Barua kwa watanzania na wapenda haki wote | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Barua kwa watanzania na wapenda haki wote

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mwana Mnyonge, Jul 28, 2011.

 1. M

  Mwana Mnyonge JF-Expert Member

  #1
  Jul 28, 2011
  Joined: Mar 3, 2011
  Messages: 348
  Likes Received: 46
  Trophy Points: 45
  Mwana mnyonge
  box jamii forums
  Tanzania

  kwa watanzania wote
  box
  tanzania

  kwa ndugu zangu

  yah:mwenendo wa bunge letu kuegemea upande wa serikali badala ya kutetea wananchi

  husika na kichwa cha habari hapo juu,napenda kutoa malalamiko yangu kwa watanzania wenzangu kuhusu mwenendo wa bunge letu.
  nadhani wote mnafahamu kwamba nchi yetu ina amini katika demokrasia ya vyama vingi vya siasa ,lakini katika utendaji wa bunge ni kama hawataki kuwatendea haki wapinzani,chama tawala kupitia spika wa bunge na wenyeviti wake wa bunge wamekua wana watendea vitendo visivyo vya misingi ya demokrasia hii sio haki kabisa.

  Tukumbuke kwamba wabunge wote wanawakilisha wananchi kwa kuwa sisi sote hatuwezi kuingia bungeni,swali langu ni hili,hivi hii hali itaendelea mpaka lini? ,na mwisho wa siku nani ataumia katika hili?,sababu kuna mambo mengi sana wapinzani wanaongea kwa ajili ya manufaa ya watzanzania wanyonge.

  Ni wakati wa kufanya maumuzi na kuwaambia wabunge kwamba wanatakiwa kufanya maamuzi kwa ajili ya watanzania wote.

  wenu katika ujenzi wa tanzania
  mwana mnyonge
   
Loading...