Barua kwako baba(na mahangaiko yangu ya kutafuta kazi hapa mjini)

bampami

JF-Expert Member
Nov 5, 2011
5,697
4,105
Kwa Baba Mzazi
S.L.P 25
Iguha

Shikamoo,
Kwa upande wangu ni mzima, Naendelea kupambana na maisha huku mjini,

Niilipata barua yako ya ulyokuwa ukiniomba pesa kwa ajili ya matibabu na kwamba uko ktandan hujiwez na umestisha shughuli za chama chako cha Mapinduzi hapo kijijini

Naskitka kukwambia kuwa tangu nije hapa mjini nimekuwa mtu wa kutembea na bahasha ofisi baada ya ofisi.

Mda mwingne naambulia matusi tu, nakumbuka cku moja niliambiwa "Wewe Mjinga unaishi Tanzania hii kweli? utapataje kazi bila kutoa chochote?, hyo kauli ilinikata maini sana

Nimefanya juu chini kazi hakuna huku wengne wakdai niwe na mdhamini nitamtoa wapi hapa mjini? na kwingne wanadai Uzoefu wa miaka 5 wakati ndo kwanza natoka masomoni, hvyo hali yangu ni mbaya hata hela ya kununua STAMPU na BAHASHA ya kutuma hii barua nimekopa na mpaka sasa naishi kwa msamaria mwema bada ya kukoswa koswa na polce kama mzururaji.

Vip Habari za hapo nyumbani? najua Mnateseka sana, Vpi ile SLOPU yako iliyokuwa imepasuka upande haikumaliziwa na mvua za mwaka huu? Choo chako kile ulshachmba kingne au bado ni kile kile cha sink la kopo la THEMOSI? Vp ile bendera yako ya chama ilyokuwa imechanika bado inapepea pale juu ya nyumba yako?

Je picha za Marais Kuanzia Nyerere n.k ulyobandika chumbani kwako na kwenye mlango wako wa MABUA bado zpo tu?

Nilskia Ulichaguliwa tena kuwa M/kiti wa kijiji(CCM) kwa Mara ya 20 mfululizo japokuwa haikusaidii lolote zaidi ya Kuiba KUKU wa mama yangu kwa ajili ya wageni wa chama kutoka wilayani, huku nyie mkila MILENDA na majani ya MHOGO

Nilstkitka pia kuskia kuwa Mdogo wangu Eda nae ameshndwa kuendelea na masomo yake kwa kukosa ada ya Tsh 20,000/= Kwa mwaka. Sasa uenyekiti wako unakusaidia nini? UTAKUFA wewe!, Mkeo naye Aliugua mwezi jana bila msada wa Wasamaria mauti yangempata.

Pole sana!
Mwanao Jenje.
 
Unamwita mama yako mkeo? Ulishndwa kumwita mama? Unamwambia bb yako utakufa wewe? Utazan unaongea na msela wako?

Hii barua inamakusudio gani? Unataka kutupa tenda ya kumfanyia bb yako opereshen?

Huko kijijin kwenu hakuna ofisi? Mpaka uje ujazane mjini na ku2zibia rizki?

Polis wanayo haki kukukamata coz unazurura!

Mwisho pole, kilio chako kilio changu, iko siku 2tatoka..mungu yu pamoja nasi!

Pole mpenzi.
 
baba galagaja
slp 25
iguha

mwanangu, mimi ni rafiki wa baba yako nimekuja mjini na nimeisoma barua yako mtandaoni nikiwa hapa nyumbani kwa mwanangu. nipo hapa kwa mwezi mmoja sasa nikiwa nimeletwa kwa ajili ya matibabu ya mafua ambayo yamekuwa yakinisumbua kwa siku tatu nahisi ni kwa ajili ya baridi. nimekuwa nikipata huduma hii kwa muda mrefu na nilishapona. kwa sasa nina faidi maisha nikiwa kwa mwanangu pia kaniambia kama mjini nimepapenda basi nikamchukue mama yako na ndugu zako wasiozidi wanne ili nije niishi huku mjini na ataninipa nyumba pale mikocheni na kila kitu nitakachokihitaji. lakini hadi sasa nimepewa miezi mitatu ya kukaaa na kutafakari hayo kwani kama ujuavyo pale nyumbani wadogo zako wapo 24 nitamchukua nani nimwache nani.

hata hivyo nimebaini kuwa moja ya ofisi uliyofukuzwa iko chini ya huyu mwanangu na ulipoingia tu kamera ilikuchukua na picha yako niliiiona na nilijaribu kumfahamisha habari zako lakini aliosema endapo utapata nafasi basi yule mwanaye ambaye anamaliza chuo mwakani hatopata nafasi hivyo ndo maana yule aliyepo anaitwa kaimu yaani hana madaraka kamili bali mwenye madaraka bado anamalizia masomo kwanza. kwa huruma niliyonayo nimeiba hii laptop ili nikuandikie na kujibu barua yako kwani hata hivyo yule ndugu yako baada ya kukosa ada sasa ana mimba ya miezi saba. pia mama yako kwa sasa ana nafuu kidogo ila hali ya baba yako iko tiamaji tiamaji. taarifa hizi ni kutoka kwa dereva ambaye hutumwa kila wiki kupeleka mahitaji muhimu pale nyumbani kwetu.

pole sana mwanangu kwani najua huna hata nauli ambayo ungerudi kule kijijini ungepata nafasi za kazi ya sensa ambayo baba yako ndiye anayepitisha fomu hizo na kugonga mihuri. ukiweza kuongea vizuri na konda wa lile ngalangala la kule kijijini, hebu akuchukue hadi huko ili ukiweza uwahi kujaza na kupeleka hizo fomu labda utawahi kwani mwisho ni kesho.

ndimi rafiki wa baba yako
baba gala g.
 
Lol...
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom