstein mwaka 1954 na
ilitarajiwa kuuzwa $1.5m (£1.2m) mnadani New York.
Mwanasayansi huyo aliyeshinda tuzo ya Nobel,
aliandika barua hiyo ya ukurasa mmoja unusu akiwa
na umri wa miaka 74.
Lilikuwa ni kama jibu kwa mwanafalsafa Mjerumani
Eric Gutkind kuhusu baadhi ya kazi zake. Gutkind
alikuwa pia Myahudi.
Huwa inatazamwa na wengi kama tangazo la
msimamo wa Einstein katika mjadala kuhusu sayansi
na dini.
"Barua hii yenye uwazi sana, ya kibinafsi iliyoandikwa
mwaka mmoja kabla ya kifo cha Einstein inasalia
kuwa nyaraka pekee yenye kudhihirisha wazi
msimamo wake wa kidini na kifalsafa," taarifa kutoka
kwa waendesha mnada wa Christie inasema.
Barua hiyo iliuzwa karibu mara dufu ya bei
iliyokadiriwa ambayo ilikuwa kati ya $1m-1.5m.
Katika barua hiyo, aliyoiandika kwa Kijerumani
ambayo ilikuwa lugha yake asilia, Einstein amekosoa
imani ya sasa kumhusu Mungu.
"Neno la Mungu kwangu tu ni jambo la kuelezea
udhaifu wa binadamu na ni matokeo ya udhaifu huu
wa binadamu," anaandika.
"Biblia ni mkusanyiko wa hadithi za kale lakini za
kuheshimiwa na kutukuzwa, ingawa kwangu
zinaonekana zaidi kuwa za kitoto."
Anaendelea: "Hakuna fasiri yoyote, hata iwe ya kina
na ya kupambanua zaidi kiasi gani, ambayo kwangu
inaweza kubadilisha mtazamo huu wangu."
Mwanafizikia huyo pia anajadili asili na utambulisho
wake, Uyahudi.
Anaandika kwamba dini hiyo "ni kama dini nyingine
zote , ni mtazamo mpya wa hadithi za kale".
"Wayahudi, ambao najivunia kuwa mmoja wao, na
ambao nimejikita kwenye mtazamo wao wa maisha,
bado kwangu hawana kitu chochote tofauti na
wengine," ameandika.
"Kwa yale niliyoyaona, si bora kulikobinadamu
wengine, ingawa wamelindwa dhidi ya saratani mbaya
zaidi kutokana na kukosa mamlaka. Kando na hayo,
sioni kitu chochote "kiteule" kuwahusu." (Aliandika
hayo miaka michache tu baada ya Vita Vikuu vya Pili
vya Dunia kumalizika, ambapo Wayahudi wengi
waliuawa na utawala wa Nazi, na pia taifa la Israel
lilikuwa bado halijapata nguvu).
Hii si mara ya kwanza kwa barua ya Enstein kuuzwa
mnadani.
Mwaka jana, barua aliyomwandikia mwanafunzi wa
kemia kutoka Italia ambaye alizuiwa kukutana naye
iliuzwa $6,100.
Iliuzwa pamoja na barua nyingine za Einstein, ikiwemo
barua moja ya mwaka 1928 iliyouzwa $103,000.
Kwenye barua hiyo alikuwa ameeleza mawazo yake
kuhusu awamu ya tatu ya kile ambacho baadaye
kiligeuka kuwa nadharia kuhusu uhusiano wa vitu
kwenye maumbile, kwa Kiingereza Theory of Relativity.
Mwaka 2017, barua yake ambapo alikuwa anatoa
ushauri kuhusu maisha yenye furaha iliuzwa $1.56m
mjini Jerusalem.
Barua hiyo yenye aya moja tu, inasema: "Maisha ya
utulivu na ya kunyenyekea yatakuletea furaha zaidi
kuliko juhudi za kutafuta ufanisi na misukosuko
inayoambatana na harakati na ufanisi huo."
Einstein aliamini kwamba Mungu
yupo?
Einstein alikuwa kwenye kundi la watu ambao imani
yao huitwa Pantheism kwa Kiingereza.
Ni watu wanaoamini kwamba "Mungu ni kila kitu".
Mara kadha, alionyesha mtazamo huu kwenye
mawasiliano yake na Rabbi Herbert S. Goldstein,
"Ninaamini katika Mungu wa Spinoza, ambaye
anajidhihirisha kupitia upatanifu wa vitu vyote
vilivyomo, si katika Mungu anayejishughulisha katika
hatima na matendo ya binadamu."
Pantheism kwa njia rahisi zaidi ni imani kwamba kila
kitu humwakilisha Mungu. Wenye kufuata imani hii
mara nyingi hueleza kwamba Mungu ni vitu vyote
vilivyopo, au kwamba mambo na vitu vyote ni Mungu.
Kwamba kila ukionacho ni sehemu ya Mungu.
Aina ya Pantheism ya Spinoza aliyoiamini Einstein
huamini kwamba kila kitu kinafanana na Mungu.
Kwamba Mungu hana ubinafsi na hayajali mambo ya
binadamu. Kwa kila kitu kimeundwa na vitu vilevile
vya msingi, ambavyo anatoka Mungu. Kwamba Sheria
za Fizikia hazina la kuzipinga, na kwamba kila jambo
lina matokeo yake. Kila jambo linalotokea au kuwepo
lilitokana na hitaji lake kuwepo na lilikuwa nia ya
Mungu. Kwamba kwa binadamu, furaha na kuridhika
maishani hutokana na kuifahamu dunia na vitu
vinavyoizingira badala ya kuomba Mungu aingilie kati.
Benedict de Spinoza alikuwa mwanafalsafa Myahudi
aliyezaliwa Uholanzi na wazazi Wayahudi kutoka
Ureno Novemba 24, 1632, Amsterdam na akafariki
Februari 21, 1677 mjini The Hague, Uholanzi.
Licha ya haya yote Einstein bado alidumisha baadhi
ya tamaduni na mila za Wayahudi.
Hali kwamba alikuwa Mwanasayansi na kwamba
aliongozwa na fikira katika kuufahamu ulimwengu
ilimzuia kuwa na imani ambayo inaweza kuwafanya
watu waseme alikuwa wa dini fulani.
Alikataa kupewa mazishi ya kitamaduni ya Wayahudi.
Ingawa bado alikuwa anazungumzia kuhusu kuamini
kuhusu Mungu, alikuwa si Mungu wa dini za
Kiabrahamu (Kikristo, Kiislamu na Kiyahudi ) na pia
hakuwa Mungu anayerejelewa na watu walioamini kwamba Mungu yupo.
Alikuwa mara nyingi anajizuia kujiingiza kwenye
mjadala kuhusu nani msema kweli, dini au sayansi.
Aidha, hakutaka kuamini kutumiwa kwa sayansi kama
kielelezo katika kuamua maadili.
Wakati wa Vita Vikuu vya Pili vya Dunia, alinukuliwa
akisema: "Bado wapo watu, wanaosema Mungu
hayupo. Lakini kinachonighadhabisha zaidi ni
kwamba huwa wananikuu wanapoeleza msimamo
wao huo.

Bwana Kiranga natamani kusikia mtazamo wako kumhusu huyu mtu.
Nimepitia jarida la Habari njema nikakutana na hii kitu, hapa wanaeleza kuhusu Mungu kuonekana katika vitu, nadhani inaendana na mtazamo wa kina Einstein

"2. Mungu yukoje?

Hakuna mwanadamu ambaye amewahi kumwona Mungu kwa kuwa yeye ni Roho. Mungu hana mwili wa nyama na damu kama viumbe wanaoishi hapa duniani. (Yohana 1:18; 4:24) Hata hivyo, tunaweza kutambua utu wa Mungu kupitia vitu alivyoumba. Kwa mfano, matunda na maua ya aina mbalimbali yanafunua upendo na hekima ya Mungu. Ukubwa wa ulimwengu unafunua nguvu za Mungu.—Soma Waroma 1:20."

Yohana 1:18

18Hakuna mwanadamu ambaye amemwona Mungu wakati wowote; mungu mzaliwa-pekee aliye kifuani pa Baba, ndiye ambaye ameeleza juu yake.

Waroma 1:20

20Kwa maana sifa zake ambazo hazionekani, zinaonekana waziwazi tangu kuumbwa kwa ulimwengu na kuendelea, kwa sababu zinaeleweka kwa vitu vilivyofanywa, yaani, nguvu zake za milele na Uungu, hivi kwamba hawana sababu ya kujitetea.
 
Nimepitia jarida la Habari njema nikakutana na hii kitu, hapa wanaeleza kuhusu Mungu kuonekana katika vitu, nadhani inaendana na mtazamo wa kina Einstein

"2. Mungu yukoje?

Hakuna mwanadamu ambaye amewahi kumwona Mungu kwa kuwa yeye ni Roho. Mungu hana mwili wa nyama na damu kama viumbe wanaoishi hapa duniani. (Yohana 1:18; 4:24) Hata hivyo, tunaweza kutambua utu wa Mungu kupitia vitu alivyoumba. Kwa mfano, matunda na maua ya aina mbalimbali yanafunua upendo na hekima ya Mungu. Ukubwa wa ulimwengu unafunua nguvu za Mungu.—Soma Waroma 1:20."

Yohana 1:18

18Hakuna mwanadamu ambaye amemwona Mungu wakati wowote; mungu mzaliwa-pekee aliye kifuani pa Baba, ndiye ambaye ameeleza juu yake.

Waroma 1:20

20Kwa maana sifa zake ambazo hazionekani, zinaonekana waziwazi tangu kuumbwa kwa ulimwengu na kuendelea, kwa sababu zinaeleweka kwa vitu vilivyofanywa, yaani, nguvu zake za milele na Uungu, hivi kwamba hawana sababu ya kujitetea.
Mbona wanasema Mussa ndio binadam pekee alieweza kumuona mungu
 
Hebu iwekeni hapa nasi tuisome.
_104608358_hi049766849.jpeg
 
hio ndio kazi pekee aliyoekewa enstain ni ku-inspre watu tu, ili watu wapate kioo cha kujitazamia na tuamini kuwa elimu imenza na hawa watu ,lakini sio ukweli kuwa alivumbua na kua muanzilishi wa sheria za physics,kila elimu ipo kwa maelfu ya miaka, saivi kila kinachovumbuliwa anapewa mtu jina ili awe yeye ndio alovumbua,kama walovumbua simu,computer umeme,elimu ya kila kitu ilikuwepo kwa maelfu ya miaka,physics yote inajulikana kwa maelfu ya miaka.hii dunia ilikua na civilizations nyingi with technological advancement,ambazo historia zao zimepotwezwa,,,,,sisi tuendelee kuamini tu kila tuanchoambiwa
Watakubishia tu.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom