Barua kwa Rais Kikwete toka Musoma Vijijini | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Barua kwa Rais Kikwete toka Musoma Vijijini

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nyangeta, Jan 5, 2010.

 1. n

  nyangeta Member

  #1
  Jan 5, 2010
  Joined: Jan 3, 2010
  Messages: 5
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kilio Chetu Kwako Mh Rais Wa Jamhuri Ya Muungano Wa Tanzania Jakaya Mrisho Kikwete.

  Sisi wananchi wa Musoma Vijijini Tarafa ya Njanja Majita tunapenda kuleta kilio chetu kwako Mh. Rais tuliyekupigia kura wakati uchaguzi uliopita na ambaye tutakupigia kura uchaguzi ujao 2010 ili uweze kumaliza kipindi chako cha miaka Kumi katika madaraka.Tunakuomba usome waraka huu vizuri kasha utujibu sisi wananchi hata kupitia vyombo vya habari,hatutaki Mbunge wetu aje aseme kwa niaba yako kwani si mpenda maendeleo hasa huku Majita.

  Tarafa ya Nyanja ina Kata 12 ,na kila kata kuna shule zaidi ya moja,Tarafa hii inasifika sana kwa uvuvi wa samaki na dagaa hasa kule Busekera,na baadhi ya vitiongoji vilivyopo kando kando ya ziwa . Wananchi tunachangia kulipa kodi ya serikali kama itavyotakiwa japokuwa hatujawahi kuambiwa ni kiasi gani cha kodi tumechangia katika mwaka wa fedha.

  Tarafa yetu hii imekuwa na matatizo mengi sana na sugu ambayo yametufanya tuachwe nyuma kimaendeleo ukilinganisha na upande wa pili wa musoma vijijini nazungumzia Butiama na vitongoji vyake .Nadhani hata wewe Mheshimiwa Rais ulipokuja kwenye Mkutano Mkuu wa Halmashauri ya Taifa miezi michahche iliyopita ulipata fursa ya kuonyeshwa maendeleo ya huo upande hasa kujengwa kwa shule za kisasa ambazo baadhi zao kuna Computer na madawati lakini kwa bahati mbaya Mbunge wetu hakuchukua jukumu la kukuleta wewe au mawaziri wengine katika tarafa yetu ili waone nini amefanya,huku majita hakuna kabisa alichofanya zaidi ya kutoa misaada ya mabati na genereta ambayo nayo ipo hapo takribani miaka mitano na itaoza.

