Ibrahimu Zuberi Mkondo
Member
- Sep 19, 2019
- 43
- 383
Bismillahir Rahmanir Rahiim
JUMUIYA NA TAASISI ZA
KIISLAMU TANZANIA
Barua Pepe- jtkt.tz@gmail.com
S.L.B, 2055, Dar es Salaam
Kumb: JTKT/WKS/B1/21/F-SHR. 31. 08. 2021.
JAMUHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA.
WAZIRI WA SHERIA NA MAMBO YA KATIBA
S.L.P. 315, DODOMA.
YAH: TAMKO LA UHALALI WA NDOA YA KIISLAMU
Ndugu Waziri hivi karibuni umetoa kauli ya kuelekeza ndoa halali na haramu Tanzania. Miongoni mwa ndoa hizo ni ndoa ya Kiislamu. Katika hotuba yako umesema:
“Kiongozi wa Dini ambaye hajapata (idhini au), hajatambuliwa (au) kuruhusiwa na RITA kuwa msajili wa ndoa, ndoa anayoifunga kisheria ni batili”.
Katika maelezo hayo umeeleza kwamba ndoa itakayofungwa na mtu ambaye hajasajiliwa na serikali ndoa hiyo ni haramu. Ukifafanua zaidi ulisema ndoa hiyo inabatilishwa na sheria ya nchi.
Ndugu Waziri maelezo yako si sahihi kwa mizani ya Dini, Itifaki na Sharia ya nchi.
Kidini: Tunapenda uzingatie yafuatayo:
Ndoa ya Kiislamu ni ibada iliyoshushwa na Mwenyezi Mungu kwa Mtume Muhammad (SAW). Aya za ibada hiyo zimebainisha kila kitu kuhusu ndoa, tanzu zake na zimehifadhiwa vizuri ndani ya kitabu kitakatifu cha Qur’an na vile vile Sunna ya Mtume (SAW).
Ndoa ya Kiislamu inapofungwa kwa kuzingatia misingi hiyo ya Qur’ani Tukufu na Sunna ya Mtume (SAW), inakuwa halali. Kwa hiyo kiasili ndoa ya Kiislamu ni halali toka iliposhushwa na haijaharamishwa kwa Waislamu katika mazingira au zama zozote zile.
Katika misingi hiyo Mitukufu ya Qur,an na Sunna, hakuna kipengele cha cheti cha ndoa wala kipengele cha usajili wa mfungishaji. Bali kuna sifa za Maharusi na hao wafungishaji wa ndoa. Ndoa inapofungwa na Walii au Wakala muadilifu, ndoa hiyo inakua halali bila ya shaka yoyote. Itadumu kuwa halali mpaka pale itakapo koma au kuvunjika kwa misingi hiyohiyo ya Qur’an na Sunna.
Itifaki: Katika taifa letu kuna ndoa kubwa nne: Ndoa ya Kiislamu, ndoa ya Kikristo, ndoa ya Kimila na ndoa ya Serikali. Ndoa hizo zina wenyewe na wenyewe ndio wenye kauli na mamlaka kwa mujibu wa misingi ya ndoa hizo na Katiba ya nchi. Sheikh anapotoa kauli kuhusu ndoa ya Kikristo, au Padri anapotoa kauli kuhusu ndoa ya Kiislamu au Waziri anapotoa Fatwa kuhusu ndoa ya Kiislamu au ya Kikristo, mtu huyo anakuwa amechupa mipaka na kwenda kinyume na itifaki ya ustawi wa jamii.
Sheria: Kuhusu mtazamo wa sheria tunalo Bunge la kutunga sheria. Bunge hilo limeundwa na Wananchi. Makusudio ya wananchi kwa bunge lao ni kupanga na kuweka nidhamu ya mambo yao kwa pamoja. Kubwa miongoni mwa hayo ni kulinda haki zao za msingi kupitia sheria. Kwa muktadha huo bunge halina makusudio wala mamlaka ya kubadilisha Aya za Qur’an Tukufu au Biblia.
Katika dhana hiyo ya sheria na itifaki, bunge limetunga kanuni ya usajili wa ndoa zinazofungwa katika jamii. Lengo halisi la kanuni hiyo ni serikali kutambua kila ndoa na vilevile kuwa na takwimu za jambo hilo kubwa la kitaifa. Lengo la sheria ya tasjila kwa ndoa si sheria hiyo kuhalalisha au kuharamisha ndoa. Bali ni kufanya sensa itakayoiwezesha serikali kuwa na picha halisi ya jambo hilo pale itakapotaka kupanga au kutoa huduma stahiki katika jambo hilo.
Ndugu Waziri, tunakubaliana na wewe kwamba mtu ambaye atakayefungisha ndoa bila ya kusajiliwa RITA atakuwa amefanya kosa kwa mujibu wa sheria ya nchi. Ndugu Waziri jambo ambalo unatakiwa kuzingatia hapo ni kwamba kosa hilo halizuwii ndoa iliyofungwa chini ya misingi yake kuwa halali. Ndoa itakua halali hata kama mfungishaji hakusajiliwa na serikali. Kwa hiyo sheria uliyoitaja haiwezi kutengeneza adhabu kwa ndoa bali itatengeneza adhabu kwa yule aliyefungisha ndoa bila ya kusajiliwa. Maelezo yako kwamba: “…Ndoa anayoifungisha mtu huyo kisheria ni batili” yanatoa adhabu kwa ndoa na maharusi badala ya mfungishaji.
Kwa mujibu wa madhumuni ya sheria hiyo ulitakiwa utamke “wafungishaji batili wa ndoa wataadhibiwa”. Au “Ndoa iliyofungishwa na mfungishaji batili haitasajiliwa RITA”. Ni kinyume na sheria kutamka “ndoa hiyo ni batili”. Sheria uliyoitaja haina madhumuni wala mamlaka ya kuhalalisha na kubatilisha chochote katika Qur’an na Sunna.
Tumalizie kwa kukutakia kheri na utendaji mwema katika majukumu yako. Hata hivyo kuteleza ni jambo linalotokea kwa binadamu. Ni muhimu ukasimama tena kwenye vyombo vya habari kwaajili ya kusahihisha kasoro hiyo kubwa.
Tunatanguliza shukrani:
Wako katika utumishi wa Umma
* Sheikh PONDA ISSA PONDA
KATIBU MKUU*
Nakala:
• Baraza Kuu la Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania (BARAZA KUU).
• Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA).
• Baraza la Sunna Tanzania (BASUTA).
• Shura ya Maimamu Tanzania.
• Umoja wa Wanazuoni wa Kiislamu (Hayatul-Ulamaa Tanzania).
• Tanzania Islamic Foundation (TIF).
• Baraza Kuu la Wanawake wa Kiislamu Tanzania.
• Chama cha Wanataaluma wa Kiislamu (TAMPRO).
• Alhikma Foundation.
• Jumuiya ya Wahadiri wa Kiislamu (ALMALID).
• Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC).
• Baraza la Wakristo Tanzania (CCT).
• Kanisa la Kilutheri Tanzania (KKKT).
• Uongozi wa Walokole (Tanzania).
• Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.