JERUSALEMU
JF-Expert Member
- Sep 19, 2012
- 3,106
- 3,523
Salamu to you the Sixth president of the united republic of Tanzania!
Baada ya salamu ningependa niende moja kwa moja kwenye kusudio la barua hii. Lengo la waraka huu ni kukushauri ukipata nafasi uyasemee haya yafuatayo kwa mapana yake na kwa Lugha shawishi ili Chama chetu kishinde kwa kishindo uchaguzi huu wa 2020.
Mosi, KUWALIPA KIFUTA MACHOZI FAMILIA ZA WALIOPOTEZWA AU KUUAWA KATI 2016 HADI 2020.
Watu walio potezwa au kuuawa kikatili kisiasa ni wengi na familia zao zina uchungu usio isha. Napendekeza ulisemee hili kuwa ukiingia madarakani utawafuta machozi familia ambao wapendwa wao walipotezwa kuuawa kisiasa. Nia ni kuleta amani na utulivu katika jamii.
Pili, KUWATOA MAGEREZANI MASHEIKH WOTE WALIO MAHABUSU NA MAGEREZANI KWA SABABU ZA KISIASA NA KUWALIPA KIFUTA JASHO.
Hakika kuna kundi kubwa sana la Masheikh ambao wamefungwa kwa sababu za kisiasa na wengine tu kwasababu wanaikataa BAKWATA au wanashinikiza wawe na mahakama ya kadhi.Ahidi kwamba ukiingia madarakani utawatoa haraka pamoja kuwapa kifuta jasho ili kiwawezeshe kurudi uraiani na kuendelea na maisha yao.
Tatu, Ahidi kinaga ubaga bila kupepesa macho kuwa ukiingia madarakani UTAWAFIDIA WATU WOTE WALIO BOMOLEWA NYUMBA ZAO BILA KULIPWA FIDIA.
Kama kuna watu walionewa kupitiliza ni hawa walio bomolewa nyumba zao. Wengine walikuwa na zuio la kimahakama lakini serikali ya Kidikteta haikuheshimu mahakama wakabomoa. Watu hawa wanahitaji faraja. Ahidi chochote kwao.
Nne, KUWAPA KIFUTA JASHO WAHANGA WA TETEMEKO LA ARDHI KULE KAGERA.
Watu waliofikwa na tukio lile walifedheheshwa sana. Wanahitaji faraja kutoka kwa watanzania wapenda amani na umoja. Sema neno moja tu na roho zao zitafarijika. Walifanyiwa ukatili wa kishetani.
Tano, AHIDI KUFUTA UBAGUZI WOWOTE KATIKA UTOAJI MIKOPO KWA WANAFUNZI ELIMU YA JUU.
Awamu ya tano wamekuwa wakitekeleza ubaguzi wa waziwazi katika utoaji mikopo elimu ya juu. Imekuwa ni dhambi kusoma shule za binafsi hususan za mashirika ya dini au hizi zinazo itwa St.... hivyo kutositahili kupewa mkopo japo Mwanafunzi anatoka familia ya kipato cha kawaida.
Sita, AHIDI KUWA MAMA MARIA NYERERE ATAENZIWA KWA VITENDO NA KUPEWA ANAYO STAHILI.
Kumekuwa na tabia ya kutokumheshimu Mama Maria Nyerere hata wakati mwingine kumtumia kisiasa. Baba Wa Taifa aenziwe kwa vitendo ikiwa na kumheshimu mama Maria Nyerere.
Saba, AHIDI KUWAPANDISHA MADARAJA WAFANYAKAZI WOTE WALIO STAHILI KUPANDISHWA MADARAJA KATI YA 2016 na 2020.
Ili kurudisha ufanisi kazi ahidi kuwapandisha madaraja na kuwalipa stahiki zao kila mmoja. Jambo hili litakujengea heshima kubwa sana miongoni Mwa watumishi wa umma.
Nane, AHIDI KUWALIPA WASTAAFU WOTE AMBAO HAWAJALIPWA KATI YA 2016 na 2020.
Kuna kundi kubwa sana la watumishi walio staafu kati ya mwaka 2016 na 2020 ambao hawajalipwa fedha zao pamoja na kuingizwa katika mpango wa kulipwa Pension kila mwezi.
NB ; Makundi haya yapo Nchi nzima na ni wengi sana. Nakuomba tafuta muda Watie faraja watu hawa ambao kwa kiasi kikubwa Rais wa awamu ya tano aliwabeza na kuwafanya wajione dhalili kwenye Nchi yao.
WAPI UTAPATA FEDHA HIZI ZA KUWEZESHA MAMBO YOTE HAYA?
Kwanza napendekeza kwako ufanye yafuatayo.
Ukiingia madarakani, ongeza bei ya petrol tu siyo dizeli au mafuta ya taa, shilling moja kwa kila Lita. Tanzania nzima kuna magari takribani milioni nne yanayo tumia Petrol. Ikiwa kila Gari linatumia lita mbili kwa siku, maana yake kwa siku serikali itakusanya shs milioni 8. Kwa mwezi itakuwa milioni 240! Kwa miezi mitano serikali itakuwa imekusanya takribani shs Trilioni 1 na ushee.
Vyanzo vingine ni pamoja na kuongeza shs 1 tu kwenye vinywaji vikali na sigara kwa muda miezi Sita tu. Kwa kufanya hivyo utaweza kuponya majeraha na kurudisha furaha katika Jamii. NA MUNGU ATAKUBALIKI.