Barua ya Albert Einstein kumhusu Mungu yauzwa kwenye mnada kwa bei ya $2.9m(£2.3m).

maisha bora =f sijaelewa mkuu
Maana yake ni kwamba "maisha bora" ni seti (function) ya factors nyingi. Nilitaka kuonesha tu kwamba kila unachokisoma kina matumizi/application ktk maisha halisi ya kila siku (real life situation).

NB: huwezi ku-apply/kutumia kila ulichokisoma ktk maisha ya kila siku kwa sababu matumizi/applications hizo zinatumika/hutumika ktk mazingira mbalimbali mfano mtaani, hospital, viwandani, n.k.
 
Ahsante kwa kutuletea taarifa hii.

Mi ni moja wasio amini uwepo wa Mungu kwa zaidi ya miaka kumi sasa.
Nilianza kuamini hivi toka nikiwa form two na bado ninadunda tu.

Mungu hakuwahi kuwepo, hayupo, hana sababu ya kuwepo na hata kuwepo milele.
 
Princeton, 3. 1. 1954
Dear Mr Gutkind,
Inspired by Brouwer's repeated suggestion, I read a great deal in your book, and thank you very much for lending it to me. What struck me was this: with regard to the factual attitude to life and to the human community we have a great deal in common. Your personal ideal with its striving for freedom from ego-oriented desires, for making life beautiful and noble, with an emphasis on the purely human element. This unites us as having an "unAmerican attitude."
Still, without Brouwer's suggestion I would never have gotten myself to engage intensively with your book because it is written in a language inaccessible to me. The word God is for me nothing more than the expression and product of human weakness, the Bible a collection of honorable, but still purely primitive, legends which are nevertheless pretty childish. No interpretation, no matter how subtle, can change this for me. For me the Jewish religion like all other religions is an incarnation of the most childish superstition. And the Jewish people to whom I gladly belong, and whose thinking I have a deep affinity for, have no different quality for me than all other people. As far as my experience goes, they are also no better than other human groups, although they are protected from the worst cancers by a lack of power. Otherwise I cannot see anything "chosen" about them.
In general I find it painful that you claim a privileged position and try to defend it by two walls of pride, an external one as a man and an internal one as a Jew. As a man you claim, so to speak, a dispensation from causality otherwise accepted, as a Jew the privilege of monotheism. But a limited causality is no longer a causality at all, as our wonderful Spinoza recognized with all incision, probably as the first one. And the animistic interpretations of the religions of nature are in principle not annulled by monopolization. With such walls we can only attain a certain self-deception, but our moral efforts are not furthered by them. On the contrary.
Now that I have quite openly stated our differences in intellectual convictions it is still clear to me that we are quite close to each other in essential things, i.e; in our evaluations of human behavior. What separates us are only intellectual "props" and "rationalization" in Freud's language. Therefore I think that we would understand each other quite well if we talked about concrete things.
With friendly thanks and best wishes,
Yours,

A. Einstein
 
In short Albert eistein,haamini uwepo wa mungu,anadai biblia ni hadithi za kitoto(childish) na pamoja na kuwa yeye myahudi,haamini kama wayahudi ni wateule wa mungu,yaani chosen one,yeye kwake binadamu wote ni sawa,hakuna wa maana zaidi ya mwenzake na anamtaka rafiki yake wajadili mambo ya maana kuliko hayo mambo ya alinacha
 
Ahsante kwa kutuletea taarifa hii.

Mi ni moja wasio amini uwepo wa Mungu kwa zaidi ya miaka kumi sasa.
Nilianza kuamini hivi toka nikiwa form two na bado ninadunda tu.

Mungu hakuwahi kuwepo, hayupo, hana sababu ya kuwepo na hata kuwepo milele.
Zaburi 14
1 Mpumbavu amesema moyoni, Hakuna Mungu; Wameharibu matendo yao na kuyafanya chukizo, Hakuna atendaye mema.