  Matizo tuliyo nayo sisi wananchi ni mengi ambayo Mbunge wetu hameshindwa kuyatatua kabisa na kuegemea upande mmoja wa kwao.
  • Naomba nianzie upande wa shule za Msingi kwa ujumla shule si nzuri na hazipo kwenye hali ya kuridhisha kabisa ,wanafunzi wanakaa nchi kutokana na ukoisefu wa madawati ,vyoo hakuna ,na isitoshe hata kama vyoo vipo basi vimejaa tayari Kwahiyo ,watoto wetu wanakuwa kwenye hatari ya kupata maambukizo kutokana na kutokuwepo na vyoo safi .Mbali na hilo shule hazina madawati ya kutosha ambapo wanafunzi wanakaa kwenye mawe kama enzi ya Mkoloni.Walimu pia hakuna kabisa,mtoto anamaliza shule hafahamu hata kuandika au kuongea kiingereza sababu kubwa wanadai uhaba wa walimu ,vifaa vya kufundishia hakuna kabisa japokuwa tunalipa kodi zetu kwa Serikali ili tuweze kunufaika kodi yetu.Kwa kweli Mh Rais kama kuondoa ujinga katika tarafa yetu hii itakuwa ni historia.Tunasikia kwenye radio kuwa kumetokea ubadilifu wa pesa za ualimu,Serikali inawasomi kwani wasitatufe njia ya kufatilia ni walimu wangapi wamelipoti kazini na pia kuwe na unique namba za ku track record za walimu.
  • Sekondari zipo 15 katika tarafa ya njanja ,tatizo ni uhaba wa ualimu hakuna ,vifaa hakuna vya kufundishia wanafunzi,mahabara kw ajili ya kufanya practical hakuna kabisa,watoto tunawalipia karo kila mwaka lakini inapofikia wakati wa kumaliza shule na matokeo yakitotoka ni zero ndiyo nyingi na wachache tu hawafiki hata 20 ndiyo wanachaguliwa kuendelea na kidato cha tano.Ili tatizo limekuwa sugu nenda rudi lakini hakuna uvumbuzi wowote ule,tumejaribu kumwambia Mbunge wetu amekuwa ni Mbunge wa kuturidhisha na vijibati vichache huku akiegemea kwake tu.Zaidi la hilo walimu hawaingii darasani kabisa na wanalipwa mishahara mwisho wa mwezi,kumbuka pesa ya mshahara niya walipa kodi.Inaumiza kama mlipa kodi hapewi huduma ya kuridhisha.Kadhalika amekuwa akijenga shule huko kwao tu na kupeleka wafadhili kuona maendeleo je huku majita hapaoni?na kama wafadhili wanatoa misaada je wanatoa kwao?Rais tusaidie ili na sisi Majita tuendelee.
  • Hospitali ambayo ndiyo huduma muhimu hapa katika tarafa yetu ya Nyanja,cha kushangaza tuna dhahanati moja tu ya Mrangi ambayo imekuwepo hapa tangu enzi ya Mkoloni hadi leo na haijawahi kufanyiwa marekebisho ya haina yoyote yale wa upanuzi,Kweli Mh Rais fikiria tu,tangu enzi ya Mkoloni idadi ya watu itabakia kuwa ile ile?Hapana idadi ya watu imeongezeka sana kwa hiyo dhahanati hii ni ndogo sana na haiwezi kukidhi huduma kwa jamii kwa hiyo tunaishia kupoteza watu,Mbali na hilo wakina mama wajawazito wanakufa sana hasa wakati wa kujifungua,sababu kubwa ni ukosekanaji wa wakunga na vifaa au wakunga hawapati mafunzo ya kutosha na siyo tu wakina mama pia watoto wetu wanafariki kila kukicha kutoka na kutokuwa na Zahanati nzuri na kubwa yenye huduma bora zikiwemo na madawa,Zahanati yetu hii wakati wote haina madawa kabisa.Mbali na watoto kuna magonjwa mengine yanatumaliza bila sisi wenyewe kufahamu mfano,Kisukari,Ugonjwa wa Moyo,Shinikizo la damu,Malaria ,Transmission disease.Kisa hakuna waganga,ma nurse,mahabara,madawa,pia choo hazilidhishi kabisa.Kwa kifupi hudumu hakuna kabisa wakina mama,watoto,wazee wanakufa kila kukicha,kwa wale walio na ndugu wenye uwezo ndiyo watasafirishwa kwenda Musoma Hospital kutibiwa japokuw ana yenyewe mpaka ufahamiane na mtu.
  • Huduma ya Maji hakuna kabisa ,bado wananchi wanasafiri mile 10 kwenda kuteka maji ili aje atoe huduma nyumbani,Kweli serikali inashindwa kupata wafadhili wa kusambaza maji majita wakati ziwa lipo?Kama Musoma mjini wamepata wafadhili kutoka Ufaransa na wemetoa kiasi cha bilioni 14 ,je sisi tunashindwa nini?Mbunge anafanya kazi gani?Yeye ni kwao tu ,tumechoka Rais na Mh Mkono.Sisi wazee tunakuomba baba utuletee mfadhili wa kusambaza maji safi.Mpaka tunazeeka hatujawahi kuona bomba japokuwa enzi za mkoloni kulikuwapo na bomba.
  • Barabara bado ni mbovu sana hasa ukizingatia tunatoa huduma ya uvuvi wa samaki huku ,wakati mvua zikinyesha inakuwa shida kubwa sana.Kwa ujumla barabara ni mbovu sana,kwa hiyo tunahitaji lami kama itawezekana Hatufahamu serikali inatoa kiasi gani cha pesa hasa katika tarafa yetu hii,sisi hatujui kabisa,tunasemewa na viongozi tu ambao hata kufika huku hakuna,report unayopewa niya uongo kwa wakandarasi hawajawahi kufika huku kujionea taabu tunazopata..
  • Umeme hakuna japokuwa ,tunasikia kwenye vyombo vya habari ya kuwa serikali ya Marekani ilitoa pesa kwa ajili ya kusambaza umeme vijijini lakini na kama ni kweli sisi wananchi hatupati taarifa kabisa hata Mh Mkono hasemi chochote.Hayo ni baadhi ya huduma kwa jamii ambayo kwayo sisi wananchi wa Majita hatupati na hatufahamu tunapata fedha kiasi gani katika bajeti.

  Mh. Rais unaweza kutuuliza swali sisi wananchi kwanini hatujapeleka haya malalamiko kwa Mbunge wetu ili yeye aweze kuyafikisha kwenye vyombo husika vya Bunge?,Jibu ni kwamba Mbunge wetu ni shida sana kumpata ,pia anatudharau sisi wananchi kwa sabau hatujui kitu na hatujasoma ni kweli hatujaenda shule lakini ni vyema atusikilize sisi lakini cha ajabu ,anadiriki kusema kwetu kwenye ubunge hawezi kutoka kabisa hata msiponipigia kura ,anadai ataununua ubunge kwa gharama ya aina yoyote ile ili kwamba aendelee kubakia madarakani.

  Hii inamaanisha kuwa rushwa itatolewa kwa wananchi hasa kwa wale watakao rubunika ili kwamba wampigie kura mwakani aendelee kubakia Mbunge.Mbunge wetu anadiriki kudharau hata baadhi ya viongozi wa kata na Wilaya kwa sababu ya pesa aliyo nayo na kuleta mabati tu,na kutoa vijisenti kwa mfano alileta generator kwenye sekondari miaka mitano iliyopita baada ya muda akaleta simtank la lita 1000 kutokea hapo hakuna kitu chochote kile ,sisi kama wananchi hatuna uwezo.Japokuwa vyote vipo hapo havifanyi kazi anasubiri uchaguzi ufike amwage pesa,khanga na vitenge ili achaguliwe tena.RUSWA AU TAKRIMA

  Mh Rais sisi wananchi hatuelewi tunachangia kiasi gani kwenye kodi ,na pia hatujui inatumika vipi,mbali na hilo serikali inatoa pesa kwakila wilaya lakini sisi tukimwuliza Mbunge wetu hatuambii kitu chochote kile,zaidi ya kutuambia nyie nyamazeni tutawaletea maendeleo wakati yeye anaishi Dar es Salaam kwenye jumba zuri,tunafahamu ya kuwa anazo pesa nyingi sana ambazo hata kama akitokea mtu mwingine wa kugombea atamshinda tu.

  Mh. Rais tumechoka kutawaliwa na watu wenye pesa kama hawa,hawatujali kabisa hasa pale wanapopata ubunge ,udiwani.Kazi yao ni kupeana posho lakini sisi wananchi tunaendelea kuteseka na hali ngumu ya maisha na kukoswa huduma kwa jamii.Tunashindwa kufahamu sisi tarafa ya Nyanja tunapewa kiasi gani cha pesa kutoka central government wakati wa budget,mbali .Mbali na hilo Mbunge ameshindwa kutuelezea matumizi ya pesa hizo ,Mkuu wetu wa wilaya hatujawahi kumwona zaidi ya kwenda ofisini kwake pale musoma Mjini.

  Mh Rais imefikia wakati tunataka serikali yetu iwe ya wazi kwa wananchi ili kwamba tufahamu ni nini kinachofanyika kwetu,wabunge na watenda kazi wanakula 10% kila kukicha,chukulia walimu hawaingii darasani lakini ikifika mwisho wa mwezi wanalipwa na kuna walimu wengi ambao ni hewa na wanaendelea kulipwa mishahara.

  Mh Rais kuna kipindi tuliomba jimbo ili likatwe mara mbili ili kwamba na sisi tuwe na mbunge wetu,lakini lilipofikishwa katika mkutano wa halmashauri kuu ya taifa ya CCM ,mbunge wetu alitupilia mbali hoja yetu.Sababu kubwa ni Tarafa ya Nyanja ina vyanzo vingi vya utajiri hasa samaki na dagaa ,pia kuna madini mbali na hilo kuna wapiga kura wengi .Kwa Mh Rais tunahitaji kwa lazima kwa kufuata taratibu za serikali ili na sisi tuwe na jimbo letu linalojitegemea.Mh.Rais tunahitaji jimbo ili likatwe mara mbili ikiwezekena iwe ni wilaya inayojitegemea.Au kuna sifa zinazohitajika kuwa wilaya?

  Mbunge wetu anapoenda kwenye vikao vya bunge hatusikii chochote zaidi ya kusema amejenga shule lakini ukitazama shule nyingi zimejengwa upande wa kwako ,hii inaonyesha ubaguzi ambao na sisi hatuutaki kabisa,na pia hatutaki tufikie kukatana mapanga kama ilivyokuwa Rorya.Tumemchoka Mkono

  Mh Rais kuna hii Basket Fund je na sisi tunafaidika vipi na huu mfuko hasa vijijini?Mbali na hilo hatuna huduma zingine kama bank,vituo vya polisi je lini huduma hizi zitawekwa?.Hata pia viongozi wa juu wa Serikali wakija wanafikia Butiama na Wilaya zingine au kusikia Rais , Wawaziri ,Mkuu wa Mkoa amekuja kututembelea sisi wananchi zaidi ya kuishia Butiama,tatizo lipo wapi?Kwanini wajita wamesahaurika katika nyadhifa za juu za serikali hasa kwenye uwaziri na sekta zingine ?Tangu wakati wa Mwl Nyerere mpaka leo hii bado tupo nyuma jetulikosea nini Serikali ya Jamhuri ya Muungano?.

  Mh Mbunge (Mkono) amekuwa akija kwetu hasa kwa sabubu ya uchaguzi ambao umekaribia,na kutoa vijipesa vidogo kwa wananchi na kuhaidi kutuletea au kuto mabati kwenye mashule ,Na pia kukutana na baadhi ya viongozi wa Tarafa na kuwapa pesa kidogo ili waanze kampeni taratibu kwa wananchi .Sisi tunasema hapana hizi pesa chafu hatuzitaki kabisa na hazituletei maendeleo katika tarafa ya Nyanja.Tunafahamu anazo pesa nyingi sana na anaweza kufanya chochote ili aendeleaa .

  Mh. Rais sisi wananchi na hasa kupitia wazee wetu ambao hawana uwezo wa kujieleza hasa kwa Kiswahili wameshindwa kuelewa uongozi wa huyu Mbunge tajiri Mkono,Kwani yeye ni Butiama tu na sehemu zake hasa upande wa kwao ndizo anazoendeleza na kutafuta wafadhili.

  Sisi hatutaki Mbunge tajiri tena mfanya biashara kwa sababu hawa ndiyo chanzo cha kuwepo na vurugu ,rushwa na pia hawatusaidii .Tunadhani kutoka na kauli yako ulisema wabunge wafanya biashara ndiyo mwisho wao wa kugombea ubunge kwani wanaharibu sifa ya nchi yetu Tanzaia ,wanatumia pesa zao chafu kutuharibia nchi na amani na utulivu tulio nao.Tunaomba kama ikiwezekana tume ya kudhibiti rushwa itumwe huku kwetu kutadhimini hali ya uchaguzi wa mwakani 2010.pesa chafu zinameanza kutembezwa.Tunafahamu ya kuwa Mkono ni mjumbe wa NEC ila hasitumie ubavu wake ili kwamba kwenyekura za maoni apitishe.Wajita tumechoka kununuliwa kwa pesa Mh.Rais tunahitaji maendeleo yanayoonekana na pia serikali iwe wazi inapotoa fedha hasa kwenye tarafa yetu.


  Kilio chetu tumekuwa nacho zaidi ya miaka 10 na hakuna ufumbuzi wa matatizo yetu inawezekana unaletewa reporti yenye kupotosha ,kwahiyo sisi wananchi kupitia wazee wetu tumeona leo tuchukue jukumu la kukuletea wewe mh rais ili jambo kabla ya mwaka kuisha kwa kupitia vyombo vya habari,

  Tumemchoka Mbunge wetu kabisa japokwa anadai ya kuwa hakuna wa kumwondoa mpaka hapo atakapoachia madaraka,pesa anadai anayo na viongozi hakuna wa kumtoa hata wewe Rais .Tukimpigia simu kutoa shida anatujibu vibaya kiongozi gani asiye tujali sisi tuliomweka madarakani?.

  Mh.Rais uchaguzi umekaribia sana tunafahamu sana utashinda tena kupitia tiketi ya CCM na tutakupatia kura zote ila mbunge wetu hapana tunaomba mtupatie jina ili kwamba sisi wananchi tumchague .,tumechoka kununuliwa kwa pesa chafu ambazo hatujui zimetoka wapi ,sasa Mh Rais tumeamka na macho yameona mbali .Tunasema ,RUSHWA HAINA MAHALI PAKE TENA, Sisi Tarafa ya Nyanja tunaomba wananchi wenzetu walio na matatizo kama yetu hasa wa Vijijini tusinunuliwe kwa rushwa ya baiskeli kwani inatulemaza kabisa.

  Rais tunakuomba haya matatizo utupatie ufumbuzi wa kina hasa katika Tarafa yetu ya Nyanja na pia tunakuomba kabla ya kuanza kampeni uje Tarafa ya Nyanja na kama siyo wewe basi waziri Mkuu.

  Tunakutakia Heri ya Mwaka Mpya 2010


  WANANCHI TARAFA YA NYANJA MAJITA MUSOMA VIJIJINI
   
 2. Kichuguu

  Kichuguu Platinum Member

  #2
  Jan 5, 2010
  Joined: Oct 11, 2006
  Messages: 7,203
  Likes Received: 867
  Trophy Points: 280
  Interesting;

  Je kuna haja ya kutenganisha majimbo kwa msingi wa ukabila?

  BTW: Karibu sana jamvini dada Nyangeta, naona hii ndiyo post yako ya kwanza kabisa na imeandaliwa kwa kirefu sana. Nadhani ingefaa upeleke kopi ya barua hii kwa mbunge wako, mkuu wa mkoa wako, ofisi ya waziri mkuu na ofisi ya Rais.
   
 3. M

  Mbunge wa CCM JF-Expert Member

  #3
  Jan 5, 2010
  Joined: Nov 13, 2009
  Messages: 476
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  kwa jinsi nilivyokereka hata sikumaliza kuisoma.
  anaahidi kumchagua tena mungu wake kikwete,
  halafy anaomba kikwete apeleke mfadhili awajengee sikui nini.....,
  mara hamtaki mbunge..........,
  mara sisi wazee..........
  mara mbunge maendeleo anapeleka kwao...........khaaa!

  yoooote pumba tu!!!!!!!!!!!!!!

  hawa ndio wanaorudisha nchi nyuma. analia wakat anaahidi kuwarejesha tena madarakani waliomliza!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!

  anategemea waliomliza miaka mitano wampelekee wafadhili wa kuwafuta machozi!!!!!!!!!!!!!!!!

  hao wazee si ndio vinara wa kugida kangara za wagombea wakati wa uchaguzi???????????????????/// eti tena wanaahidi kuwachagua!!!!!!! lakini hawawataki na kangara zao bado wanataka!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!

  maajabu ya dunia, upuuuzi mtupu!
   
 4. Edson

  Edson JF-Expert Member

  #4
  Jan 5, 2010
  Joined: Mar 7, 2009
  Messages: 9,202
  Likes Received: 722
  Trophy Points: 280
  haieleweki, uchochez, fitina,
   
 5. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #5
  Jan 5, 2010
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,514
  Likes Received: 19,932
  Trophy Points: 280
  mi sijamalizia kusoma.yaani miaka mitano ishaisha halafu bado mnampenda?maajabu .au mnajua jk ni kama nn vile cjui. kazingua msimchague
   
 6. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #6
  Jan 5, 2010
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,384
  Likes Received: 22,263
  Trophy Points: 280
  Mtalia sana safari hii,
  raisi hana mpango na watu wa musoma.
  Rais mpango wake ni jamaica kwenye mabembea, marekani na ulaya.
  Nyie wananchi wake mtajuta kuzaliwa bongo.
  Wenzenu wa same walipofikiwa na mlima, alienda jamaika kubembea,
  hii inaonyesha kuwa matatizo ya watanzia hayamwimgii kabisa akilini.
  Na alipokuwa ufaransa akijibu maswali ya waandishi wa habari, alipoulizwa kwa nini tanzania ni masikini wakati ina utajiri mkubwa wa rasilimali, akajibu kuwa hajui kwa nini tanzania ni masikini.
  Hii inamaanisha kuwa yeye ana muda na matajiri tu wa kihindi,
  ndio maana kina rostam aziz na kina jeetu patel ndio watu wake wa jirani kuliko sisi kina ndukulukudusucho.
   
 7. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #7
  Jan 5, 2010
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Yaani hawa ndugu zangu wa Majita wanasikitisha sana. Wampe tena kura 2010? Abakoreyeki? ( Amewafanyia kitu gani?)
   
 8. G

  Genda Member

  #8
  Jan 5, 2010
  Joined: Mar 23, 2009
  Messages: 82
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Huyo m-Bunge wenu amefanya makubwa huko kwao Uzanakini:

  Shule za primari na sekondari alizojengwa huko kwao Uzanakini ni za pamoja na misaada ya akina Jaeetu Patel & Co!

  Akishirikiana na wakina Jeetu Patel, alianzisha Benki M kwa sababu eti Tanzania haiwasaidii wazawa. Kwahiyo, ikamlazimu ajiunge na hao wa-Hindi.

  Yeye ni mwanasheria na m-Bunge. Ikiwa anajua wazi kuwa Tanzania haiwasaidii wazawa kuendeleza biashara, kama za mabenki, kwa nini asitunge muswada binafsi Bungeni wa kurekebisha uozo uliopo?

  Huyo huyo m-Bunge wenu alitaka kulamba pesa za National Bank of Commerce na kuwa mmojawapo ya walioibinafsisha...ingawa moyoni alijua kuwa kwa kufanya hivyo haikuwa kwa maslahi ya taifa.

  Lakini shauri ya uchu wa pesa alizoahidiwa kulipwa alisaliti hayo maslahi ili ajinufaishe binafsi na hao wenzake walioingia mchakato huo!

  Nimrodi Mkono ametumia u-Bunge wake na mengineyo kutafuta misaada kwa jina la Musoma Rural Development kumbe ni kwa ajili ya Uzanaki Rural Development.

  Fungueni: musomarural.org muone ni akina nani waliochangia hizo shule zenye majina ya Wazanaki maarufu:

  Chief Ihunyo National Secondary School (Girls); Chief Wanzagi National Secondary School (Girls); Busegwe Primary School; Oswald Mang'ombe High School; Butuguri Secondary School (Mkono).

  Sasa yu mbioni kujenga hapo Butiama Chuo Kikuu chenye jina la "Mwalimu Nyerere United World College for Self - Reliance".

  Enyi wapigakura wa Majita, mna usemi wa mwisho!

  Kama mnaona kuwa hawafai, msimpe kura zenu! Na sio hiyo tu, hata kama CCM itamchagua tena kama mgombea bila upinzani, kuna vyama zaidi ya CCM!

  Kwa kuwa Mkono ni CCM, mkimnyima kura msimpte na huyo Rais Kikwete kura zenu, kinyume cha mnavyopendekeza kufanya 2010!
   
 9. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #9
  Jan 5, 2010
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145

  Mzee Jasusi
  Musoma ya maeneo ya Majita hakuna mashujaa wanapenda sana nyama na Mathayo anajua atawachinjia wanyama kama last time wanakula wanampa kuta then wanenda kuanika sura juani ziwani wanangioja miaka 5.Ndiyo yaliyo tokea CUF na CCM na huko majita kwa huyu nani sijui wa hapo Zanaki hawana ubavu na umeona wanaomba kumpa JK kura unadhani kuna nini ?
   
 10. Kichuguu

  Kichuguu Platinum Member

  #10
  Jan 5, 2010
  Joined: Oct 11, 2006
  Messages: 7,203
  Likes Received: 867
  Trophy Points: 280
  Wewe jasusi sikuwezi kabisa.

  Kutokumpigia kura hakutafanya asiwe mbunge wao kwa vile wilaya ile ina watu wengi upande wa mashariki kuliko wajita wa upande wa magharibi; mbunge mwenyewe ndiye anayetakiwa kuwe na leadership morals za kujua kuwa jimbo zima ni kama watoto wake na anatakiwa awatumikie wote equally kama alivyokuwa akifanya Nyerere. Vinginevyo ili kuwasaidia wajita wa Nyanja, ni afadhali jimbo la Musoma vijijini ligawanywe kati ya magharibi na mashariki kama walivyofanya lile la Bunda lilogawanywa kati ya Bunda na Mwibara.

  Katika mojawapo ya mikakati ya kampeini zake za ubunge wa Bunda miaka ya nyuma, mbunge mmoja maarufu kutoka Mashariki aliwahi kusema kuwa ataelekeza nguvu zake zaidi kule kwenye maeneo ya magharibi kwa vile wajita wa upande wa mashariki ni rahisi kuzoa kura zao akishawapa fulu tu. Labda hali ndiyo hiyo hata huko Nyanja.
   
 11. N

  Nikupateje JF-Expert Member

  #11
  Jan 5, 2010
  Joined: Dec 22, 2009
  Messages: 1,314
  Likes Received: 106
  Trophy Points: 160
  Mimi inabidi niwajibu kwa kijita labda watanielewa:

  Emwe abhajita emwe. Kasi muli mamumu kutyo. Omwenda niga abhaelete amagendelelo.

  Toga nemwe mwamamwenda oyo omubunge wemwe. Omwenda chibhwila amainduka achali kukingya emiakya mitano. Mwaga mutakumumenya.

  Kwani mtakutula kuchanga jiela mukombaka bila omubunge wemwe. Omwenda abhombakile jishule. Omutoga ati jihela jo kumbaka kajisosya aki. Omwenda abhe fisadi.

  Jishule lilabhee lilomo la chalo chone cha Tanzania. Omutaga ati nemwe abhene. Muje D'Salaam mulole kutyo abhana mushule abhenyanja bhatana madawati.

  Omubunge itali ibenki. Nemwe mwamakola Nimrod Mkono abhe mwifi wokugega jihela mamilioni bhuli lusiku BOT.

  Mubhe kama Nyerere. Atamombaka Butiama no omulola Butiama yamambo kumbakwa miaka jinu.

  Namala kwo kwaika ati nemwe abhene omuja kuleta magendelelo gemwe. Atalio undi wo kubhaletela. Obhwenywa bhwo kwiyanja mwi baraza na okuganila jingani lwa kara ejo jilatulile.

  Mu kiswahili ejibhilikizwa zimepitwa na wakati.

  Mwakyonda.
   
 12. Kichuguu

  Kichuguu Platinum Member

  #12
  Jan 5, 2010
  Joined: Oct 11, 2006
  Messages: 7,203
  Likes Received: 867
  Trophy Points: 280
  Ngoja nisubiri Masatu na Jasusi waingie; tutajua tu umeandika nini.
   
 13. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #13
  Jan 5, 2010
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Nikupateje,
  Ingawa kimantiki nakubaliana na mtazamo wako,lakini pia huyu Mbunge analo jukumu la kuwajibika kuwawakilisha Wajita na kuwasaidia kujikwamua na matatizo yao. Nimeshafika Butiama na ni eneo dogo sana, sasa shule zote zile si angalau angezisambaza hata huko Nyanja wawe na angalau shule moja yenye sifa kama hizo aa Butiama? Nasikitika kusikia kuwa tangu enzi za ukoloni zahanati ya Murangi ni ile ile. Na Mukono ana uwezo wa kuhamasisha uchangiaji wa misaada ya maendeleo sikwa Butiama tu bali hata Nyanja. Angalia wenzetu wa Kyela wanavyoshupalia maendeleo ya kwao sisi nani anasema kwa niaba yetu kama si mbunge wetu?Tuendelelee na mada.
   
 14. N

  Nikupateje JF-Expert Member

  #14
  Jan 5, 2010
  Joined: Dec 22, 2009
  Messages: 1,314
  Likes Received: 106
  Trophy Points: 160
  Mkuu,
  Nashukuru umekuwa muangalifu kutumia neno kuhamashisha. Lakini tuangalie huko nyuma.

  Dr. Chinuno Charles Magoti alikuwa anachukua PhD yake Ujerumani mwaka 1980. Research yake ilikuwa ni matatizo ya mkoa wa Mara na hasa Majita. Nadhani wewe unaelewa kwamba Majita si wilaya ila ni eneo lote wanakokaa wajita, waruri, wakywaya nk.

  Mwaka huo Magoti akagombea na Herman Kirigini baba yake na Rose Kirgini huyu mbunge wa sasa akashindwa na akarudi Ujerumani kumalizia PhD yake.

  Mwaka 1985 Magoti akagombea tena na wakati ule alisema wazi katika PhD yake aligundua matatizo ya Musoma vijijini ni shule. Alishinda. Shule zikajengwa kama vile Mabhui Melafulu, Nyegina Sekondari nk.

  Magoti alikuwa ni mbunge wa mfano. Fikiri shule hizo ni za kijijini na zilinza kwa juhudi yake. Lakini na uchanga wa shule hizo Magoti alifikia hatua ya kusomesha watoto wake kwenye shule hizo. Mmoja alisoma Nyegina Sekondari na mwingine msichana Kitinda mimba marehemu alisoma Mabhui.

  Leo hii ni kiongozi gani anafikiria kuanzisha shule halafu watoto wake wanasomea shule hizohizo. Wanapiga kelele shule za kata wakati wao hata special school hawapeleki watoto wao. Wanawapeleka Uingereza, South Africa wakijinyima sana Uganda. Ukweli ni kwamba matatizo ya shule za kata za sasa ni nafuu kuliko shule zile za CHinuno Magoti kule Musoma vijijini.

  Sipigi kampeni lakini naeleza niliyoyaona. Kampemi ya mwaka 1985 Magoti aliwaambia wapiga kura wake kuwa yeye atakuwa "maguru mangu" miguu yenye speed kali. Wakihitaj hiki wachange yeye atakimbilia.

  Leo tunadhani mbunge ndiye mleta hela. NImrod Mkono atatoa hela wapi yeye kama yeye. Sana sana atawadekeza na kudhani kuwa ni watu wa kuletewa tu bila kujibidiisha.

  1995 wabunge wengine walifuata. Sijui zile shule zilifuatiliwa vipi lakini ukweli ni kwamba shule zilisimikwa tangu 1987.

  Leo tumtegemee Mkono badala ya kusisitiza uwajibikaji kwenye Halmashauri zao. Hela ya Mkono sidhani kama itangara zaidi ya miaka sita ijayo. Yatarudi yaleyale kama shule alizoazisha Magoti mwaka 1987 na leo zinaonekana kama magofu.
   
 15. Kichuguu

  Kichuguu Platinum Member

  #15
  Jan 5, 2010
  Joined: Oct 11, 2006
  Messages: 7,203
  Likes Received: 867
  Trophy Points: 280
  Mkuu Jasusi ngoja na mimi nikusaidie kumjibu mheshimwa huyu baada ya kuunganisha maneno yake na kumpata sawasawa at least 90%.
  Hapa ni kweli, baada ya kuona katika kipindi cha kwanza kuwa hafai, basi angalau wangem-beep kwa kumnyima kura. lakini baadala yake walimpa kura zote kama vile walikuwa wameridhika na utendaji wake katika kipindi cha kwanza.
  (1) hapa ni kuwaonea wananchi wa Nyanja kwani hata huko Butiama siyo wananchi waliochanga na kujenga shule zile. Sehemu zote zinazofanikiwa kupata shule za kisasa, sehemu kubwa hutokana na misaada itolewayo na wafadhaili mbalimbali: wazawa wenye uwezo kutoka eneo line na sympathizers wao.

  (2)Huyu mbunge anajulikana kuwa ni fisadi tu, hakuna utetezi. Alipata ubunge huo baada ya kuwa ameshakuwa fisadi chini ya Mkapa na Chenge.
  (1)Sidhani kama wanataka mbunge ndiye awape hela za kutoka mfukoni mwake. Wanalotaka ni yeye kuwaondoza na kuwawakilisha sehemu mbalimbali anakopata wafadhili kama hao anaopata wa kujenga Butiama.

  (2) Kama nilivyosema huko nyuma, huyu bwana alishakuwa fisadi kabla ya kuwa mbunge, kwa siyo kweli kuwa "mwifi" ili kukidhi matakwa ya wananchi wake. Labda swali la kuwauliza wananchi hao liwe ni kwa nini walimchagua mtu fisadi kuwa mbunge wao
   
 16. G

  Genda Member

  #16
  Jan 6, 2010
  Joined: Mar 23, 2009
  Messages: 82
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nijaribu tafsiri yangu ya ki-Jita cha kujifunza:

  Ninyi Wajita, ninyi. Kweli ninyi ni wajinga. Nina nani mnataka awaletee maendeleo. (abhaelete ISOMEKE abhaletere).

  Ni ninyi mliompenda huyo mbunge wenu. Mnataka kutuambia kuwa kabadilika kabla ya kumaliza muda wake wa miaka mitano. Hamkujua hayo.

  Kwani hamwezi kuchanga pesa kujenga bila huyo mbunge. Mnataka awajengee mashule. Hivi mnafikiri hizo pesa anazitoa wapi. Mnataka awe fisadi.

  Tatizo kuhusu mashule ni hoja sugu nchini Tanzania. Mnadhani ni ninyi tu. (Omutaga ISOMEKE Omutoga). Njooni DÂ’Salaam muone jinsi watoto wanavyokaa bila madawati.

  Mbunge si benki (Omubunge ita ibenki ISOMEKE Omubunge itali benki). Ni ninyi mliomfanya Nimrod Mkono akawa mwizi wa kuchukua mamilioni ya pesa kila siku BoT.

  Muwe kama Nyerere. Yeye hakujenga Butiama na mnaona Butiama imeanza kujengeka miaka ya karibuni.

  (Namala kwa kwo kwaita ISOMEKE Namala no kwaika)

  Namaliza kwa kusema ni ninyi wenyewe mtakaoleta maendeleo yenu. Hakuna mwingine wa kuwaletea. Mchezo wa kukaa vijiweni na kuhadithiana hadithi kama zamani hayo ni ya zama za kale.

  Asanteni

   
 17. N

  Nikupateje JF-Expert Member

  #17
  Jan 6, 2010
  Joined: Dec 22, 2009
  Messages: 1,314
  Likes Received: 106
  Trophy Points: 160
  Mkuu,

  Hauko mbali sana na nilihcokisema. Nilitumia kijita makusudi kwa sababu nawafahamu hawa ndugu zangu vizuri sana na nilitaka wajue kuwa ninawajua kisawasawa.

  Kwako tatizo ni dogo nalo ni kwamba hukujui kijita na tafsiri yako ni kwa sababu ya kushabihiana kwa maneno ya kibantu. Ila kila unachosema nimekisema nandiyo maana Jasusi au yeyote anayejua kijita hatanipinga.

  NImeshuhudia kampeni ya 1985 na 1990 kwa macho yangu ambazo zote mbili ameshinda huyo Charles Chinuno Magoti ambaye mwaka jana alipigwa chini na Makongoro Nyerere uenyekiti wa mkoa wa Mara.

  Magoti aliwaambia wazi kuwa yeye hana hata senti tano na kwamba haitatokea aje mbunge Musoma awadanganye ana hela. NImesema shule si kwamba hazikujengwa, nimesea zilijengwa na watoto wa Magoti wamesoma shule zile.

  Ukitaka nitakutajia. Malima Magoti na Magoti Magoti wamesoma Nyegina Sekondari. Marehemu Immakulata Magoti amesoma sekondari Mabhui Melafulu. Bwisya kulifunguliwa sekondari. Nadhani hata Nyambono kulifunguliwa sekondari. Hizo ni zile tu nilizofahamu.

  Machine za kusaga nafaka hizo ndizo usiseme.

  Visima vya maji kupitia kampuni ya HESAWA vilichimbwa kiasi chake.

  Kuna jamaa alianzisha hata mtandao uitwao Juasun ili wana-musoma kwa ujumla waweze kuutumia kwa project yake ya rural communication. Click here and here.

  Yote haya ni kabla hata kujua kwamba kuna kiumbe duniani kinaitwa Nimrod Mkono.

  Hivyo kilichotakiwa ni kuendeleza yaliyokuwepo. Mkono kaanzisha shule mbili tatu basi imepigwa kelele kumbe wenzake walifanya kazi hiyo miongo miwili iliyopita.

  Sasa hivi mtasema Mkono si mjita. Magoti alikuwa mjita mwenzenu na alikataa waziwazi kwamba hatawahonga hata senti tano. Alipokwepo nyinyi mliachana hela na mlimuelewa na mkampa ushirikiano.

  Walipokuja mliodhani wana mvua ya hela mkasahau kwamba ni jukumu lenu kuchanga. Mkabweteka. Mkaona yote mliyoanzisha 1987 haya maana. Mkono kafungua vishule viwili kelele zimesikika Tanzania nzima kana kwamba ndiyo wokovu umeingia.

  Kila mtanzania anajua kwamba Mkono na Musoma ni shule tu. Imefika mahala hadi watu wanahalalisha ufisadi wake eti kwa sababu pesa yake inatumika ndani kujengea watoto wetu shule.

  Shule hakujenga Magoti. Shule mlijenga wana-musoma-vijijini na Magoti wala hakuwa mhamasishaji. Mlikuwa mnatuma mnamuita kwenye vikao tunataka hiki tunataka kile na tutachanga hivi.

  Walichotakiwa kufanya sasa hivi ni kuendeleza shule za zamani kama Nyegina, Mabhui na zinginezo.

  Nyinyi mnabweteka na Nimrod Mkono kwa ahadi zake mpya. Kubukeni alichosema Chinuno Magoti kwamba hakuna mbunge atakayewaletea maendeleo bila juhudi zenu. Siku hizi hamtaki kuambiwa hivi kwenye kampeni.

  Musoma nzima au mkoa wa Mara mlitakiwa muendelee na dhana hiyo ambayo kwa kweli ilikuwa ni dana ya mwana-musoma mwenzetu mwalimu Nyerere.

  Oneni wenzetu wa Tarime, Mkono ameenda huko! Si ni kazi ya kina Rasta (Chacha Wangwe) na halmashauri ya Tarime.

  Tena bahati nzuri wajita ni moja kabila pekee mkoani Mara ambalo halijaathirika na mila potofu kama ukeketaji au kuchapana makonde kama wakurya. Sasa kwa utulivu huo mngeendeleza mliyoanzisha mngekuwa kama tarime au zaidi.

  Nasikia Rose Kirigini anataka kuwania jimbo hilo kama alivyokuwa baba yake. Mkimdhani kuwa na yeye atawaletea hela basi mtakuwa na tatizo sugu.

  Kwani Rose Kirigini amekulia pale Kamunyonge na mnamjua. Hizo hela atakuwa ametoa wapi maana hata kule Dar alikuwa anafanya kazi kiwanda cha miswaki. Asipokuja kifisadi hakuna matatizo vinginevyo shule mlizoanzisha miaka 20 iliyopita zitasahaulika, ulimwengu utadhani Mkono kaanzisha na wenzake waliomfuata wa type ile.

  Misadanganyike
   
 18. Mpaka Kieleweke

  Mpaka Kieleweke JF-Expert Member

  #18
  Jan 6, 2010
  Joined: Feb 27, 2007
  Messages: 4,137
  Likes Received: 68
  Trophy Points: 145
  Hii barua imeandikwa kutokea Dar ama ni kweli musoma vijijini?
   
 19. N

  Nikupateje JF-Expert Member

  #19
  Jan 6, 2010
  Joined: Dec 22, 2009
  Messages: 1,314
  Likes Received: 106
  Trophy Points: 160
  Mkuu,
  Ndiyo maana ninashangaa na kupiga kelele zote hizi.

  Ninavyowajua wana-musoma kama kweli wana jambo basi hawatumitumi barua.

  Nyerere alikuwa anaogopwa nchi nzima lakini wao walikuwa wanamsubiri Butiama likizo. Na kama inabidi basi walikuwa wanamfuata Msasani kwa kutuma ujumbe wa watu na si kutuma barua.

  Hawana woga wana-musoma na hili aliwahi kulisimulia Marehemu Jaji Francis Nyalali. Nyerere alitaka kumuhamisha Nyalali wakamfuata moja kwa moja Msasani.

  Woga wa kitoto wa kuandika barua za wazi sijawahi kuziona hata magazetini. Wanamusoma hata maofisini ama watakuambia ondoka na ofa zako acha nife masikini. labda hiki ndicho kinachofanya waonekane wako nyuma lakini ni kwa sababu hawana tabia kujinyenyekeza kwa binadamu mwenzio hata kama ni tajiri dunia nzima.

  Si mmeona kule Tarime FFU na bunduki zao ilibidi wagwaye kwa marungu yenye misumari. na CHADEMA ikang'aa.

  Umeonaje Busanda na Biharamuro tena nasikia huko baadh ya wanamusoma walikodiwa lakini hawakuwa wengi wa kutosha.
   
 20. Kibunago

  Kibunago JF-Expert Member

  #20
  Jan 6, 2010
  Joined: Jan 11, 2008
  Messages: 288
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Waraka unasema,


  Kwanza niwape Hongera nyingi kama mnamaanisha kweli katika hii kauli!


  Ufahamu na ushauri wangu:

  Kama kweli mnayosema ni kweli yaani hayana majungu, wala kukolezwa chumvi na ni kauli ya wengi na siyo wachache tu, basi addressee wa waraka huu si Rais bali WANANCHI WA JIMBO HUSIKA LA UCHAGUZI.

  Rais hawezi kuingilia uchaguzi wa wananchi kama mnaona kuna mwenye sifa kuliko huyu si mfanye kweli mumchague huyo?
  Pili kwa nini mkubali kupokea rushwa. Kwa nchi yetu mtoa na mpokea rushwa iwe ya baiskeli au ya kofia na hata ya 'bhunu mbundi' wote mna hatia. Na kama ni kweli mnayoeleza basi mlikuwa mnavuna mlichopanda. Maana ni nani atakaye amua kutumia fedha zake nyingi mfano kununulia vijiji baiskeli na baadaye awe busy kuwatumikia? Ni lazima atumie sasa muda wake mwingi kutafuta kurejesha mlichomchomoa! It is as simple as that!

  Pengine kama mna ujumbe au ombi jingine kwa Rais mseme lakini la kupokea rushwa na halafu kuumia chini ya nira mliyojichagulia hilo si la Rais, sana sana ninyi mnaingia katika journal kama 'case study' ya kujifunzia katika somo la uraia na madhara ya matumizi mabaya ya haki ya kuzaliwa!
   
Loading...