Barua kwa waziri wa kilimo, mifugo na uvuvi: Mhe Mwigulu Nchemba, kama hutaki kuwa mzigo fanya hivi

shikulaushinye

JF-Expert Member
Aug 29, 2014
828
456
Kwanza kabisa napenda kumpa pole kwa kuteuliwa kuwa waziri katika serikali ya awamu ya tano chini ya Rais John Pombe Magufuri, natoa pole kwa sababu siyo kazi nyepesi kuwa waziri kwenye wizara hii ambayo ina changamoto nyingi tena zinazogusa maisha ya watu. Wizara hii inagusa maisha ya watu kwa sababu asilimia 70 ya watanzania ni wakulima na wafugaji. Ndiyo maana kila waziri aleyeteuliwa huko nyuma alionekana kupyaya katika nafasi hii mpaka wengine wakaitwa mawaziri mizigo.

CHANZO CHA MIGOGORO:
Kwa muda mrefu mikoa ya kanda ya ziwa yaani Shinyanga, Mwanza, Tabora sasa na Simiyu, Geita, pia mikoa ya Dodoma, Manyara na Arusha hasa wilaya ya Monduli kwa wamasai na n k.

1.Mifugo mingi kupita kiasi:
Hakuna mipango ya marisho endelevu kwa wafugaji, mfugaji huwa anaangalia mifugo yake ipate chakula na maji leo lkn haangalii kesho. Kama tunavyojua kama ilivyo kwa mfanya biashara kuwa na lengo la kuongeza faida, kwa mfugaji naye hupata faraja anapoona ng?ombe wakiongezeka. Ongezeko hili huwa haliendani na ongzeko la marisho katika maeneo wanayoishi hivyo huwabidi kutafuta marisho sehemu nyingine.

2.Uharibifu wa mazingira:
Makundi ya ng?ombe si rafiki kwa mazingira, ardhi hubadirika na kuwa ngumu huku miti ikifyekwa kwa kiwango cha juu, hivyo kiasili mazingira katika eneo husika, mfano harisi na mikoa ya kanda ya ziwa na Dodoma ambayo imebaki jangwa hivyo mazingira kuwa siyo rafiki kwa wafugaji na kuhama mikoa hiyo kwa wingi katika mikoa ambayo bado ina sehemu zenye mapoli na kilimo.

3.Wafugaji kuwadharua wakulima:
Ni ukweli usiofichika mfugaji ni tajiri kwaani kuwa na ng?ombe 300-2000 ni pesa nyingi, kupta shilingi laki 2 ni kitu kidogo sana, hivyo basi wafugaji hujisikia kama wao ni matajiri kuliko wakulima. Hivyo wakati mwingine hupitisha mifugo kwenye mashamba ya wakulima makusudi kwa kujua kwamba hakuna anayeweza kupambana nao.

4.Rushwa kwa viongozi wa serikali za vijiji wilaya na mikoa.
Wafugaji kwa kutumia rasilimali walizo nazo huzitumia vibaya wanapohitaji kitu Fulani, kwa utafiti wangu wafugaji kupitia umoja wao ule unaotamulika kisheria ambao kiongozi wao ni mfugaji mkubwa kule KATORO GEITA ambaye anakadiliwa kuwa na ng'ombe 24,000.

Na umoja usio rasmi wa wafugaji pale walipo. Siku moja nilikuwa naongea na mfugaji mmoja msukuma ambaye familia yake ina ng'ombe 8000 ambao wamesambaa katika maeneo ya GEITA, SHINYANGA, RWANDA, MVUHA NA KILOSA (MOROGORO) nilishangaa kusikia kuwa ana ng'ombe mpaka Rwanda, niliomba maelezo kidogo kuhusu swala hili, alinambia kuwa wana mtandao mkubwa katika nchi za UGANDA hasa wanyonkole, na wafugaji wa RWANDA, hata wao wanyarwanda wana mifugo mingi humu nchini japo haichungwi na wanyarwanda. Alizidi kunieleza kuwa ng'ombe hugawanywa katika makundi madogo madogo ya kuanzia ng?ombe 300 kutegemeana na upatatikani wa marisho.

Hivyo hugawiwa watu wa kuchunga ambao hulipwa ujira wa ndama jike mmoja kila baada ya miezi 6. Hivyo akanieleza kuwa wale tunaowaona na makundi ya ng'ombe siyo wamiliki bali ni wachungaji tu. Nilimuuliza swali kuwa wanawezaje kwenda kila maeneo nchini? Alinipa jibu kuwa wao wakifika katika kijiji huweka mambo sawa na viongozi wa vijiji na kata husika baada ya hapo huweza kuanzisha maisha mapya.

Lakini pia kuna mgogoro uliwahi kutokea katika mikoa ya Kigoma, Mbeya, Iringa na Morogoro wafugaji huchanga pesa na mifugo za kuwahonga wakuu wa wilaya, wakuu wa polisi wa wailaya na mikoa, ndiyo maana kila kwenye tukio km hili wanaokamatwa kwa wingi ni wakulima huku wafugaji wakikamatwa wachache sana.

HITIMISHO:
Serikali itenge pesa kwa kuiwezesha TUME YA ARDHI ili iweze kupima ardhi za vijiji ili kuwepo na mipango bora ya matumizi ya ardhi (LAND USE PALNNING) bila kufanya hivyo migogoro itammfanya waziri aonekane ni mzigo. Nasikia gharama za ipimaji ya kijiji ni shilingi milioni 2. Kiasi hiki ni kikubwa kipunguzwe ikiwezekana iwe bure kwani tume ya ardhi ni watumishi wa serikali wanaolipwa mishahara kwa kodi za wananchi.
 
Waraka wako una upendeleo, biased. Wakulima waoahodhi maeneo makubwa bila ya kuyatumia nao wanaleta mtafaruku. Mfugaji hawezi kuangalia unachoma moto yasi wakati ng'ombe wake wanakufa kwa njaa.
 
Back
Top Bottom