2 Toka mbinguni Bwana aliwachungulia wanadamu, Aone kama yuko mtu mwenye akili, Amtafutaye Mungu.

3 Wote wamepotoka, wameoza wote pamoja, Hakuna atendaye mema, La! Hata mmoja.

4 Je! Wote wafanyao maovu hawajui? Walao watu wangu kama walavyo mkate, Hawamwiti Bwana.

5 Hapo ndipo walipoingiwa na hofu nyingi, Maana Mungu yupo pamoja na kizazi cha haki.

6 Mnalitia aibu shauri la mtu mnyonge, Bali Bwana ndiye aliye kimbilio lake.

7 Laiti wokovu wa Israeli utoke katika Sayuni! Bwana awarudishapo wafungwa wa watu wake; Yakobo atashangilia, Israeli atafurahi.
 
hio ndio kazi pekee aliyoekewa enstain ni ku-inspre watu tu, ili watu wapate kioo cha kujitazamia na tuamini kuwa elimu imenza na hawa watu ,lakini sio ukweli kuwa alivumbua na kua muanzilishi wa sheria za physics,kila elimu ipo kwa maelfu ya miaka, saivi kila kinachovumbuliwa anapewa mtu jina ili awe yeye ndio alovumbua,kama walovumbua simu,computer umeme,elimu ya kila kitu ilikuwepo kwa maelfu ya miaka,physics yote inajulikana kwa maelfu ya miaka.hii dunia ilikua na civilizations nyingi with technological advancement,ambazo historia zao zimepotwezwa,,,,,sisi tuendelee kuamini tu kila tuanchoambiwa

Tuko pamoja katika hili na hapa natilia mkazo. Sijawahi kiamini katika kuvumbua bali kinacjofanyika ni watu kutoa majina tu.

Hii maana ya uvumbuzi inatakiwa iangaliwe upya kiutendaji na uhalisia.

Mathalani hivi ni sahihi mtu kusema ameuvumbua mlima kilimanjaro,au ni sahihitu kusema amevumbua umeme,au mtu kusema amevumbua ugali ? Hili ukifikiria kwa undani na kwa uhalisia ukweli ni kinyume chake.
 
Ahsante kwa kutuletea taarifa hii.

Mi ni moja wasio amini uwepo wa Mungu kwa zaidi ya miaka kumi sasa.
Nilianza kuamini hivi toka nikiwa form two na bado ninadunda tu.

Mungu hakuwahi kuwepo, hayupo, hana sababu ya kuwepo na hata kuwepo milele.
...ni nini hatima ya MTU kufa mkuu I,e binadamu akifa anaenda wapi ?
...nataka kujua mtazamo wako kwenye hili mkuu
 
Zaburi 14
1 Mpumbavu amesema moyoni, Hakuna Mungu; Wameharibu matendo yao na kuyafanya chukizo, Hakuna atendaye mema.

2 Toka mbinguni Bwana aliwachungulia wanadamu, Aone kama yuko mtu mwenye akili, Amtafutaye Mungu.

3 Wote wamepotoka, wameoza wote pamoja, Hakuna atendaye mema, La! Hata mmoja.

4 Je! Wote wafanyao maovu hawajui? Walao watu wangu kama walavyo mkate, Hawamwiti Bwana.

5 Hapo ndipo walipoingiwa na hofu nyingi, Maana Mungu yupo pamoja na kizazi cha haki.

6 Mnalitia aibu shauri la mtu mnyonge, Bali Bwana ndiye aliye kimbilio lake.

7 Laiti wokovu wa Israeli utoke katika Sayuni! Bwana awarudishapo wafungwa wa watu wake; Yakobo atashangilia, Israeli atafurahi.
Hicho kitabu ni cha kipuuzi tu
 
ninachoshukuru wao wameishia kumkosoa Mungu ila Majibu mhimu ya maswali yetu yanayotusumbua kama haya(1)Tumetoka wapi? (2)kwanini tuko hapa? Lengo ni nini hasa
(3)Tunakwenda wapi baada ya Kufa? (4)Nini kisababishi pakuwepo na Wanyama binadamu wadudu na ndege(ihali vimekuepo katka maumbile tofaut ke/me ili vizaliane??( siku wakiweza kuyajibu haya na kuacha kumkosoa Mungu tu basi nitajiunga nao.
 
Barua iliyoandikwa kwa hati ya mkono na Albert Einstein, ambapo anajadili suala la dini na imani, imeuzwa kwenye mnada kwa bei ya karibu $2.9m (£2.3m).
Bei hiyo imepita makadirio.
Barua hiyo ambayo kwa utani imekuwa ikiitwa "Barua ya Mungu" aliiandika Einstein mwaka 1954 na ilitarajiwa kuuzwa $1.5m (£1.2m) mnadani New York.
Mwanasayansi huyo aliyeshinda tuzo ya Nobel, aliandika barua hiyo ya ukurasa mmoja unusu akiwa na umri wa miaka 74.
"Barua hii yenye uwazi sana, ya kibinafsi iliyoandikwa mwaka mmoja kabla ya kifo cha Einstein inasalia kuwa nyaraka pekee yenye kudhihirisha wazi msimamo wake wa kidini na kifalsafa," taarifa kutoka kwa waendesha mnada wa Christie inasema.

Katika barua hiyo, aliyoiandika kwa Kijerumani ambayo ilikuwa lugha yake asilia, Einstein amekosoa imani ya sasa kumhusu Mundu.
"Neno la Mungu kwangu tu ni jambo la kuelezea udhaifu wa binadamu na ni matokeo ya udhaifu huu wa binadamu," anaandika.
"Biblia ni mkusanyiko wa hadithi za kale lakini za kuheshimiwa na kutukuzwa, ingawa kwangu zinaonekana zaidi kuwa za kitoto."
Anaendelea: "Hakuna fasiri yoyote, hata iwe ya kina na ya kupambanua zaidi kiasi gani, ambayo kwanu inaweza kubadilisha mtazamo huu wangu."
Mwanafizikia huyo pia anajadili asili na utambulisho wake, Uyahudi.
Anaandika kwamba dini hiyo "ni kama dini nyingine zore, ni mtazamo mpya wa hadithi za kale".
"Wayahudi, ambao najivunia kuwa mmoja wao, na ambao nimejikita kwenye mtazamo wao wa maisha, bado kwangu hawana kitu chochote tofauti na wengine," ameandika.
"Kwa yale niliyoyaona, si bora kulikobinadamu wengine, ingawa wamelindwa dhidi ya saratani mbaya zaidi kutokana na kukosa mamlaka. Kando na hayo, sioni kitu chochote "kiteule" kuwahusu." (Aliandika hayo miaka michache tu baada ya Vita Vikuu vya Pili vya Dunia kumalizika, ambapo Wayahudi wengi waliuawa na utawala wa Nazi, na pia taifa la Israel lilikuwa bado halijapata nguvu).

Einstein aliamini kwamba Mungu yupo?
Einstein alikuwa kwenye kundi la watu ambao imani yao huitwa Pantheism kwa Kiingereza.
Ni watu wanaoamini kwamba "Mungu ni kila kitu".
Mara kadha, alionyesha mtazamo huu kwenye mawasiliano yake na Rabbi Herbert S. Goldstein, "Ninaamini katika Mungu wa Spinoza, ambaye anajidhihirisha kupitia upatanifu wa vitu vyote vilivyomo, si katika Mungu anayejishughulisha katika hatima na matendo ya binadamu."
Pantheism kwa njia rahisi zaidi ni imani kwamba kila kitu humwakilisha Mungu. Wenye kufuata imani hii mara nyingi hueleza kwamba Mungu ni vitu vyote vilivyopo, au kwamba mambo na vitu vyote ni Mungu. Kwamba kila ukionacho ni sehemu ya Mungu.

Aina ya Pantheism ya Spinoza aliyoiamini Einstein huamini kwamba kila kitu kinafanana na Mungu. Kwamba Mungu hana ubinafsi na hayajali mambo ya binadamu. Kwa kila kitu kimeundwa na vitu vilevile vya msingi, ambavyo anatoka Mundu. Kwamba Sheria za Fizikia hazina la kuzipinga, na kwamba kila jambo lina matokeo yake. Kila jambo linalotokea au kuwepo lilitokana na hitaji lake kuwepo na lilikuwa nia ya Mungu. Kwamba kwa binadamu, furaha na kuridhika maishani hutokana na kuifahamu dunia na vitu vinavyoizingira badala ya kuomba Mungu aingilie kati.
Benedict de Spinoza alikuwa mwanafalsafa Myahudi aliyezaliwa Uholanzi na wazazi Wayahudi kutoka Ureno Novemba 24, 1632, Amsterdam na akafariki Februari 21, 1677 mjini The Hague, Uholanzi.
Licha ya haya yote Einstein bado alidumisha baadhi ya utamaduni na mila za Wayahudi.
Hali kwamba alikuwa Mwanasayansi na kwamba aliongozwa na fikira katika kuufahamu ulimwengu ilimzuia kuwa na imani ambayo inaweza kuwafanya watu waseme alikuwa wa dini fulani.
Alikataa kupewa mazishi ya kitamaduni ya Wayahudi.
Ingawa bado alikuwa anazungumzia kuhusu kuamini kuhusu Mungu, alikuwa si Mungu wa dini za Kiabrahamu (Kikristo, Kiislamu na Kiyahudi ) na pia hakuwa Mungu anayerejelewa na watu walioamini kwamba Mungu yupo.
 
Source BBC SWAHILI.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom