Barua ya Albert Einstein kumhusu Mungu yauzwa kwenye mnada kwa bei ya $2.9m(£2.3m).

Na Mimi naungana na Einstein kwamba biblia ni hadithi za kale kubwa zaiidi ni zakitoto.

Nilikuwa napitia machapisho ya bwana Alvin Plantinga na mtazamo wake,mchango na maoni yake kwa The problem of evil;
Felix culpa.

Alidai kwamba vitabu vya Ayub na zaburi vinatoa mchango na mtazamo mzuri kuhusu The Problem of evil "Kama Mungu ni Mwema kwanini karuhusu Mateso..??? "

Sasa ukijaribu kusoma kitabu cha Ayub ambacho wengine hukihesabu kama kitabu cha hekima,utang'amua ni hadithi za kale au kama hadithi za mamba na kima, sadiki na chitemo,Mfalme anataka apelekewe La!la!la! au hadithi za zena na betina.

Ayubu Mtu tajiri na Mcha Mungu katika Nchi ya Usi aliangushiwa mfulilizo wa matatizo watoto wake kufariki mifugo yake kondoo,Punda,Farasi na wajakazi lukuki hii ni baada ya "shetani" kupiga soga na Mungu.

Kisha Mwishoni Mungu akamubariki sana akapata mali zaiidi ya mwanzo,Sasa ukisoma kwa uzuri Maswali ya Mungu katika upepo wa kisulisuli kwa Ayubu utaona vichekesho.

Biblia inahadithi za kitoto kweli,Nuhu, Sodoma na Gomora.

Ati Taifa Teule..??? WTF

Hapo Bado hujakutana na Jehovah's Witness
"We are the pure and chosen few,and all the rest are damned,there's room enough in hell for you-We don't want heaven crammed"

Mungu wa Qur'an na biblia anamapungufu Mengi Mno.

Some time's people don't want to hear truth,because they don't want their illusions destroyed.

"He that will not reason is a bigot,
He that cannot reason is a fool,
He that dares not reason is a slave."
By William Drummond.

A godless Mind is a free mind.


Ahsantee
Wenye dini watakuambia chanzo cha dhambi ni shetani baada ya kumshawishi adamu na hawa kula tunda

Ajabu inakuja mungu anamuhukumu kiumbe ambaye yemwenyewe amemuumba akiwa ni dhaifu, alafu shetani aliyesababisha hayo yote amemuacha bila kumfanya chochote, tena wanapiga stori vizuri tu kama walivyokua wakimuongelea ayubu na mipango yao kuhusu kumjaribu ayubu

Hakuna sehemu ambayo shetani aliambiwa kua kwakosa la kumrubuni hawa kumpa lile tunda basi nawewe uta tafuta kwa jasho na nagonjwa yatakua juu yako halafu utakufa. Ila ni binadamu peke yake ambaye amepewa laana hiyo

Binadamu ataugua,atajifungua kwa uchungu,atakula kwa jasho,atapata shida na hatimae lazima afe alafu mwisho wa siku atapekekwa jehanamu kuchomwa. sasa kama kulikua na jehanamu baada ya kifo kwanini ulikua ukinipa mateso wakati niko duniani?

Ilitakiwa kama kosa kafanya duniani mmalizane huko huko duniani siyo tena umuandalie moto kwa ajili ya makosa ambayo ulisha muadhibu akiwa duniani

Mungu ni chanzo cha uovu wote duniani

I form the light, and create darkness: I make peace, and create evil: I the Lord do all these things." (Isaiah 45:7)
 
tapatalk_1536076454249.jpeg
akili ya kuambiwa changanya na yako
 
Mungu ni idea za watu. Watu baada ya kujiuliza maswali hayo na wakakosa majibu ndio waka assume kua lazima kutakua na jitu likubwa lenye uwezo wote nguvu zote na upendo wote ndio limesababisha haya kutokea

Bahati mbaya hoja yao ikakosa nguvu kua nini chanzo cha ilo lijitu?

Hapo ikatungwa idea nyingine kua ikitokea kuna jitu jingine ndio limemuumba huyu mwingine basi huyu wa kwanza hawezi kua mwenye nguvu kama mzazi wake na itakua continuation yani hata huyo baba yake na hilo jitu lazima anamzazi wake,

Kwaiyo kuondoa hiyo continuation wakapata wazo kua tukisema alikuwepo kabla,baada na milele ataendelea kuwepo, hivyo kutaondoa maswali

Lakini watu walivyotaka kuikosoa hiyo dhana kwa kuuliza nini chanzo cha huyo mungu wakaambiwa kua ni dhambi kuuliza swali hilo kuhusu chanzo chake

Hivyo ili mungu huyo akubalike ikabidi watu watiwe uoga wa kutohoji chanzo cha huyo mungu huku wakisema ili umjue inabidi uwe na imani, na imani huja kwa kukubali kwanza ndio uanze kumsoma kitu ambacho ni uongo mtupu
Maelezo yoote lakini bado hujajibu maswali yake.
 
Maelezo mafuupi lakini bado hujaeleza maswali yanani
Mkuu Anikajema alikuuliza maswali haya hapa chini,rejea post yako niliyoku equate.

(1)Tumetoka wapi? (2)kwanini tuko hapa? Lengo ni nini hasa
(3)Tunakwenda wapi baada ya Kufa? (4)Nini kisababishi pakuwepo na Wanyama binadamu wadudu na ndege(ihali vimekuepo katka maumbile tofaut ke/me ili vizaliane??.

Mjibu halafu tuendelee.
 
Mkuu Anikajema alikuuliza maswali haya hapa chini,rejea post yako niliyoku equate.

(1)Tumetoka wapi? (2)kwanini tuko hapa? Lengo ni nini hasa
(3)Tunakwenda wapi baada ya Kufa? (4)Nini kisababishi pakuwepo na Wanyama binadamu wadudu na ndege(ihali vimekuepo katka maumbile tofaut ke/me ili vizaliane??.

Mjibu halafu tuendelee.
Nilishamjibu kua baada ya watu kukosa majibu ndi wakapata idea ya kitu kinachoitwa mungu

Mungu alizuka baada ya hayo maswali kukosa majibu

Je huyo mungu alitokana na nini?

Kama mungu mnadai hana chanzo kwanini vitu vingine visiwe na chanzo kama mungu?
 
Scientist my fi
Scientist my foot ungekuwa silicon valley muda huu sio hapo masuguru korogwe
Unajua nilipo mkuu

Au unaona masihara yangu ndo unanchukulia poa ...

Ach dharau mkuu , wengine maisha yetu tumeamua yawe simple tu , since 20 unajua nipo wapi !!?

Sory mkuu ila umenikera sana , usiwe na dharau hivyo kiongozi
 
ninachoshukuru wao wameishia kumkosoa Mungu ila Majibu mhimu ya maswali yetu yanayotusumbua kama haya(1)Tumetoka wapi? (2)kwanini tuko hapa? Lengo ni nini hasa
(3)Tunakwenda wapi baada ya Kufa? (4)Nini kisababishi pakuwepo na Wanyama binadamu wadudu na ndege(ihali vimekuepo katka maumbile tofaut ke/me ili vizaliane??( siku wakiweza kuyajibu haya na kuacha kumkosoa Mungu tu basi nitajiunga nao.
Kama lengo la Mungu kukuumba nakukuleta dunia alafu ufe uende mbinguni tena ama jehanam.. na isitoshe anaujua mwanzo wako na mwisho wako...

Kwanini asinge umba huyu anapelekea jehanam na huyu mbinguni... Ama kuangamiza jehenam kwa neno tuu na kusambaratika..

Maswala ya sini yanafikirisha sanaa haswa ukiacha ubongo ufikirie na sio kuwaza yale tunayo karirishwa
 
Mkuu britanicca wakati mwingine tunaogopa kuishi uhalisia wetu kwa kuhofia jamii inayotuzunguka inatuonaje, wazazi watanionaje, nafikiri kama mtu anaamini moyoni mwake hakuna Mungu haina haja ya kwenda kwenye nyumba za ibada kupoteza muda, ishi mawazo yako.
Sikuhizi watu wengi sana wanazikwa kawaida tuu bila dini sema wanaongea maneno makali sanaa et chagua dini yoyote uzikwe nayo... Mambo haya yanafikirisha sana
 
Mkuu kinundu huo ni aina nyingine ya ubabaishaji wa kileo kwenye haya madhehebu yetu, nani aliwaambia watu au kuwadanganya kuwa ukizikwa kwa kufuata dini fulani utaenda mbinguni? Tumesahau kuwa matendo yetu ndio yatatoa hukumu yetu? Ata kama ukiswaliwa katika msikiti mtukufu wa pale Maca au kanisa takatifu la st Peter's Basilica pale Roma kama wewe ni muovu na umekufa katika uovu wako, makazi yako kulingana na hivyo vitabu vitukufu ni jehanamu na hakuna kinachobadilika.
 
Barua iliyoandikwa kwa hati ya mkono na Albert Einstein, ambapo anajadili suala la dini na imani, imeuzwa kwenye mnada kwa bei ya karibu $2.9m (£2.3m).

Bei hiyo imepita makadirio.

Barua hiyo ambayo kwa utani imekuwa ikiitwa "Barua ya Mungu" aliiandika Einstein mwaka 1954 na ilitarajiwa kuuzwa $1.5m (£1.2m) mnadani New York.

Mwanasayansi huyo aliyeshinda tuzo ya Nobel,aliandika barua hiyo ya ukurasa mmoja unusu akiwa na umri wa miaka 74. Lilikuwa ni kama jibu kwa mwanafalsafa Mjerumani Eric Gutkind kuhusu baadhi ya kazi zake. Gutkind alikuwa pia Myahudi.
Huwa inatazamwa na wengi kama tangazo la msimamo wa Einstein katika mjadala kuhusu sayansi na dini.

"Barua hii yenye uwazi sana, ya kibinafsi iliyoandikwa mwaka mmoja kabla ya kifo cha Einstein inasalia kuwa nyaraka pekee yenye kudhihirisha wazi msimamo wake wa kidini na kifalsafa," taarifa kutoka kwa waendesha mnada wa Christie inasema.

Barua hiyo iliuzwa karibu mara dufu ya bei iliyokadiriwa ambayo ilikuwa kati ya $1m-1.5m. Katika barua hiyo, aliyoiandika kwa Kijerumani ambayo ilikuwa lugha yake asilia, Einstein amekosoa imani ya sasa kumhusu Mungu.

"Neno la Mungu kwangu tu ni jambo la kuelezea udhaifu wa binadamu na ni matokeo ya udhaifu huu wa binadamu," naandika. "Biblia ni mkusanyiko wa hadithi za kale lakini za kuheshimiwa na kutukuzwa, ingawa kwangu zinaonekana zaidi kuwa za kitoto."

Anaendelea: "Hakuna fasiri yoyote, hata iwe ya kina na ya kupambanua zaidi kiasi gani, ambayo kwangu inaweza kubadilisha mtazamo huu wangu."

Mwanafizikia huyo pia anajadili asili na utambulisho wake, Uyahudi.

Anaandika kwamba dini hiyo "ni kama dini nyingine zote , ni mtazamo mpya wa hadithi za kale". "Wayahudi, ambao najivunia kuwa mmoja wao, na ambao nimejikita kwenye mtazamo wao wa maisha, bado kwangu hawana kitu chochote tofauti na wengine," ameandika.

"Kwa yale niliyoyaona, si bora kulikobinadamu wengine, ingawa wamelindwa dhidi ya saratani mbaya zaidi kutokana na kukosa mamlaka. Kando na hayo, sioni kitu chochote "kiteule" kuwahusu." (Aliandika hayo miaka michache tu baada ya Vita Vikuu vya Pili vya Dunia kumalizika, ambapo Wayahudi wengi waliuawa na utawala wa Nazi, na pia taifa la Israel lilikuwa bado halijapata nguvu).

Hii si mara ya kwanza kwa barua ya Enstein kuuzwa mnadani. Mwaka jana, barua aliyomwandikia mwanafunzi wakemia kutoka Italia ambaye alizuiwa kukutana naye iliuzwa $6,100.

Iliuzwa pamoja na barua nyingine za Einstein, ikiwemo barua moja ya mwaka 1928 iliyouzwa $103,000.

Kwenye barua hiyo alikuwa ameeleza mawazo yake kuhusu awamu ya tatu ya kile ambacho baadaye kiligeuka kuwa nadharia kuhusu uhusiano wa vitu kwenye maumbile, kwa Kiingereza Theory of Relativity.

Mwaka 2017, barua yake ambapo alikuwa anatoa ushauri kuhusu maisha yenye furaha iliuzwa $1.56m mjini Jerusalem.
Barua hiyo yenye aya moja tu, inasema: "Maisha ya utulivu na ya kunyenyekea yatakuletea furaha zaidi kuliko juhudi za kutafuta ufanisi na misukosuko inayoambatana na harakati na ufanisi huo."

Einstein aliamini kwamba Mungu yupo?
Einstein alikuwa kwenye kundi la watu ambao imani yao huitwa Pantheism kwa Kiingereza. Ni watu wanaoamini kwamba "Mungu ni kila kitu". Mara kadha, alionyesha mtazamo huu kwenye mawasiliano yake na Rabbi Herbert S. Goldstein, "Ninaamini katika Mungu wa Spinoza, ambaye anajidhihirisha kupitia upatanifu wa vitu vyote vilivyomo, si katika Mungu anayejishughulisha katika hatima na matendo ya binadamu."

Pantheism kwa njia rahisi zaidi ni imani kwamba kila kitu humwakilisha Mungu. Wenye kufuata imani hii mara nyingi hueleza kwamba Mungu ni vitu vyote vilivyopo, au kwamba mambo na vitu vyote ni Mungu.

Kwamba kila ukionacho ni sehemu ya Mungu.Aina ya Pantheism ya Spinoza aliyoiamini Einstein huamini kwamba kila kitu kinafanana na Mungu.

Kwamba Mungu hana ubinafsi na hayajali mambo ya binadamu. Kwa kila kitu kimeundwa na vitu vilevile vya msingi, ambavyo anatoka Mungu.

Kwamba Sheria za Fizikia hazina la kuzipinga, na kwamba kila jambo lina matokeo yake. Kila jambo linalotokea au kuwepo
lilitokana na hitaji lake kuwepo na lilikuwa nia ya Mungu.

Kwamba kwa binadamu, furaha na kuridhika maishani hutokana na kuifahamu dunia na vitu vinavyoizingira badala ya kuomba Mungu aingilie kati.

Benedict de Spinoza alikuwa mwanafalsafa Myahudi aliyezaliwa Uholanzi na wazazi Wayahudi kutoka Ureno Novemba 24, 1632, Amsterdam na akafariki Februari 21, 1677 mjini The Hague, Uholanzi.

Licha ya haya yote Einstein bado alidumisha baadhi ya tamaduni na mila za Wayahudi.

Hali kwamba alikuwa Mwanasayansi na kwamba aliongozwa na fikira katika kuufahamu ulimwengu ilimzuia kuwa na imani ambayo inaweza kuwafanya watu waseme alikuwa wa dini fulani.

Alikataa kupewa mazishi ya kitamaduni ya Wayahudi.

Ingawa bado alikuwa anazungumzia kuhusu kuamini kuhusu Mungu, alikuwa si Mungu wa dini za Kiabrahamu (Kikristo, Kiislamu na Kiyahudi ) na pia hakuwa Mungu anayerejelewa na watu walioamini kwamba Mungu yupo.

Alikuwa mara nyingi anajizuia kujiingiza kwenye mjadala kuhusu nani msema kweli, dini au sayansi.

Aidha, hakutaka kuamini kutumiwa kwa sayansi kama kielelezo katika kuamua maadili.

Wakati wa Vita Vikuu vya Pili vya Dunia, alinukuliwa akisema: "Bado wapo watu, wanaosema Mungu hayupo. Lakini kinachonighadhabisha zaidi ni kwamba huwa wananikuu wanapoeleza msimamo wao huo.

Bwana Kiranga natamani kusikia mtazamo wako kumhusu huyu mtu.
Impressive
 
Nilishamjibu kua baada ya watu kukosa majibu ndi wakapata idea ya kitu kinachoitwa mungu

Mungu alizuka baada ya hayo maswali kukosa majibu

Je huyo mungu alitokana na nini?

Kama mungu mnadai hana chanzo kwanini vitu vingine visiwe na chanzo kama mungu?
Hujajibu swali hata moja hapo,unaleta porojo tu.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom