Barua kwa Rais Kikwete

Saint Ivuga

JF-Expert Member
Aug 21, 2008
54,377
58,384
Naamini watendaji wako Mh. Rais Kikwete wanasoma taarifa mbalimbali kupitia jukwaa hili hivyo watakupa salaam zangu. Ninaandika haya kama raia wa Tanzania mwenye nia njema na maendeleo na uendelevu wa taifa hili. Ninapenda kutumia fursa hii kukupongeza kwa kuendelea kuongoza Tz kwa miaka mingine mitano. Ushauri wangu kwako mheshimiwa ni huu:

1. WATANZANIA TUNAHITAJI MABADILIKO KATIKA MUUNDO NA UTENDAJI WA SERIKALI.

* Mheshimiwa tunajua tayari umepanga serikali utakayoiunda iwe na muundo gani, ombi langu kwako PUNGUZA UKUBWA wa BARAZA LA MAWAZIRI. Muhula uliopita Mh. baraza ulilounda lilikuwa kubwa mno na lilihitaji gharama kubwa sana kuendesha. Ukubwa huu usingekuwa tatizo endapo utendaji wa mawaziri/ wizara hizi ungekuwa na ufanisi. Sihitaji kuorodhesha hapa wizara ambazo ziliboronga ktk kipindi kilichopita kwani unazijua. Wako mawaziri waliokuwa mzigo na hata kufanya wananchi tukose imani na serikali yako. (Rejea tafiti zilizofanyika ambazo nyingi zilionesha kuwa wananchi tuna imani nawe Rais lakini hatuna imani na baraza lako na watendaji wengine). Ikafika mahali baadhi tulihoji UWEZO WAKO WA KUWAWAJIBISHA WATEULE WAKO. Mheshimiwa, baadhi ya wizara zilifanya vibaya sana na hata kutia doa serikali yako kutokana na utendaji na tabia binafsi za walioziongoza. Usimpe wizara mtu ambaye hajui atafanya nini na hataki kujifunza.

* Mheshimiwa, miongoni mwa wizara zinazohitaji mtu makini (waziri, naibu, katibu mkuu na wakurugenzi) ni wizara ya Elimu. Mheshimiwa miongoni mwa watanzania mil. 40 tafuta mtu MAKINI, ANAYEFAHAMU TUNATAKA KUJENGA TAIFA LA NAMNA GANI, MWENYE MAONO MEMA KUHUSU KUKUZA ELIMU YA TANZANIA UMPE WIZARA HII. Pamoja na kuwa ulipounda baraza la kwanza (2005) ulisema, .."uwaziri hausomewi.." lakini tupe mtu makini si mtu anayeyumbisha SEKTA HII MUHIMU KWA UHAI NA MUSTAKABARI WA TAIFA. Ukimpata muache hapo kwa muda mrefu ili aboreshe.

* Mheshimiwa, angalia upya uteuzi wa wakuu wa wilaya na mikoa uliowateua na utakaowateua. Wako wakuu wa wilaya ambao utendaji wao unatufikisha mahali tuanze kuhoji kama KWELI BADO TANZANIA INAHITAJI NGAZI HII YA UTAWALA?!

* Mheshimiwa, ninaomba usiongeze/ usiunde wilaya na au mikoa mipya mingine. Kwa sasa watanzania tutafarijika sana tutakapoona serikali ikijikita katika kuimarisha wilaya na mikoa mipya ulizounga mwaka huu. Mh. ninajua unafahamu kuwa ongezeko la wilaya ni ongezeko la gharama za uendeshaji na ongezeko la mzigo kwa wananchi.

* Mheshimiwa, tafuta mbinu za kufahamu utendaji wa wateule wako. Miaka mitano iliyopita kila mara ulipofanya ziara wananchi tuliibua masuala mengi yenye kuonesha udhaifu katika utendaji. Binafsi sikuupenda utaratibu uliokuwa ukiutumia wa kuwataka watendaji hao wajibu hoja hizo papo hapo. Wengi walitoa majibu kwako zaidi na hayakuwa halisi. Mheshimiwa, jiulize, kama kweli kiongozi wa idara/ halmashauri fulani ni muwajibikaji na anatoa taarifa kwa wananchi ipasavyo kwa nini wananchi tusubiri wewe uje ndio tuhoji? Au ni kusema wananchi ni wachongezi? La! Mheshimiwa, watanzania tumechoka kuishi katika dunia ya ndoto!

* Mheshimiwa, pamoja na ahadi yako ya nyongeza ya mishahara kwa watumishi wa umma/ serikali lakini ONGEZEKO HILO HALITAKUWA NA MAANA kama PAYE itaendelea kuwa katika viwango vya sasa. Tafadhali Mheshimiwa tambua kwamba wafanyakazi Tanzania (wawe wa sekta binafsi au serikali) tunabeba mzigo mkubwa sana wa kodi. Kila tunachogusa ni kulipa kodi tu. Kwa viwango hivi vya PAYE si rahisi kuwa na uwajibikaji. Fahamu kuwa wafanya biashara wanafursa ya kupata punguzo la kodi na hata kusamehewa lakini wafanyakazi hilo halipo. Wafanyabiashara hupewa fursa ya kujadili viwango vya kodi, lakini sijasikia wafanyakazi wakipewa fursa hii. Aidha kila bidhaa tunayonunua tunakatwa kodi. Mheshimiwa je, kuwa mwajiriwa ni adhabu?????

* Mheshimiwa, tekeleza mapendekezo ya kamati/ tume kuhusu sekta ya madini. Walao watanzania tuanze kunufaika na rasilimali zetu.

* Mheshimiwa, wakati wa kampeni uliahidi mambo mengi sana hadi wengine tukajiuliza hivi yatatimia? Ninajua nyingine ulipanga na nyingine ulijikuta umehidi. Sasa mh, kaa chini na watendaji wako zipitieni moja baada ya nyingine ili kuona uhalisia wake, je, utekelezaji wake utachocheaje maendeleo ya walio wengi?. Kisha mchambue na kama ziko ambazo kwa sasa hazitakuwa na manufaa sana si vibaya kurudi kwa wananchi na kutueleza kuwa tutatekeleza kwa vipaumbele. Mfano wa ahadi zako Mheshimiwa (binafsi ninazotilia shaka) ni ujenzi wa viwanja vya ndege (tena vya kimataifa). Mheshimiwa, si kila mahali ulipoahidi kiwanja cha ndege kinaweza kuwa kichocheo cha maendeleo kwa walio wengi. Mh. kuoboresha uwanja wa ndege Bukoba inaweza kuwa vema lakini si ujenzi wa uwanja wa kimataifa Misenyi. Aidha fikiri ni wananchi wangapi watanufaika na uwanja wa ndege kam watavyonufaika na kuwepo kwa meli ya kubwa, nzima na ya kisasa au barabara bora. Kigoma- kuboresha uwanja uliopo ni vema lakini elekeza nguvu zaidi katika ujenzi wa barabara na reli mpya.

* Mwisho, mheshimiwa ninaomba urudishe imani ya yetu watanzania kwa chama chako na serikali yako. Awamu hii tunataka kuona UWAJIBIKAJI ktk serikali yako. Tunahitaji kuona ukifanya mabadiliko makubwa kuhusu baadhi ya watendaji wakuu katika Chama chako. Sitafurahi ukitimia utabiri wa baadhi ya watu kuwa CCM ITAFIA MIKONONI MWAKO.

* Mheshimiwa sasa tunahitaji kuona kwa vitendo kuwa HUNA UBIA NA MTU KATIKA URAISI WAKO

Ninarudia tena kukupongeza Mheshimiwa kwa kupata heshima ya kuongoza taifa hili. Imani yangu kuwa hutadharau HESHIMA HII TULIYOKUPA. Ninaamini HUTAPENDA KUWEKA HISTORIA MBAYA ya kukatisha tamaa watanzania.


NAKUTAKIA UTENDAJI MWEMA

Lugano E.
Call +255786806028
 

tukianzia na hii misheni yao ya kusafishana CCM itamfia mikononi
 
Last edited by a moderator:
Angeua Mrisho angekuwa lupango siku nyingi. Atapata adhabu yake hapa hapa duniani.
 
:evil:
tatizo kazungukwa na washauri bomu. na miongoni mwao wapo wanotumia nafasi zao kumkaanga. safu yake ni chafu. mimi hili la kusafishana wakati ccm bado inaugulia majeraha yaliyotokana na kutofanya vizuri kwa kukumbatia ufisadi haliniingii. nani asiyejua kuwa agenda kuu ya upinzani hadi wanchukua viti vingi bungeni ilikuwa ni ufisadi? nani asiyeelerwa kuwa kuwa huu ungekuwa ni wakati mzuri kwa ccm kufanya mambo kisyansi badala ya kukurupuka? yote yalitendeka, tukachelea tukapongezana kwa ushindi wa kishindo.
binafsi sitegemei mabadiliko yoyote. sanasana watakuwa niwalewale tu.
 
Wembe ule ule uliyotunyoa 2005 - 2010 ndiyo huo huo unatumika kutunyonyoa 2010- 2015, tutegemee hali kuwa mbaya zaidi ya hii iliyopita.
Binafsi sina imani kabisa na CCM na JK, kwa hiyo mzee kumwandikia mkubwa waraka huu ni sawa na kupoteza muda, ushauri wako ni mzuri lakini kumbuka nchi hii inaongozwa ka kakundi ka watu kama 4 hivi, kwa hiyo usitegemee chochote.

Hii nchi ni YATIMA kwa sasa. pole sana tanzania..
 
Hawazi kutekeleza maoni hayo kama aliwanadi mafisadi. Sasa chenge anapewa form za kugombea usipika
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom